Fikra Sahihi Katika Mtazamo wa Kiis...

Egypt's Dar Al-Ifta

Fikra Sahihi Katika Mtazamo wa Kiislamu

Question

Ni zipi sifa za fikra sahihi katika mtazamo wa kiisalamu?

Answer

 Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:

Kufikiria ni neema ya Mola Mwenyezi Mungu amempa mwanadamu zawadi, na katika kuishukuru neema ya Mwenyezi Mungu ni kuizungumzia; Amesema Allah Mtukufu: {Na neema za Mola wako Mlezi zisimulie} [WADH-DHUH'AA: 11]. Na akasema Mtume: S.A.W. “Hakika Mwenyezi Mungu anapenda kuona athari ya neema yake kwa mja wake” ([1]), Na akasema pia kuhusu jambo la kupunguza swala- kisha kauli yake hiyo ikawa ni kanuni inayoendelea: (Sadaka Mwenyezi Mungu amekupeni sadaka basi ipokeeni sadaka yake) ([2]). Na dalili ya kwamba kufikiria ni neema ni kuwa tumeamrishwa katika maisha yetu yote, na katika Qur-ani tufanye hivyo. Anasema Mola Mtukufu: {Kwa Ishara wazi na Vitabu. Nasi tumekuteremshia wewe Ukumbusho ili uwabainishie watu yaliyo teremshwa kwao, wapate kufikiri} [AN NAH'L: 44]. Akaunganisha kati ya kuwajibika na maamrisho na makatazo katika sheria na tabia, na kati ya kufikiri ambako ndio msingi wa ufahamu.

1-   Fikra: Ni kupangilia mambo yanayofahamika ambayo mtu anapata kufikia mambo yasiyojulikana. Na mambo yanayofahamika yanakuwa katika sura ya sentensi yenye kufahamika, inayokusanya fikra ya sentensi na sentensi na kuziunganisha na kutoa matokeo katika sentensi hizo mbili, na kila sentensi yenye kufahamika ina uwezo wa kuelezea uhalisia na ina uwezo wa kuelezea ombi. Na kufikiri vizuri kunaanzia katika kutafiti sentensi ambayo inaelezea uhalisia na kutaka kuthibitisha usahihi wake, na kama si hivyo fikra huelekea kwenye uongo na haiwi fikra sahihi. Na kila sentensi sahihi ina nyanja zake, na kila nyanja zina njia zake za kuzithibitisha, na dalili ni hoja ya kuzithibitisha, na viwango vya kukubali au kukataa masuala ya sentensi.

2-   Kuna mambo yanarudi kwenye akili ya kuhisi na majaribio, mfano wa sentensi: Moto wenye kuunguza, na jua lenye kuchomoza. Na dalili ya mambo haya inakuwa ni kwa akili ya kuhisi, au kwa habari yenye kuaminiwa. Na kuna mambo mengine yanarejea kwenye akili mfano wa mambo ya hesabu. Na kuna mambo mengine yanarejea kwenye kunukulu kama vile hukumu za kilugha na hukumu za kisheria, na yote hayo yanahitaji mbinu au mfumo wa majaribio, uchunguzi na hitimisho, na kujirudia hayo mara kadhaa hadi ukweli wake utulie katika akili na iwe tayari kwa kutumiwa. Watu wa mantiki wanaiita sentensi sahihi “Asilimia kamili” na hufafanuliwa kama: Kuthibitisha amri kwa amri au kuikana. Inapokuwa sentensi ya kawaida na ya hisia huongeza ibara “Kulingana na marudio” na inapokuwa ni ya kunukulu husemwa: “Kulingana na hali ya muwekaji”, na inapokuwa ya akili wanasema: “Isiyotegemea kujikariri au hali ya muwekaji”.

3-   Na katika aina ya kupotoka kwenye fikra sahihi ni kutafuta dalili ya masuala ya akili na kunukulu, au masuala ya hisia katika akili, au kuhusu masuala ya kunukulu. Na jambo linalodhibiti yote hayo ni elimu. Na elimu katika ufahamu wa kiarabu haiishii kwenye maana ya kufasiri neno Scienceambalo limeishia kwenye elimu ya majaribio tu; Lakini inamaanisha uwezo wa kuainisha katika maarifa au elimu; kwa ajili hiyo neno hilo linatofautisha kati ya dalili isiyokuwa na shaka (iliyothibitishwa) na dalili ya dhana na kufahamisha mipaka ya kila kimoja miongoni mwake.

Kuchanganya kati ya dalili isiyokuwa na shaka (iliyothibitishwa) na dalili ya dhana ni katika tabia ya fikra iliyopotoka. Na kuchanganya kati ya nyaza za hisia, akili na kunukulu na kutobainisha kati yao ni katika tabia ya fikra iliyopotoka pia. Na kwenda mwendo wa kipofu bila ya kuweka wazi namna ya kufaidika na kila nyanja, kwa kuwa inawakilisha uhalisia wa maisha miongoni mwa tabia hizo za fikra zilizopinda/ zisizo sahihi, na kudharau nyanja dhidi ya nyanja zingine ni katika tabia za fikra iliyopinda pia.

4-   Na fikra potofu zinatupeleka kwenye akili potofu, na kwenye mfumo potovu na uongo ambao unamaanisha kwenda kinyume na uhalisia na kwenda kinyume na uhalisia na itikadi; kwa ajili hiyo katika lugha ya kikureshi waliuita uongo kosa, kama alivyosema Mtume S.A.W. siku ya kuifungua Makka: “Uongo wa Saad” aliposema Saad bin Ubaada: Leo ni siku ya vita kali, Akasema S.A.W.: “Bali leo ni siku ya rehema” na kusema uongo hapa ina maana alikosea katika aliyoyasema, Mtume S.A.W. akamuondoa katika uongozi, akamteuwa katika nafasi yake mtoto wake Qaysi.

Hakika fikra potofu inawafanya watu waishi katika ndoto, na inapoenea fikra hii mambo huchanganyika, na hicho kinakuwa ni kikwazo kikubwa mbele ya maendeleo ya watu na mbele ya ubunifu wa binadamu, na mbele ya maendeleo na kushikilia mambo muhimu  mbele ya elimu na kupatikana nguvu, na ikiwa ni hivyo basi majaribio yote ya kuboresha yatafeli na kuenea kwa fujo na uholela.

5-   Tutakapolinganisha hali yetu pamoja na fikra ongofu na fikra potofu pamoja na hali ya waliotutangulia; ambapo maendeleo yalijengwa na yakawanufaisha watu katika kila sehemu- tutakuta kuwa wao  walijenga fikra sahihi na kupiga vita fikra zote potovu, na tutakapo linganisha hali zetu pamoja na hali ya maendeleo ya kimagharibi tutawakuta pia na wao walipozipiga vita fikra potofu na kuzikataa, na katika hali ya kuzikataa ni swala  miongoni mwa masuala ya utaalamu na marejeo, waliamini utaalamu na kuamini marejeo, na hakutambulika mtu kama [Abu Al-Arif] mwenye sifa  iliyoenea katika tamaduni za kiasili kwa sifa ya mtu mzuri na mwenye kupendeka  bali ni sifa ya mtu aliyo katika dimbwi la kuchelewa na uhuni- na  alikuwa sawa na muongo kwao wao- sawa sawa iwe kwa wa wale waliotangulia au kwa wamagharibi- ni kiwango hasi anachohesabiwa mtu anayefanya hayo kwa ngazi zote. Na uongo unakuwa ni uhalifu unapotoka kwa afisa au anayeongoza katika kuwahudumia watu.

6-   Na chini ya fikra ya kuheshimu marejeo waliweza kutofautisha kati ya uhalisia na rai; hakuna mitazamo katika mambo yanayohitaji majaribio na hisia, mitazamo inakuwa katika kutatua mambo ya umma, na inakuwa katika nyanja zinazotegemea rai, sawa sawa ikiwa ni kwa watu waliobobea au watazamaji wa kawaida na waandishi, na lazima rai iasisiwe – ili kuifanya ni yenye kuheshimika – mbele ya fikra sahihi, na hakuna budi kutafuta manufaa na maslahi ya umma, na itakapotoka kwenye fikra sahihi au kutafuta shari na ufisadi fikra itarejeshwa kwenye fikra ya aliyetengwa na yapasa kujitenga naye.

Inaonekana kuwa ukweli huu rahisi uliokubalika inakuwa vigumu kwa watu wengi kuufuata, na hawawezi isipokuwa waendee katika ujinga wao wa kifkra na jeuri yao ya kikazi kwa sura mbaya inayokosesha ukweli wa neno na kupoteza  njia ya mazungumzo.

7-   Hakika kusisitiza katika kufuata fikra potofu na chafu, na kuingilia katika taaluma mbali mbali kwa sura inayokusanya kati ya ujinga na kati ya kibri – ni lazima kupigwa vita kwa utaratibu, kuanzia kwenye mfumo wa elimu hadi kwenye vyombo vya habari; mpaka turudi kwenye matumaini ya kubadilisha hali zetu. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Hakika Mwenyezi Mungu habadili yaliyoko kwa watu mpaka wabadili wao yaliyomo naf-sini mwao} [AR-RAA'D:11].

Ni wajibu sote kufahamu kuwa Fiqhi ya kiislamu ni elimu miongoni mwa elimu. Wanachuoni waliielezea kuwa ni: “Elimu ya hukumu za kisheria kivitendo zilizochukuliwa kwenye dalili au ushahidi wa kina”, nayo ni elimu yenye masuala yake, ina njia zake, ina zana zake, ina kozi zake za utafiti, ina shule zake za kifikra, ina elimu zake saidizi, ina faida zake na matokeo yake. Na hakuna uwezekano wa kuikwepa kwa kila anayetaka au kufikiria bila kuitegemea elimu hiyo. Ni elimu isiyojuwa ubaguzi na wala haiutaki; kila mwanamke au mwanaume na kila mweupe au mweusi lazima apite njia ya elimu hiyo. Lakini haifai kwa hali yoyote iwayo avuke mipaka yake na kusema mambo ambayo hatakiwi kuyasema. Hakuna kwa walebrali kupinga elimu ya Kemia katika yale waliyofikia kwa mfumo wake na zana zake, na sio haki kwa walebrali kuingilia masuala ya tiba na kuwasilisha  rai za watu ndani yake, bali haya ni katika mawazo dhaifu na ya uongo ambayo yanaukokota ulimwengu kwenye hisia, matakwa, tamaa na mitazamo, na hii si hali yake.

Na Fiqhi ni elimu miongoni mwa elimu; atakayekabiliana nayo kwa njia hii itamfanya awe mwenye kujua ukweli, kucheka kicheko kilichochanganyika na kilio. Hakika janga baya ni kinachochekwa, amesema Mola Mtukufu: {Sema: Mola Mlezi wangu ameharamisha mambo machafu ya dhahiri na ya siri, na dhambi, na uasi bila ya haki, na kumshirikisha Mwenyezi Mungu na asichokiletea uthibitisho, na kumzulia Mwenyezi Mungu msiyo yajua} [AL-A'RAAF: 33]. Na Allah akazidi kutuonya kutokana na njia hii yenye kuangamiza pale aliposema: {Basi ni nani aliye dhalimu zaidi kuliko yule anaye mzulia uwongo Mwenyezi Mungu na akazikanusha Ishara zake? Hakika hawafanikiwi wakosefu} [YUNUS:17].

Chanzo: kitabu cha, Simat El Asri. Dk. Ali Gomua, Mmufti wa Zamani wa Misri.([1])  Ameitoa Al Tirmidhiy katika kitabu (Al Adab) mlango (yaliyokuja kuwa Mwenyezi Mungu anapenda kuona athari ya neema zake kwa mja wake) hadithi (2819) katika hadithi ya Amru bin Shuaibu kutoka kwa baba yake kutoka kwa babu yake, na akasema Al Tirmidhiy  (hadithi hii ni nzuri).

([2])  Ameitoa Muslim katikabu (sala ya wasafiri na kupunguza kwake) hadithi (686) katika hadithi Umar Bin Khatab R.A.

Share this:

Related Fatwas