Mpangilio wa Kusali (kukidhi) Swala...

Egypt's Dar Al-Ifta

Mpangilio wa Kusali (kukidhi) Swala Zilizopita.

Question

Mimi ninaishi Australia, na ninaanza kazi saa sita mchana, na siwezi kuziswali Swala kwa wakati wake, na hurudi nyumbani kwa ajili ya kufuturu na kusali Swala ya Magharibi, kisha hurudi tena kazini. Sasa je, ninaweza kuswali Swala ya Magharibi kabla ya (kukidhi) Swala ya Adhuhuri na Alasiri kwa kuziswali baada ya kurudi nyumbani saa nne (usiku)?

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Ndio, unaweza kuswali Swala ya Magharibi kabla ya kusali (kukidhi) Swala ya Adhuhuri na Alasiri, kwa mujibu wa Imamu Shafi na Malik ya kwamba mpangilio wa kuswali Swala za Faradhi ndani ya wakati wake na Swala zinazosaliwa kwa kuzilipa (kuzikidhi) ni kitu kinachopendeza na sio lazima. Na kwa Malik walipolazimisha mpangilio kama wanavyozingatia –katika madhehebu yao- hawakulazimisha kuwa ni sharti la kusihi, lakini ni Swala ya lazima inayosaliwa kabla ya Swala iliyopita, kwa mtazamo wao na ni Swala sahihi ingawa kuna madhambi. Na kinachoeleweka kuwa madhambi huondoka iwapo hukuwa na budi kuichelewesha Swala.
Isipokuwa sisi hapa tunatahadharisha kuwa haifai kukusudia kuitoa Swala katika wakati wake, na inawezekana iwapo ni wakati wa Swala ya Adhuhuri unaingia kabla ya kuanza kwa kazi zako, unaweza kusali Swala ya Adhuhuri pamoja na ya Alasiri, kwa kuzikusanya pamoja, hii ni bora kuliko kuziacha kabisa mpaka wakati wake upite. Kwa kuchukua ruhusa ya Mtume iliyopo katika Hadithi ya Ibn Abbas –radhi za Mwenyezi Mungu ziwashukie – kuwa Mtume – rehma na amani zimshukie– alisali Adhuhuri na Alasiri pamoja alipokuwa Madina bila ya kuwa na sababu ya hofu au kuwa msafiri. Na Ibn Abbas amesema: “Alifanya hivyo ili asimweke mtu yeyote wa umma wake matatizoni.” Imepokewa na Muslim.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi ya wote.

Share this:

Related Fatwas