Kuigusa Quraani kwa mwenye Hadathi...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kuigusa Quraani kwa mwenye Hadathi (mwenye janaba au kwa asiyekuwa na udhu)

Question

Mara nyingi huwa siwezi kuendelea kuwa na udhu kwa muda mrefu, jambo ambalo hunanizuia kuisoma Quraani mara kwa mara, kwa hivyo, na huudhoofisha uamuzi wangu wa uvumilivu wa kuendelea kuihifadhi Quraani na kuipitia pitia. Je, kama udhu wangu ukivunjika wakati ninapokuwa naisoma Quraani au naiihifadhi na kuijifunza, naruhusiwa kuendelea kuishika na kuzifunuafunua kurasa zake mpaka niimalize sehemu niliyojipangia mwenyewe kuimaliza?

Answer

Namshukuru Mwenyezi Mungu na rehma na amani ziwe juu ya Bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu na familia yake na waliomfuata. Na baada ya hayo:

Kutenguka udhu kwa sababu ya mambo yasiyolazimisha josho ni miongon mwa yanayoitwa hadathi ndogo. Na hadathi katika lugha: Ni kutuka kwa kitu. Nayo kutuka kwakitu ambacho hakikuwepo hapo kabla [Rejea: Al-Sahah kwa Al-Jawhariy 1/278, kidahizo cha . (hadathi), Dar Al-Elmu Lelmalayiin - Beirut ].

Na maana ya Hadathi kisheria: ni kitu kinachozuia kusihi kwa swala ambacho hakikubaliki. Jina hili pia hutumika kwa vitu ambavyo huondosha usafi na uzuiaji wake. [Mughni Almuhtaj 1/115 , Dar Al-Kutub Al-Elmiya] .

Inajulikana kwa wanavyuoni wote kwamba hadathi ina migawanyiko miwili: 1) Hadathi kubwa: Na 2) Hadathi ndogo. Hadathi kubwa ni ile inayowajibisha josho. Na Hadathi ndogo ni ile inayolazimisha kutia udhu. [Rejea: Al-Manthur fii Al-Qawaid kwa Zarkashiy 2/41 , Wizara ya waqfu ya Kuwaiti ].

Baadhi ya wanavyuoni wameigawanya hadathi mara tatu: Hadathi kubwa, Hadathi ya kati na kati na Hadathi ndogo. Wamefanya hivyo kwa kuzingatia yale makatazo kutokana na kusababisha kwake Hadathi. Kwa msingi huu, Hadathi kubwa ni kama damu ya hedhi na damu ya nifasi. Na Hadathi ya katikati: ni kama Janaba. Na Hadathi ndogo, ni kama kulala, kutokwa na upepo na kukojoa na mengine ambayo yanatengua udhu wala hayawajibishi josho. Izz Ibn Abdul Salam katika [Al-Qawaid Al-Kubra, 2/ 179, Dar Al-Kalamu - Dimishq na rejea: Tuhfatu Al-Muhtaj 1/65, Dar Ihyau Al-Turath Al-Arabiy.] Izz Ibn Abdul Salam anasema: “Hadathi ndogo ni sababu ya kukatazwa swala, kuzunguka Ka'abah, kusujudu kwa ajili ya kumshuku Mwenyezi Mungu, kusujudu kea kusahau, kusujudu kwa wakati wa kuisomo Quraani, kuigusa na kuibeba Quraani. Na inaongezeka katika hayo, Hadathi ya janaba – ambayo ni ya kati na kati (si kubwa wala si ndogo)- inayozuia kuisoma Quraani na kukaa katika msikitini. Na inaongezeka hedhi -ambayo ni Hadathi kubwa- inayozuia kufunga saumu, kuingiliana na talaka”. Na mwanchuoni Al-Zarkashi anaigawa hadathi katika migawanyiko minne: Hadathi kubwa zaidi, Hadathi kubwa, Hadathi ndogo zaidi na Hadathi ndogo. Na mgawanyiko huu ni kwa mujibu wa kile kinachoonekana katika ugawanyaji wa madhehebu ya Shafiiy katika matawi yao: akasema katika kitabu chake [Al-Manthur fii Al-Qawaid, 2 / 41-42]: “Kinachonekana kufuatana na maoni yao (ya wanavyuoni) kwamba (hadathi ) ina migawanyiko minne: Hadathi kubwa zaidi: ambayo huwa inawajibisha udhu na josho. Na Hadahti kubwa, ambayo huwa inawajibisha josho tu. Na Hadathi ndogo zaidi: ambayo huwa inawajibisha udhu tu. Na ndogo: ambayo huwa inawajibisha kuosha miguu tu katika kuvua khufu (viatu vya ngozi vinavyofunika visigino viwili)”.

Mwislamu hazuhusiwi kuigusa Quraani akiwa na hadathi kubwa au ndogo mpaka atakapoondosha hadathi hiyo, kwa kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Hakikahii bila ya shaka ni Quraani Tukufu, 77, Katika Kitabu kilicho hifadhiwa,78, Hapana akigusaye ila waliotakaswa,79, Ni uteremsho unao toka kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote,80.} [Al-Waaqiah: 77-80 ]. Aya hizi ni ishara ya wazi ya uharamu wa kuigusa Qura’n ila kwa anayejitakasa, basi kauli ya Mwenyezi Mungu: {Hapana akigusaye ila waliotakaswa} ni katazo linalomaanisha uharamu ingawa limekuja katika muktadha wa taarifa; kwa sababu taarifa ya Mwenyezi Mungu kwa waja wake haiendi kinyume na hali halisi, kama kusudio lingekuwa ni taarifa tu na wala si katazo, basi ingelikuwa ni kinyume cha hali halisi; kwani sisi tunawaona wale wanaoigusa Quraani bila ya kuwa na Twahara} [Al-Muntaka Sharhu Al-Muwatta 1/343, Dar Al-Kitabu Al-Islamiy]. Na Kuelezea katazo kwa taarifa ni sanifu zaidi kuliko agizo au katazo la wazi, kama wanavyosema wanavyuoni wa Elimu ya Fasihi; kwa sababu ili msemaji alisisitizie takwa lake ameliweka katika nafasi ya Hali halisi. [Sharhu Al-Kawkab Al-Muniir uk. 59, Al-Sunna Al-Muhamadiya] . Na kauli ya Mwenyezi Mungu: {Ni uteremsho} anakusudia Quraani, na wala si kitu kingine. Na hakiusiki kitu kingine chochote isipokuwa kwa kuwepo dalili ya wazi. Na mtu mwenye udhu huitwa kuwa ni msafi aliyejisafisha. [Al-Majmuu: 2/72, Dar Al-Fikr] na wala haisemwi kuwa kwamba kama aliekusudiwa ni binadamu basi aya ingekuja kuwa: (Hapana akigusaye ila waliojitakasa). Na kama tukisalimu amri kwamba kwamba kilichokusudiwa katika aya hizo ni; Qura’n Tukufu iliyoandikwa katika (Al-lauhul – Mahfudh) ambayo hapana akigusaye ila malaika tu waliotakaswa na mabaya, basi inafaa pia kuchukua aya hiyo kama dalili - kama anavyosema Imam Al-Tibiy - kwa sababu maana yake ni kwamba kitabu hiki kina heshima kwa Mwenyezi Mungu, na kutokana na heshima hiyo Mwenyezi Mungu Mtukufu amekiandika katika kitabu kilichohifadhiwa (Lauhun Mahfuudh) na amekipa heshimu kwa kukifanya kisiguswe ila na malaika walio karibu, na akakilinda na wale wasiokaribu, basi ni lazima hukumu ya Quraani iwe kwa watu kama ilivyokuwa kwa malaika, kwa sababu hukumu inayotokana na maelezo yafaayo huleta hisia za juu; kwa sababu muktadha wa maneno ni kwa ajili ya kuitukuza Quraani. [Al-Bahru Al-Raiq Sharhu Kanzu Al-Daqaiq 1/211, Dar Al-Kitabu Al-Islamiy].

Kwa mujibu wa kitabu cha Mtume S.A.W. kwa Amr Ibn Hazm: (haigusi Quraani ila na msafi). Imepokelewa na Malik, Ibn Hiban, Al-Hakim, Bayhaqiy na Al-Daramiy, na umaarufu wa kitabu hicho hautatufanya tuhitaji mapokezi yake. Imam Ahmad anasema: “Hakuna shaka kwamba Mtume S.A.W. alimwandikia (yaani kwa Amr Ibn Hazm)”. [Al-Fatawa Al-Kubra kwa Ibn Taymiyyah 1/280, Dar Al-Kutub Al-Elmiya]. Al-Haafidh Ibn Abd Al-Bar katika [Al-Tamhiid, 17/ 396 397, Wizara ya wqafu na masuala ya Kiislamu – Al-Maghrib.]: “Tulitaja kuwa kitabu cha Mtume S.A.W. kwa Amr Ibn Hazm kwa watu wa Yemen katika Sunan na fardhi na diya ni Kitabu kinachojulikana sana kwa wanavyuoni kwa hivyo, hawawezi kamwe kuacha kutumia mapokezi yake kutokana na umaarufu wake”. Kisha akasema: “Dalili ya usahihi wakitabu cha Amr Ibn Hazm ni kupokelewa na kukubaliwa na idadi kubwa ya wanvyuoni”.

Na imepokelewa kwa Abdullah Ibn Omar R.A. alisema: Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W. amesema: “haigusi Quraani ila msafi” imepokelewa kwa Al-Tabarani katika vitabu vyake viwili, kikubwa na kidogo, na Daaraqutni katika Sunan yake, Al-Hiythamiy alisema katika [Majma Al-Zawaid, 1/616 , Dar Al-Fikr]: “wanaume waaminifu” Al-Hafidh Ibn Hajar alisema katika [Al-Talkhis Al-Habir, 1/ 361, Dar Alkutub Al-Elmiya]: “Mapokezi yake si mabaya, Al-Athram ametaja kwamba Ahmed alichukua hadithi hiyo kama dalili”.

Kauli yake: "ila mwenye kujitakasa na mabaya" ina maana ya kuwa mtu hawezi kuigusu Quraani ila katika hali ya kuwa kwake msafi na siyo katika hali nyinginezoalizokutana nazo na ambazo zinauondosha usafi wake wa mwili.Na hii ni dalili ya kwamba Usafi hapa unamaanisha ni hali inayotofautiana na hali nyingine ambayo humtokea kila mtu nayo ni hali ya kuwa na Hadathi. Maana ya Hadathi hapa kamwe haiwezi kuwa inamaanisha Imani na kinyume chake Ukafiri; kwa sababu imani katika sheria si hali ya inayojitokeza na kukabiliana na hali nyingine iliyozoeleka katika maisha ya watu, bali imani ni hali imara kama mti mzuri ambao mizizi yake ni imara na matawi yake yamenyooka juu, na kufuru ni hali mbaya ya kipekee inayokwenda kinyume cha maumbile ambayo Mwenyezi Mungu alilowaumbia watu.

Na imepokelewa kutoka kwa Othman Ibn Abi Al-Aas amesema: tulikwenda kwa kwa Mtume S.A.W. akanikuta mimi ni mbora wao wa kuihifadhi Quraani, na nilikuwa mbora wao katika kuhifadhi suratu Al-Baqarah zaidi kuliko wao, Mtume S.A.W. akasema: "nimekuteua ili uwe kiongozi wamarafiki zako na wewe ni mdogo wao, kama ukiwasalisha watu wasalishe kwa kuwajali waliodhaifu miongoni mwao, kwani nyuma yako kuna wazee, watoto, madhaifu, na watu wenye nyudhuru, na kama ukikusanya Sadaka, basi usichukui (Al-Shafii au Al-Makhadh) ni ng’ombe au mbuzi ambaye mjamzito, wala (Al-Rabii) mbuzi anayechungwa kwa ajili ya maziwa, wala (Fahlu Al-Ghanam) beberu (mbuzi dume), mali bora ya mtu ni haki yake zaidi kuliko wewe, na usiigusa Quraani ila unapokuwa msafi". Imepokelewa na Al-Tabariy katika kitabu chake Alkabiir, na pia Ismail Bin Raafiu. Na Yahya Ibn Maain, na Al-Nasaaiy wamesema hadithi hiyo ni dhaifu, lakini Al-Bukhari anasema: “siyo dhaifu”. [Majma Al-Zawaid 1/277], Al-Haithamiy anasema: “kundi la Maimamu wamesema hadithi hiyo ni dhaifu, lakini Al- Bukhari amesema si dhaifu”. [Majma Al-Zawaid 3/74]. Na dalili katika hadithi ile ni kauli ya Mtume S.A.W. akimwambia mmoja wa masahaba wake: "usiigusa Quraani ila unapokuwa msafi". Inaonesha wazi kwamba sahaba yule ana hali mbili za kawaida, nazo nihali ya usafi na hali ya kutokuwa msafi. Mtume S.W.A amemkataza kugusa Quraani katika hali ya kutokuwa msafi, Hii inamaanisha kwamba hali ile ya kutojisafisha inakusudiwa hadathi na haikusudiwi ukafiri, kwa sababu mwenye kuambiwa katika hadithi hiyo ni mmoja wa masahaba waheshimiwa.Na kamasi hivyo basi Mtume S.A.W. angekuwa anamwambia mmoja wa masahaba kuwa: usiiguse Quraani ila unapokuwa na hali ya imani, na utakapokuwa na hali ya ukafiri basi usiigusa. Ni wazi kuwa maana hii ni mbovu na iko mbali na yaliyozoelewa katika Quraani ya Mwenyezi Mungu.

Hivyo hadithi iliyopokelewa kwa Amr Ibn Hazm pekee yake ni sahihi, na tukidhani kwamba hadithi hiyo ni dhaifu – dhana hiyo si kweli- basi udhaifu wake uanaweza kuimarika kupitia njia nyingine za mapokezi kwa mujibu wa elimu ya hadithi, na hadithi ina dalili ya wazi ya kukataza kugusa Quraani katika hali ya kutojisafisha, kama ilivyopokelewa kwa Imam Abdul Razzaq Al-Sanaaniy katika “tasnifu yake” [1/341 , Al-Maktab Al-Islamiy] imepokelewa kwa Muammar, Abdullah Ibn Abu Bakr, baba yake akasema: katika kitabu cha Mtume S.A.W. kwa Amr Ibn Hazm: "mtu yeyote haigusiQura’nila katika hali ya kuwa msafi". Haimaanishi kuwa najisi haimtokei mtu mwenye Imani, hapatwi nahadathi inayomlazimisha kujitaharisha upya. Kama ni hivyo basi kumkalifisha awe msafi kusingelikuwa na maana yoyote. Na jambo hili ni muhali. Na imezoelekka matika maandiko matakatifu ya Sheria ya Kiislamu kwamba kinachokusudiwa katika usafi ni kuondosha hadathi kama ilivyokuja katika tamko lake Mwenyezi Mungu alivyowaambia Waumini: {Na mkiwa na janaba basi ogeni} [ Al-Maida: 6], na kauli yake: {Wala msiwaingilie mpaka wat'ahirike. Wakisha t'ahirika basi waendeeni kwa namna alivyo kuamrisheni Mwenyezi Mungu} [Al -Baqarah: 222 ].

imepokelewa na idadi ya masahaba kauli yao kuhusu kuzuia mwenye hadathi kugusa Quraani, na hajawahi kujulikanwa mpinzani wao katika jambo hili, kwa hivyo kulikuwa na makubaliano, Al-Imam Al-Nawawiy anasema katika [Al-Majmu, 2 /82]: “marafiki zetu walichukua hadithi hiyo kama dalili na kwamba kauli ya Ali, Saad Ibn Abi Waqas, na IbnUmar R.A. kuwa hakujulikna mpinzani wowote kwao miongoni mwa masahaba”. Sheikh Ibn Taymiyyah Alijibu katika [Fatawa kuu, 1/280] aliyemwuliza: Je, ni halali kugusa Quraani bila kutia udhu au la? Akasema: “wanavyuoni wa madhehebu ya maimamu wanne, wanaona kuwa Quraani haiguswi ila na mwenye twahara ... Nayo pia ni kauli ya Salman Al-Farisiy, Abdullah Ibn Umar, na wengine, na hajulikani yeyote anayewapinga”.

Ni kawaida katika maandiko ya sheria kukiheshimu kitabu cha Mwenyezi Mungu na kuonesha ubora wake juu ya vitabu vingine vya Mwenyezi Mungu vilivyotangulia, kukielezea sifa ya utakaso na heshima, Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: {Hawakuwa walio kufuru miongoni mwa Watu wa Kitabu na washirikina waache walio nayo mpaka iwajie bayana, 1, Yaani Mtume aliye toka kwa Mwenyezi Mungu anaye wasomea kurasa zilizo takasika, 2, Ndani yake mna maandiko yaliyo nyooka.3} [Al-Bayyina: 1-3], na Mwenyezi Mungu alisema pia: {Na tumekupa Aya saba zinazo somwa mara kwa mara, na Quraani Tukufu.} [AL-HIJR: 87], na alisema pia: {Lau kuwa tumeiteremsha hii Quraani juu ya mlima, basi bila ya shaka ungeli uona ukinyenyekea, ukipasuka kwa khofu ya Mwenyezi Mungu.} [AL-HASHR : 21] na akasema: {Mwenyezi Mungu ameteremsha hadithi nzuri kabisa, Kitabu chenye kufanana na kukaririwa; husisimua kwacho ngozi za wenye kumuogopa Mola wao Mlezi. Kisha ngozi zao na nyoyo zao hulainika kwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu. Huo ndio uwongofu wa Mwenyezi Mungu, na kwa huo humwongoa amtakaye. Na ambaye ameachwa na Mwenyezi Mungu kupotea, basi hapana wa kumwongoa.} [ Al-ZUMAR: 23], na Mwenyezi Mungu alisema: {Na isomwapo Quraani isikilizeni na mnyamaze ili mpate kurehemewa.} [AL-AARAF: 204], {Hakika Sisi tumeifanya Quraani kuwa ya Kiarabu ili mfahamu, 3, Na hakika hiyo imo katika Asili ya Maandiko yaliyoko kwetu, ni tukufu na yenye hikima.4} [AL-ZUKHRUF: 3.4 ], na kuheshimu kilichoheshimiwa na Mwenyezi Mungu ni wajibu wa kweli, na heshima ya Quraani Tukufuina uzito zaidi mbele Mwenyezi Mungu kuliko kujengwa kwa misikiti.Na mwenye janaba na mwenye hedhi wanazuiliwa wawili hawa kuingia msikitini.Basi kuzuiliwa kwao kugusa Msahafu kunastahiki zaidi. Heshima na utukufu wa Quraani inapelekea pia kumzuia mwenye hadathi ndogo kugusa Quraani isipokuwa mpaka atakapoogana kuondosha hadathi yake kwa ajili ya kuyaheshimu maneno ya Mwenyezi Mungu na utukufu wa kitabu chake.

Wanavyuoni wingi wa umma wamekubaliana hivyo katika vipindi tofauti, Al-Hafidh Ibn Abd Al-Barr alisema katika [Al-Tamhid, 17/ 397]: “Wanavyuoni wa Fiqhi wa Madina, Iraq na Sham hawakupinga kwamba Quraani haiguswi ila na mwenye twahara na mwenye kutia udhu, nayo ni kauli ya Al-Imam Malik, Al-Shafiiy, Abu Hanifa, Al-Thawriy, Al-Awzaaiy, Ahmad Ibn Hanbal, Ishaq Ibn Raahawayh, Abi Thawr, Abi Obaida, na hawa ni Maimamu wa Fiqhi na Hadith katika zama zao, na imepokelwa kutoka kwa Saad Ibn Abi Waqas, Abdullah Ibn Omar, Tawoos, Al-Hassan, Al-Shabiy, Al-Qasim Ibn Muhammad na Ataa, Ishaq Raahawayh Ibn alisema: “hairuhusiwi kwa yeyote kusoma Quraani, ila anapokuwa na udhu”.

Ibn Taymiyyah katika [Al-Fatawa Al-Kubra] Anasema [1 /357]: “Kuhusu kugusa Qura’n mtazamo sahihi ni kwamba inalazimika kuwa na udhu, sawasawa kama walivyosema wanavyuoni wengi wa umma, na ndivyo inavyojulikana kutoka masahaba kama Saad, Salman, na Ibn Omar”.

Na haiwezikani tukasema kwamba kwa kuwa mtu ana nia ya kuhifadhi kitabu cha Mwenyezi Mungu, kujifunza, na kukifahamu mara kwa mara anaweza kudharau kuondosha hadathi ndogo kwa ajili ya kuwahamasisha wazembe ili wafanye hizo kazi nzuri, kwa sababu Mwenyezi Mungu ndiye ambaye aliahidi kukilinda kitabu chake na Quraani ni kitabu cha mwanga na uongozi, basi aliyetaka awe miongoni mwa watu wa Quraani ambao ni watu wa Mwenyezi Mungu na makhsusi Kwake, aache uvivu wake na afuate mfumo wa maswahaba waheshimiwa na Ahlul Bayt (Watu wa nyumba ya Mtume S.A.W. ambao ni safi nao walilelewa na Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W. juu ya upendo wa kitabu cha Mwenyezi Mungu, kukitakasa na kuzingatia maagizo yake na amri yake, hivyo, hivi sasa kuna zana nyingi za teknolojia ambazo inawezikana kuzitumika katika kuhifadhi Quraani, kuipitia, kuzikariri aya zake na kuifahamu maana yake katika nyakati na mazingira tofauti, iwapo mtumiaji atakuwa ameoga au la, basi hakuna haja ya ruhusa ya kugusa Quraani pasipo na twahara.

Aidha, kuzihifadhi sura za Quraani Tukufu si wajibu kwa kila Mwislamu, bali inapendeza, lakini kuihifadhi Sura ya Al-Fatiha ni wajibu kwa kila mwenye uwezo kwa sababu kuisoma ni nguzo ya swala kufuatana na wanavyuoni wengi wa Fiqhi [Al-Majmu, 3/ 361] na wanavyuoni wa madhehebu ya Hanafiy wanaona kwamba kiasi kinachotosha kwa kila Mwislamu kukihifadhi ni Sura ya Al-Fatiha na sura nyingine pamoja nayo; kwa sababu kuisoma hiyo ni miongoni mwa wajibu unaopaswa kutekelezwa katika swala [Al-Durr Al-Mukhtar katika Hashiat Ibn Abidin 1/538, Dar Al-Kutub Al-Elmiya.]

Ibn Hazm anasema katika kitabu cha [Maratibu Al-Ijmaa, 1/ 156, Dar Al-Kutub Al-Elmiya]: “Wanavyuoni Walikubaliana kwamba kuhifadhi kitu kutoka katika Quraani wajibu, na hawakukubaliana juu ya kitu hicho ni kitu gani, au kiasi gani, lakini walikubaliana kuwa mwenyekuihifadhi Sura ya Al-Fatiha na Sura nyingine, basi amefanya jambo la faradhi ya kuhifadhi na halazimishwi kuhifadhi zaidi ya hivyo. Walikubaliana pia juu ya kupendeza kuhifadhi sura zote za Quraani kwamba kuisoma vizuri pasipo na makosa ni wajibu wa kutoshelezeana kwa waislamu wote”. Ibn Mofleh Al-Hanbaliy katika [Al-Furuu, 1/ 525, Alam Al-Kutub] anasema: “sura miongoni mwa sura za Quraani inayolazimika kwa ajili ya kuifanya swala iwe sahihi ni Sura ya Al-Fatiha, kufuatana na madhehebu”.

Na Daudi na Ibn Hazm wa madhehebu ya Al-Dhahiriya kwawanasema kuwa inaruhusiwa kugusa Quraani kwa hali yoyote iwayo, kwa mwenye hadathi kubwa au ndogo [Rejea: Al-Mahaliy kwa Ibn Hazm 1/94 , Dar Al-Fikr], na imepokelewa kwa Al-Hakim na Hammad kusema kuwa inaruhusiwa kuigusa Quraani kwa ncha za vidole tu wala kwa kiganja, na walisema kwa sababu Mtume S.A.W. aliandika kitabu kwa Herekali na ndani yake Quraan na Herekali ni mwenye hadathi, na amekigusa na wenzake, na pia kwa sababu watoto wanabeba Allauhu (bao la Quraani) bila ya kukataa, kwa hivyo, kama hakuwa na kukataa kwa kuisoma, basi kuigusa inastahiki zaidi, na walipima kubeba kwake juu ya kubeba kwake katika mizigo.

walijibiwa kuhusu hadithi ya Herekali kwamba kitabu hiki kilikuwa na aya na wala hakikuitwa Msahafu, na inaruhusiwa kubeba ubao kwa watoto kwa ajili ya dharura, na inaruhusiwa kuisoma kwa ajili ya haja na ugumu wa kutia udhu wakati wote, na inaruhusiwa pia kuibeba katika mizigo; kwa sababu haikusudiwi kufanya hivyo [Al-Majmuu: 2/ 72], na tofauti kati ya ncha za vidole na kiganja cha mkono ni kwamba hakuna dalili juu yake, kila kitu kimeungana na kingine, kwa hivyo vimegusana [Al-Mughni 1/199, Dar Ihyaa Al-Turath Al-Arabiy], na kilicho sahihi zaidi katika suala hilo ni ule mtazamo wa wanavyuoni wengi wa Fiqhi kutokana nanguvu za dalili zao walizozitoa kinyume na msimamo wa wapinzani wao.

Kuhusu swali hilo na kufuatana na yaliyotangulia hapo juu: hairuhusiwi kwa Mwislimu kuigusa Quraani akiwa hana usafi kamili, kwa kutokwa na hadathi kubwa au ndogo, ingawa hali hiyo inaweza kumzuia kuisoma Quraani kwa wingi au kuihifadhi au kuirejearejea, kwa sababu ya kuwepo njia nyingi ambazo anaweza kunufaika nazo katika kuisikiliza kwa wingi na kuzikariri aya zake, kuzihifadhi na kuzirejea kwa kusikiliza bila ya kulazimika kuwa na twahara kamili.
Na Mwenyezi Mungu anajua zaidi ya wote.
 

Share this:

Related Fatwas