Saumu ya Mwenye Hedhi

Egypt's Dar Al-Ifta

Saumu ya Mwenye Hedhi

Question

Je, inajuzu kwa mwenye hedhi kula na kunywa katika mchana wa Ramadhani, au atosheke na kula pamoja na kunywa kidogo na kisha ajizuie siku nzima, kwa ajili ya kuheshimu utukufu wa Ramadhani?

Answer

Sifa zote njema ni zake Mwenyezi Mungu, rehma na amani zimfikie Mtume Muhammad S.A.W., watu wake, masahaba wake na waliomfuata. Ama baada ya hayo:

Maamuzi ya kisheria ni kuwa haisihi kwa Mwenye Hedhi kufunga na wala si wajibu kwake, na ni haramu kwake kufunga na analazimika kulipa.

Na uharamu wa Saumu na kutosihi kwake ni kwa aina zote za Saumu iwe za faradhi au Sunna, na Al Bukhariy na Muslim wanasimulia katika Sahihi mbili kutoka kwa Abi Said Al Khudriy R.A. kwamba Mtume S.A.W. amesema: "Sikuwahi kuwaona wapungufu wa akili na dini na watumiao zaidi moyo kuliko nyie wanawake wale wenye akili miongoni mwenu". Kisha akasema: "Na atakaa nyusiku zake na wala haswali na atakula katika mwezi wa Ramadhani basi huu ni upungufu wa dini." Na katika riwaya ya Al Bukhariy: Je haiwi pale anapokuwa na hedhi haswali na wala hafungi? Nalo ni swali la kufafanua linakusudiwa kumfanya aambiwaye kukiri na kukubali jambo ambalo analijua vilivyo.

Mwanachuoni mkubwa Al Jamal amesema katika kitabu chake; [Hashiyat Ala Sharh Manhaj Al Ttlaab, 239/1, Ch. Dar Al Fikr]: "Na ni haramu kwake, kwa maana kwa mwenye hedhi kuanza kufunga huku akiwa tayari ana hedhi, na katika hali nyingine ni kuwa mwanamke huyo ikamjia hedhi huku yeye akiwa amefunga basi itakuwa haramu kwake kuendelea na saumu hiyo, baada ya kugundua kuwa alikuwa katika funga na kwamba alikuwa anaikamilisha sehemu iliyobakia. hali hii inatofautiana na iwapo aligundua kutokuwa na damu hiyo au hakugundua chochote, kwa hivyo uharamu hapa uko katika sura moja (ya kwanza), na haipo katika sura mbili (za mwisho). Kwa maana kuwa atakapopatwa na hedhi hali ya kuwa amefunga".

Mwenye hedhi analazimika kula, na ni haramu kwake kufunga, na pahali pa uharamu ni pale anapokusudia kujizuia kula kwa nia ya Saumu, ama iwapo hakula kifungua kinywa na wala hakunuiya Saumu basi hakuna uharamu wowote.

Imamu An Nawawiy akasema katika kitabu cha [Al Majmou', 259/6, Ch. Al Mambariyah]: "Na mwenye hedhi akifunga siyo kwa nia ya Saumu basi hapati dhambi, lakini -yaani hupata dhambi- akinuiya Saumu hata kama ilikuwa si sahihi".

Na baadhi ya wanachuoni wanaona kwamba inapendeza kwake kujizuia na hasa katika mwezi mtukufu wa Ramadhani kwa ajili ya kujifananisha na waliofunga, kwani kujizuia ni miongoni mwa mambo maalumu ya Ramadhani wakati ambapo baadhi ya wengine wanaona kuwa haipendezi kwake kujizuia kula.

Al Sheikh Abdulhameed Al Sharawaaniy alisema katika kitabu chake; [ Hashiyatahu ala Tuhafat Al Muhtaaj, 433/3, Ch. Dar Ihiyaa Al Turaath Al Arabiy]: "Na matokeo yake, ni kuwa yule ambaye inajuzu kwake kula kwa kuonekana au kwa kificho si lazima kwake kujizuia kula bali ni Sunna, na yule ambaye ni haramu kwake kula kwa kuonekana na kwa kificho au kwa kificho tu basi ni lazima ajizuie kula".

Na kupendeza huku ni kwa yule asiyenuia saumu, ama katika haki ya yule anayedhani kuwa kula kwake ni katazo la kisheria -kama vile wanawake wengi wa leo- kimsingi hakuna sheria inayomtaka ajizuie, bali ni wajibu kwake kuamini kutokuwepo uzito wowote juu yake kwa kula chakula na kutekeleza amri ya sheria ya kuacha saumu, na iwapo hili halitamtokea isipokuwa kwa kula kitu miongoni mwa vyakula basi atalazimikia kwa wakati huo kufanya hivyo.

Ama wajibu wake wa kulipa saumu ya faradhi baada ya kuwa msafi ni jambo lisilo na pingamizi yoyote -kama ilivyotangulia katika kauli ya Imamu An Nawawiy-; na Al Bukhariy na Muslim walipokea -na tamko ni lake- kutoka kwa Bibi Aisha R.A. kwamba amesema: "Tulikuwa tukiamrishwa kulipa Saumu na wala hatujaamrishwa kulipa Sala.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni mjuzi zaidi ya wote.
 

Share this:

Related Fatwas