Hukumu ya Kuwajibika na Mikataba ya Jinsia
Question
Jinsia ni nini? Na nini hukumu ya kuwajibika na mikataba yake kwa mujibu wa Fiqhi ya Kiislamu (Muwafaka wa Umoja wa Mataifa wa kuwatambua wapenzi wa jinsia moja)?
Answer
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Al Jindar ni neno la kiarabu lililotoholewa kutokana na neno la Kiingereza lenye asili ya Kilatini ambalo ni genda, na maana yake Kiswahili ni jinsia kwa maana ya uume na uke, na linatumika kwa ajili ya kusanifisha majina, viwakilishi na vivumishi.
Na neno hili linafafanuliwa na Shirika la Afya la Kimataifa kama ni: sifa fulani kwa mwanamume na mwanamke kama vile, sifa za kijamii zenye mchanganyiko ambazo hazina uhusiano na tofauti za kimaumbele, na linafafanuliwa kwenye Insaikolopidia ya Uingereza kwamba ni: Hisia ya mwanadamu katika nafsi yake kama vile dume au jike. Na kwa hivyo mwanamume akifanya kazi ya kike kimaumbile, au mwanamke akafanya kazi ya kiume kimaumbile, basi hapatakuwepo tofauti baina ya dume na jike, lakini kwa hakika ni kuwa kutakuwa na aina nyingine ya jinsia ambayo ndio hiyo "gender", na hii ina maana kuwa tofauti ya kibaiolojia ya mwanamume na mwanamke haitakuwa na uhusiano wa kuchagua uchangamfu wa kijinsia ambao unafanywa na wote wawili. Na hapa kuna wito wa wazi wa uhusiano wa watu wa jinsia moja, na ina maana pia kuwa mwanamume anachukua nyadhifa za mwanamke kimaumbile, na mwanamke anachukua nyadhifa za mwanamume kimaumbile, kwani kimaumbile, nyadhifa zinazohusiana na kila mmoja wao kati ya mwanamume na mwanamke zilipangwa na jamii, na maumbile hayakupanga uume na uke, kama wanavyodai, na hii maana ya kuivunja familia ambayo ndio msingi wa jamii zote, na bila yake jamii hiyo itaporomoka.
Basi wanasema kuwa familia inajengwa na mwanamume na mwanamume, na inaweza kujengwa na mwanamke na mwanamke, wanawake wawili na mwanamume mmoja, wanaume kadhaa na mwanamke mmoja, mwanamke mmoja na watoto kwa njia ya mkataba, au wanaume kadhaa na watoto kwa njia ya mkataba, na hayo pia yana maana ya kumpa mwanamake nguvu zaidi ya kisiasa, ya kijamii na ya kiuchumi sawa na nguvu anayopewa mwanamume katika viwango vyote hata katika familia.
Na hivi ndivyo yote yanavyogongana na Sheria ya Kiislamu na misingi yake isiyotetereka. Basi Mwenyezi Mungu Mtukufu ameujenga ulimwengu kwa misingi ya uwili uwili. Basi akasema: {Na ardhi tumeitandaza na tukaiwekea milima, na tukaiotesha mimea mizuri ya kila namna.} [Qaaf 7], na Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema: {Na ndiye aliyeitandaza ardhi na akaweka humo majabali na mito. Na katika kila matunda akafanya humo namna mbili (dume na jike). Huufunika usiku juu ya mchana (na mchana juu ya usiku). Hakika katika haya zimo ishara (kubwa kuwa Mwenyezi Mungu yuko); kwa watu wenye kufikiri.} [AR RAAD 3]
Na Mwenyezi Mungu akatuumbia mwenza kutokana nasi ambaye ni mwanamke ili tuwe na utulivu, mapenzi na huruma. Basi Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema: {Enyi watu! Mcheni Mola wenu ambaye amekuumbeni katika nafsi (asili) moja. Na akamuumba mkewe katika nafsi ile ile. Na akaeneza wanaume wengi na wanawake kutoka katika wawili hao.} [AN NISAA 1]. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema: {Na katika Ishara zake (za kuonyesha ihsani zake juu yenu) ni kuwa Amekuumbieni wake zenu katika jinsi yenu ili mupate utulivu kwao, naye Amejaalia mapenzi na huruma baina yenu. Bila shaka katika haya zimo Ishara kwa watu wanaofikiri.} [AR-RUM 21].
Na kutokana na hayo, familia ambayo Mwenyezi Mungu Mtukufu anaitaka hujengwa kwa mme na mke. Anasema S.W. {Enyi watu! Kwa hakika tumekuumbeni (nyote) kwa (yule) mwanamume (mmoja; Adamu) na (yule yule) mwanamke (mmoja; Hawaa)} [ AL-HUJURAT 13].
Na katika Qurani Mwenyezi Mungu amewasema vibaya watu wa Luti ambao walitaka kuunda familia kwa watu wa jinsia moja ambao ni wanaume wawili, na kuacha waliyohalalishiwa na Mwenyezi Mungu katika sheria yake, na akawaelezea kuwa huo ni ujinga na ni kwenda kinyume. Basi Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema: {Na (tulimpeleka Luti. Basi (wakumbushe watu wako) alipowaambia kaumu yake: "Je! Mnafanya jambo chafu ambalo hajakutangulieni yoyote kwa jambo hilo katika walimwengu!". (80) "Nyinyi mnawaendea wanaume kwa kuwa ndio mnaowatamani badala ya wanawake! Ama nyinyi ni watu wafujaji" (81) [ AL AARAF 80,81]
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: {Na (wakumbushe) Luti alipowaambia watu wake: "Je, mnaufanya uchafu, na hali mnaona?". Mnawaingilia wanaume kwa matamanio mabaya badala ya wanawake? Hakika nyinyi ni watu mfanyayo ya ujinga kabisa. [AN-NAML 54 - 55]. Na akawaelezea kuwa na ufuska ni uchafu. Basi akasema S.W.: {Na Luti tukampa hukumu na elimu na tukamuokoa na (watu wa) ule mji uliokuwa ukifanya maovu. Bila shaka wao walikuwa watu wabaya, wavunjao (Sheria ya Mwenyezi Mungu) amri.} [AL-ANBIYAA 74]
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu Amemjaalia mume uongozi na matumizi ya familia kuwa ni jukumu lake, na akamjaalia mke unyonyeshaji na malezi ya mtoto kama ni jukumu lake, Na huu ni mfumo wa Sheria wa Mwenyezi Mungu kwa mwanadamu ambaye amemuumba, kwani yeye anayajua zaidi yanayomfaa mwanadamu, akasema S.W.: {Wanaume (wawe) ni walinzi wa wanawake; kwa sababu Mwenyezi Mungu amewafadhilisha baadhi yao kuliko wengine, na kwa sababu ya mali zao wanazozitoa. Basi wanawake wema ni wale wenye kutii, wanaojihifadhi (hata) wasipokuwapo (waume zao); kwa kuwa Mwenyezi Mungu amewaamrisha wajihifadhi. Na wanawake ambao mnaona uasi wao kwenu waonyeni na waacheni peke yao katika vitanda na wapigeni, Na kama wanakutiini msiwatafutie njia (ya kuwaudhi bure). Hakika Mwenyezi Mungu ndiye Aliye juu (na) ni Mkuu.} [AN NISAA 34].
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: {Wawekeni humo humo mnamokaa nyinyi, kama mpatavyo (ijapokuwa mumewawacha; maadamu eda yao haijesha). Wala msiwadhuru kwa kuwatia dhiki. Na kama wakiwa na mimba, wagharamieni mpaka wajifungue. Na kama wakikunyonyesheeni watoto wenu, basi wapeni ujira wao, na shaurianeni kwa wema. Na kama mkiona kuna udhia baina yenu, basi mwanamke mwingine (asiekuwa mkewe) amnyonyeshee mwanawe.} [AT-TALAQ 6]. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu anakataza mwanamke kutamani yale aliyomfadhilishia mwanaume, na anakataza pia mwanamume kutamani yale aliyofadhilishia mwanamke. Basi Akasema S.W.: {Wala msitamani vile ambavyo Mwenyezi Mungu amewafadhilisha baadhi yenu (kwa vitu hivyo) kuliko wengine. Wanaume wanayo sehemu (kamili) ya vile walivyovichuma, na wanawake nao wanayo sehemu (kamili) ya vile walivyovichuma. Na mwombeni Mwenyezi Mungu fadhila zake. Hakika Mwenyezi Mungu ni mjuzi wa kila kitu.} [AN NISAA 32].
Na Mtume S.A.W amewalaani wanaume wanaojifananisha na wanawake, na wanawake wanaojifananisha na wanaume. Kwa hivyo basi, Imamu Bukhariy na Imamu Tirmadhiy walipokea kutoka kwa Abdullahi Bin Abaas Radhi za Allah ziwafikie wote wawili, aliyesema: "Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W. amewalaani wanaume wenye kujibadilisha na wanawake wenye kujibadilisha, na akasema: watoeni majumbani mwenu". Na katika simulizi nyingine alisema: "Na Mtume S.A.W amewalaani wanaume wanaojifananisha na wanawake, na wanawake wanaojifananisha na wanaume.
Na nyasia hizi na uongozi wa mwanaume si utenzaji nguvu kwa mwanamke, na si dhuluma kwake, bali ni kumlinda na kumhifadhi kwa uongozi huo, na kwa hiyo Mtume S.A.W aliwausia wanaume juu ya wanawake. Kwa hivyo basi Imamu Muslim, Nassaiy na Ibn Majah walipokea Hadithi kutoka kwa Ummu Salamah R.A kuwa alisema: wasia wa mwisho wa Mtume S.A.W ni mambo matatu: alikuwa akiyazungumzia mpaka ulimi wake ukawa mzito na akakata kauli, alikuwa akisema: Sala tano na wale mnaowamiliki kwa mikono yenu ya kulia, msiwabebeshe majukumu wasioweza kuyabeba. Allah Allah katika wanawake, nakutilieni mkazo kwa wanawake kwani wao ni wasaidizi wenu walio katika mikono yenu, -yaani mateka- hawana uwezo, mmewachukua kwa amana ya Mwenyezi Mungu na mkazihalalisha tupu zao kwa neno la Mwenyezi Mungu.
Ama hukumu ya kuwajibika na utekelezaji wa mikataba ya jinsia, kama vile, sisi kuwatambua wapenzi wa jinsia moja - nao ni uhusiano wa watu wa jinsia moja - basi mikataba hiyo haijuzu kwani inakwenda kinyume na sheria ya Mwenyezi Mungu, na wala haijuzu kwa mtawala wa kiislamu kuikubalia. Kwa hivyo basi, katika hili, anasema Imamu Tirmadhiy kutoka kwa Amru Bin Auof Al Mazniy kwamba: Mtume S.A.W. alisema: "Waislamu hufuata masharti yao, isipokuwa sharti linaloharamisha halali au kuhalalisha haramu."
Na Bukhariy alipokea kutoka kwa Aisha R.A. akisema: Mtume S.A.W amesema: "Sharti lolote lisilokuwemo ndani ya Quraani halikubaliki" yaani sharti ambalo halimo katika aliyoyaandikia Mwenyezi Mungu na aliyoyawajibisha katika sheria yake ambayo aliifaridhisha basi hilo ni sharti batili, na mikataba inayohusika nalo nayo ni batili na wala haijuzu, na kama mtawala alilazimika kuingia kwenye mikataba inayokwenda kinyume na sheria ya Mwenyezi Mungu basi haujuzu kuitii na kuitekeleza kwake, na atanasihiwa na kuonywa hadi pale atakapoacha mikataba hiyo na kuwa mbali nayo, kwani hakuna utiifu kwa mwanadamu katika kumuasi Mwenyezi Mungu.
Bukhariy alipokea kutoka kwa Ibn Omar Radhi za Allah ziwafikie wote wawili, kutoka kwa Mtume S.A.W. akisema: "Usikivu na utiifu juu ya mtu aliye mwislamu huwa kwa yale anayoyapenda na yale anayoyachukia, kama hakuamrishwa kufanya maasi, na kama ataamrishwa kufanya maasi basi hakuna kusikia wala kutii."
Al Qurtubiy alisema katika tafsiri yake: "Ibn Khoiz Mandad, kuwa: Na ama utiifu wa Sultani basi unawajibika katika mambo ya utiifu wa Mwenyezi Mungu na hauwajibiki katika mambo ya kumuasi Mwenyezi Mungu. [Al Jaamei La Ahkaam Quraani 259/5, Ch. Dar Al Kutub Al Masriyah].
Na Al Nawawiy akasema: "Ni wajibu kuwatii viongozi kwa magumu na yanayochukiza katika nafsi na mengineyo mengi miongoni mwa yale ambayo si katika maasi, na yakiwa ni maasi basi hakuna kuyasikiliza wala kuyatii." [Sharh Sahih Muslim kwa Al Nawawiy 224/12, Ch. Dar Ihiyaa Al Turaath Al Arabiy]
Na kutokana na hayo; Al Jindar; ni istilahi na fikra inayokwenda kinyume na sheria ya Kiislamu, Na wala haijuzu kisheria kuikubali na kuwajibika nayo kwa kutekeleza mikataba yoyote inayoihusu.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni mjuzi zaidi ya wote.