Hukumu ya Kudharau Taurati na Injil...

Egypt's Dar Al-Ifta

Hukumu ya Kudharau Taurati na Injili

Question

Nini hukumu ya kudharau Taurati na Injili?

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Kupuuza ni kudharau [Abi Hafs Al Nassafiy, Uk. 18, Uh. Al Matba’a Al Amira & Muhammad Al Qula’giy, Mu’gam Al Fuqaha’, Uk. 89, Ch. Dar Al Nafai’s].
Taurati: ni kitabu kilichoteremshwa kwa Mtume Mussa (amani ya Mwenyezi Mungu ni juu yake) inasemekana kuwa ni lafudhi inayotokana na kiebrania yenye maana ya “sheria” [Mu’gam Al Fuqaha’, Uk. 150], na inasemekana kuwa maana yake inachukuliwa kama ni nuru; kwani hiki ni kitabu cha Mwenyezi Mungu ambacho watu wanaongoka kwacho [Al Musbah Al Munir fi Gharib Al Sharh Al Kabir, Uk. 656, Al Maktaba Al Elmiya].
Injili: ni kitabu alichoteremshiwa Mtume Isa mwana wa Mariamu (amani ya Mwenyezi Mungu juu yake) Al Zamakh-shariy anasema: “Lafudhi hii haitokani na Kiarabu” [Al Faek fi Gharib Al Hadith, 2/262, Ch. Dar Al Fikr, Beirut].
Inasemekana kwamba neno “Injili” linatokana na neno “najaltuhu” ukilitohoa; kwani Injili inajumuisha ndani yake elimu na hekima [Al Musbah Al Munir, Uk. 594].
Ibn Qutaiba anasema: “Kama kwamba haki ilikuwa imefichika na vipande vyake vingi vilikuwa vimechunguzwa licha ya kuwa watu wa Kitabu walizidi kubadilisha maneno kuyatoa mahali pake na mambo mapya ambayo watu waliyazua yalifichika kwao na Mwenyezi Mungu Akadhihirisha hayo yote” [Ibn Qutaiba, Gharib Al Hadith, 1/246, Dar Al Kutoob Al Elmiya].
Taurati na Injili ni miongoni mwa Vitabu vya mbinguni ambavyo Sheria imetuamrisha tuviamini na kuvitukuza; kwani vinakusanya Wahyi uliyoteremshwa kwa Mitume wawili watukufu Musa na Isa (amani ya Mwenyeze Mungu juu yao wote wawili) nayo ni maneno ya Mwenyezi Mungu, na ikiwa Qurani Tukufu ilifuta baadhi ya hukumu za Taurati na Injili, lakini hiyo haiathiri kitu katika kuvitukuza na kuviheshimu Vitabu hivyo viwili; kwa kuwepo amri ya kuviamini, jambo ambalo linalazimisha kuvitukuza. Mwenyezi Mungu Mtukufu Ameamrisha kuviamini Vitabu vyote vya mbinguni ambapo Amesema: {Semeni nyinyi (Waislamu waambiwe Mayahudi na Manasara; waambieni): “Tumemwamini Mwenyezi Mungu na yale tuliyoteremshwa, na yale yaliyoteremshwa kwa Ibrahimu na Ismaili na Is-haqa na Yaaqubu na kizazi (chake Yaaqubu); na waliyopewa Musa na Isa na pia yale waliyopewa Manabii (wengine) kutoka kwa Mola wao; hatutafautisha baina ya yoyote katika hao. (Wote tunawaamini); na sisi tumenyenyekea kwake”} [AL BAQARAH 136].
Hukumu inayokuwa na habari ni hukumu ya kuwajulisha wale walioambiwa (waliopewa ile habari) -nayo hapa ni hukumu ya kuamini-, Ibn Abdeen alisema katika maelezo yake juu ya kitabu chake [Al Durr Al Mukh-tar]: “hukumu inayokuwa na habari inalazimisha kuwatanguliza waliosemwa” [Rad Al Muh-tar juu ya Al Durr Al Mukh-tar, 3/323, ch. Dar Al Kutoob Al Elmiya].
Kadhalika Mwenyezi Mungu ametoa habari ya kwamba kuviamini Vitabu vyake vilivyoteremshwa kumethibitika moyoni mwa Mtume wake Muhammad S.A.W. pamoja na wanaoamini ili kila Mwislamu amfuate Mtume S.A.W. katika kuviamini ili apate sifa ya kuwa Mumini. Mwenyezi Mungu Amesema: (Mtume ameamini yaliyoteremshwa kwake kutoka kwa Mola wake, na Waislamu, {(pia wameamini hayo): wote wamemwamini Mwenyezi Mungu, na Malaika wake, na Vitabu vyake, na Mitume yake}[AL BAQARAH 285].
Kadhalika imepokelewa katika maneno ya Mtume S.A.W. yale yanayoambatana na kuitukuza Taurati pamoja na ushahidi wake juu ya Taurati ambapo Mtume S.A.W. alisema: “Lilikuja kundi moja la Mayahudi, wakamwita Mtume S.A.W aje Quf “jina la bonde lililopo Madina, basi Mtume S.A.W akaenda akaonana nao katika nyumba ya shule, wakasema: Ewe baba wa Kasem! Yupo mmoja wetu alimwingilia mwanamke katika haramu, basi toa hukumu baina yao. Halafu wakaweka mto kwa Mtume S.A.W akae juu yake. Mtume S.A.W akasema: nileteeni Taurati. Wakamletea, naye Mtume S.A.W. akatoa mto na akawekea Taurati juu yake na akasema: nakuamini na namwamini Aliyekuteremshia” (imepokelewa na Ibn Umar).
Ilithibitika kwamba Maulamaa walimkufurisha kila anayekufuru Kitabu chochote kilichoteremshwa au anayekipuuza au kukitukana.
Sheikh Muhammad Al Khadmiy Al Hanbaliy anasema: “sehemu ya tatu katika sehemu tatu za ukafiri (ukafiri wa hukmu) ni ile inayokuwa ukafiri kwa kulingana na hukumu ya sheria, nayo ikiwa kwa maneno au vitendo vilivyoainishwa na Mtungaji wa sheria ya Kiislamu (Mwenyezi Mungu na Mtume wake S.A.W.) kuwa ni alama ya uongo hata zikipatikana alama za kuamini au kukiri; basi yeyote akifanya mambo ya kupuuza Qurani, kubadilisha baadhi ya maneno kuyatoa mahali pake, kutupa Msahafu katika palaha pa takataka, kukanusha herufi moja ya Quraani, kubadilisha herufi hata moja au kuzidisha herufi hata moja, kusoma Qurani kwa mzaha kama kuisoma kwa dufu, kusema nimetosheka na kusoma Qurani, kusema Qurani kulingana na baadhi ya vitendo k.v. kusema: (Na gilasi zilizojaa “vinywaji vizuri vizuri”) akijaza kikombe, na kusema: (Kinywaji safi kabisa) akimaliza kunywa, na kusema: (Lakini wanapowapimia kwa (kipimo cha) vibaba au mizani (au vinginevyo), wao hupunguza) wakati wa kupima, kadhalika kusema kwa kuumbwa kwa Quraani au kuitia aibu katika kitu chochote cha Quraani au kukanusha Taurati na Injili au kuvitukana Vitabu hivi viwili” [Barika Mahmudiya katika maelezo ya Tarika Muhammadiya, 2/60: 61, Ch. Ihiya’ Al Kutub Al Arabiya].
Mbali ya hayo, Al Safariny alitaja katika maelezo ya Mandhumat Al Adab kutoka kwa kadhi Ayadh jambo la makubaliano juu ya hayo akasema: “ujue kwamba yeyote atakaefanya mambo ya kupuuza Qurani au Msahafu au kitu cho chote kutoka katika Qurani, kukanusha herufi moja kutoka Qurani, kukadhibisha kitu kilichohusiana na amri au hukumu, kuthibitisha kitu kilichokanushwa na Qurani ilhali anafahamu anavyofanya au kuwa na wasi wasi nacho, basi yeye ni kafiri kwa makubaliano ya Waislamu. Halikadhalika ni kafiri kila anayekanusha Taurati au Injili au Vitabu vya Mwenyezi Mungu vilivyoteremshwa au anayevitukana au anayevipuuza” [Ghiza’ Al Albab katika maelezo ya Mandhumat Al Adab, 1/414, ch. Mua’sasat Qurtuba].
Naye Mwenyezi Mungu Ametubainishwa kwamba watu wa Kitabu walibadilisha maneno ya Taurati na Injili kwa kuyatoa mahala pake, na walibadilisha maneno ya Mwenyezi Mungu. Hivyo Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema: {Ambao hubadilisha maneno kuyatoa mahali pake} [AN NISAA, 46]. Na hiyo haimaanishi kwamba Vitabu hivyo vilibadilishwa kikamilifu, kwani baadhi ya haki bado imo ndani ya Vitabu vyao. Ibn Hajar Al Haytamiy alisema: “katika kuibadilisha -Taurati- kauli nyingi; ya kwanza: ilibadilishwa kikamilifu, ya pili: aghalabu yake na kauli hii ina dalili nyingi, ya tatu: uchache wake ulibadilishwa, na ya nne: maana yake ilibadilishwa lakini lafudhi zake zimebaki hivyo hivyo” [Ibn Hajar Al Haytamiy, Al Maliky, Al Fatawa Al Fiq-hiya Al Kubra, 1/49, Al Mak-taba Al Islamiya].
Ilitajwa katika maelezo ya [Al Sharwaniy juu ya Tuh-fat Al Muhtaj, 1/178, ch. Dar Ihiya’ Al Turath Al Arabiy] ya kwamba: “ni kweli vitabu hivyo -Taurati na Injili- vinakuwa na vitu ambavyo vinadhaniwa kuwa hakuvipata mabadiliko; kwani vitu hivyo vinalingana na tulivyojifunza na sheria yetu”.
Kwa hiyo, haifai kuvitukana kikamilifu, bali ni lazima kuviheshimu, na heshima yake inakuwa hasa kwa vitu ambavyo havikupata mabadiliko vikiwa vinajulikana, au kwa Vitabu kikamilifu vikiwa -vitu vilivyopata mabadiliko– havijulikani, licha ya kuheshimu Majina ya Mwenyezi Mungu na Sifa zake na majina ya Mitume na Malaika hata yakiwa miongoni mwa vitu ambavyo vilipata mabadiliko; kwani kuyaheshimu maneno ya Mwenyezi Mungu -ambayo bado Vitabu vyao vinakuwa na baadhi yao- ni wajibu kisheria, hali kadhalika kuyaheshimu Majina yake Mwenyezi Mungu na Sifa zake na majina ya Manabii ambayo Vitabu hivi havina budi kuwa nayo. Mafuqahaa walitaja maana hiyo ya kuwepo baadhi ya yaliyo kweli katika Vitabu vyao ambapo ilitajwa katika maelezo ya [Al A’dawiy juu ya Kifayat Al Taleb Al Rabaniy] ambapo alisema: “Al Qushairiy alisema: Mwenyezi Mungu Ana majina elfu moja; majina mia tatu yamo katika Taurati, mia tatu yamo katika Zaburi, mia tatu yamo katika Injili, majina tisini na tisa yamo katika Quraani na jina moja limo katika kurasa za Ibrahimu” [2/483, Ch. Dar Al Fikr].
Al Kharshiy anasema: “vitabu hivyo -Taurati na Injili- ni kama Msahafu -katika heshima-, Majina ya Mwenyezi Mungu na majina ya Manabii kwa utukufu wake” [Maelezo juu ya Mukhatsar Khalili, 8/63, Ch. Dar Al Fikr].
Sheikh Al Hatab Al Malikiy anasema: “maneno ya Vitabu hivyo -Taurati na Injili- yaliyoandikwa haifai kuyatumia kuwasha moto. Pia alizidi kueleza: hivyo kwa utakatifu wa herufi zake unaotofautiana kulingana na yaliyoandikwa yenyewe licha ya kuwa haifai kuyawasha moto maneno yoyote yakiwa yameandikwa hata yakiwa maneno ya batili kama uchawi; kwani utakatifu wake umo katika herufi. Al Damaminiy alisema katika maelezo yake juu ya Al Bukhariy katika kitabu cha Al Haji katika Hadithi ya Al Sahifa: Ibn Munir alisema: na hiyo ndiyo dalili juu ya kuwajibika kuyaheshimu Majina ya Mwenyezi Mungu hata yakiwa katika Vitabu vya Taurati na Injili vivyobadilishwa, basi inafaa kuyawasha na kuyaangamiza lakini haifai kwa hali yo yote kuyatukana kwa nafasi ya majina hayo, na kauli hiyo ni inahitalifiana na kauli ya waliosema kwa kufaa kuyatumia kustanji; kwani ni batili kwa yaliyokuwa nayo na mabadiliko, lakini utukufu wa Majina ya Mwenyezi Mungu haubadiliki … ” [Mawahib Al Jalili, 1/287, Ch. Dar Al Fikr].
Sheikh Muhammad Al Khadimiy Al Hanafiy alisema: “Inawajibika kuheshimu Taurati na hali ya tashwishi inayoambatana na Taurati haiathiri kitu katika kuiheshimu; kwani uchache wake ndio uliobadilishwa na hukumu haitolewi kwa uchache na pengine kwa hiyo inachukiza kusoma Taurati kwa mwenye janaba na hiyo haitakuwa kwa kitu zaidi ya kuiheshimu. Inasemekana na baadhi ya watu ya kwamba mtu mmoja aliingia kanisani akaifanyia mzaha Taurati mpaka aliipuulizia. Basi alipoteza hali ya dini na maisha yake mpaka alikufa kifo kilicho kibaya zaidi ambapo alijiua mwenyewe. Kwa jumla haifai kutukana Vitabu vya kiungu vilivyofutwa” [Barika Mahmudiya katika maelezo ya Tarika Muhammadiya, 1/81].
Baadhi ya Mafakihi wa madhehebu yanayofuatwa walibainisha hukumu ya kuharamisha jambo la kupuuza Taurati na Injili kwa njia tofauti; miongoni mwa njia hizo ni:
- Baadhi ya Mafakihi walisema kwamba inachukiza kwa mwenye hadathi kubwa kugusa Vitabu hivyo; kwani vinakuwa na maneno ya Mwenyezi Mungu. Ilitajwa katika kitabu cha [Mughniy Al Muh-taj, 1/149, Dar Al Kutoob Al Elmiya]: “Al Mut-waliy alisema: ikidhaniwa kuwa Taurati au Vitabu vingine vya Mwenyezi Mungu hakuvipata kuwa na mabadiliko, basi inachukiza kuvigusa …”
- Pia baadhi ya Mafakihi walisisitiza hukumu ya kuchukiza kwa mwenye hadathi kubwa kusoma Vitabu hivyo kwa heshima za maneno ya Mwenyezi Mungu yaliyomo ndani yake. Hivyo kama ilivyotajwa katika kitabu cha [Tanwir Al Absar na maelezo yake]: “Inachukiza kwa mwenye hadathi kubwa kusoma Taurati, Injili au Zaburi; kwani zote ni maneno ya Mwenyezi Mungu, na yaliyopata kubadilishwa hayajulikani kwa yakini. Naye Al A’yniy alisisitiza katika maelezo yake juu ya Al Majma’ kuharamisha na akayapa sifa ya mto ambayo haibadiliki”.
Ibn A’bedin alisema katika maelezo yake: “hiyo -hukumu- inakuwa bora kwao; mwenye janaba, mwenye hedhi na mwenye nifasi. Ingawa mwishoni mwa maelezo yake katika muhtasari alirudi kusema kwamba inakuwa haina machukizo kwao. Aidha alisema katika Sharh Al Maniya: lakini iliyo sahihi ni machukizo; kwani yaliyobadilishwa -kutoka Taurati na Injili- ni uchache wake na aghlabu yake haikupata kubadilishwa, kwa hiyo inawajibika kuiheshimu na kuihefadhi. Na ikikutana iliyoharamishwa na iliyoruhusika -katika hukumu moja-, basi iliyoharamishwa inakuwa na kushinda. Mtume S.A.W. alisema: “Acha linalokutatiza na shika lisilokutatiza”, na kwa maneno ya Mtume S.A.W. inadhihirika wazi ufisadi wa kauli ya wafuasi wa madhehebu ya Ash-Shaafi’iy wasemao kwamba inafaa kustanji kwa yaliyokuwa mikononi mwao (Taurati na Injili); kwani jambo hilo lina hatari yake kubwa kwa sababu Mwenyezi Mungu hajatuambia kwamba waliyabadilisha kikamilifu, hata zikiwa -Taurati na Injili- zilifutwa, basi hazitoki kuwa ni miongoni mwa maneno ya Mwenyezi Mungu kama zile Aya za Qurani Tukufu zilizofutwa” [Ibn A’bedin, Rad Al Muh-tar juu ya Al Durr Al Mukh-tar, 1/175].
Bali inasemekana kutoka kwa baadhi ya Maulamaa kwamba walisema ni haramu tena haifai kama iliyotajwa katika kitabu cha Tanwir Al Absar na maelezo yake: “inachukizwa kwa mwenye janaba kusoma Taurati, Injili na Zaburi; kwani zote ni maneno ya Mwenyezi Mungu, na yaliyopata kubadilishwa kutoka hizo hayajulikana kwa yakini. Naye Al A’yniy alisisitiza katika maelezo yake juu ya Al Majma’ kuharamisha na akayapa sifa ya mto ambayo haibadiliki” [Durr Al Mukh-tar pamoja na maelezo ya Ibn Abdeen, 1/175].
Pia alisema Ibn Abdeen katika maelezo yake juu ya [Al Bahr Al Rai’q, 1/210, Ch. Dar Al Kitab Al Islamiy]: “kadhalika alisema katika Al Seraj Al Wahaj: haifai kwao -mwenye janaba ya hedhi na nifasi -kusoma Taurati, Injili na Zaburi; kwani zote ni maneno ya Mwenyezi Mungu”.
- Baadhi ya Mafakihi walisema kwamba haifai kuingia chooni pamoja na Vitabu hivyo, na miongoni mwa waliyoyasema, ni yale yaliyotajwa katika kitabu cha [Nihayat Al Muhtaj katika Sharh Al Menhaj, 1/132, Ch. Dar Al Fikr]: “wala hairuhusiwi kuwa na kitu kinachokuwa na maneno ya Mwenyezi Mungu; kitu kinachokuwa na maandishi ya Quraani au Vitabu vingine na hukumu hii inajumulisha Majina ya Mwenyezi Mungu na majina ya Manabii (hata wakiwa wasio Mitume) na Malaika (wakiwa ni miongoni mwa waliojulikana kwa kazi zao maalumu au kutaja jina lao kwa jumla), pia inajumulisha kila jina kuu linalokusudiwa nalo ukuu na ukubwa linalomhusu mtu binafsi au kundi la watu au jina linalokuwa na hoja iliyo wazi ya kuwa na uhusiano na yaliyotajwa”.
Al Shubramalsiy alisema katika maelezo yake juu ya [Nihayat Al Muhtaj katika Sharh Al Menhaj]: “ni lazima hukumu hiyo ijumulishe kila sehemu isiyo nadhifu, na ikiwa ilitosheka na choo (katika maelezo yao), basi itakuwa kwa sababu walikuwa wanaongea juu yake tu”.
Aidha alisema katika maelezo: “(maneno yake: aghlabu) aliyasema katika [Sharh Al Irshad] bila ya kutaja Taurati na Injili, ila hukumu iliyopita -hapo huu- inajumulisha baadhi tu ya vitu (ilivyomo ndani ya Vitabu hivyo) ambavyo vinajulikana au vinadhaniwa kuwa hakuvibapata mabadiliko; kwani ni maneno ya Mwenyezi Mungu, hata yakiwa yalifutwa”.
Ibn Qassem Al A’bidiy katika maelezo yake juu ya [Tuhaft Al Muhtaj, 1/160] alisisitiza juu ya utukufu wa Vitabu hivyo ingawa vinadhaniwa kuvipata mabadiliko, ambapo alisema: “haichukizwi kubeba vile Vitabu; Taurati na Injili wakati wa kuingia chooni ila ikijulikani kwamba vina vitu ambavyo hakuvipata mabadiliko ingawa vitu vilivyodhaniwa kuwa hakuvipata mabadiliko vinaelekewa kutoingia katika hukumu hii; kwa kuthibitika utukufu wake licha ya kuwa na shaka, na dalili ya kauli hii ni kutoruhusika kuvitumia kustanji”.
- Mafuqahaa waliharamisha kustanji kwa Taurati na Injili - kama ilivyobainika na baadhi ya kauli zilizopita - ikiwa inajulikana kutobadilishwa au ikiwa kuna shaka. Al Khabeeb Al Sherbiniy alisema: “inafaa kustanji kwa vitu visivyokuwa na heshima naye Al Kadhi aliruhusisha hiyo; kustanji kwa karatasi za Taurati na Injili; ingawa kauli hii inahusu vitu vilivyopata mabadiliko kwa yakini sharti kutokuwa na Jina la Mwenyezi Mungu” [Mughniy Al Muh-taj, 1/162, 163].
Na tukisema kwamba Vitabu hivyo vyote vilipata mabadiliko, na havina kitu cho chote ambacho Sheria inakitukuza -na hiyo si kweli-; kwa yote yaliyopita, basi haifai kuvitukana; kwani Mwenyezi Mungu Mtukufa Amesema: {Wala msiwatukane wale ambao wanawaabudu kinyume cha Mwenyezi Mungu, wasije wakamtukana Mwenyezi Mungu kwa jeuri zao bila kujua}{[AL AN-AM, 108]; maana Mwenyezi Mungu Ametuharamisha kutotukana vilivyotukuzwa na wasio Waislamu hata vikiwa batili au vinatofautiana na Sheria yetu wasije kufanya hiyo na haki ambayo tunaiamini na tunaitukuza.
Kutokana na yaliyopita; haifai kudharau Taurati na Injili au Vitabu vingine vyo vyote vilivyoteremshwa hata vikiwa vilibadilishwa; kwani vinakuwa na sehemu ya maneno ya Mwenyezi Mungu na Majina yake, sifa zake, majina ya Manabii na Malaika na hayo ni miongoni mwa vitu vilivyoadhimishwa na sheria. Naye Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi ya wote.
 

Share this:

Related Fatwas