Mke Humwosha Mume wake Aliyefariki Dunia
Question
Je, Inajuzu kwa mke kumwosha mume wake?
Answer
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Uoshaji katika lugha unamaanisha kukisafisha kitu na kukitakasa. Na ukoshaji ni maana pevu zaidi katika kuosha viungo vyote [Rejea kidahizo cha Ghasal katika Muajam Maqaiys Al Lugha kwa Ibn Fares 242/4, Ch. Dar Al Fikr].
Na kisheria ni kuyachuruzisha maji juu ya mwili mzima kwa kuwapo nia ya kufanya hivyo. [Mughniy Al Muhtaaj kwa Al Khatweb 212/1, Ch. Dar Al Kutub Al Elmiyah]
Na kumuosha maiti na kumzika ni faradhi ya kutoshelezeana ambapo watakapoifanya baadhi ya watu basi jukumu lake litafutika kwa wengine pia. Ad Darderiy amesema katika kitabu cha [As Sharhu Al Kabeer kwa Muhtasari wa Khalil]: "Na Swala juu yake ni faradhi ya kutoshelezeana kama vile kumzika na kumvika sanda" [As Sharahu Al Kabeer 407/1, Ch. Eisa Al Halabiy].
Na Al Bukhariy alisimulia kutoka kwa Hadithi ya Umm Atia Nasibah Al Nsaariyah, kwamba amesema: Binti mmoja miongoni mwa mabinti wa Mtume (S.A.W) alikufa, basi Mtume akajitokeza na akasema: "Mwosheni mara tatu au mara tano au zaidi ya idadi hiyo iwapo mtaona hivyo, kwa maji na majani ya mkunazi, na mlifanye josho la Mwisho liwe kwa kafuri au kitu chochote cha kafuri"
Na Abu Dawud alipokea kutoka kwa Al Hasswen Bin Wahawah kuwa Twalha Bin Al Baraa alipata ugonjwa basi Mtume (S.A.W) akamtembelea kwake ili amhudumie na akasema: "Mimi simuoni Twalha isipokuwa amepatwa na umauti, basi nipeni idhini mimi kwa ajili yake na muharakishe kwani haifai kwa mfu mwislamu afungiwe kati ya pande mbili za watu wake"
Na asili ni kwamba wanaume hawaoshwi isipokuwa na wanaume wenzi wao. An Nawawiy alisema katika kitabu cha [Raudhat At Twalibeen] "Basi kwa hiyo asili ni kwamba wanaume wawaoshe wanaume wenzi wao na wanawake wawaoshe wanawake wenzi wao ni bora zaidi kuliko mwanamke kuoshwa kwa hali nyingine zozote" [Raudhat At Twalibeen kwa AN Nawawiy 105/2, Ch. Al Maktab Al Islamiy].
Lakini inajuzu kwa mke kumwosha mumewe kwa makubaliano ya wanazuoni bali pia mke anatangulizwa mbele watu wengine katika Madhehebu ya Malik. Abu Dawud, Ibn Habaan na Al Hakem walipokea kutoka kwa Aisha alisema: Lau ningekubaliana na jambo langu/haki yangu nisingerejea nyuma . Asingeoshwa isipokuwa na wakeze.
Ibn Abdeen alisema: "Na wala mke hazuiliwi kumwosha mume wake ni sawasawa aliwahi kumwingilia au hapana, kama ilivyo katika kitabu cha [Miraaj] na mfano wake katika kitabu cha [Al Bahru] kutoka kwa Almujtabaa, nikasema: kwa sababu mwanamke analazimika kukaa eda ya kufiwa na mumewe; hata kama hajamwingilia. Na katika kitabu cha [Albadaaiu]: mke humwosha mume wake aliyekufa kwa kuwa uhalali wa kumwosha unatokana na ndoa na yataendelea kuwepo yale yanayokuwepo kutokana na ndoa. Na ndoa baada ya mauti inaendelea kuwepo hadi eda itakapomalizika." [Hashiyat Ibn Abdeen 576/1, Ch. Dar At Turaath].
Sheikh Al Islam Zakariya Al Ansaariy alisema: "Na mke asiyepewa talaka rejea anapaswa kumwosha mumewe; kwani katika ndoa yao, haki zao hazipotei kwa dalili ya kurithiana". Na Mtume (S.A.W) alimwambia Aisha: "Kama ungelikufa kabla yangu mimi, basi ningelikuosha na kukuvika sanda" Hadithi hii Imepokelewa na Ibn Majah na wengineo. Na Aisha akasema: "Lau ningekubaliana na jambo langu/haki yangu, nisingerejea nyuma. Asingeoshwa Mtume (S.A.W) isipokuwa na wakeze Mtume". Hadithi hii Inapokelewa na Abdu Dawud na Al Haakem, [Sharhu Manhaj Al Twlaab 150/2, Ch. Dar Al Fikr]
Ibn Qudamah amesema katika kitabu cha [Al Mughniy]: "Na mke humwosha mume wake, Ibn Al Munzer akasema: Wanazuoni wamekubaliana kuwa mke atamwosha mume wake atakapofariki dunia". Aisha amesema: Lau tungekubaliana na jambo letu.tusingerejea nyuma asingeoshwa Mtume (S.A.W) isipokuwa na wakeze. Hadithi hii imepokelewa na Abu Dawud, na Abuu bakri (R.A) ameusia kuwa aoshwe na mkewe Asmaa binti Umais. Na mke huyo alikuwa na swaumu akatakiwa afungue, na alipomaliza kumwosha mume wake akasema: leo sitamfuata nikiwa hivi, akaomba maji na akayanywa na Abuu Musa alimwosha mke wake Mama Abdillahi, na Jabir Ibnu Zaidi akausia kuwa: aoshwe na mkewe, na akasema: na maana iliyopo ndani yake ni kuwa kila mmoja wa wanandoa wawili ni rahisi kwake kuuangalia uchi wa mwenzake, kinyume na mtu mwingine kwa jinsi walivyokuwa wakati wa uhai wao. Na atamwosha mwenzake kwa kila njia ya ukamilifu aiwezayo kutokana na mapenzi yaliyopo baina yao na huruma. [290/2, Ch. Maktabat Al Qahirah]
Al Kharashiy amesema: "Na wana ndoa wawili wametangulizwa kama ndoa yao ilikuwa sahihi isipokuwa (Kadhi) atoe fatwa ya kuvurugika kwa ndoa hiyo, kwa hukumu za kisheria, inamaanisha kwamba kila mmoja kati ya wanandoa wawili atakapokufa mmoja wao basi hutangulizwa katika kumuosha mwenzake kwa kuwatangulia walezi wake wote na hukumu itatolewa ikimpendelea yeye kama patatokea mvutano kati yake na walezi kwani yule ambaye haki ya asili imemthibitikia basi atapendelewa na hukumu. Hii itawezekana kama ndoa yao itakuwa sahihi, iwe pametuka ujenzi au hapana." [Sharh Al Kharashiy juu ya Muhtasari wa Khalil 114/ 2, Ch. Dar Al Fikr].
An Nafrawiy Al Malikiy amesema: "Ameandika mwandishi wa Risala kama Khalili, juu ya mmoja kati ya wanandoa wawili kumwosha mwenzake." [Al Fawakeh Al Dawaniy Sharh Ar Resaalah 287/1, Ch. Dar Alfikr]
Kutokana na hayo, inafaa kwa mume kumwosha mke wake kwa makubaliano ya wanazuoni.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni mjuzi zaidi ya wote.