Jamii Yenye Maadili ya Hali ya Juu ...

Egypt's Dar Al-Ifta

Jamii Yenye Maadili ya Hali ya Juu ya Kuigwa

Question

Je, kuna kitu tunachoweza kukiita jamii yenye maadili ya hali ya juu ya kuigwa, na nini misingi yake katika Uislamu?

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:

Katika karne ishirini na tano zilizopita, tunaona shani ya kifalsafa ambayo inakuwa ni asili ya fikra za kifalsafa itoayo matokeo kamili kwa mfumo wa fikra kwa mwanafalsafa yoyote, shani hiyo ni suala la jamii yenye maadili ya hali ya juu ya kuigwa kama sura ya kifalsafa wanayoielewa wanafalsafa waliojaribu kuweka utaratibu wa miji bora na mfumo bora wa kuigwa wa jamii madhubuti.

Jamii kigezo yenye maadili ya juu katika fikra za kibinadamu inamaanisha mifumo mingi na mielekeo kadha ya kisiasa, kijamii na kiuchumi. Hali kadhalika uchunguzi wa kiuhakiki wa Kiislamu kwa falsafa kiujumla na mielekeo ya kijamii hasa unaweza kutoa uongofu wa kidini na uongozi wa kiroho kwa vijana wasiotulia.

Ulimwengu wote unaelekea kwa Mwenyezi Mungu kwa utiifu na unyenyekevu, ulimwengu ukikubali hivyo wote au baadhi yake au ukikataa. Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: {Na humsujudia Mwenyezi Mungu waliomo mbinguni na ardhini kwa khiari au kwa nguvu. Na (pia) vivuli vyao (vinamsujudia) asubuhi na jioni} [Al RAAD 15].

Maisha yanakuwa chini ya matakwa ya kimungu, naye binadamu ni mja pekee miongoni mwa viumbe vya Mwenyezi Mungu aliyekubali kubeba amana (jukumu) ya kuendesha mambo ya maisha chini ya utaratibu sahihi wa Mwenyezi Mungu, kwa hiyo mfumo wa kisiasa na kijamii unakuwa ni sehemu mojawapo ya mfumo huo wa kimungu. Aidha unakuwa na uhusiano wa karibu na sehemu za imani na itikadi zake.

Matokeo ya utafiti wa kiuhakiki wa jamii yenye maadili ya hali ya juu katika fikra za kifalsafa katika enzi tofauti za kifalsafa kuanzia Aflatun katika jamhuri yake ambapo alitoa uchambuzi wa kina akiweka nadharia kamili kuhusu jamii yenye maadili ya hali ya juu, hadi Alfarabiy katika mji bora ambao unakuwa na sehemu mbili; itikadi na kiongozi, ingawa hajatoa mfumo wa maisha wala katiba kwa kuendesha mambo ya maisha labda hajajaribu kutoa mfumo huo kwani Sheria ya Kiislamu ilitoa mfumo huo kwa watu. Aidha miongoni mwa wanafalsafa wa enzi za maendeleo ambao waliathirika na ustaarabu wa Kiislamu uliokuwa katika Andalus na miji mengine iliyokuwa ni bendera za elimu za Kiislamu ni Jan Jack Russu mwenye nadharia ya mkataba wa kijamii ambaye alikuwa na makosa yanayohusiana na dini ya kimaumbile na wito wake wa umoja wa kidini na msimamo wake dhidi ya Manabii, Mitume na mwanamke, hadi Marks na falsafa ya kimaada inayopinga dini mpaka Pintisha na katiba yake ya maisha ya kijamii inayopinga kanuni za maisha hali ambayo falsafa zake ingalitekelezwa angalikuwa yeye mhanga wa kwanza wa fikra zake.

Makusudio ya jamii kigezo yenye maadili ya hali ya juu ni: jamii yenye lengo linalotakikana kufanikishwa ili kusahihisha mwenendo wa kijamii, kisiasa na kiuchumi. Na maadili ya hali ya juu yanamaanisha: mambo yanayotakiwa kupatikana.

Kutokana na utafiti huo inadhihirika kuwa:
• Uislamu ni dini pekee ambayo imezindua ubinadamu na sifa zake katika binadamu, ukamtukuza binadamu, ukamjaalia ni muhimili na bwana wa dunia, na kiongozi wa duniani kwa amri ya Allah S.W .
• Msingi wa ustaarabu unategemea haki, kheri na uzuri, nayo ni maadili ambayo Uislamu unaweza kuyafanikisha kutokana na itikadi zake na sheria zake pamoja na kutimiza matakwa ya binadamu ya hali ya juu.
• Naye Aflatun alitoa wito wa kuwekwa kila mwanadamu katika pahala pake pa kielimu na kijamii anapostahiki kwa mujibu wa nguvu na sifa zake anazokuwa nazo, jambo ambalo halipingani na fikra za Kiislamu, maana misingi ya Kiislamu inaafikiana na rai hiyo, lakini lililo baya zaidi katika maoni ya Aflatun ni rai yake kuhusu Ukomunisti ambapo alikuwa anataka wanawake na watoto wawe ni mali kwa dhana ya Ukomunisti, hapa amekosea njia, akatoa wito na dhana potofu, na mtazamo wake wa kumdharau mwanamke unatafautiana na Uislamu, kwani mwanamke ndani ya Uislamu anatukuzwa na kupewa haki ya kushirikiana na mwanamume katika sekta za maisha. Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema: {Na hakika tumewatukuza wanadamu na tumewapa vya kupanda barani na baharini, na tumewaruzuku vitu vizuri, na tumewatukuza kuliko wengi katika wale tuliowaumba, kwa utukufu ulio mkubwa (kabisa)} [BANI ISRAIL 70]. Neno “wanadamu” lililotajwa katika Aya tukufu linajumuisha mwanamume na mwanamke ambao wote wawili walitukuzwa na Mwenyezi Mungu. Ama wazo la kuwa wanawake na watoto wako miongoni mwa mali kwa dhana ya Ukomunisti, basi Uislamu unaangalia zaidi familia pamoja na kuhifadhi mali binafsi na kuongoza mambo hayo yote kwa mifumo ya kina yenye uwiano ambayo inadhamini furaha kwa binadamu.
• Licha ya kuthamini kwetu uchambuzi wa kina uliotolewa na Aflatun ambaye aliutoa kwa sababu mbili; ubaguzi na ugomvi wa kitabaka ambapo aliona kwamba sababu hizo zote mbili zinasababishwa na ufisadi wa mfumo wa malezi na elimu, basi Uislamu una msimamo safi uliowazi kuhusu ufisadi wa mataifa, jambo ambalo tutalizungumzia baadaye katika maudhui peke yake.
• Fikra ya Kiislamu inaona kuwa jamii ina haja ya wakulima mafundi, askari na viongozi, na wote hawa wana haki sawa ya heshima hata kama wana daraja duni ya kitabaka. Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema: {Enyi mlioamini! Wanaume wasiwadharau wanaume wenzao; huwenda wakawa bora kuliko wao, wala wanawake wasiwadharau wanawake wenzao, huwenda wakawa bora kuliko wao. Wala msitukanane kwa kabila, wala msiitane kwa majina mabaya (ya kejeli): Jina baya kabisa kuambiwa mtu ni asi baada ya kuwa ni Mwislamu. Na wasiotubu, basi hao ndio madhalimu (wa nafsi zao)}[AL-HUJURAT 11].
• Uislamu katika utukufu wake na utakatifu wake unanadia kuwa ubinadamu unatokana na asili moja. Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema: {Enyi watu! Mcheni Mola wenu ambaye Amekuumbeni katika nafsi (asili) moja. Na Amemuumba mkewe katika nafsi ile ile. Na Akaeneza wanaume wengi na wanawake kutoka katika wawili hao. Na mcheni Mwenyezi Mungu Ambaye kwaye mnaombana. Na (mwatazame) jamaa. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mlinzi juu yenu (Anayeona kila mnayoyafanya)}[AN NISAA, 1].
• Uislamu umejaalia tofauti za lugha na jinsia ni alama mojawapo ya ishara za Mwenyezi Mungu, na si sababu ya kugombana na hitilafu, bali ni sababu ya kujuana na kushikamana. Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema: {Na katika Ishara Zake (za kuonyesha uwezo wake) ni kuumba mbingu na ardhi, na kuhitalifiana lugha zenu na rangi zenu na (mengine hali ya kuwa Muumbaji ndiye huyo huyo mmoja). Kwa yakini katika haya zimo Ishara kwa wenye ujuzi} [AR-RUM, 22], pia Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Enyi watu! Kwa hakika tumekuumbeni (nyote) kwa (yule) mwanamume (mmoja; Adamu) na (yule yule) mwanamke (mmoja; Hawwa). Na tumekufanyeni mataifa na makabila (mbali mbali) ili mjuane (tu basi; siyo mkejeleane). Hakika ahishimiwaye sana miongoni mwenu mbele ya Mwenyezi Mungu ni yule amchaye Mungu zaidi katika nyinyi. Kwa yakini Mwenyezi Mungu ni Mjuzi, Mwenye habari (za mambo yote)}[AL-HUJURAT 13].
• Wahyi wa Mwenyezi Mungu haukuishia katika ibada za kidini tu na kuwaacha watu na mambo yao ya kidini; kwani akili pungufu ya binadamu haiwezi kutambua kanuni zote za maisha kiujumla wala haiwezi kutenganisha kati ya kanuni hizo na ada za jadi au mila. Kwa hiyo, Quraani Tukufu imekuja na misingi ya kiujumla na Sunna Tukufu ilipambanua vizuri misingi hiyo, nayo Sheria ya Kiislamu ilichukua jukumu la kujali masilahi ya binadamu. Mwenyezi Mungu Mkufu tuAmesema: {anawaamrisha mema na anawakataza yaliyo mabaya, na kuwahalalishia vizuri na kuwaharamishia vibaya, na kuwaondolea mizigo yao na minyororo iliyokuwa juu yao (yaani Sheria ngumu za zamani na mila za Kikafiri)} [AL AARAF, 157].
• Sheria ya Kiislamu iliweka misingi ya kuunda jamii yake kwa wepesi, na kukataa dhiki na kuondoa uzito. Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema: {Mwenyezi Mungu Anakutakieni yaliyo mepesi wala hakutakieni yaliyo mazito} [AL BAQARAH, 185]. Aidha Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema: {Hapendi Mwenyezi Mungu kukutieni katika taabu; bali Anataka kukutakaseni na kutimiza neema Yake juu yenu ili mpate kushukuru} [AL MAIDAH, 6].
• Aidha Uislamu uliunda jamii yake kwa msingi wa kupinga uchawi na pasiwepo kundi fulani ambalo linahusika na sheria bila ya jingine. Pia katika jamii kuna wanachuoni na wanafiqhi. Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema: {Wamefanya wanavyuoni wao na watawa wao kuwa ni miungu badala ya Mwenyezi Mungu, na (wamefanya) Masihi mwana wa Maryamu (pia Mungu), hali hawakuamrisha isipokuwa kumuabudu Mungu mmoja, hakuna anayestahiki kuabudiwa ila Yeye. Ametakasika na yale wanayomshirikisha nayo} [AT TAWBA 31].
• Miongoni mwa misingi ya jamii yenye maadili ya hali ya juu katika Quraani Tukufu ni: Kumtii Mwenyezi Mungu, Mtume wake s.a.w. na wenye madaraka. Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: {Enyi mlioamini! Mtiini Mwenyezi Mungu na mtiini Mtume na wenye mamlaka juu yenu, walio katika nyie (Waislamu wenzenu). Na kama mkikhitalifiana juu ya jambo lolote basi lirudisheni kwa Mwenyezi Mungu na Mtume, ikiwa mnamwamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho. Hiyo ndiyo kheri, nayo ina matokeo bora kabisa} [AN NISAA, 59].
• Na kati ya misingi yake ni kwamba: Jamii ya Kiislamu ina ujumbe ambao jamii inabeba jukumu la kuutekeleza na kuufikisha. Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema: {Na hivyo tumekufanyeni umati bora (kama kibla chenu tulivyokifanya bora) ili muwe mashahidi juu ya watu, na Mtume awe shahidi juu yenu} [AL BAQARAH, 143].
• Miongoni mwa misingi yake ni kwamba Uislamu una mipaka ambayo inadhibiti matakwa ya watu wenye tabaka na mamlaka tofauti. Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema: {Na wahukumu baina yao kwa yale aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu, wala usifuate matamanio yao. Nawe jihadhari nao wasije kukugeuza na baadhi ya yale aliyokuteremshia Mwenyezi Mungu. Na kama wakikengeuka, basi jua kwamba hakika Mwenyezi Mungu Anataka kuwafikishia (adhabu) kwa baadhi ya dhambi zao. Na bila shaka wengi katika watu ni maasi} [AL MAIDAH 49].
• Na miongoni mwa misingi yake: kuamrisha mema na kukataza maovu; jambo ambalo linakuwa ni nguzo ya salama kwa jamii na lenye uwezo wa kuikuza jamii. Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema: {Nyinyi ndio umma bora kuliko zote zilizodhihirishiwa watu (ulimwenguni) – mnaamrisha yaliyo mema na mnakataza yaliyo maovu, na mnamwamini Mwenyezi Mungu} [AALI IMRAN 110].
• Na miongoni mwa misingi yake: mambo yote ya jamii yanaongozwa kwa mashauriano, amana na uadilifu baina ya watu katika viwango vyote. Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema: {Na ushauriane nao katika mambo. Na ufungapo nia mtegemee Mwenyezi Mungu (tu ufanye hili ulioazimia). Hakika Mwenyezi Mungu Anawapenda wanaomtegemea} [AALI IMRAN 159]. Aidha Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema: {Hakika Mwenyezi Mungu Anakuamrisheni kuzirudisha amana kwa wenyewe (wanaozistahiki). Na mnapohukumu baina ya watu mhukumu kwa haki. Bila shaka mawaidha Anayokutoleeni Mwenyezi Mungu ni mazuri sana. Hakika Mwenyezi Mungu ndiye Asikiaye (na) Aonaye} [AN NISAA, 58]. Pia Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Enyi mlioamini! Kuweni wasimamizi (wa kupitisha haki) kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, muwe mkitoa shahada kwa uadilifu. Wala kuchukiana na watu kusikupelekeeni kutowafanyia uadilifu. Fanyeni uadilifu; huko ndiko kunakomkurubisha mtu na uchamungu. Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu Anazo habari za (yote) mnayoyatenda} [AL MAIDAH 8].
(Profesa Muhamad Sayed Ahmad Al Musayar, Almujtamaa Almithaaliy fi Alfikri Alfalsafiy Wamawqifu Islaamu Minhu, Cairo, cha. Dar Al Maarif, 1989, uk. 9: 22, 86: 95, 112: 119).
 

Share this:

Related Fatwas