Kuhudhuria kwa Asiye kuwa Mwislamu ...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kuhudhuria kwa Asiye kuwa Mwislamu katika mazishi ya Mwislamu.

Question

Je, inaruhusiwa kwa asiye Mwislamu kushiriki katika mazishi ya Mwislamu?

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:

Baadhi ya watu wasio Waislamu huwa wanashiriki kwenye mazishi ya Mwislamu, na huwa wanasimama na watu wengine kwenye kaburi la mwislamu huyo marehemu mpaka watapomaliza kumzika na kuondoka kwa pamoja. Na jambo hili limeruhusiwa na wala hakuna uharamu ndani yake; na ushahidi wa jambo hili ni: kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Mwenyezi Mungu hakukatazeni kuwafanyia wema na uadilifu wale ambao hawakukupigeni vita, wala hawakukutoeni makwenu. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wafanyao uadilifu.} [AL-MUMTAHINA: 8], na si uadilifu au wema kumkataza mtu yeyote asiye Mwislamu kushiriki kwenye mazishi ya Mwislamu ambaye ni miongoni mwa jamaa zake au rafiki yake, na pia hakuna maelezo yoyote yaliyopokelewa na ambayo yanahusisha uadilifu huu uliotolewa wito na katika aya hiyo.

Al-Qasimiy amesema katika tafsiri yake [Mahasin Al-Tawil: 9/207, Dar Al-Kutub Al-Elmiya], alipoizungumzia aya hiyo: “Mwenyezi Mungu hakukatazeni kuwafanyia wema na uadilifu wale ambao hawakukupigeni vita wala hawakukutoeni makwenu miongoni mwa watu wa Makkah, kiwango hiki cha ufuasi hakikatazwi, bali kimekokotezewa katika haki yao. Na mwelekeo wa Aya hii hata kama wanaoambiwa ni makafiri wa Makka, lakini kinachozingatiwa zaidi hapa ni Aya kuwajumuisha wote, baadhi ya wanachuoni wa Tafsiri ya Quraani wamejaribu kuliweka wazi jambo hili, lakini Imamu Ibn Jarir alikataa hivyo na akasema: Na iliyo sahihi ni kauli ya aliyesema: maana ya kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu {Mwenyezi Mungu hakukatazeni wale ambao hawakukupigeni vita} miongoni mwa aina zote za dini {kuwafanyia wema na uadilifu}; Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: {ambao hawakukupigeni vita, wala hawakukutoeni makwenu} ina maana watu wote wenye sifa hiyo. Mwenyezi Mungu hakuweka wazi kuwa ni watu fulani. Hakuna maana yoyote kwa yule asemaye kuwa: hayo yamefutwa; kwa sababu wema wa mwislamu kwa wasio waislamu ambao kati yake na wao kuna ukaribu wa udugu, au ambao si karibu naye kiundugu na yeye si au hata nasaba ya kiukoo, si haramu na wala haikukatazwa, ikiwa Mwislamu hakuwaonesha watu hawa aibu ya Waislamu, au hakuwasaidia kwa nguvu.

Pia inawezekana kusindikiza jeneza kutokana na sifa na tabia nzuri za marehemu, ambazo zinamfanya asiye Mwislamu ahuzunike kwa hasara ya kupotelewa na mtu huyo mwema, ambaye baraka zake zinatarajiwa, na jambo hilo limetokea katika historia ya Waislamu, na wala halikukanwa; ilikuja katika [Tarikhu Al-Islam kwa Al-Hafedh Al-Dhahabi: 8/545, Dar Al-Kitabu Al-Arabiy] kwamba Abad Ibn Al-Awam alihudhuria mazishi ya Mansour Ibn Zadhan akasema: nimeona Wakristo peke yao na Mayahudi peke yao, kwa hivyo basi mjomba wangu aliushikilia mkono wangu kutokana na misongamano ya watu. Yazid ibn Harun alisema: Mansour Ibn Zadhan alikufa mwaka wa thelathini na moja na mia moja.

Kwa mujibu wa kitabu cha [Tarikh Dimishq kwa Al-Hafedh Ibn Asakir: 20/81, Dar Al-Fikr LelTibaa wa Al-Nashr wa Al-Tawzii]: “Salem Bin Mundhir amesema: "tulikwenda kwenye mazishi ya Al-Awzaai na tukiwa Makundi manne; Mayahudi, Wakristo na Wakristo wa madhehebu ya Othodox ya Misri, na wote hawa walikuwa katika upande mmoja (walijitenga na waislamu)".

Na pia [35/103]: “Abdul Al-Aziz Al-Kitani alisema: alikufa sheikh wetu Abu Muhammad Abdul Rahman Ibn Othman Ibn Al-Qasim Ibn Maaruf Ibn Abi Nasr Mwenyezi Mungu amrehemu katika Jumatano siku ya pili ya mwezi wa Jamada Al-Akher baada ya adhuhuri ya mwaka wa ishirini na mia nne na alizikwa siku ya Alhamisi mchana na sikuona mazishi makubwa zaidi ya mazishi yake, walikuwa pamoja naye kundi la watu wa hadithi wanasema “Mwenyezi Mungu ni Mkubwa” na wanaonesha Sunna ya Mtume S.A.W, na watu wote wa nchi walihudhuria mazishi yake na hata Mayahudi na Wakristo. Sikumwona mzee anaefanana naye kwa kujiepusha na anasa, anayesifika kwa uchamungu, ibada na uongozi, na alikuwa mwaminifu, mwadilifu, na jina lake la utani ni Abu Muhammad ibn Abi Nasr Al-Afif”.

Pia katika kuthibitisha hali hiyo ni kwamba wanavyuoni mbalimbali wanaruhusu kwa asiye Mwislamu kumwosha Mwislamu marehemu ikiwa hakuna mtu mwengine, na kama ikiruhusiwa kumwosha Mwislamu, ambako asili yake ni ibada, na sala haisimamishwi ila baada yake, basi kushiriki kwa asiye Mwislamu kwenye mazishi ya Mwislamu ni kitu kidogo kuliko kumwosha mwislamu aliye marehemu.
Makhoul alisema kuhusu mwanamke ambaye amekufa katika safari, akiwa pamoja na ndugu yake wa kiume asiyeruhusiwa kumwoa pamoja na wanawake Wakristo: wanawake hao wanaweza kumwosha. Sufiyan alisema kuhusu mtu aliyekufa pamoja na wanawake na hakuna mtu yeyote pamoja nae, alisema kuwa hakuna kosa kama wakimpata Mkristo au Majusi ili amwoshe Mwislamu baada ya kutia udhu, na wanawake wanaweza kumsalia. Mke wa Alqamah alimwosha mwanamke Mkristo. [Al-Mughni: 2/203, Dar Ihyaa Al-Turath Al-Arabi.

Al-Sarkhasi katika kitabu cha [Mabsoot, 10/161 Dar Al-Maarifa] anasema: “Mwanamume akifa pamoja na wanawake, na hayupo mke wake basi mwanamke yeyote anaruhusiwa kumfanyia tayamum kama tulivyoeleza, hata hivyo, kama akiwa mwanamke atakayemfanyia tayamum ni mwanamke muungwana, basi amfanyie tayamum kwa kitambaa juu ya mkono wake ... kama akiwa pamoja na mtu kafiri, basi wamjulishe namna ya kuosha, na kama vile akiwa mwanamke mtumwa kafiri pamoja na wanaume, basi wamjulishe namna gani kumwosha mwanamke Mwislamu marehemu; kwa sababu kuona wanaume kwa wanaume au wanawake kwa wanawake hakutofautiani kwa mujibu wa dini kuhusu kukubali au kupinga, lakini kafiri hajui Sunna ya Mtume S.A.W. katika kuosha maiti, basi ajulishwe”.

Imamu Nawawi amesema katika kitabu cha [Al-Majmuu: 5/120, Al-Muniriyah]: “Kama mwanamke aliye katika Dhima akifa, basi inajuzu mume wake Mwislamu kumwosha, na pia inajuzu kwa bwana wake ikiwa mwanamke huyo hajaolewa wala hana eda, wala hajawa msafi, na mumewe Mwislamu akifa, mke wake huyo akamwosha, basi inachukiza kwa mujibu wa Imamu Shafiy.”.
Na kwa mujibu wa tuliyoyasema, wanavyuoni wengi pia wamesema hivyo hivyo:

Imepokelewa na Saeed Ibn Jubair, alisema: Nilimwuliza Ibn Abbas, R.A kuhusu mtu ambaye baba yake amekufa akiwa Mkristo, akasema: anaruhusiwa kuhudhuria mazishi yake na kumzika. Al-Khallaal alisema: Abu Abdullah anakusudia Imamu Ahmad, hakupendelea hivyo, kisha akapokea kutoka kwa watu hawa kuwa si vibaya kuhusu jambo hilo, na amethibitisha hivyo kwa hadithi, kwa maana kuwa alirejea katika kauli hii. Na Mwenyezi Mungu ni mjuzi zaidi. [Rejea: Ahkam Ahlu Al-Dhimma Li Ibn Al-Qayim: 1/437, Rumady Lel-Nashr – Al-Damma].

Ibn Al-Qasim na Ash-hab wanasema: kama mtoto wa Kiislamu akifa, basi hairuhusiwi kuoshwa na babake kafiri. Ama kuhusu kutembea naye na kumuombea dua haikatazwi. [Al-Taju wa Al-Iklil kwa Al-Mowaq: 3/78, Dar Al-Kutub Al-Elmiya].

Kutokana na yaliyotangulia na yaliyothibitishwa, inaruhusiwa kwa Waislamu kumwacha asiye Mwislamu ashiriki katika mazishi ya Mwislamu bila ya tatizo lolote katika jambo hilo.
Na Mwenyezi Mungu anajua zaidi.
 

Share this:

Related Fatwas