Kushikilia Pazia za Kaaba
Question
Nini hukumu ya kushikilia pazia za Kaaba na kuzing`ang`ania?
Answer
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Kaaba katika lugha ya Kiarabu ina maana mbili:
Maana ya kwanza: kwamba Kaaba imeitwa kwa jina hili kwa sababu ni umbo la mraba kwa jinsi lilivyo. Kwa hivyo basi kila nyumba yenye umbo la mraba kwa Waarabu ni Kaaba. Kinyume cha nyumba nyingi za Waarabu zilizokuwa na maumbile ya duwara. [Lisan Al-Arab 1/718, kidahizo cha: Kaaba, Dar Sadir].
Ibn Al-Arabi alisema: “Kaaba imeitwa kwa jina hili kwa sababu sura lina umbo la mraba , Mujahid na Ikrima pia wamesema hivyo”. [Ahkam Al-Quraani 2/206, Darul Kutub Al-Elmiyyah].
Maana ya pili: Kaaba imeitwa hivyo kwa jina lake hili kwa sababu ya mwinuko wake na urefu wake kihisia na kimaana, basi kila kitu kikiwa na mwinuko wa kwenda juu na ujazo ni Kaaba [Ahkam Al-Quraani, Ibn Arabiy 2/206].
Ukweli ni kwamba maana mbili hizi za Kaaba ni dhahiri na wazi. Kaaba ni umbo la mraba, lililopanda juu na ni tukufu na lenye heshima ya hali ya juu.
Maana ya Kaaba katika sheria: Ni nyumba ya Mwenyezi Mungu, ni Kibla na ni Msikiti Mtakatifu. Napo ni mahali pa heshima na utukufu, kwani Mwenyezi Mungu ameifanya Kaaba kuwa ni nyumba yake, kwa ajili ya utukufu na heshima. Mwenyezi Mungu anasema katika Quraanii kupitia Mtume wake Ibrahim: (A.S) {Mola wetu Mlezi! Hakika mimi nimewaweka baadhi ya dhuriya zangu katika bonde lisilo kuwa na mimea, kwenye Nyumba yako Takatifu} [IBRAHIM: 37], na Mwenyezi Mungu amesema pia: {Na isafishe Nyumba yangu kwa ajili ya wanaoizunguka kwa kutufu, na wanao kaa hapo kwa ibada, na wanao rukuu, na wanao sujudu.} [AL-HAJJ: 26].
Nayo ni nyumba ya kwanza iliyowekwa katika ardhi kwa ajili ya ibada ya Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu amesema: {Hakika Nyumba ya kwanza walio wekewa watu kwa ibada ni ile iliyoko Bakka, iliyo barikiwa na yenye uwongofu kwa walimwengu wote} [AAL IMRAN: 96].
Mwenyezi Mungu amefanya pande zake nne za Makkah ni nchi takatifu ina amani, kwa ajili ya kuiheshimu Nyumba yake tukufu, pia ameifanya kibla kwa Waislamu ili waelekee kwake katika sala zao mara tano, na hairuhusiwi kwa mtu yeyote kuelekea kwa kitu kingine, bali kama mtu yeyote ameelekea upande mwingine kwa makusudi hazikubaliwi sala zake isipokuwa tu katika baadhi ya hali ya kipekee, kama katika sala ya hofu, Mwenyezi Mungu anasema: {Basi elekeza uso wako upande wa Msikiti Mtakatifu; na popote mnapokuwa zielekezeni nyuso zenu upande huo} [AL-BAQARAH: 144], Mwenyezi Mungu ameifanya tawafu kwa maana yake ya kisheria ni maalum kwa kuizunguka Kaaba tu, Mwenyezi Mungu amesema: {Na waizunguke Nyumba ya Kale} [AL-HAJJ : 29].
Maana ya kushikilia pazia za Kaaba: Ni kushikamana na nguzo zake na nguo yake. Na nguo: Ni iliyotumika kama vazi na pambo, na katika kitabu cha: [Al-Misbah Al-Muniir, Al-Faiumi 2/534, kidahizo: Nguo]: “Nguo:Ni vazi”.
Kushikilia pazia za Kaaba ni ishara ya kusisitiza kwa kutaka msamaha, na kuomba amani, kama mwenye hatia anayeshikilia nguo ya rafiki yake kwa ajili ya kuomba msamaha wake kwa unyenyekevu kama kwamba yeye hana hila yoyote isipokuwa kuomba msamha wake tu. Ibn Asakir amesema katika kitabu cha Tariikh Dimashq: “Abdul Bari alimwambia Abu Fiyaadh: Nini maana ya kushikilia pazia za Kaaba? Alisema, kama mtu fulani alifanya hatia kwa rafiki yake, basi yeye anamshikilia na kuomba msamaha wake akitumai kumsamehe kwa hatia yake”. [Tariikh Dimashq 6/352, Darul Fikr].
Waarabu walikuwa kabla ya Uislamu kama mtu akitaka kujiamini nafsi yake anaingia Kaaba na kushikilia pazia zake, na inaonekana kwamba hali hii wao wameirithi kutoka mabaki ya mila ya Ibrahim (A.S) ambapo hali hii iliendelea mpaka zama za Mtume Muhammad, (S.A.W) na iliendelea baada yake pia, na miongoni mwa yaliyopokelewa kuhusu jambo hili ni kwamba: Siku ya kutekwa kwa Makka Mtume aliwapa watu usalama isipokuwa watu wanne na wanawake wawili, akasema: "wauweni hata kama mkiwaona wanashikilia pazia za Kaaba: Nao ni Ikrima Ibn Abu Jahl, Abdullah Ibn Khtal, Maqis Ibn sababah, na Abdullah Ibn Saad Ibn Abi Sarh". [Musannaf Ibn Abi Shaybah 8/52, Darul Rushd].
Imepokewa kutoka katika maneno ya wanafiki wengi kwamba wamesema hivyo ingawa wana madhehebu tofauti:
Imamu Al-Ghazali alisema: “Kuhusu kushikilia pazia za Kaaba na kuzing`ang`ania kati ya sehemu ya jiwe jeusi na mlango wa Kaaba, basi awe na nia ya kuomba ukaribu kwa upendo na hamu kwa ajili ya nyumba na kwa Mola wa nyumba, pia kwa nia ya kupata baraka kwa kuigusa, akitumai kujikinga na moto katika kila sehemu ya mwili wake, na uwe na nia katika kung`ang`ania pazia na kusisitiza kwa kuomba msamaha na kutaka usalama kama ilivyo kwa mwenye hatia anayeshikilia nguo ya rafiki yake kwa unyenyekevu akimwombea msamaha wake akionesha kwamba hana yeyote isipokuwa yeye tu na hana isipokuwa ukarimu wake na msamaha wake tu, na kwamba hataacha kumshika nguo yake isipokuwa baada ya kumsamehe na kumpa usalama katika siku zijazo” [Ihyaa Ulum Al-Din 1/269, Ch. Darul Maarifa].
Sheikh Al-Jamal amesema: “Hupendeza kabla ya sala kuja kati ya sehemu ya jiwe jeusi na mlango wa Kaaba kwa sababu Mtume (S.A.W) alikuja sehemu hiyo na alisema kwamba kulikuwa na Malaika anamwomba Mwenyezi Mungu aijibu dua hii, Malaika huyu yupo kati ya jiwe jeusi na usawa wa mlango kutoka chini, upana wake ni dhiraa nne, akigusisha kifua chake na uso wake kwenye ukuta wa nyumba na akiweka ameweka shavu lake la kulia kwenye ukuta huo akiinyoosha/akikunjua mkono wake wa kulia mpaka mlangoni, na mkono wake wa kushoto ukiwa katika nguzo akishikilia pazia za Kaaba, akisema Ewe Mola wa Nyumba hii ya Kale iache huru shingo yangu kutokana na moto na nikinge kutokana na Shetani aliyelaaniwa na ninajikinga kutokana na vishawishi vyake na kisha akaomba dua kama atakavyo". [Hashiyat Al-Jamal ala Sharhil Manhaj 2/441, Darul Fikr].
Sheikh Al-Dardiir amesema: “(Na) hupendeza (kuomba dua) baada ya kumaliza kuzunguka na kabla ya kusali rakaa mbili kati ya (Al-Multazam): Nayo ni ukuta wa nyumba (Kaaba) kati ya jiwe jeusi na mlango wa nyumba: ِِAkiweka kifua chake, na akinyoosha mikono yake juu yake na ataomba dua kama atakavyo”. [Al-Sharhul Saghiir maa Hashiatul Sawi 2/43, Ch. Darul Maarifa].
Na Buhutiy amesema "(Atakapo maliza ibada ya kuaga na akashika Jiwe Jeusi na kulibusu atasimama Al-Multazam) nayo ni (kati) ya sehemu ambayo lipo (Jiwe Jeusi na mlango wa Al-Kaaba) hali ya kugusisha kifua chake,uso wake na tumbo lake na atainyoosha mikono yake, mkono wa kulia upande wa mlango na mkono wa kushoto upande wa Jiwe Jeusi) Kwa mapokezi ambayo Amr bin Shuaib amepokea kutoka kwa baba yake, alisema: "Nilitufu pamoja na Abdallah alipofika mbele Al-Kaaba nilimwambia: Hujikingi? Akasema najikinga kwa Mwenyezi Mungu kutokana na moto, kisha akalishika Jiwe jeusi akasimama kati ya kona na mlango akaweka kifua chake na mikono yake na viganja vyake akainyoosha na kusema: Hivi ndivyo nilivyomuona Mtume (S.A.W) akifanya. [Imepokewa na Abu Daud.] (Na ataomba kwa anayoyataka miongoni mwa kheri za Dunia na Akhera)." [Kashafu Al-Qinaa 3/513, Darul-Fikr]
Ibn Qudamah amesema “Tawoos alisema: Nilimuona Bedui mmoja alikuja Al-Multazam, akashikilia pazia za Kaaba, na akasema: "Najikinga kwako, Ewe Mola, kwa kutaka ukarimu wako, na kuridhia kwa dhamana yako, nifanye kuwa na raha nisiwe kama mabahili, nitosheleze kwa yaliyomo ndani ya mikono ya wanaojipendelea, Ewe Mola ukarimu wako ambao ni karibu, na wema wako ambao ni wa zamani, na tabia zako ambazo ni nzuri. Kisha nimepotea miongoni mwa watu, nikamkuta akisimama katika Arafat, akisema: Ewe Mola, kama hukukubali Hijja yangu na kazi yangu na taabu yangu, basi usiache kumlipa kheri kwa aliyepatwa na bahati mbaya, sijui aliye na msiba mkubwa zaidi kuliko yule aliyeondoka kanyimwa kutoka kwako”. [Al-Mughni 3/407, Ch. Maktabat Al-Kahirah].
Al-Zaylai amesema: “Kuwa katika Al-Multazam, ushikilie mapazia na ung`ang`anie ukuta” na Al-Multazam ni ile ambayo ni kati ya mlango na jiwe jeusi, na akitoe kifua chake na makusudio ya mapazia: Ni mapazia ya Kaaba, Na inapendeza kwake aje mlango wa nyumba jambo la kwanza abusu kizingiti, na aiingie nyumba bila ya viatu kisha aje Al-Multazam akiweke kifua chake, uso wake juu yake, na ashikilie mapazia atamuomba Mwenyezi Mungu dua kama anavyopenda kutika mambo ya dunia na akhera.” [Tabiin Al-Haqaiq Sharhu Kanzul Daqaiq 2/37. Al-Amiriyah].
Kutokana na yaliyotanguliwa hapo juu: Basi kushikilia pazia za Kaaba au kuigusa nyumba na kuomba dua, mambo haya yote yanapendeza kwa maana yake ilivyo ni kuomba msamaha wa Mwenyezi Mungu kwa kusisitiza, vile vile kutafuta baraka, heshima na utukufu, wala haipaswi kwamba hukumu hii isababishe machafuko katika kuyafanya hayo katika Kaaba, ambayo inachukuliwa kuwa ni unyanyasaji na upuuzaji wa Nyumba hii takatifu, pia inaruhusiwa kwa wale wasimamizi wa msikiti Mtakatifu kupanga jambo hilo, hata kama likifikia kuzuiwa kwa hofu ya nguo ya Kaaba kutaka kukatika na kwa ajili ya kumaliza mchafuko huu, lakini kuzuia hivyo siyo kwa madai ya kuharimishwa kwa kitendo hicho au kuwa ni ushirikina.
Na Mwenyezi Mungu ni mjuzi zaidi ya wote.