Kuirejearejea Swala ya Jeneza

Egypt's Dar Al-Ifta

Kuirejearejea Swala ya Jeneza

Question

Mtu mmoja akifariki dunia nje ya nchi yake, basi marafiki na jirani zake humtayarisha na humswalia pale alipofia. Na iwapo atapelekwa kwa mji wake ili kumzika, basi jamaa zake watamswalia tena. Basi, je, inajuzu kurejearejea swala ya maiti?

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Sura hii inajulikana katika vitabu vya Fiqhi kuwa katika mlango wa Swala ya Jeneza, kama ni kurejea rejea kumswalia maiti.Na hukumu ya kurejea huko ni kuchukiza, isipokuwa kwa haja kama vile kwa mtu aliyepitwa kwa ajili ya swala ya jeneza, na hasa iwapo mtu huyo ni walii wa maiti, au amefika yule mnayezitarajia Baraka zake miongoni mwa watu bora na wema. Na yeyote atakayepitwa na swala miongoni mwa mfano wa watu hawa hadi maiti ikazikwa basi anaweza kuliswalia kaburi lake.
Na dalili ya hayo, ni kwamba Mtume S.A.W. alimswalia maiti baada ya kumzika. Na haisemwi kuwepo kwa umaalumu hapo; kwani kama ingelikuwa ni kwa ajili ya umaalumu huo basi maswahaba wasingeliacha kuswali pamoja naye. Na kuna Hadithi kadhaa zimetajwa katika mambo hayo, miongoni mwake ni zile ziliyokuja katika vitabu viwili sahihi kutoka kwa Abi Hurairah alisema: "Mtu mmoja mweusi, au mwanamke mmoja mweusi alikuwa akija msikitini mara kwa mara, baada ya kupita muda mrefu mtu huyo akafa, na Mtume S.A.W. akamuulizia, maswahaba wakasema: amekufa, Mtume akasema: kwanini msiniambie kuwa amekufa? Nionesheni kaburi lake, akaliendea kaburi lake na akaliswalia".
Al Khatwabi amesema: "Na ndani yake kuna ubainishaji wa kujuzu swala ya jeneza kwa yule ambaye hakuiwahi swala hiyo kabla ya mazishi". [Maalem Al Sunan 315/1, Ch. Al Matwbaah Al Elimiyah, Halab]
Na Ibn Hajar Amesema: "Na ndani yake kuna kuzawadiwa kwa dua na kwa kuhimiza katika kuyashuhudia majeneza ya watu wema na kukokotezewa kuwaswalia maiti waliopo na pia kuyaswalia makaburi yao kwa yule ambaye hajawaswalia maiti hao". [Fatih Al Baariy 553/1, Ch. Dar Al Maarifah]
Ama kwa upande wa chukizo ni kwamba kukariri bila ya haja ya kufanya hivyo hakujanukuliwa kutoka kwa waliotutangulia, na ni kwa sababu haikuzoeleka katika sheria yetu ya Kiislamu kuifanya hii kuwa Sunna kwa jinsi ilivyo.
Na kama tulivyotaja, upande miongoni mwa wasomi wamesema:
Ibn Habaan amesema: "Kutaja Hadithi inayomaanisha kuwepo kwa sababu ya Mtume S.A.W. kuyaswalia makaburi haikuwa dua yake peke yake bila ya dua ya umma wake. Imraan Bin Musa Bin Mujashe alituambia akasema: Othmaan Bin Abi Shaibah alituzungumzia akisema: Hasheem alituzungumzia akasema kuwa: Othmaan Bin Hakeem Al Answariy alituzungumzia akisema kutoka kwa Kharijah Bin Zaid Bin Thabit kutoka kwa ami yake Yazid Bin Thabit na alikuwa ni mkubwa zaidi kuliko Zaid alituambia: "Tulitoka tukiwa na Mtume S.A.W. na tulipofika Baqiiu tukalikuta kaburi moja, Mtume akaulizia kuhusu maiti huyo, wakasema: ni la mtu Fulani. Akamtambua na kusema: kwanini msinijulishe kuhusu mtu huyu? Wakasema: wewe ulikuwa na saumu na ulikuwa ukipumzika, akasema: mimi nilikuwa najisemea moyoni mwangu: akasema: msifanye hivyo, kwa nini mimi nisimjue aliyekufa miongoni mwenu, kama sikuwa pamoja na nyinyi basi nijulisheni aliyekufa, kwani swala yangu juu ya maiti huyo ni rehma. Akasema: kisha akalijia kaburi hilo akatupanga safu nyuma yake na kutoa takbira nne".
Abu Haatem R.A. akasema: "Kwa mtu asiyebobea kielimu anaweza kuwaza kuwa kuyaswalia makaburi sio jambo linalojuzu kwa tamko ambalo amelitoa Abuu Huraira: (hakika Mwenyezi Mungu huwapa nuru kwa kuwaonea huruma wafu kutokana na swala zangu)". Na tamko lililokwepo katika Hadithi ya Yazid Bin Thabit ni "Kwani swala yangu ni rehma juu yao".
Na sababu sio kile kinachofikiriwa na wale wenye kufikiria ndani yake kuwa uhalali wa sunna hii ya Mtume S.A.W. ni maalumu kinyume na Umma wake, kwani kama ingelikuwa hivyo angeliwakemea Mtume S.A.W. na kuwataka wajipange safu nyuma yake na wakayaswalia makaburi pamoja naye. Kwani katika kutokuzuia kwake S.A.W. kwa kuchukiza kwa yule aliyeyaswalia makaburi kuko wazi zaidi kwa yule aliyewafikishwa na Mwenyezi Mungu kwa ajili ya uongofu na usahihi kwamba yeye alifanya hivyo na ni halali kwake na kwa Umma wake kwa pamoja bila ya kuwa kitendo hicho ni kwa ajili yake pekee kinyume na Umma wake. [Sahihi ya Ibn Hayaan 356/7, Ch. Dar Al Resalah]
Ashaafiy amesema: "Iwapo mtu awe walii wa maiti au asiwe walii wa maiti, atakahudhuria akiwa na wanawake kwa ajili ya maiti mwanaume au mwanamke basi ana haki ya kumswalia kuliko wanawake iwapo atakuwa na akili ya kuitambua swala hiyo, na ikiwa bado hajabaleghe au anamilikiwa au yuko huru, na kama haitambui swala kiakili basi wanawake hao wataiswalia maiti hiyo wakiwa safu moja au mmoja mmoja, na hata kama mmoja wao atawaongoza katika swala hiyo, na akasimama katikati yao, mimi siuoni ubaya wowote wa kufanya hivyo". Kwani watu walimswalia Mtume S.A.W. kila mtu peke yake (mmoja mmoja) bila ya imamu kuwa mbele yao.
Na hiyo ni kutokana na utukufu wa jambo la Mtume S.A.W. na kushindana kwao juu ya kwamba asishikilie jukumu la uongozi wa swala mtu mmoja, na wakamswalia mara nyingi, na ni Sunna ya Mtume S.A.W. kwa wafu, na jambo hili linafanyika hadi leo. Na hii ni kwamba watu waswalishwe na imamu, na kama watamswalia maiti watu mmoja mmoja, swala zao zitaswihi na kuwatoshelezea kwa utashi wa Mwenyezi Mungu. Na inapendeza zaidi kwa swala ya maiti iwe moja, na hivi ndivyo nilivyowaona watu wakiswali, na hakuna yeyote baada ya kumalizika kwa swala hiyo, anaekaa kwa ajili ya kuiswali baada yakumpita swala hiyo, na kama atakuja walii wa marehemu na hapaogopewi kuharibika kwa maiti na kisha akamswalia maiti, natamani kuwa hivyo hakuna ubaya wowote kwa utashi wa Mwenyezi Mungu. [Al Umm kwa Imamu Ashaafiy 244/1, Ch Bulaaq]
Na Al Khatweb Asherbiniy amesema: "Na swala hii sio ya kujitolea. Imesemwa katika kitabu cha Almajmuui: maana yake ni kuwa haijuzu kuanza kwa sura yake hiyo bila ya kuwapo jeneza kinyume cha swala ya adhuhuri ambayo inakuja kwa sura yake ya kuanza bila ya sababu yoyote". Kisha akasema: "Lakini waliyoyasema yanatenguka kwa swala ya wanawake pamoja na wanaume, kwani swala hiyo kwao ni Sunna, na hivi ndio sahihi"
Na Azarkashiy amesema: "Maana yake ni kuwa, yeye haifanyi mara moja baada ya nyingine, kwa maana kuwa yule atakaeiswali swala hii hairejei tena, na wala hatakiwi kufanya hivyo, lakini itakuja kwamba lau aliirejea basi itakuwa sunna kwake. Ni kama vile jambo hili limetengeka kwa kauli yao: hakika swala isiyotakiwa haituki. Ama kama mtu ambaye hajamswalia maiti hapo mwanzo, akamswalia basi faradhi itatuka kwake". [Mughniy Al Muhataaj 27/2, Ch. Dar Al Kutub Al Elmiyah]
Kisha baada ya hayo akasema: "(Na iwapo atamswalia maiti) na akawepo yule ambaye hakumswalia mwanzo, akimswalia basi hiyo ni Sunna kwake. Kwani Mtume S.A.W. aliyaswalia makaburi ya wengi. Na inavyoeleweka ni kwamba wao walizikwa baada ya kuswaliwa, na swala hiyo inatuka kama ni faradhi kama vile ya mwanzo, ni sawa sawa ilikuwa kabla ya mazishi au baada ya mazishi, anaeswali atanuia faradhi kama ilivyoelezwa katika Almajmuui kutoka kwa Mutawalliy, na atapata thawabu za swala hiyo ya Faradhi. Na aliyeiswalia maiti akiwa peke yake au katika swala ya jamaa, basi asiiswali tena, yaani sio Sunna kuirejea; Kwani swala ya jeneza haigeuki na kuwa Sunna, na ya pili, inakuwa Sunna, ndio. Asiye na twahara mbili atakaposwali kisha akayapata maji atajisafisha kwayo, na hakika yeye atairejea swala yake kama alivyotoa fatwa Alkafaal, na ya pili inakuwa Sunna kuirejea kwa kuiswali jamaa kama swala nyingine. Na ya tatu: iwapo ataiswali peke yake kisha akaipata jamaa inasuniwa kwake kuirejea swala hiyo pamoja nao kwa kupatikana kwa ubora wake na kama sio hivyo basi hapana. Na ya nne: inachukiza kuiswali tena. Na ya tano: ni haramu. [Mughniy Al Muhataaj 27/2, Ch. Dar Al Kutub Al Elmiyah]
Na Ibn Qudamah amesema: "Na atakayeiswali swala ya maiti mara moja basi sio Sunna kwake kuirejea swala hiyo… na ama yule atakayewahi jeneza miongoni mwa wale ambao hawajamswalia maiti basi anaweza kumswalia." Aliyu, Anas, Salmaan Bin Rabiah, Abu Hamzah na Muamar Bin Samir waliyafanya hayo. [Al Mughniy 382/2, Maktabat Al Qahirah]
Asheikh Adarder amesema: "(Na) inachukiza (kukariri kariri) yaani swala ya maiti (kama itakuwa imeshatekelezwa) kwanza kama jamaa. (na laa sivyo) itaswaliwa jamaa kama itakuwa imeswaliwa na mtu mmoja mmoja (itaswaliwa) tena kama ni Sunna (kwa jamaa) na wala sio mtu mmoja mmoja. Kwani katika sura nne inachukiza kuiswali tena kwa sura tatu na moja inakuwa ni Sunna kuiswali tena". [Asharh Aswagher Min Hashiyat Aswawi 569/1, Ch. Dar Al Maarif]
Na kutokana na yaliyotangulia; Inachukiza kuirejearejea swala ya jeneza, isipokuwa kwa haja ya wazi ya kisheria, kama vile swala ya aliyepitwa na ibada hiyo hususan akiwa ni walii wa maiti, au swala ya wanaotakiwa Baraka zao miongoni mwa watu wema wenye fadhili.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni mjuzi zaidi ya wote.

Share this:

Related Fatwas