Hukumu ya Swala ya Jamaa

Egypt's Dar Al-Ifta

Hukumu ya Swala ya Jamaa

Question

Ni ipi Hukumu ya Swala ya jamaa? Na, Je ,Swala ya jamaa ni wajibu, na mtu yeyote anaeswali peke yake anakuwa ni mwenye makosa na swala yake inabatilika?

Answer

 

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:

            Asili ya neno la swala katika lugha ya kiarabu ni duaa (kuomba ) kwa kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu : {Na uwaombee dua }.[Al TAWBA:103 ]. Kwa maana omba, na baadaye matendo haya mashuhuri ya ibada yaitwa kwa jina hilo la swala,  kwani duaa inaambatana na matendo haya yote . [ Al-Mesbah Al-Kabeer kwa Al- Fayuomiy, mada, Sly, uk. 346, Ch. Al-Maktabah Al- Elmiyah – Bairut].

             Na makusudio ya Swala ya jamaa ni: Unganishaji wa Swala ya wanaoswali nyuma ya imamu, na Swala ya jamaa inakuwa sahihi kwa watu wawili au zaidi. [Hashuyat Al-Allamah Al-Bejory Ala Fateh Al-Qareeb 1/199, Ch. Al-Halabiy].

             Na Swala ya jamaa inaitwa kwa jina hilo kwa sababu ya kuukusanya watu wanaoswali katika sehemu moja na wakati mmoja, wakati wa Swala . [ Al-Fatawa Al-Kubra kwa Ibn Taimiyah, 2/325, Ch. Dar Al-Kutub Al-Elmiyah].

           Na fatwa tuliyoichagua ni kwamba Swala ya jamaa ni faridhi ya kutoshelezeana, na hii ni sahihi katika madhehebu ya Al Shafiy, ndiani ya kitabu cha [Al-Menhaaj kwa Al Nawawiy : "Kitabu cha Swala ya jamaa": Swala ya jamaa ni miongoni mwa faradhi isipokuwa swala ya ijumaa, kwani Swala ya ijumaa ni Sunna ya lazima. Na inasemekana kwamba ni faradhi ya kutoshelezeana kwa wanaume, kwa hivyo inakuwa ni lazima inapoonyesha alama ya kuwepo kwake kijijini, na lau wote wangeliakataa kwenda msikitini baasi ni lazima kuwaua. Ama kwa wanawake kwa kweli siyo lazima kama wanaume. Nimesema: Swala ya jamaa ni faradhi ya kutoshelezeana kama inavyokuja katika baadhi ya maandiko ya sharia, na inasemwa pia ni faradhi ya lazima, na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi zaidi “ .[Menhaaj Al-Ttalibeen kwa Al Nawawiy, uk.118, Ch. Dar Al- Menhaaj]. 

            Na hakuna upinzani baina ya kuwa Swala ya jamaa ni Sunna ya lazima ama ya kuwa ni faradhi ya kutoshelezeana, kwani Sunna yake inaelekea kwa mtu peke yake, na faradhi yake ya kutoshelezeana inaelekea kwa jamaa au watu wote kwa ujumla. Na faradhi ya kutoshelezeana kwa wafuasi wa Imam Al-Shafiy ni kwa sababu ya kudhihirisha alama ya swala hiyo na kulazimu kwa Swala ya jamaa –kama Al-Bejermiy anavyosema katika maelezo ya pembeni mwa [Aliqnaai  na katika maelezo ya Almanhaj]: “Na udhibiti wa kudhihiri alama ni Swala ya jamaa isiwe ngumu kwa aitakae, na wala asione haya mkubwa au mdogo kuingia mahala pake. Na iwapo itaswaliwa katika sehemu moja ndani ya mji mkubwa kwa namna ambayo inakuwa vigumu kwa aliye mbali kufika au ikiswaliwa katika nyumba za watu ambako mtu anaogopa kuingia kwa kuona haya basi hatakuwepo kujitokeza kwa alama ya kuswaliwa kwake na Faradhi itaendelea kuwa bado haijatekelezwa.[ Hashiyat Al-Bejermy juu ya Sharh Al-Menhaaj, 1/290, Ch. Al-Halabiy, na Hashiyatuh juu ya Al-Eqnaa, 2/123, Ch. Dar Al-Fikr].

            Na hii ni kauli ya kundi la baadhi ya wanachuoni wa kiislamu- kama Imam Al-Nawawiy anasema katika kitabu chake [Al-Majmou Sharh Al-Mohadhab kwa Al-Nawawiy, 4/189] bila ya kuwataja.

            Na Al-Ttahawiy na Al-Karkiy kutoka Al-Hanafiyah waliosema kwa kauli hii . [Hashiat Al-Ttahawiy juu ya Maraqiy Al-Falah, 1/286, Ch. Dar Al-Kutub Al- Elmiyah,Werd Al-Mohtaar ala Al-Durr Al- Mukhtaar, 1/552, Ch. Dar Al-Fikr] na Ibn Rushd na Ibn Basher kutoka Al-Malekiyah, [Hashiyat Al-Dusoqiy juu ya Sharh Al-Kabeer 1/319, Ch. Dar Al-Fikr, na Hashiyat Al-Ssawy juu ya Sharh Al-Ssagheer 1/425, Ch. Dar Al-Maarif ].

            Ibn Abdulbar katika kitabu ch [Al-Tamheed] anasema: “Nayo -yaani kauli hii- ni kauli nzuri na sahihi, kwa sababu wote wameafikiana juu ya kwamba haijuzu kukusanyika kwa ajili ya juu ya kusimamisha misikiti yote kusaliwa jamaa. Iwapo Jamaa itaswaliwa katika msikiti mmoja, basi Swala ya mtu peke yake nyumbani ni rinajuzu.” [Al-Tamheed 18/333, Ch. Wizarat Umum Al Awqaaf na Al-Shu'un Al-Islamiyah, Al-Mmaghreb].

            Na dalili ya kuwa Swala ya jamaa ni faradhi ya kutoshelezeana ni:

             Kwanza: Kuna maoni yasemayo kuwa Swala ya jamaa ni faradhi ya kutoshelezeana kutokana na yaliyosimuliwa na Ahmad na Abu-Dawud na Al-Nesaaiy na IBN Hayaan katika sahihi yake na Al-Baihaqiy katika sunan yake ( vitabu vyake ), na Al-Hakim katika Musadrakihi (Maelezo yake). Na amesahihisha marejeo yake (Isnadih), na ameafikiana na Al-Dhahabiy katika Al-Talkhees (ufupisho ) kutoka kwa Aby-Al-Dardaa alisema: Nilimsikia Mtume S.A.W. anasema "Kama watu watatu wapo kijijini au mahali jangwani na hawasimamishi Swala mahala hapo, basi shetani anawashikilia pande zote, kwa hivyo, lazima uswali Swala ya jamaa kwani mbwa mwitu humla kondoo yoyote aliye peke yake." Na hadithi hii ni dalili juu ya faridhi ya Swala ya jamaa, lakini kauli ya Mtume S.A.W. katika hadithi kwa lafudhi ya "haisimamishi miongoni mwao", na haisemi "hawasimsmishi" inafahamika kutoka kauli hii kwamba faradhi ni faradhi ya kutoshelezeana na siyo faradhi ya lazima, kwani kuna tofauti baina ya lafudhi mbili, ya kwanza ina maana ya jumla au majumlisho, na ya pili ina maana ya (watu ) wote.

            Pili: Dalili ya kwamba Swala ya jamaa siyo faridhi ya lazima inayosimuliwa na sahihi mbili kwa Al-Bukhariy kutoka kwa  Abdullahi Ibn Omar alisema kwamba: Mtume S.A.W. amesema: "Swala ya jamaa ni bora kuliko Swala ya pekee kwa daraja ishirini na saba" na mwelewekeano (mshabihiana) baina ya hayo katika maana ni kwamba upendeleo daima unakuwa baina vitu viwili vizuri na vinavyoruhusiwa.

           Na kutokana na dalili hizo zote ni kwamba: Swala ya jamaa siyo faradhi ya lazima lakini ni sunna juu ya mtu binafsi, na hadithi hii na hadithi nyinginezo zinasema kwamba Swala ya jamaa ni faradhi ya kutoshelezeana.

            Na kwa hivyo, hakika Swala ya jamaa ni faradhi ya kutoshelezeana na siyo ya lazima, na atayeswali swala ya faradhi peke yake basi swala yake haibatiliki kwa sababu tu ya kuiswali peke yake, na wala hana dhambi iwapo tu wengine wameswali jamaa ambayo inatosha kudhihirisha alama iliyotajwa.

            Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi ya wote.  

Share this:

Related Fatwas