Mwanamume Humwosha Mama yake

Egypt's Dar Al-Ifta

Mwanamume Humwosha Mama yake

Question

Je. Inajuzu kuwa mwanamume kuuosha mwili wa mamake aliyefariki?

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Mada ya uoshaji katika kugha ya Kiarabu inamaanisha kukisafisha kitu na kukitakasa. Na ukoshaji ni maana pevu zaidi katika kuosha viungo vyote na kisheria ni kuyachuruzisha maji juu ya mwili mzima kwa kuwapo nia ya kufanya hivyo. [Rejea kidahizo cha Ghasal katika Muajam Maqaiys Al Lugha kwa Ibn Fares 242/4, Ch. Dar Al Fikr, na Taj Al Arus kwa Az Zubaidiy 102/30, Ch. Dar El Hidayah].
Na Kisheria ni kumiminika maji juu ya mwili mzima pamoja na nia. [Tazama: Mughniy Al Muhtaaj kwa Al Khatweb As Sherbiniy 2i2 /1, Ch. Dar Al Kutub Al Elmiyah]
Na kumuosha maiti na kumzika ni faradhi ya kutoshelezeana ambapo watakapoifanya baadhi ya watu basi jukumu lake litafutika kwa wengine pia. Ad Darderiy amesema katika kitabu cha [As Sharhu Al Kabeer kwa Muhtasari wa Khalil]: "Na Swala juu yake ni faradhi ya kutoshelezeana kama vile kumzika na kumvika sanda" [As Sharahu Al Kabeer 407/1, Ch. Eisa Al Halabiy].
Na Al Bukhariy alisimulia kutoka kwa Hadithi ya Umm Atia Nasibah Al Nsaariyah, kwamba akasema: Binti mmoja miongoni mwa mabinti wa Mtume S.A.W. alikufa, basi alijitokeza na akasema: "Mwosheni mara tatu au mara tano au zaidi ya idadi hiyo iwapo mtaona hivyo, kwa maji na majani ya mkunazi, na mlifanye josho la Mwisho liwe kwa kafuri au kitu kinachotokana na kafuri"
Na Abu Dawud alipokea kutoka kwa Al Hasswen Bin Wahawah kuwa Twalha Bin Al Baraa alipata ugonjwa basi Mtume S.A.W. alikuja kwake kwa ajili ya kumhudumia na akasema: "Mimi simuoni Twalha isipokuwa amepatwa na umauti, basi nipeni idhini mimi kwa ajili yake na muharakishe kwani haifai kwa mfu mwislamu afungiwe kati ya pande mbili za watu wake"
Na asili katika kumwosha mwanamke kuwa hamwoshi mwanamke isipokuwa mwanamke mwenzake, kwani Mwenyezi Mungu Mtukufu aliharamisha kutazama uchi wa mwanamke na kumgusa mwili wake. {Waambie Waumini wanaume wainamishe macho yao, na wazilinde tupu zao. Hili ni takaso bora kwao.} [An Nuur 30] Na Atwbaraniy imepokewa kutoka kwa Maqal Bin Yasaar Al Mazniy: "Ni bora kwa mtu achomwe kwa sindano ya chuma katika kichwa chake kuliko kumgusa mwanamke asiye halali kwake."
An Nawawiy alipokea katika kitabu cha [Raudhat At Twalibeen] "Basi kwa hiyo asili ni kwamba wanaume wawaoshe wanaume wenzi wao na wanawake wawaoshe wanawake wenzi wao ni bora zaidi kuliko mwanamke kuoshwa kwa hali zote nyingine" [Raudhat At Twalibeen kwa AN Nawawiy 105/2, Ch. Al Maktab Al Islamiy]
Na Kama hawakuwepo wanawake wa kumwosha mwanamke mwenzao, basi ndugu wa karibu kama vile mwanae au kaka yake amwoshe, kwani ana haki ya kumwangalia, na inajuzu kumgusa katika uhai wake, isipokuwa uchi wake kutoka kitovuni mpaka gotini katika upande wa mbele wa mwili na upande ya nyuma yake, na hali hii ya kujuzu haikatishwi na kifo na ni bora zaidi asiuguse mwili wake, na kwa sharti la kutomgusa kwa mkono mtupu isipokuwa kwa kitambaa kizito atakachokizungushia mkononi mwake na atamwosha akiwa chini ya nguo ili izuie kumwangalia.
Al Kharashiy alisema alipokuwa akitaja utaratibu wa wanaojuzu kumwosha mwanamke: "Kisha atamwosha na ndugu wa karibu katika wanaume, chini ya kitambaa kizito atakachokizungushia mkononi mwake na atamwosha akiwa chini ya nguo ili izuie kumwangalia na hamgusi kwa mkono wake." [Sharh Al Kharashiy juu ya Muhtasari wa Khalil 117/ 2, Ch. Dar Al Fikr].
Asheikh Ad Darder amesema: "Kisha iwapo hakupatikana mwanamke asiye ndugu basi maiti wakike ataoshwa na ndugu zake wa karibu na atalazimika kumsitiri mwili mzima na wala hapitishi mikono yake katika kumsugua isipokuwa kwa kitambaa kizito anachokizungushia mkononi mwake yeye mwoshaji na kusugulia kwacho [As Sharhu Al Sagheer 546/1, Ch. Dar Al Maarif].
Imamu An Nawawiy alisema: "Na asili ni kwamba mwanaume amwoshe mwanaume mwenzake, na wanawake kwa wanawake; na wanawake ni bora zaidi kumwosha mwanamke mwenzao kwa hali zote, na mwanaume halazimiki kumwosha mwanamke isipokuwa kwa sababu tatu: ya kwanza ni: ndoa, kwa hivyo, anapaswa kumwosha mke wake mwislamu au dhimiya asiye mwislamu. Na mke pia anapaswa kumwosha mumewe hata kama alimwoa dada yake au wanawake wanne kwa usahihi wake. Na sababu ya Pili ni undugu wa karibu: na uwazi wa maneno ya Ghazali ni kuwa inajuzu kwa wanaume ndugu wa karibu kumwosha mwanamke pamoja na kuwepo wanawake lakini sijaona maswahaba kwa ujumla wakilizungumzia hili jambo. Isipokuwa wao wanalizungumzia kwa utaratibu na wanasema: Ndugu wa karibu baada ya wanawake ni bora zaidi. Na sababu ya tatu ni umiliki wa kijakazi. [Raudhat Atwalibeen kwa An Nawawiy 103-104/2, Ch. Al Maktab Al Islamiy]
Na juu ya hayo: Asili ni kwamba mwanamke haoshwi isipokuwa na mwanamke mwenzake lakini wanapokosekana basi huoshwa na ndugu zake wa karibu katika wanaume na kwa hivyo: inajuzu kwa mwanaume kumkosha mama yake: kwa sharti tu kwamba asimguse kwa mkono wake isipokuwa kwa kitambaa kizito.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni mjuzi zaidi ya wote

Share this:

Related Fatwas