Ismailia na Ibadhi

Egypt's Dar Al-Ifta

Ismailia na Ibadhi

Question

 Wataalamu wa mambo ya Mashariki mara nyingi wanatoa mafunzo na semina za kielimu katika vyuo vikuu vya Ujerumani, wakigusia "makundi yanayojitenga" na Uislamu. Na mara nyingi wanazungumzia “Ismailia” na “Ibadhi”. Je, makundi hayo mawili ni kweli yanajitenga na Uislamu au ni madhehebu maalumu? Je, Ahlu Sunna wanafahamu kwamba makundi hayo mawili ni miongoni mwa madhehebu ya Kiislamu? Je, inaruhusiwa kwa Ahlu Sunna kuoana nao? Kwa kuwa maelezo kwa Kijerumani yaliyopo katika tovuti za mtandao yana upungufu kuhusu madhehebu mawili haya, na mtu hawezi kuamini kwa urahisi yanayosemwa na wataalamu wa mambo ya Mashariki hawa wanapozungumzia Uislamu, basi nitashukuru mkinitajia baadhi ya maelezo yanayohusu itikadi za makundi haya mawili na marejeo wanayoyarejea katika fiqhi ya Kiislamu, je, wanakubali hadithi za Al-Bukhari, Muslim na Ahlu Sunna au madhehebu ya Ahlu Sunna?

Answer

Sifa zote njema ni zake Mwenyezi Mungu, rehma na amani zimfikie Mtume Muhammad S.A.W., jamaa zake, masahaba wake na waliomfuata. Ama baada ya hayo:

Ismailia ni: kikundi miongoni mwa vikundi vya Mashia kinachoitwa “Batinia” (yaani wana itakidi kwamba matini za Kiislamu zina maana mbili, ya kwanza iko wazi kwa watu wote, na ya pili haiko wazi isipokuwa kwa aliowachagua Mwenyezi Mungu tu), watu wa kikundi hicho wanajinasibisha na Imamu Ismail bin Jafar Al-Sadiq, wafuasi wa kikundi hicho wanonekana ni Mashia, lakini ukweli wao ni kwamba wanataka kuharibu itikadi za Kiislamu, kikundi hicho kina matawi mengi sana tangu zamani mpaka sasa, na ukweli wao ni kinyume na itikadi za Kiislamu ambazo ni sahihi, walielekea katika msimamo mkali katika dini hata wafuasi wa kikundi kinachoitwa Ithna Ashria ya Mashia wanafahamu kwamba watu wa Ismailia ni makafiri.

Al-Ghazali ambaye ni hoja ya Uislamu –ni mmoja wa wanaofahamu kikundi hicho kwa undani- anasema kuhusu ulinganiaji wa Ismailia katika kitabu chake [Fadhaih Al-Batiniah, Uk.18, Muasasit Darul Kutub Al-Thakafiah- Kuwait], “Makala nyingi sana zimekubaliana kwamba hukuna mwenye dini au mwenye itikadi sahihi au anaamini utume anaweza kulingania katika kikundi hicho (kikundi cha Ismailia), basi anayelingania kwa kikundi hicho anaendeshwa na anajiweka nje ya dini ya Kiislamu kama nywele inavyojipenyeza nje ya unga”. Imamu Fakhr Al-Din Al-Razi katika kitabu chake [Itikadat Firaq Al-Muslimiin wa Al-Mishrikiin, Uk. 76, Dar Al-Kutub Al-Elmiyya] anasema: “Sehemu ya tisa: Kuhusu wale wanaojidai Uislamu, lakini wao si Waislamu, vikundi hivi ni vingi mno lakini tutavitaja vikundi maarufu sana. Kikundi cha kwanza: “Al-Batiniyya” jua kuwa ufisadi wa watu hawa juu ya dini tukufu ya Uislamu ni zaidi kuliko ufisadi wa makafiri wote. Vikundi hivi viko vingi na lengo lao ni kubatilisha sheria nzima na kumkanusha mwumbaji, hawaamini dini ya aina yoyote na wala hawatambui Uislamu wa kweli, lakini wao hawadhihirishi mwenendo wao huo na wanadai kkuwa wao ni watu wa akhera na wala si watu wa duniani”.

Kikundi hicho kimezungukwa na usiri na hali isiyofahamika, na kina matawi na kimepata umaarufu kwa majina mbalimbali: kama Al-Batiniyya, Al-Khermiah, Al-Qaramita, Al-Muhammara, Al-Sabaiah, Al-Taalimiyah, Al-Ismailia n.k, na Al-Ghazali ambaye ni hoja ya Uislamu anaelezea sababu za kuitwa kwa baadhi ya majina hayo, katika kitabu chake [Fadhaih Al-Batiniyya, Uk.11- 12] anasema: “Kuhusu wafuasi wa Al-Batiniyya, wameitwa kwa jina hilo kwa madai yao kwamba mambo yaliyo wazi katika Quraani na habari zake yanahusiana na mambo mengine yasiyo wazi nayo ni kama kokwa na ganda lake, na kwa picha zake wajinga wanadhani ni ishara tu wakati ambapo wenye hekima na akili wanaona ni alama na ishara wazi kwa ukweli fulani, na kwamba ambaye akili yake haikuweza kufahamu kwa ndani yaliyofichika na ameridhika na yaliyo wazi akidanganywa atakuwa chini ya mizigo na minyororo na anahusika na makosa, na minyororo wanakusudia jukumu la kisheria, basi ambaye anafahamu mambo yasiyo wazi ataondolewa jukumu la kisheria, na atastarehe kutoka majukumu yake, nao wanakusudiwa katika kauli ya Mwenyezi Mungu: {na anawaondolea mizigo yao na minyororo iliyo kuwa juu yao...} [AL ARAAF 157], na pengine wanadai kwamba: wajinga wanaokataa mambo yasiyo wazi ni wale ambao wamekusudiwa katika kauli ya Mwenyezi Mungu: {Utiwe baina yao ukuta wenye mlango - ndani yake mna rehma, na nje upande wake wa mbele kuna adhabu.} [AL HADID 13], na lengo lao kuu ni kubatilisha sheria, wao kama wataondolewa mambo ambayo ni wazi kutoka itikadi wataweza kuhukumu kwa kudai mambo yasiyo wazi kwa mujibu wa kutengwa na misingi ya dini katika hali ya kutokuwepo uaminifu, basi bado hakibaki chochote kinachohusiana na sheria ili kukirejelea na kukiaminia."

Kisha Al-Ghazali anasema katika [Uk 14]: Wafuasi wa kikundi cha Al-Khermiah wameitwa jina hilo kutokana na yanayopatikana ndani ya madhehebu yao, jina hilo linamaanisha wanaofanya ibada wameondolewa majukumu ya kisheria na kuwataka watu kufuata matamanio, tamaa na haja inayoruhusiwa na isiyoruhusiwa, na neno Kharam ni neno la kigeni, linamaanisha jambo linalopendwa na mwanadamu, jina hilo lilikuwa la watu wa Mazdikiah, nao ni watu majusi wanaohalilisha kila kitu, walikuwepo katika zama za mfalme anayeitwa Kabbaz, na wakahalilisha wanawake hata kama ni maharimu wao, na wamehalilisha haramu na waliitwa Kharamdiniah, pia wameitwa kwa jina hilo kwa sababu wanafanana na kikundi cha Al-Khermiah katika mwisho wa madhehebu, ingawa wanatofautiana nao katika vitu vingine vilivyotangulia katika madhehebu yao.”

Kisha anasema katika [Uk 17]: “Pia wameitwa kwa jina la Al-Taalimiyah; kwa sababu msingi wa madhehebu yao ni kubatilisha maoni na akili, na kuwatia watu kujifunza kutoka kwa Imamu asiyekosea, na kwamba hakuna njia ya kupata elimu isipokuwa kupitia kwake, na husema mwanzoni mwa mijadala yao kuwa haki inaweza kujulikana kupitia maoni au kupitia kujifunza, imebatilika kutegemea maoni kwa sababu ya kupinga maoni na tofauti ya mitizamo ya wenye hekima, basi ni lazima kutegemea kusoma na kujifunza, na jina hilo linafaa sana kwa wafuasi wa kikundi cha Al-Batiniyah cha siku hizi, wanaotegemea zaidi kuwataka watu kusoma, kubatilisha maoni, kumfuata Imamu asiyekosea, ni jambo la lazima kumwamini na kumwiga kama wanavyomwiga Mtume wa Mwenyezi Mungu (SAW.)”.

Imamu Sayf Ud Din Al-Amidi anasema katika kitabu cha [Abkaru Al-Afkar, 5/63, Darul-Kutub wal Wathaiq Al-Qawmiyah – Kairo]: "asili ya wito wa hawa inategemea kubatilisha sheria, na kukanusha kanuni za kidini, kwa sababu mwanzoni mwa wito wao baadhi ya majusi wanaoitwa Ghaiariah walikutana wakikumbushana jinsi mababu zao na mfalme walivyokuwa, mfalme ambaye alishindwa na Waislamu, wakisema: hakuna njia nyingine kwetu ili kuwashinikiza kwa upanga kwa sababu ya wingi wao na nguvu zao, lakini tunadanganya kwa tafsiri ya sheria zao, kama walivyofasiri mababu zao wa majusi, na tunawavuta wale ambao ni wanyonge miongoni mwao, jambo hilo pengine linasabibisha tofauti kati yao, na hawatakuwa na neno moja”.

Wafuasi wa kikundi hicho tayari wameshatoka nje ya mzunguko wa Uislamu ambao ni mpana, na nje ya mzunguko wa madhehebu ya Kiislamu ambayo ni sahihi, wanavyuoni wote wamehakikisha kwamba wito wa wafuasi wa kikundi hicho ni batili, na wanawavuta wafuasi wao katika mambo ya uchi na mwishoni kuwavua dini kabisa, na kukanusha uungu, unabii na sheria za mbinguni, na wamefanya hivyo kwa madai ya kwamba matini za kisheria zina vipengele vilivyo wazi na vengine haviko wazi, na kwamba visivyo wazi vinakusudiwa zaidi kuliko vile vya wazi, na kwamba imamu asiyekosea peke yake anahusika katika kujua vipengele hivyo visivyo wazi, na ndiye anayefasiri matini hizo, kisha anawasiliana na wafuasi wake kupitia wasaidizi wake, ambao ni wakuu wa kikundi hicho potofu na wanaolingania. Miongoni mwa sampuli za tafsiri zao batili ni kusema kwamba udhu ni ibara ya kumtii imamu wao, na kwamba Tayammum ni kufanya yanayoruhusiwa anapokosekana Imamu ambaye ni hoja, na Sala ni msemaji ambaye ni mtume kufuatana na aya hii: {Hakika Sala inazuilia mambo machafu na maovu} [AL ANKABUT 45], na hali ya kutoka manii usingizini ni kutoa siri miongoni mwa siri zao kwa watu wasio familia yake bila ya kukusudia, na kwamba kuoga ni Mkataba mpya, na Zaka ni kutakasa nafsi kwa kujua wajibu wao katika dini. [Rejea: “Almawaaqifu wa sharhuhu” cha Sharif Al-Jerjani 3/687, Dar Al-Jiil].

Ibadhi: wao ni kikundi cha Waislamu, wana masuala maalumu ya kiitikadi yanawafanya wawe karibu na madhehebu ya Muutazila, Ibadhi ni madhehebu ya kifiqhi yanayohesabiwa miongoni mwa madhehebu manane ya Kiislamu yanayotambulika kama madhehebu ya Dhahiria, na Ibadhi yanananasibishwa na Taabiy anayeitwa Jabir bin Zaid Al-Azdi, ambaye ni mtaalamu wa hadithi, mwanafikihi, imamu katika tafsiri na hadithi, mmoja wa wanafunzi wa Ibn Abbas na amepokea hadithi kutoka kwa Bi Aisha na masahaba wengi walioshuhudia vita vya Badr. Ama kuhusu kauli iliyo maarufu kwa wanahistoria kwamba Ibadhi yanahusishwa na Abdullah bin Ibadhi, ambaye aliishi katika zama za Abdul Malik bin Marwan, basi ni uhusiano wa kiwakati tu husababishwa na baadhi ya mitazamo ya kisiasa aliyojulikana nayo Ibn Ibadhi, kwa hivyo Umawiyyuwn wakakinasibisha kikundi cha Ibadhi kwake. Ibadhi katika historia yao ya awali, hawakutumia jina hilo, lakini walikuwa wakitumia jina la kundi la Waislamu au watu wa ulinganiaji, na mara ya kwanza kutumia jina hilo ilikuwa mwishoni mwa karne ya tatu Hijriyya na kisha wamekubali jina hilo kwa mujibu wa hali halisi.

Miongoni mwa masuala ya kiitikadi ambayo wanatofautiana na madhehebu ya Ahlu Sunna ni suala la kumwona wa Mwenyezi Mungu siku ya akhera, wao wanakataa hivyo kama Mashia na Muutazila, pamoja na itikadi yao kwamba wenye madhambi makubwa miongoni mwa Waislamu wakifa bila ya kutubu – wakiwa wenye makosa au wapotovu- ni watu ambao watadumu milele motoni, ama kuhusu Waumini –kwa itikadi, kauli na amali- watadumu milele peponi peke yao. Kutokana na hayo, walisema kwamba uombezi wa Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W. hautakuwa kwa wale waliokufa hali ya kuwa wanaendelea na madhambi makubwa, lakini utakuwa kwa waumini wote kwa ajili ya kupunguza ukali wa siku ya kukusanywa na kuingia peponi haraka au kuongeza daraja na malipo kwa ajili ya baadhi ya waumini waliokufa juu ya uaminifu na toba ya kweli, na asili ya masuala hayo ni kwamba watu wa Ibadhi wanaona: anayekiri upweke wa Mwenyezi Mungu na ujumbe wa Mtume Muhammad S.A.W., lakini amekosa faradhi za kidini au amefanya madhambi makubwa kwao anaitwa mwislamu, lakini si muumini wala mshirikina, kwao anayefanya dhambi kubwa ni kafiri aliyekufuru neema, siyo kafiri wa shirki, kwao anahesabiwa mwislamu mwenye dhambi lakini hatoki nje ya Uislamu, katika maisha yake anatekelezewa hukumu za Kiislamu na Waislamu, lakini akifa juu ya madhambi atadumu milele motoni, na kwa hiyo wao wanadai kwamba imani pasipo kutekeleza hukumu ya Uislamu haina maana, na kauli yao hii pia inatokana na kwamba vitisho vya Mwenyezi Mungu haviwezi kuachwa nyuma, kama akiwa na vitisho kwa mwenye dhambi kwa kudumu motoni, basi kila anayekufa juu ya dhambi bila ya kutubu atadumu milele motoni hata ikiwa katelekezewa hukumu za Kiislamu akiwa mwislamu katika maisha yake, na wanashikamana na ujumla wa kauli ya Mwenyezi Mungu: {Na anaye muasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na akaipindukia mipaka yake, (Mwenyezi Mungu) atamtia Motoni adumu humo, na atapata adhabu ya kudhalilisha.} [AN NISAA 14].

Sheikh Dhiauddin Al-Thumaini alisema katika kitabu cha Naili: Ameangamia anayetumai malipo ya akhera akiwa katika uasi, au anayetumai kuepuka ukafiri akiwa katika ukafiri, wala haitarajiwi kheri kwa anayekufa akisisitiza uasi wake ambao amejulikana nao ingawa hakusema hivyo waziwazi, na inaruhusiwa kutiwa shaka siyo dhana kwamba mtu inawezekana kwetu awe katika hali tofauti na iliyo mbele ya Mwenyezi Mungu.

Lakini Ahlu Sunna wanaona kuwa mtazamo wa Ibadhi na Muutazila unafinya huruma ya Mwenyezi Mungu na msamaha wake ambao ni mpana, pia wanaona kwamba ujumla wa wanayoishikilia imeingia hali ya kuhusisha, basi kudumu motoni ni kwa walioasi kwa kukufuru tu sio wengine, na Ahlu Sunna walitegemea matini nyingi kutoka Quraani na Hadithi za Mtume ambazo ni sahihi, Imamu Al-Razi anasema katika majibu yake kwa suala la Muutazila kwamba kila dhambi huadhibiwa mtendaji wake akiwa hakutubu [tafsir Al-Razi Mafatihu Al-Ghaibu 10/61, Dar Ihyau Al-Turath Al-Arabi]: “Hata hivyo, tunafahamu kwa mantiki kwamba mtu ambaye anakiri upweke wa Mwenyezi Mungu, anamtakasa, anamhudumia na anamtii kwa miaka sabini, basi malipo ya jumla ya matendo mema hayo katika muda huu mrefu ni zaidi sana kuliko adhabu ya kunywa kiasi kidogo cha mvinyo, ingawa wanavyuoni wote wameafikiana juu ya kwamba kunywa mvinyo kidogo ni dhambi kubwa. Wakishikilia Muutazila- na wakasema, adhabu ya kunywa kiasi kidogo cha mvinyo ni dhambi kubwa, zaidi ya malipo ya matendo mema yote ya Ibadhi ya miaka sabini, basi wamebatilisha msingi wao wenyewe, kwa sababu msingi wao ni kujenga masuala hayo juu ya msingi unaosema mambo mazuri au mabaya kufuatana na akili, na miongoni mwa mambo yanayojulikana sana kwa akili kwamba anayejaalia adhabu kwa kiasi kidogo cha uhalifu mbele ya ibada zote hizi ni dhalimu, kama wakiamua kufuata akili katika hali hiyo, basi watabatilisha msingi wao unaosema mambo mazuri au mabaya hufuatana na akili, kisha watabatilisha sheria zao zote”.

Katika tafsiri ya aya hii: {Hakika Mwenyezi Mungu hasamehe kushirikishwa, na husamehe yaliyo duni ya hilo kwa amtakaye} [AN NISAA 48], Imamu Al-Razi katika kitabu cha [Mafatihul Ghaib 10/98] anasema: “Aya hii ni miongoni mwa dalili ambazo zina nguvu kuliko nyingine kuhusu msamaha kwa wenye madhambi makubwa. Fahamu kwamba aya hiyo ni dalili yenye mitazamo:

Mtazamo wa kwanza: kauli yake: {Hakika Mwenyezi Mungu hasamehe kushirikishwa} maana yake ni kwamba hasamehe shirki kwa kupenda kusamehe bila kulazimishwa, kwa sababu wanachuoni waliwafikiana kwamba hasamehe kwa wajibu, hivyo wakati mshirikina anapotubu, basi kama Mwenyezi Mungu akisema kwamba hasamehe shirki, yaani hasamehe kwa kwa kutaka na kupendelea si kwa lazima, basi ni jambo la lazima aseme: {na husamehe yaliyo duni ya hilo kwa amtakaye} yaani kusamehe kwa kutaka na kupendelea si kwa lazima, ili kukanusha na kutokanusha kwende sambamba katika maana moja. Je, Huoni kwamba kama mtu akisema mtu fulani hampi yoyote kwa huruma, na anatoa ziada kwa wajibu, basi kila mwenye akili timamu anahukumu kwamba maneno hayo si sawasawa, inathibitishwa kuwa kauli yake: {na husamehe yaliyo duni ya hilo kwa amtakaye} yaani kwa kutaka na kupendelea si kwa lazima. Kama ikithibitika hivyo, basi inakusudiwa wenye madhambi makubwa kabla ya kutubu, kwa sababu kwa Muutazila kusamehe dhambi ndogo na dhambi kubwa baada ya toba ni wajibu wa kiakili, kisha wakahukumu kuwa dhambi ya shirki kamwe haisamehewi, isipokuwa kwa amtakaye Allah s.w. Kwahivyo makadirio ya aya ni Mwenyezi Mungu anasamehe kila kitu kwa amtakaye isipokuwa shirki. Kwa kuwa aya imejuulisha kwamba chochote husamehewa isipokuwa shirki basi dhambi kubwa kabla ya toba husamehewa.

Mtazamo wa pili: Mwenyezi Mungu Mtukufu amegawa mambo haramu kwa sehemu mbili: shirki na yasiyo shirki. Yasiyokuwa shiriki huingia dhambi kubwa kabla ya toba, na dhambi kubwa baada ya kutubu na dhambi ndogo pia. Ama shirki huhukumiwa kuwa haisamehewi kabisa, na yasiyo shirki yanasamehewa kwa amtakaye. Kwahiyo maana ya aya ilikuwa kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufa anasamehe kila kitu kilicho duni ya shirki kwa amtakaye, na wakati ambapo aya hiyo imethibitisha kwamba Mwenyezi Mungu anasamehe kila kitu kilicho duni ya shirki, basi ni jambo la lazima dhambi kubwa kabla ya kutubu isamahewe pia”.

Wafuasi wa Ibadhi wanategemea katika fiqhi yao juu ya Quraani, Sunna na makubaliano ya wanavyuoni, lakini wanatanguliza hadithi ambazo ni sahihi za mmoja wa wanavyuoni wao, naye ni Al-Rabi ibn Habib, ambazo ameziandika katika karne ya pili ya hijra, na wanazizingatia ni sahihi zaidi kuliko hadithi za Al-Bukhari na Muslim wakikiuka madhehebu manne ya Kisunni.

Wafuasi wa Ibadhi wanakataa kabisa kwamba wao ni miongoni mwa kundi la Al-Khawarij, nao sasa hivi wanakaa nchini Oman, na katika nchi nyingine kama Algeria, na madhehebu yao ya kifiqhi yamekubaliwa na idara nyingi za kielimu, kama Baraza la Utafiti wa Kiislamu, Baraza Kuu la Mambo ya Kiislamu na Baraza la Fiqhi la Umoja wa Nchi za Kiislamu (OIC). Na tafiti nyingi sana zimefanywa kuhusu madhehebu ya Ibadhi katika Chuo Kikuu cha Al-Azhar, pia risala za uzamili na za uzamifu zimegusia misingi ya madhehebu hayo na asili yake.

Miongoni mwa vitabu vya fiqhi vya Ibadhi ambavyo ni muhimu zaidi ni [Al-Mudawanah] kitabu cha Abu Ghanem Al-Kharasani ambacho anazungumzia kupitia maimamu wa Ibadhi masuala ya vitendo kwa njia ya kifiqhi bila ya kutaja mapokezi mara nyingi, hivyo kuna mizozo ya kifiqhi kati ya Ibadhi na Ahlu Sunna kwa sababu ya tofauti ya mfumo, wala siyo kwa sababu ya uadui au migogoro au ubaguzi. Wafuasi wa Ibadhi walikataa kabisa hadithi zinazothibitisha kwamba ni lazima maimamu wakuu wawe kutoka kabila la Quraish, tofauti na Ahlu Sunna, Ibadhi hawana masharti katika Uimamu isipokuwa Uislamu, ucha Mungu, uhuru na ufanisi. Na katika madhehebu yao, mtumwa akiandika mkataba pamoja na bwana wake kuhusu uhuru wake anakuwa huru kuanzia kumalizika kwa mkataba huo, kwa kuheshimu na kutaka uhuru wa binadamu. [Rejea: Sharhu Nil wa Shifaul Alil 12/560].

Inaonekana katika vitabu vya madhehebu ya Ibadhi hutajwa dalili na maelezo ya sababu ya kifiqhi ya masuala yanayotajwa katika vitabu vya watu wengine bila ya kutaja dalili yoyote au taarifa ya wazi.
Miongoni mwa vitabu vyao ni kitabu cha [Kamus Al-Sharia Al-Hawi Turuqaha Al-Wasiah] kitabu cha mwanchuoni Jamil Ibn Khamis Al-Saadi, kiko katika juzuu ya 92, amekitunga katika karne ya kumi na moja, na juzuu zake nyingi zimechapishwa lakini hadi sasa hakijachapishwa kitabu chote. Miongoni mwa wanavyuoni wa madhehebu ya Ibadhi ni Sheikh Mohammed Ibn Yusuf Ibn Atfiyesh kutoka Algeria mwandishi wa kitabu cha: [Sharhu Nil wa Shifaul Alil] ya Dhiauddin Al-Thumaini, chenye juzuu kumi ya vitabu vikubwa.

Zaidi Hitimisho: Madhehebu ya Ibadhi yanatambulika, yana wanavyuoni wake, vitabu vyake, istilahi zake, na njia yake ya kutoa dalili haitofati sana na njia za madhehebu za kifiqhi yanayotambulika, na katika zama zetu hizi inawekezekana kufaidika na Ibadhi kukiwa kuna faida. Madhehebu haya ingawa wafuasi wake ni wachache lakini ni miongoni mwa madhehebu manane yanayokubalika na kufanyiwa kazi.
Na Mwenyezi Mungu anajua.

Share this:

Related Fatwas