Kutumia Maji yaliyobadilika katika ...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kutumia Maji yaliyobadilika katika Kujitoharisha.

Question

Nini hukumu ya kutumia maji yaliyobadilika kwa klorini na kutu ya chuma katika Tohara?

Answer

 Sifa zote njema ni zake Mwenyezi Mungu, rehma na amani zimfikie Mtume Muhammad S.A.W., watu wake, masahaba wake na waliomfuata. Ama baada ya hayo:

 Klorini ni: elementi ya kikemia inayotokana na chumvi ya chakula na michanganyiko mingine, na hutumika kusafishia maji ili kuua vijidudu, aina ya bakteria na vingine vinavyopatikana katika maji.

 Ama kutu ya chuma ni: elementi yenye rangi nyekundu inayokaribia hudhurungi, hujitengeneza juu ya uso wa madini ya aina mbali mbali pale madini hayo yanapokutana na unyevu nyevu juu ya tabaka la juu, kama vile nguzo za taa, kwa hiyo unakuta kutu ya chuma katika sehemu iliyozikwa ardhini zaidi kuliko sehemu ya juu.

 Ama maji yanayobadilika kwa klorini, hayo ni maji safi (ya kujitoharisha), yanatumiwa katika kutoharisha hadathi na uchafu, kwani maji hayo yaligeuka kwa kitu safi ambacho hakishindi maji ya asili katika sifa zake, na dalili ya hayo ni kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na tunayateremsha kutoka mawinguni maji safi (kabisa)} [AL FURQAAN 48].

 Na ushahidi hapa: neno “maji” ni Nakira (neno lisilojulisha kitu maalumu). Kwahiyo hujumuisha kila aina ya maji.

 Aidha katika Sahihi mbili kutoka kwa Ibn Abbas kuhusu mtu muhrim (aliyevaa mavazi ya kuhirimia katika Hijja) ambaye alitekwa na ngamia wake na alifariki dunia, Mtume S.A.W. alisema: "Mwosheni kwa maji na mkunazi", na uthibitisho hapa ni kwamba mkunazi unazigeuza baadhi ya sifa za maji, licha ya kuwa maji ya kumwoshea maiti yanatakikana yawe tohara. Hadithi hiyo inaashiria kutoathirika maji kutokana na mkunazi, kwa kuwa mkunazi unatumiwa katika kusafisha na kutakatisha.

 Na Al Nassaaiy alitoa kutoka kwa Umm Haany, kwamba Mtume S.A.W. alikoga katika chombo ambacho kina athari ya unga laini.

 Kutokana na tuliyoyasema juu, baadhi ya wanachuoni walisema: Ibn Mawduud wa madhehebu ya Hanafiy alisema katika kitabu cha [Al Ikhtiyaar Litaalil Al Mukhtaar, 1/14, Ch. Al Halabiy]: "Na Tohara inajuzu kwa maji yakichanganyika na kitu kisafi kinachogeuza moja ya sifa zake, na hakiondoshi uwepesi wake kama vile zafarani, ama kuhusu maziwa kuna kauli mbili. Tohara haijuzu kwa maji yaliyobadilika kwa kuweka kitu (kama vile vinywaji, siki na arki) kinachoyashinda maji na kuondosha sifa za maji na tabia yake. Na maumbile ya maji ni mmiminiko wenye kurutubisha na kukata kiu. Na maji yaliyochanganyika na sehemu ya udongo yanafaa kwa udhu, kwa kuwa bado yanaendelea kuitwa maji. Lakini haifai kutia udhu kwa maji yaliyochanganyika na siki, kwa kuwa jina la maji hapa limeondoka na kuitwa siki. Kwa hiyo basi, kila chenye kuyazidi maji na kuondoa uhalisia wake na sifa zake huingia katika kundi la siki. Ama maji yakikizidi kitu na uhalisia wake ukabaki basi hukumu yake ni kama maji yaliyochangayika na sehemu ya udongo, kwani huwa ni kama maji ya chemchem na kisima. Na Tohara haijuzu ikiwa maji yamebadilika kwa kupikiwa kama vile mchuzi, lakini Tohara inajuzu ikiwa maji yamechanganyika na vitu vya usafi kama mkunazi au sabuni sharti maji yasigeuke uzito wake. Haya yanajuzu kwa kuwa kuna hadihiti ya Mtume s.a.w kuhusu kumuosha maiti kwa kutumia maji na mkunazi.

 Skeikh Taqiy Al Deen Ibn Taimiah (Mwenyezi Mungu amrehemu) aliitetea rai hiyo na akasema katika kitabu cha [Majmuo' Al Fatawi, 21/25, Ch. Kampuni ya Uchapishaji ya Majmau' Al Malik Fahad, ya Al Madina Al Nabawiya]: "Kauli ya pili: kwamba hakuna tofauti baina ya maji yaliyogeuka kimaumbile na kinyume cha hivyo, na wala yale yaliyogeuka kwa kitu kisichoepukika; au kwa kitu kinachoweza kuepukika. Kwa kuwa yanaitwa maji na hayakuzidiwa na vitu vingine basi yatakuwa masafi. Kama ilivyo katika madhehebu ya Abi Hanifa na Ahmad katika mapokezi mengine kutoka kwake. Na hivi ndivyo alivyozungumza katika majibu yake. Na kauli hii ni sahihi kwani Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: {Na kama mkiwa wagonjwa (mmekatazwa kutumia maji) au mmo safarini au mmoja wenu ametoka msalani au mmewagusa wanawake (mmewaingilia) wanawake kisha hamkupata maji, basi mtayammamu (ikusudieni) ardhi safi ya mchanga, pakeni nyuso zenu na mikono yenu.} [AN NISAA 43]. Kauli ya Mwenyezi Mungu: {na msipate maji} ni “Nakira” katika mfumo wa kukanusha, hujumuisha kila aina ya maji, na hakuna tofauti kati ya aina moja ya maji na nyingine. Ikisemwa: Maji yaliyobadilika hayaitwi maji? Jibu: kuitwa Maji hakubadiliki kutokana na mgeuko wa kimaumbile, wa ghafla au mgeuko ambao unaweza kuepukwa na ule usioweza kuepukwa.Ama kwa upande wa lugha, jina kiujumla na sifa maalumu hakuna tofauti baina ya haya na yale.

 Na imethibitika katika Sunna ya Mtume S.A.W. kwamba alisema kuhusu bahari: " maji yake ni safi na ni halai maiti yake". Na maji ya bahari ni maji yaliyobadilika ladha yake kwa kuwa na kiwango kikubwa cha chumvi.

 Ikiwa Mtume s.a.w ameeleza kwamba maji ya bahari ni safi -licha ya kubadilika- basi maji yenye chumvi hafifu yanafaa zaidi kuwa safi hata kama chumvi imetiwa kwa makusudi, kwani kwa upande wa lugha hakuna tofauti baina ya aini mbili hizi za maji.

 Kwa hiyo, hoja ya wazuiaji ni dhaifu; kwani kama mtu aliomba maji au alimwakilisha mwengine kununua maji, maji ya baharihayahusiki, isipokuwa bahari imeingia katika maana ya aya kiujumla, na pia kila chenye sifa mfanowe.

 Aidha imethibiti kuwa Mtume S.A.W. amemuamrisha mwenye kuhirimia kuosha kwa maji na mkunazi, pia amemuarisha binti yake kuosha kwa maji na mkunazi, na alimuamrisha mtu aliyesilimu kukoga kwa maji na mkunazi. Na inajulikana kwamba mkunazi ni lazima ubadilishe maji, na kama kubadilika huku kunaharibu maji basi asingeliamrisha.

 Ama maji yanayogeuka kwa kutu ya chuma, huwa yanabadilika katika mfereji ambao unatengeneza kutu ndani yake kwa sababu ya unyevu, au huwa yanabadilika kwa kitendo cha makusudi. Basi ikiwa yanabadilika katika mfereji, ni sawa na kitu kilichobadilika katika makao yake, kwahiyo maji yanapobadilika kutokana na mahali pake na njia yake hayadhuru, hukuma yake ni maji tohara hutumiwa katika kujitoharisha kutokana na hadathi au uchafu. Imepokelewa na Abu Dawuud kutoka kwa Abdullhai Bin Zaid, amesema: “Mtume S.A.W alitujia, basi tukamtolea maji katika sufuria ya shaba akatawadha”. Na shaba inabadilisha ladha ya maji, kwahiyo Mtume S.A.W. kutawadhia maji hayo ni dalili ya utohara wake.

 Al Hattaab Al Malikiy alisema: "Maji yakibadilika kutokana na maumbile ya ardhi au kwa kupita juu yake, basi hayaondoshi tohara ya maji, kama alivyosema katika Al Resaala isipokuwa maji yaliyogeuka rangi yake kwa sababu ya ardhi yanayokaa juu yake, kama mbolea au matope meusi yaliyovunda n.k..

 Tanbihi: Al Lakhmiy alisema: Maji yakibadilika hali ya kuwa yako katika mahali pake au kutokana na chombo kilichotengenezwa basi hakuna aliyekataza kutawadha kutokana na chombo (sufuria) cha chuma licha ya kuwa hupelekea kubadilisha maji kwa haraka. Na imethibiti kuwa Mtume S.A.W. alitawadha kutoka sufuria ya shaba. Na inajulikana kwamba shaba inageuza ladha ya maji, na Ibn Omar R.A. alikuwa akichemsha maji katika sufuria ya shaba.

 Na katika Taraaz: maji yakibadilika kutokana na sufuria ya shaba basi hakuna madhara, na aliongeza: Umma unaendelea kutumia maji yaliyochemshwa juu ya moto na maji ya bafu la mvuke hata kama ladha ya maji inabadiliki, Al Qarafiy, Ibn Haruun, Al Barzaliy, Ibn Farhuun, na Al Basaattiy walinukulu katika Mughniy na Al Zohariy katika misingi yake :na maji yaliyogeuka kwa sababu ya mbao ya kisima na nyasi zinazozunguka visima jangwani kwa dharura ya maji hayo, basi maji hayo ni tohara." [Mawahib Al Jalil kwa Al Hattaab 1/56, Ch. Dar Al Fikr].

 Na Sheikh Al Kharashiy alisema: " Maji yanayobadilika rangi au ladha au harufu kwa kiwango ambacho hakiondoshi asili yake kama vile samaki hai au kinaondosha asili yake kidogo tu kama makazi ya maji basi maji hayo yanafaa kujitoharisha." [Sharh Al Kharashiy Ala Mukhtasar Khalil 1/69, Ch. Dar Al Fikr].

 Na Imamu Al Desoqiy alisema katika Hashiyatahu juu ya Al Sharh Al Kabeer: "Yaani alichukua tahadhari sana katika kauli yake(mara nyingi) kuhusu maji yaliyobadilika kwa kiwango ambacho hakiondoshi asili yake au kinaondosha asili yake kidogo, basi mabadiliko haya hayana madhara. Hali ya kwanza: kubadilika maji kwa samaki hai au kwa samli ambapo watu wa jangwani hutumia sana sufuria zenye samli basi wanasameheka, ama wengine hawasameheki. Hali ya pili: kubadilika maji katika makazi yake." [Hashiyat Al Desoqiy Ala Al Sharh Al Kabeer 1/38, Ch. Dar Ihyaa Al Kutub Al Arabiya, kwa baadhi ya mageuko machache].

 Na Sheikh Al Islam Zakariya Al Ansaariy Al Shafiy: "Maji mengi yaliyobadilika kwa kukaa katika njia yake au kufanya ukungu hayana madhara, kwa sababu ni vigumu kuyalinda maji kutokana na vitu hivyo.". [Asny Al Mattalib Sharh Rawadh Al Ttalib katika Hashiyat Al Ramliy Al Kabeer 1/7, Ch. Dar Al Kitaab Al Islamiy].

 Na kutokana na hayo yaliyotangulia hapo juu: Basi maji yanayobadilika kwa klorini au kutu ya chuma yanajuzu kuyatumia katika kujitoharisha kutokana na hadathi na uchafu.

Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni mjuzi zaidi.

Share this:

Related Fatwas