Hukumu ya Kujifunza Mantiki

Egypt's Dar Al-Ifta

Hukumu ya Kujifunza Mantiki

Question

Ni ipi Hukumu ya kujifunza Elimu ya Mantiki? Na je, Ni sahihi kwamba Elimu ya Mantiki ni miongoni mwa Elimu zinazotajwa vibaya ambazo wema waliotangulia wameonya kuhusu elimu hizo?

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Elimu ya Mantiki inatambulishwa kama: Ni"Chombo cha kisheria ambacho kinailinda akili ya mwenye kukichunga na makosa katika kufikiri". [Tahrir El Qawaed Al Mantikia Fiy Shareh Al Resalah Al Shamsia, Uk. 12, Ch. Al Mttbaa Al Azhariya], Na elimu ya Mantiki inaitwa kwa majina mengi na miongoni mwayo ni: sanaa ya mtazamo, kipimo cha akili, na kigezo cha elimu.
Hakika Mantiki ni kundi la sheria za kiakili ambazo zikizingatiwa na mwanadamu katika kufikiria na kujenga mawazo, basi ataweza kufikia matokeo sahihi bila ya makosa. Nayo, kwa zingatio hili, ni elimu isiyotajwa vibaya kwa upande wa kuwa kwake Elimu, bali hutajwa vibaya kwa kuzingatia matumizi yake, na sio misingi na sheria zote za Mantiki ni za kimaumbile bali ipo miongoni mwake ambayo ni ya lazima na haihitaji kutazama na kuzingatia, na miongoni mwake iko ya kinadharia tu inayohitajia kuzingatia na kutanabahika.
Na kuhakiki kuwa kilichonukuliwa miongoni mwa utajo mbaya wa kujifunza elimu ya Mantiki na uonyaji dhidi yake ni jambo linalohusu Mantiki iliyochanganyika na maneno ya Wanafalsafa walio batili, basi Mantiki inayochanganyika kwa maneno ya wanafalsafa ina hitilafu katika maumbo matatu; Sheikh Al Akhdhariy aliyaashiria katika tamko lake:
Na Waliofuatia katika kujuzu kuitumia kwake juu ya matamko matatu.Basi Ibn Al Sasalah na An Nawawiy waliiharamisha na watu Fulani walisema lazima ifundishwe.Na tamko mashuhuri na sahihi ni kujuzu kwake kiukamilifu,kwa mwenye kuitumia kupitia Sunna na Kitabu, ili aongoke na kuuelekea usahihi.
Sheikh Al Damanhuriy amesema akieleza: "Na ujue kuwa tofauti hii hakika ni kwa upande wa Mantiki iliyoingiliwa na maneno ya Falsafa. Ama upande wa Mantiki iliyo safi basi hakuna tofauti ya kujuzu kuitumia, bali haiwi mbali na kuwa kuitumia kwake ni Faradhi ya Kutoshelezeana; kwa kusimamia kujua mshabihiano juu yake na miongoni mwa ile hukumu iliyojulikana kuifanya iwe Faradhi ya Kutoshelezeana."[Idhaah Al Mubham Min Maani Al Silm. Sheik Al Damanhuriy, Uk. 5, Ch. Mustafa Al Halabiy].
Na Tamko la Kwanza; ni Kuharamisha, na hili ni chaguo la Al-Imama Bin Al-Salaah, na An-Nawawiy, na Ibn-Taimia na lilisimuliziwa na AS-Suyutiy kutoka kwa wanavyuoni wengi. [Al Haawiy Lilfatawiy, 300/1, Ch. Dar Alfikr].
Na ilisemekana kuwa sababu ya kuharamisha Mantiki kwa Imam Bin Al-Salaah Kwamba hupelekea kiburi, kwani mwenye kuijua Elimu hii, hoja zake zitakuwa na nguvu na akawa na ulimi mrefu juu ya wengine, na hivyo kusababisha kiburi na majivuno yake. Na kiburi na majivuno ni miongoni mwa magonjwa ya nyoyo, na magonjwa ya nyoyo ni haramu,kwa hivyo basi, ni haramu kwa mwanadamu kujifunza Elimu hiyo. [Tazama Fatwa za Al-Subkiy, 644/2, Ch. Dar Al-Maarif.]
Na huu utoaji sababu hauishii tu katika kujifunza Elimu ya Mantiki tu, bali huwa pia katika Hadith, Nahau, Swarfu na pia katika elimu nyingine zote. Kwa hivyo elimu zote nyingine, mtu yeyote atakaejifunza bila ya malezi na matunzo na shime ya uchamungu katika kujifunza kwake elimu hiyo, basi hupelekea kiburi na majivuno.
Inasemekana kwamba sababu ya kuharamishwa Elimu ya Mantiki kwa Imamu An-Nawawiy, Kwamba Elimu hiyo inaibua mkanganyo mwingi wa kiakili na huzichokesha akili na kuzitumikisha kwa yasiyokuwa muhimu, na madhehebu yake yanaona kuwa ni haramu.
Na sehemu ya uletaji sababu ni hii Mantiki iliyochanganyika na maneno ya wanafalsafa yaliyobatili, kwani ndani yake kuna mkanganyo unaompelekea muhusika katika upotofu iwapo hakuwa akiitumia katika Qur-ani na Sunna, na wala hana Akida sahihi.Lakini aliyeitumia katika Qur-ani na Sunna na mwenye akida sahihi, mwenye ufahamu safi basi anaweza kujifunza Elimu ya Mantiki yenye kuchanganyika na maneno machafu ya wanafalsafa ili azirudi hoja za wenye kubatilisha kwa jinsi walivyotafuta dalili kwa elimu hiyo, na kwa kuwashinda kwa dalili zao hizo hizo, na kwa kuwa kujifunza kwake ni kwa lengo la kuondosha mkanganyo katika Dini, basi hoja ya kuwa ni upuuzi inaondoka., basi unaondoshwa kuharamisha kwake bali labda ni lazima juu yake kujifunza Mantiki.
Na yaliyotungwa na Sheik Ibn-Taimia katika kuwajibu wenye Elimu ya Mantiki, basi yeye hakuwajibu isipokuwa baada ya kujifunza Mantiki na kujua misingi yake; Kwani yeye alitaka kutengua kupitia misingi yake, na ambayo aliifikia baada ya hapo, ni kuwapo tu kwa mibadala ya kimantiki iliyopitishwa ili iwe mibadala ya misingi ambayo imewekwa na wataalamu wa Mantiki kabla yake, alichokifikia ni Mantiki tu lakini kwa mtazamo mwingine.
Na Tamko la Pili; kwamba ni lazima Elimu hii ifundishwe, na huu msimamo ulisimuliwa na Imamu Al-Ghazaliy katika utangulizi wa Al-Mustafa, "Na utangulizi huu si katika ujumla wa Elimu ya Misingi na wala miongoni mwa tangulizi zake maalumu, bali ni Utangulizi wa Elimu zote, na asiyejifunza Elimu hiyo vizuri basi kiasili haaminiki kwa elimu zake hizo. [Al Mustasfa, Uk. 10, Ch. Dar Al Kutub Al Elmiyah].
Na yaliyosemwa na Al Imamu Al Ghazali nao wanavyuoni kadhaa baada yake walisema, kama vile; Al Amadiy, Al Baidhawiy na Ibn Al Haajib, na idadi kadhaa miongoni mwa maimamu wa Uislamu, na tamko lake katika amani (lazima) Al Sheikh Al Malawiy alitaja katika Sharh yake: "Hakika yenyewe inaweza kuwa na maana ya kuwa wajibu wa kutoshelezeana au yaweza kuwa kwa maana ya Inapendeza". [Sharh Al Salm kwa Sheikh Al Malawiy, Uk. 40, Ch. Mustafa Al Babiy Al Halabiy].
Tamko la Tatu: ni maelezo; Inajuzu kujifunza kwa mwenye ukamilifu wa Uelewa wake, mwenye kuipitia pitia Sunna na Quraani kwa namna ambayo anazijua Imani kwa kuzitenganisha na Imani potofu. Ama kwa yule ambae Uelewa wake haujakamilika na hajawahi kuitumia Qur-ani na Sunna basi haijuzu kwake kujishughulisha na Mantiki.
Na sehemu ya kauli hizi kama tulivyokwishasema hapo awali katika Mantiki iliyochanganyika na maneno ya wanafalsafa, ama kwa upande wa Mantiki ambayo wanazuoni wa Kiislamu waliitunza na kuitumia kwenye vitabu vyao nayo haina maneno ya wanafalsafa kilichochaguliwa katika hukumu ya kujifunza kwake ni faradhi ya kinachosimama juu ya wajibu na chenyewe pia ni wajibu.
kutoshelezeana kwa yule aliyejikita katika kuulinda Uislamu; kwani Uwezo wa kuzirudi Shubuhati haupatikani isipokuwa kwa elimu hii, na kuzirudi Shubuhati hizo ni faradhi ya kutoshelezeana, na kile kinachosimama juu ya wajibu na chenyewe pia ni wajibu.
Nayo ni Mustahabu kwa wale wenye kujishughulisha na elimu za Sheria, kwa sababu asiyekuwa nayo hawezi kutofautisha kati ya Elimu sahihi na elimu mbovu, wala hawezi kuzipata elimu kiukamilifu, na pia husaidia kuifahamu vyema misamiati ya Mantiki iliyotumiwa na wanazuoni katika vitabu vyao. Basi vitabu vimetangaza vikiathirika kwa elimu hiyo katika Usulu Al-Fiqhi, Fiqhi, na Elimu ya Hadithi, na katika Elimu za Lugha; kama vile Nahau, Sarufi na Balagha, na hayumkini kufahamu elimu hizi tofauti na wala kuwahi kuunda baadhi yake juu ya nyingine, isipokuwa kwa kujua istilahi za kimantiki.
Na Al Shehaab Bin Hajar Al Haithamiy alinukulu katika fatwa zake kutoka kwa Al-Qarafiy Al-Malikiy kuzingatia kwake kwamba Elimu ya Mantiki ni moja kati ya Masharti ya kujitahidi, na kwamba mwenye kujitahidi akiwa hana Elimu hii basi hupokonywa jina la mwenye kujitahidi. [Tazama Al Fatawa Al Fiqhiyah Al Kubra, 51/1, Ch. Al Maktabah Al Islamiyah]
Na kutokana na yaliyotangulia; Basi ni kwamba kujifunza Elimu ya Mantiki ambayo inamsaidia mwanadamu juu ya kufikiria na kujenga mawazo sahihi, inamfanya aweze kufikia matokeo sahihi bila ya makosa, kwa ajili hii basi hiyo ni halali. Lakini kujifunza Mantiki iliyochanganyika na maneno potofu ya wanafalsafa, basi hiyo ina hitilafu baina ya wanavyuoni katika maumbo matatu kama tulivyoyaelezea hapo juu.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi ya wote.

Share this:

Related Fatwas