Kuomba Msamaha kwa ajili ya Kafiri ambaye ni Hai
Question
Je, inaruhusiwa kumuombea msamaha kafiri ambaye bado yuhai?
Answer
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Kuomba msamaha: yaani kuomba maghfira, husemwa kuwa: amemuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu msamaha kwa ajili ya makosa yake au kutokana na makosa yake, amemsamehe dhambi zake, na asili ya kusamehe: ni kufunika na kusitiri. Mwenyezi Mungu Mtukufu amesamehe dhambi zake, yaani amezisitiri. [Lisan Al-Arab 2/25, Dar Sader, Mukhtar Al-Sahah uk. 228, Al-Maktaba Al-Asriya].
Mwenyezi Mungu Mtukufu amewakataza waja wake waumini kuwaombea msamaha wale waliomkufuru Mwenyezi Mungu Mtukufu, na ameonesha kwamba yule aliye kufuru imemwajibikia hukumu ya adhabu kwa kufa kwake akiwa katika ushirikina, au kuelezea kwa wahyi kwamba watu hawa ni wa Jahanamu kama vile Abu Lahab na mkewe; Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: {Haimpasii Nabii na wale walio amini kuwatakia msamaha washirikina, ijapo kuwa ni jamaa zao, baada ya kwishabainika kuwa hao ni watu wa Motoni} [AL-TAWBAH 113], Mwenyezi Mungu pengine anasamehe dhambi zote za mja ila ushirikina, hivyo, kuomba msamaha kwa aina ile ni kuanza kwa uadui katika dua; kwa sababu wakati huo itakuwa ombi ambalo sheria ilikataa uwezekano wa kutokea kwake, bali ni ombi la kutompendeza Mwenyezi Mungu wala hatakiwi mtu kufanya hivyo wakati wowote, kama alivyosema Mwenyezi katika kitabu chake kitakatifu; Mwenyezi Mungu anasema: {Hakika Mwenyezi Mungu hasamehe kushirikishwa, na husamehe yaliyo duni ya hilo kwa amtakaye.} [AN-NISAA: 48], (Imam Fakhr Al-Din Al-Raziy anasema katika tafsiri yake [16/158, Dar Ihyaa Al-Turath Al Arabiy) akisema: “Haimpasi Nabii na wale walio amini kuwatakia msamaha washirikina", inawezekana maana kuwa: hawapaswi kufanya hivyo, basi itakuwa kama wasifu, na kwamba maana yake: siyo kwao kufanya hivyo, kwa maana ya katazo. Kwanza hii ina maana kwamba unabii na imani inazuia kuowambea msamaha washirikina. Ya pili ina maana kwamba msiowaombee msamaha, na maagizo mawili yanafanana. Sababu katazo hilo: ni kwa mujibu wa alivyoyasema Mwenyezi Mungu Mtukufu katika kauli yake: {baada ya kwishabainika kuwa hao ni watu wa Motoni} na alisema pia {Hakika Mwenyezi Mungu hasamehe kushirikishwa, na husamehe mengine yasiyokuwa hilo kwa amtakaye.} Na maana ni: Mwenyezi Mungu anaposema kwamba wao wataingia motoni, basi kuwaombea msamaha ni kama ombi la kuvunja ahadi yake Mwenyezi Mungu na hiyo hairuhusiwi. Na pia wakati ambapo Mwenyezi Mungu ametangulia kuamuru jambo la kuwaadhibu, basi kama wangeliomba msamaha wake wasingelikubaliwa, na hali hiyo inalazimisha upungufu wa cheo cha Mtume S.A.W. na nafasi aliyonayo, na anasema pia: {Na Mola wenu Mlezi anasema: Niombeni nitakuitikieni.} Na amesema kuhusu wao: hao ni watu wa Motoni, na kuwaombea huko kunalazimisha ukinzani katika aya hizi mbili, hali ambayo haiwezekani”.
Ama mwenywe uhai miongoni mwa makafiri, basi hakuna kibaya kuomba msamaha kwake, kwa maana ya ombi la kuruzukiwa imani, ambayo ni sababu ya msamaha, na siyo kwa maana ya kughufuria kwa kufuru kwake akifa na hali hiyo.
Al-Imam Al-Tabariy katika tafsiri yake [14/515, Muasasatu Al-Risalah] anasema: “Watu wamefasiri kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Haimpasi Nabii na wale walio amini kuwatakia msamaha washirikina, ijapo kuwa ni jamaa zao} Kuwa katazo la Mwenyezi Mungu la kuwaombea msamaha washirikina ni baada ya kufa kwao, kwa ajili ya kauli yake: {Baada ya kwishabainika kuwa hao ni watu wa Motoni}. Na wakasema kuwa: hali hiyo haibainishwi na chochote ila kwa kufa kwake hali ya kuwa kafiri, ama katika hali ya uhai, basi haiwezekani hali hiyo, kwa hivyo, waumini wanaweza kuwaombea msamaha makafiri”.
Al-Imam Al-Qurtubiy katika tafsiri yake [8/274, Dar Al-Kutub Al-Misriyah] anasema: “wanavyuoni wengi walisema: hakuna kibaya kwa mtu kufanya dua na kuwaombea msamaha wazazi wake ambao ni makafiri iwapo bado wako hai. Ama kuhusu aliyekufa, basi haiwezekani kumfanyia dua. Ibn Abbas alisema: waumini walikuwa wakiomba msamaha kwa wafu wao, mpaka aya ile ikateremka, wakaacha kuowambea msamaha, na Mwenyezi Mungu hakuwakataza kuomba msamaha kwa wale ambao bado wako hai mpaka watakapokufa”.
Katika tafsiri ya Ibn Kathir [4/224, Dar Taiba]: “Ali Ibn Abi Talha Ibn Abbas anasema katika aya ile: waumini walikuwa wakiwaombea msamaha makafiri mpaka aya ile ikateremka, basi ilipoteremka wakaacha kuwaombea msamaha wafu wao makafiri, na Mwenyezi Mungu hakuwakataza kuwaombea msamaha wale ambao bado wako hai mpaka watakapokufa (wakiwa makafiri): {Lakini ilipombainikia kwamba yeye ni adui wa Mwenyezi Mungu, alijiepusha naye.} Ibn Abbas alisema: Ibrahim aliendelea kumuombea msamaha baba yake mpaka alipokufa (ndipo alipoacha kumuombea msamaha), Lakini ilipombainikia kwamba yeye ni adui wa Mwenyezi Mungu, alijiepusha naye. Katika hadithi nyingine: baba yake Ibrahim alipokufa Ibrahim alijua kuwa yeye ni adui wa Mwenyezi Mungu. Na hivyo ndivyo alivyosema Mujahid, Al-Dahhaak, Qatada, na wengine, Mwenyezi Mungu awarehemu”.
Imepokelewa na Ibn Abi Shaybah katika tasnifu yake [3/228 229, Dar Al-Fikr] kutoka kwa Saeed Ibn Jubair amesema: mkiristo mmoja alikufa na alikuwa na mwanawe mwislamu hakumfuata, Ibn Abbas akasema: anapaswa kumfuata, kumzika na kuomba msamaha kwa ajili yake katika maisha yake.
Na imepokelewa naye: Mkristo mmoja alikufa, basi mtoto wake akamwacha kwa watu wa dini yake, Ibn Abbas alipojua hivyo akasema: atakuwa na nini kama akitembea naye, akamzika na akaomba msamaha kwake iwapo yuko hai, kisha akasoma: {Wala haikuwa Ibrahim kumtakia msamaha baba yake…}
Maana hiyo imetajwa na wengi wa wanavyuoni; Al-Kadhi Al-Baydhawiy anasema katika tafsiri yake [Anwar Al-Tanzil, 3/99, Dar Ihyaa Al-Turath Al-Arabiy] anasema: “{baada ya kwishabainika kuwa hao ni watu wa Motoni}; ni mwamba wamekufa wakiwa makafiri, na kuna dalili ya kuruhusiwa kuwaombea msamaha watu wao ambao bado wako hai, nalo ni ombi la kutaka waruzukiwa imani”.
Mwanachuoni Al-Nasafiy anasema katika kitabu chake [Madarik Al-Tanzil, 1/713, Dar Al-Kalim Al-Tayib] anasema: “{baada ya kwishawabainikia kuwa wao ni watu wa Motoni} baada ya kugundua kwamba wao wamekufa hali ya kuwa katika ushirikina”.
Al-Khazen katika kitabu chake [Lubabu Al-Tawil fi maani Al-Tanzil, 2/412, Dar Al-Kutub Al-Elmiya] anasema: “maana ya aya hii: Mtume na wale ambao wanaamini hawapaswi kuwaombea msamaha washirikina, wala hawatakiwi kufanya hivyo; Kwa sababu Mwenyezi Mungu hawasamehe washirikina, na haijuzu kumuomba Mwenyezi Mungu jambo asilolifanya. Ndani yake kuna dalili ya katazo la kuwaombea msamaha washirikina, hata kama watakuwa ni jamaa zao; kwa sababu katazo hili la kuwaombea msamaha ni kwa washirikina wote kwa ujumla, kwa kulingana kati ya ndugu na wasio ndugu. Kisha akataja Mwenyezi Mungu sababu ya kuzuia; Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema: {baada ya kwisha wabainikia kuwa wao ni watu wa Motoni.}; maana ya kuonyeshwa kwamba wao walikufa hali ya kuwa ni washirikina, nao ni watu wa motoni, na pia, Mwenyezi Mungu akasema: {Hakika Mwenyezi Mungu hamsamehe menye kumshirikisha}, na Mwenyezi Mungu havunji ahadi yake”.
Mwanachuoni Ibn Attiya, katika tafsiri yake [3/90 Dar Al-Kutub Al-Elmiya] anasema: “Na inaruhusiwa kumuombea msamaha mshirikina aliye hai, iwapo anatarajiwa kuongoka na kuingia katika Uislamu, na katika hili ni kauli ya Abu Huraira R.A.: Mungu amrehemu mtu aliewaombea msamaha kwa Abu Huraira na mama yake, aliambiwa: na baba yake. Akasema: Hapana, baba yangu alikufa kafiri”.
Mwanachuoni Al-Alusi katika kitabu cha [Roho Al-Maanim 8/418, Al-Muniriyh] anasema: “Uchunguzi wa suala hili: kwamba kumuombea msamaha kafiri aliye hai asiejulikana mwisho wake, kwa maana ya kumtakia uongofu wa imani, ni miongoni mwa mambo yasiyozuiliwa kwa ushahidi wa kiakili na wa kunukulu, na kumuombe jambo hilo kafiri anaejulikana na ambaye ukafiri umetulizana katika moyo wake, na Mwenyezi Mungu mtukufu amekwishaelezea kuwa kuwa mtu huyo hataamini, na ikatambulika hivyo kuwa hakuna cha kukizungumzia kuhusu jambo lake kimsingi, basi ni kitu ambacho kinaeleweka kiakili na kwa kunukulu kuwa hakifai
Kwa maana hiyo inafahamika katika Hadithi iliyopokelewa na Al-Bukhari katika Sahihi yake kutoka kwa Abdullah bin Masud R.A. kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W. alisema: “Ee Mwenyezi Mungu, wasamehe watu wangu, kwa sababu wao hawajui”; Al-Imam Al-Aini katika kitabu chake [Umdatu Al-kariy, 23 / 19, Dar Ihyaa Al-Turath Al-Arabi] anasema: “Maana yake: waongoze katika Uislamu, ambayo inaswihi kuambatana na kuwaombea msamaha, kwa sababu dhambi ya kamwe ukafiri haisamehewi”.
Al-Malt Al-Hanafi anasema katika kitabu chake [Al-Mutasar min Al-Mukhtasar min Mushakal Al-Athar, 1/121, Alam Al-Kutub] anasema: “Dalili ya kuruhusiwa kumuombea msamaha mshirikina ambaye bado yuhai: ni kauli ya Mtume S.A.W. “Ewe Mwenyezi Mungu, uwasamehe watu wangu, kwa sababu hawajui”.
Kwa mujibu wa yaliyotangulia hapo juu: basi inaruhusiwa kumuombea msamaha kafiri anayetarajiwa kuongoka kiimani, kwa maana kwamba kuruzukiwa imani hiyo, si kwa maana ya kwamba Mwenyezi Mungu anamsamehe kwa ukafiri wake, na Mwenyezi Mungu Mtukufu anajua zaidi ya wote.