Kuuchunguza Utoaji wa Zaka ya Chaku...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kuuchunguza Utoaji wa Zaka ya Chakula

Question

Je, Ni lazima kuchunguza deni la mpewaji wa Zaka ya Fitri, katika mji ambao wengi wa wakazi wake ni waislamu?

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:

Jambo hili limezungumziwa mno kwa wale wenye kuzoea kuwapa sadaka wenye kuomba au wale ambao uwazi wa hali zao ni mafakiri na masikini, hasa wale wenye kazi za kawaida, basi mwenye kuwapa sadaka hajui mpewaji ni mwislamu au siye mwislamu katika mji ambao wengi wa wakazi wake ni waislamu.

Na jambo hili ambalo linajulikana kwa istilahi ya wanachuoni wa fiqhi kama ni uchunguzi, ambapo mtu aliyepewa jukumu anatakiwa achunguze katika mlango wa Zaka kwa kuifikisha mali kwa mtu anaestahiki; kwani yeye anatakiwa aitoe mali hiyo kwa aina maalumu za watu. Na iwapo ataitoa mali hiyo kinyume cha aina hizo maalumu za watu, atakuwa amefanya baadhi tu ya alichotakiwa kukifanya, na wala sio chote, kama ambavyo mtu huyu anatakiwa kuitoa Zaka kwa uyakinifu na hawezi kuiepuka dhimma isipokuwa kwa kuwa na uhakika.

Na asili katika Zaka ya Fitri ni wajibu, kutokana na yaliyotajwa katika vitabu viwili sahihi kutoka kwa Ibn Omar R.A kuwa: "Kwamba Mtume S.A.W, aliwafaradhishia watu Zaka ya Fitri katika mwezi wa Ramadhani kwa iwe pishi mbili na nusu za tende au pishi moja ya ngano kwa kila mwislamu aliye huru au mtumwa, awe mwanamke au mwanaume."

Kwa upande wa suala la uchunguzi, inatosha kwa mwenye jukumu kujitahidi na kuhangaika kama haikudhihiri kinyume chake kwani hicho ndicho anachokimiliki na kipo katika uwezo wa nguvu zake.

Al Khatwab Al Malikiy alisema: "Amesema Ibnu Rushdi katika kitabu chake cha: [Nawaazil], akizungumzia suala la Kuzuia mwanzoni wa waraka wa nne wa suala la Kuzuia: kwa yule aliyoitoa Zaka mali ya yatima kisha ikagundulika kuwa amempa mtu tajiri akimdhania kuwa ni fakiri, basi hana zaidi ya hivyo alivyofanya; kwani yule aliyefanya hivyo kiibada alifanya kwa kujitahidi katika jambo hilo, hivi huoni katika wanazuoni asemaye: iwapo mtu atampa zaka mtu tajiri hali ya kuwa hajui kama mtu huyo ni tajiri, Zaka yake itakuwa imetimia? Na hakuna tofauti yo yote kuwa ni lazima irejeshwe kwake iwapo atamjua na akaweza kufanya hivyo. [Mawaheb Al Jalil 359//2, ch. Dar Al Fikr]

Basi kama ikisemwa: "Kuna tofauti kati ya suala la tajiri na kutokuwa mwislamu, la kwanza kuna mitazamo tofauti kinyume cha la pili, basi jawabu ni kuwa: hali hii inadhihirika katika mazingira ambayo inabainika tofauti ya jitihada za mwenye jukumu, na hivyo wakati huo, yeye anatakiwa kurejesha alichokitoa kama Zaka, na kama haikubainika kinyume cha hali hiyo basi suala lililopo ni Zaka kutimia. Na imepokelewa maneno ya wazi ya jambo hili katika yale waliyoyasema wanachuoni.
Ibn Qudamah alisema: "Na pindi atakapompa mtu anaemdhania kuwa ni fakiri na akaja kuonekana kuwa ni tajiri. Kutoka kwa Ahmad, kuna riwaya mbili: ya kwanza ni kwamba hiyo Zaka inatosha. Na ameichagua riwaya hii Abuubakar. Na hii ni kauli ya Hassan na Abuu Ubaida na Abuu Hanifa; kwani Mtume S.A.W, aliwapa watu wawili wenye nguvu na akasema: "mkitaka nitawapa katika hizo mali, na sio tajiri mwenye bahati wala mwenye nguvu hapati kwa nguvu zake. Na akasema kwa mtu aliyemwombea sadaka: "Ukiwa miongoni mwa aina hizo nitakupa haki yako". Na kama akizingatia uhakiki wa utajiri basi haikutosheleza kauli yao. Na Abu Huraira akapokea kutoka kwa Mtume S.A.W. akisema: "Mtu mmoja akasema: nitatoa sadaka kwa sadaka, akatoka na sadaka yake, na kuiweka kwenye mikono ya tajiri, wakawa wanazungumza: tajiri amepewa sadaka, akaletwa na kuambiwa: sadaka yako imekubalika, huwenda tajiri akapata mazingatio na akawa mtoaji wa kile alichopewa na Mola wake." Hadithi hiyo ni "Mutafaqu alaihi" ( Hadithi hii imekubaliwa na Bukhari na Muslim) . Na mapokezi (riwaya) ya pili: Sadaka hiyo haitoshi, kwa kuwa mtoaji ametoa utoaji wa wajibu kwa mtu asiestahiki, kwa hiyo bado hajatoka katika jukumu lake la utoaji Zaka. Ni kama vile lau angelitoa na kumpa kafiri au ndugu yake. Na hili libakuwa kama madeni ya watu. Kauli hiyo ni kauli ya Al Thawriy na Al Hassan Bin Swaleh, na Abi Yusuf na Ibn Al Munzer, na kwa Al Shafiy kauli mbili kama riwaya mbili: Na iwapo itabainika kuwa mchukuaji wa zaka ni mtumwa, kafiri au kabila la Hashimiy au ana undugu na mtoaji wa Zaka katika wale wasiojuzu kuwapa Zaka hiyo, basi haitahesabika, riwaya moja; kwani mtu wa aina hii hastahiki kupewa Zaka, na mara nyingi hali yake huwa haijifichi. Kwa hiyo Zaka iliyotolewa haihesabiki kuwa ni Zaka, ni kama madeni ya watu. Na akatofautisha kati ya mtu atakaekuja kujulikana kuwa ni tajiri; kwani ufukara na utajiri ni katika mambo magumu kuyajua ukweli wake. Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: {Asiye wajua hali zao huwadhania kuwa ni matajiri kwa sababu ya kujizuia kwao kuombaomba. Utawatambua kwa alama zao} [AL BAQARAH 273], Na akatosheka na muonekano wa ufukara, na wito wake ni tofauti na mwingine. [Al Mughniy 498, uk. Maktabat Al Qahirah].

Na katika yanayolipanua jambo hili ni kwamba kuna miongoni mwa wanachuoni walionena kuwa inajuzu kumpa zaka ya fitri mtu asiyekuwa mwislamu (yu katika himaya ya waislamu) kwa hiyo mtu mwenye jukumu anapaswa kuifungamanisha kauli hii iwapo ataihitaji.

Al Kassaniy Al Hanafiy alisema: "Na masuala yaliyojengewa juu yake tumeyataja katika Zaka ya mali na masharti ya nguzo hii pia ni katika tuliyoyataja huko isipokuwa kusilimu kwa anayefanyiwa ibada hii ya kupewa, hapa sio sharti la kujuzu kufanyika kwa mujibu wa Abu Hanifa na Muhammad, kwa hiyo inajuzu kumpa Zaka mtu aliye chini ya himaya ya waislamu (dhimiyu)." [Badai'e Al Swanai'e 74/2, uk. Dar Al Kutub Al Elmiyah].

Ibn Rushd Al Hafeed Al Malikiy alibainisha sababu ya hitilafu baina ya pande zote mbili: Kwa hiyo, akasema kuwa Sura ya Tano katika utowaji wa Zaka ya Fitri: "Ni nani wa kupewa Zaka hiyo? Wamekubaliana wanachuoni kwamba Zaka hutolewa na kupewa Waislamu mafakiri kwa kauli yake Mtume S.A.W: "waepushieni kuomba omba katika siku hii ya furaha". Na wakatofautiana wanachuoni katika kujuzu kuwapa zaka mafakiri wasio waislamu. Na Jamhuri ya wanachuoni inaona kwamba haijuzu kuwapa Zaka mafakiri wasio waislamu. Na Abu Hanifa alisema: "Inajuzu kwao. Na sababu ya kutofautiana: Je? sababu ya kujuzu kwake ni ufukara tu, au ufukara pamoja na Uislamu? Na atakaesema: Ufukara pamoja na Uislamu atakuwa hakujuzisha kwa wasiokuwa Waislamu (walio chini ya Himaya yao), na atakaesema: Ufakiri tu, atakuwa amejuzisha hata kwa wasiokuwa Waislamu." [Bedayat Al Mujtahed 44/2, uk. Dar Al Hadeeth, Al Qahirah]

Kutokana na yaliyotangulia tunaweza kusema: Hakika mwislamu anapaswa kufanya uchunguzi wa nani wa kumpa Zaka yake kwa mkono wa mtu mwenye kustahiki kwani hii ndio asili ya Zaka, na kujiepusha na mambo waliyotofautiana wanachuoni ni jambo linalopendeza. Lakini akijitahidi kisha akagundua kinyume cha jitihada zake atachagua ima arejee kutoa Zaka kinyume cha mwanzo au atosheke na hiyo aliyoitoa kwanza kwa kufuata wanazuoni waliojuzisha jambo hili.

Share this:

Related Fatwas