Hukumu ya uhamiaji haramu

Egypt's Dar Al-Ifta

Hukumu ya uhamiaji haramu

Question

Ni nini hukumu ya uhamiaji haramu ambao tunauona na tunausikia katika nchi yetu siku hizi?

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:

Uhamiaji katika Elimu ya Makazi,ni kuondoka kwa mtu mmoja au watu wengi kutoka mahali na kuelekea mahali pengine; kutafuta hali bora zaidi ya kijamii, kiuchumi, kisiasa ua ya kidini.

Na uhamiaji huwa haramu: Iwapo utatokea kwa kiwango kisichoruhusiwa na nchi inayohamwa au kuhamiwa au zote mbili, kwa mujibu wa sheria zilizoundwa za kuingia na kutoka, nazo zinaruhusu kuingia mtu fulani katika mipaka ya nchi fulani bila ya nyaraka zozote za kisheria zinazothibitisha kukubali nchi hiyo jambo hilo, na hili hufanyika kwa njia ya kupenya kwa siri, kupitia njia za nchi kavu au za baharini au kwa nyaraka za kugushi, na pia zinaruhusu kuingia kwa nyaraka za muda, kisha kukaa baada ya muda huo kumalizika bila ya kukubalika kisheria.

Na kutokana na hayo; inajulikana kwamba kisheria hapa hapanasibiani nasheria tukufu, bali maana yake ni uwafikiano wa sheria na katiba zinazoupangilia uhamiaji huo baina ya nchi mbali mbali.

Na uhamiaji huu unaitwa kwa majina mengi; miongoni mwa hayo ni: "Uahamiaji wa siri", "Uhamiaji haramu", na "Uhamiaji bila ya Nidhamu", kwa hivyo basi majinahayoyote tofauti yana maanamoja. Na uhamiaji unaokubaliwa huitwa: "Uhamiaji wa Kisheria", au "Uhamiaji wa kinidhamu", Uhamiaji unaozingatia sheria za uhamiaji katika nchi mbili; inayohamwa na inayohamiwa kupitia njia na nyaraka zinazotambulikakisheria.

Uhamiaji kinyume cha sheria unazingatiwa kuwa ni tukio la kimataifa na ni tatizo sugu linalozisumbua nchi nyingi, kutokana na madhara yake yanayofungamana na magomvi mbali mbali ya kiuchumi, kijamii, kitamaduni na kijimbo kwa nchi hizi.

Uhamiaji haramu ambao siku hizi tunauona na tunausikia katika nchi yetu, unakusanya na kupelekea kuwapo kwa kikundi cha uhalifu na ufisadi miongoni mwawahusika:

Kwanza: Ushahidi uliopo kwa yule anaeenda kinyume na kiongozi, na uhalifu huo kutojuzu madamu kiongozi au mtawala huyo hakuamrisha jambo la haramu, basi Mwenyezi Mungu analazimisha utiifu wa viongozi au watawala; anasema; {Enyi mlio amini! Mt'iini Mwenyezi Mungu, namt'iini Mtume na wenye madaraka katika nyinyi. Namkizozana katika jambo basi lirudisheni kwa Mwenyezi Mungu na Mtume, ikiwa mnamuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho. Hayo ndiyo bora zaidi na ndiyo yenye mwisho mwema.} [AN NISAA 59]

Mwanachuoni mkubwa Ibn Ashour amesema katika tafsiri yake [97-98/5, Ch. Adaar Al Tunisia Lilnasher]: "Viongozi wanatokana na umma na wananchi: wao ndio wanaopewa jukumu la kuendesha mambo ya wananchi hao na wanawategemea, na hivyo jambo hili linakuwa kama ni moja ya mambo yao yanayowahusu… Viongozi hapa ni wale wote isipokuwa Mtume S.A.W, ni makhalifa hadi msimamizi wa ngazi ya chini, wakuu wa majeshi, wanachuoni maswahaba na mujtahideen, hadi wataalamu wa zama za mwishoni, na viongozi hao ndio wanaoitwa pia: Ahlul-Halli wal-Iqdi (yaani watu wa kutatua matatizo na wanafunga mikataba ya umma).

Na imepokelewa nawanachuoni sita, kutoka kwa Ibn Omar R.A. kwa yeye na mzazi wake, kutoka kwa Mtume S.A.W. amesema: "Usikivu na utiifu wa mwislamu (kwa kiongozi wake)ni kwa yale anayoyapenda au anayoyachukia, iwapo tu hajaamrishwa maasi, na ikiwa ataamrishwa maasi basi hakuna kusikia wala kutii". Na kuna dalilinyingi za hayo.

Na imetajwa katika vitabu vya wanavyuoni wa madhehebu ya Shafiikwamba Kiongozi anapoamrisha jambo linalopendeza, linalochukiza au lililo halali, basi ni lazima litekelezwe; Imamu Ibn Hajar Al Haitamiy amesema katika fatwa zake za Mambo yafikhi {Al Fatawa Al Fiqhiyah 278/1, Ch, Al Maktabah Al Islamiyah]: "Tamko lao; ni wajibu kumtii imamu kwa yale aliyoyaamrisha iwapo hayaendi kinyume na sheria ya Mwenyezi Mungu. Na ni wazi kuwa lengo lao wanaposema kwenda kinyume na sheria ya Mwenyezi Mungu: ni kuwa anapoamrisha maasi au akakataza jambo la wajibu, na hili limekusanya jambo linalochukiza.Na iwapo imamu ataamrisha hivyo basi ni lazimaagizo lake litekelezwe, kwani wakati huo hakuna kwenda kinyume naye. Kisha uwazi wa maneno yao: kwamba sadaka hugeuka na kuwa wajibu iwapo imamu ataamrisha itolewe.Na hivyo ndivyo ilivyo, lakini uwajibu wake hupatikana kwa kiasi kidogo cha kile kitu chochote kinachoitwa sadaka, kama ilivyo wazi.

Na sababu ya yote hayo ni kuwa utiifu wa kiongozi ni sababu ya kuwa na tamko moja (kwa maana ya kuungana) na maisha yakawa na mpangilio mzuri; basi watu wanapaswa kuwa na marejeo yao wanayoyaamini kwa amri zake; kwa ajili ya kuondosha ugomvi na mgawanyiko. La sivyo, vurugu zitaenea katika mfumo mkuu wa uongozi, na watu watakumbwa na ufisadi mkubwa katika dini na dunia yao.

Kiongozi wanchi anatakiwa kuweka sheria ambazo anaona kuwa zitakuwa na masilahi kwa watu na kuyafikia masilahi hayo: na utendaji wa Kiongozi kwa anaowaongoza unayaangalia masilahi yao, na ni wajibu wa anaowaongoza kumtii na kupigana kwa ajili yake, na anayetaka kuhama kutoka nchi mpaka nyingine, basi anapaswa kufuata sheria zanazokubalika baina ya nchi husika katika mambo hayo ambayo kiongozi ameamurishayafuatwe na akakataza kwenda kinyuma nayo, kwa hiyo ni lazima kumtiipale anapoamrisha, na hautajuzu uahamiaji wowote nje ya utaratubu huu uliopangwa.

Kipengele cha sheria namba ya 97 ya mwaka wa 1959 iliyofanyiwa marekebisho ya sheria namba ya 78 ya mwaka wa 1968 kuhusu pasipoti au hati za husafiria, imetaja kuwa haijuzu kwa mmisri yeyote kutoka nje ya nchi au kururejea, isipokuwa awe na pasipoti yake na ni kutoka maeneo maalumu yaliyokusudiwa na piaiwe na viza.Namtu yeyote anaeenda kinyume na utaratibu huu huadhibiwa kwa mujibu wamaamuzi ya katiba hiyo,adhabu ya kifungo cha muda usiozidi miezi mitatu na faini isiyopindukia paundi hamsini.

Pili: Ni ile hali ambayo, baadhi ya sura zake huwa ni kujihatarishia maisha kwa kuwepo hatari za aina mbali mbali na maangamizi,kinyume cha sheria, ambapo wahamiaji huthubutu kupanda majahazi yasiyo na vibali vya kusafiria baharini kutokana na ukuukuu wake. Ingawa hayafai, majahazi hayo hubeba zaidi ya uwezo wake na kupita katika mawimbi makali ya hatari ya baharini – ambapo mabaharia huyakwea katika hali za kawaida - kwa ajili ya kukwepa wanausalama wanaozichunga pwani za bahari. Wao, kwa mwenendo huo, wanaziangamiza roho zao ijapo kuwa wanajua hatari ya njia hii.Wao kwa njia hii wanacheza pata potea kwa roho zao na kwa kujua wanachokifanya, huku wakijua fikapia kuwa chombo wanachosafiria ni kibovu na kinaweza kuzama.Kisha ung’ang’anizi wao wa kukipanda chombo hicho baada ya kuyajua hayo yote, jambo ambalo linawafanya kuwa wazembe wa kuzilinda nafsi zao na wanazihatarishakwa kutaka kuziangamiza. Wanachuoni wameafikiana kuwa iwapo bahari itaonekana kuwa inaweza kuangamiza basi haijuzu kusafiri katika bahari hiyo. Alhaafidh Bin Abdulbarry anasema katika kitabu chake cha Atamhiid 234/1, Ch. Wizara ya mambo ya Waqfu ya Morocco]. Na wala wanachuoni hawatofautiani kuwa bahari inapochafuka haijuzu kwa mtu yeyote kusafiri kwa njia hiyo,kwa vyovyote vile wakati inapochafuka ni hatari mno.
Na kuilinda nafsi ni moja kati ya makusudio au malengo makuu matano ya sheria ya kiislamu ambayo ni yote ni ya kiwangocha mambo ya dharura, na kuna matini nyingi za Sheria zilizokuja kukataza au kuzuia uhatarishaji wa nafsi katika kutaka kuiangamiza.

Na hifadhi ya nafsi ni kusudio moja miongoni mwa makusudio matano ya sheria ambayo yanakuwa katika kiwango cha madharura, na matni za kisheria zilikuja katika kukataza kuangamiza nafsi; miongoni mwao ni tamko la Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na toeni katika njia ya Mwenyezi Mungu, walamsijitie kwa mikono yenu katika maangamizo. Na fanyeniwema.Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wafanyao wema.} [AL BAQARAH 195].

Mtaalmu mkubwa Ibn Ashuor akaema katika tafsiri yake [214/2, Ch. Adaar Al Tunisia Linashri, Tunesia]: "Na maana ya kuzuiwa kujiangamiza kwa mikono ya mtu ni kuzuia kusababisha uangamizaji wa nafsi au watu kutokana na kuwapo uhakika wa kuangamia bila ya kujiepusha nao kwa makusudi"

Na kadhalika tamko la Mwenyezi Mungu Mtukufu pia: {Enyi mlio amini! Msiliane mali yenu kwa dhulma,isipo kuwa iwe biashara kwa kuridhiana wenyewe. Walamsijiuwe. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenyekuwarehemun} [AN NISAA 29], Imamu Al Qurtubiy akasema katika tafsiri yake [156-157/5, Ch. Dar El Kutub Al Masriyah]: "Wafasiri wamekubaliana kuwa maana ya aya hii: ni kukataza watu wasiuwane. Baada ya hapo, tamko lake linazungumzia kuwa mtu ajiuwe yeye mwenyewe kwa makusudi kwa sababu tu ya kuitaka Dunia na mali, ni kwamba aitumbukize nafsi yake katika hali ya kuangamia".

Tatu: Yaliyomo katika aina hii ya uhamiaji kama vile mwislamu kujidhalilisha yeye mwenyewe, kwani kuingia nchi ya kigeni kwa njia isiyotambulika huwafanya wahamiaji wa aina hii kuwa chini ya ufuatiliaji endelevu unaofanywa na maafisa wa nchi husika, Basi, kwa hiyo mtu huwa hatarini kukamatwa na kuadhibiwa, pamoja na yale ambayo wahamiaji wengi kinyume cha sheria hulazimika kuyafanya na kuchafua sifa zao na za nchi zao, bali wakati mwingine sura yao huchafuliwa kama vile kuwa omba omba na kuwashambulia watu barabarani.

Na Mtume S.A.W. amemzuia mwislamu kuwa ajidhlilishe, basi inapokelewa na Atarmiziy –na anaiporesha- kutoka kwa Huzaifah Bin Al Yamaan R.A. kutoka kwa Mtume S.A.W. akasema: "Muumini wa kweli hapaswi kujidhalilisha. Wahenga wanasema: mtu hujidhalilisha vipi? Akasema: "Ni pale anapojitumbukiza katika janga asiloliweza".

Na Al Ttabaraniy amesimulia katika kitabu cha [Al Awsat] kutoka katika hadithi ya Abi Dhari R.A. akasema: Mtume S.A.W. akasema: "Yeyote atakaejidhalilisha yeye mwenyewe kwa kutaka na bila yakulazimishwa basi si katika sisi".

Nne: Yaliyomo katika uhamiaji wa aina hii ni kama ukiukaji wa mikataba ya kimataifa ambayo inapangilia uingiaji na utokaji kati ya nchi na nchi nyingine, kwa hivyo basi, Imamu Atirmidhiy amepokea katika kitabu chake cha Sunna, na akasema: -"ni bora na sahihi"- kutoka kwa Amro Bin Auf Al Mazniy R.A. kuwa Mtume S.A.W. anasema: "Waislamu hufuata miongozo yao ispokuwa mwongozo wa kuharamisha halali, au kuhalalisha haramu", Al Munawiy akasema katika maelezo yake kwa hadithi hiyo katika kitabu cha [Fayidh Al Qadeer 272/6, Ch. Al Maktabah Al Tujaria Al Kubra]: "(Waislamu hufuata miongozo yao) ambayo inajuzu kisheria; yaani: wana uhakika nayo na wanaisimamia kidete. Na hii ni dalili ya ubora wao wa hali ya juu. Na katika kuwasifu kwa Uislamu, kuna hali inayowalazimishia wao kutekeleza masharti na kuwahimizia wafanye hivyo."

Tano: Yanayokuwa katika baadhi ya sura zake kama vile kudanganya, kugushi na kuchanganya kunakofanywa na wahusika wa nchi mbili, inayohamwa na inayohamiwa. Na hili ni katika aina za uwongo: nao ni kutoa maelezo tofauti na ukweli ulivyo, na asili yake ni haramu. Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: {Ndio hivyo iwe! Na anaye vitukuza vitakatifu vya Mwenyezi Mungu basi hayo ndiyo kheri yake mbele yaMola wake Mlezi. Na mmehalalishiwa nyama hoaila wale mlio somewa. Basi jiepusheni na uchafu wa masanamu, najiepusheni na usemi wa uwongo.} [AL HAJI 30], na katika aya hiyo ni agizo la wazi kwa ajili ya kujiepusha na uwongo.

Imamu Muslim amepokea katika kitabi cha sahihi kutoka kwa Abuu Hurairah R.A. kutoka kwa Mtume S.A.W. anasema: "Mtu yeyote atakaetufanyia udanganyifu si katika sisi"

Sita: Mara nyingi Uhamiaji kama huu huwa unaambatana na ushirikiano kwa ajili ya maasi, ambapo mhamiaji anaweza kumwendea yule anayemtengenezea hati bandia za kusafiria au kwa yule anaemsaidia kufika na kuingia katika nchi lengwa kwa njia angamizi, kila mmoja kati ya wasaidizi hawa ana fungu lake maalumu la fedha. Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: {Na saidianeni katikawema na ucha Mngu. Wala msisaidiane katika dhambi nauadui. Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Munguni Mkali wa kuadhibu.}.

Al Hafedh Ibn Katheer amesema katika tafsiriya aya hiyo [106/2, Ch. Dar Ttebah]: Mwenyezi Mungu Mtukufu anawaamrisha waja wake waumini kushirikiana na kufanya mambo ya heri. Nayo ni: kutenda wema, kuacha yanayokatazwa, kwa njia ya Uchamungu, na anawazuia kusaidiana katika jambo lililo batili na kushirikiana katika madhambi na mambo yaliyoharamishwa.

Na sababu hizi zote kwa pamoja, zinaweza zikakusanyikakatika sura moja, na baadhi yake zinaweza kutokuwapo, lakini yoyote kati ya sura hizi za uhamiaji kinyume cha sheria haiepuki ufisadi ndani yake, na kufanikiwa kwa yoyote kati ya sura hizikunatosha kuzuia na kuharamisha.

Kutokana nayaliyotangulia, tumeona kuwa uhamiaji haramu kwa namnaunavyotokea katika nchi yetu hivi sasa, haujuzu kisheria kuufanya au kuujongelea.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni mjuzi zaidi ya wote.

Share this:

Related Fatwas