Historia ya Jinsi Waislamu Walivyow...

Egypt's Dar Al-Ifta

Historia ya Jinsi Waislamu Walivyowatendea Watu wa Dhima.

Question

Nimeulizwa na rafiki yangu mkristo: Ni kwa sababu gani mnasema kuwa Uislamu umewatendea wema watu wa Dhima, wakati ambapo Wakristo wamekuwa chini ya utawala wa Waislamu kwa mujibu wa maelezo yaliyotajwa na Birnard Lewis kuwa haikuruhusiwa kwa Wakristo kujenga makanisa au kuyafanyia matengenezo makanisa waliyokuwa nayo, na hawakuwa na haki ya kuyafikisha masuala yao mahakamani, kwa hivyo, hawakuwa na uwezo wa kujitetea dhidi ya shutuma za uongo, na walikuwa hawana uwezo wa kujitetea dhidi ya mashambulizi ya Waislamu, na walikuwa hawaruhusiwi kupaza sauti zao katika ibada na sherehe zao, na ilikuwa rahisi kwao kubakwa, kuibiwa, kuuawa, na walilazimishwa kulipa kodi mara Zaidi ya zile zilizolipwa na Waislamu. Natarajia mtanifafanulia suala hili.

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Dhima katika lugha ni: Ahadi na usalama, watu wa Dhima ni watu wa ahadi, na mtu wa Dhima ni Mtu aliyeahidiwa (asiye mwislamu aliyewekeana mkataba na waislamu) [Al-Misbaah Al-Muniir / kidahizo cha Dhima].
Watu wameitwa kwa jina hili; kwa sababu wamekuwa katika Dhima ya Waislamu, wakawa na usalama katika maisha, heshima, na mali zao, na wakawa wakilipa Jizyah (yaani kodi inayolipwa na asiye mwislamu) nayo ni pesa chache kwa ajili ya kuwalinda na kuwatunza, na kutojiunga na jeshi. Kodi hii ilikuwa gramu nne za dhahabu kwa mwaka na inalipwa na matajiri na wenye hali ya kati, lakini hailipwi na maskini.
Mwenyezi Mungu alituamuru kutendeana wema na watu wa Dhima akisema: {Mwenyezi Mungu hakukatazini kuwafanyia wema na uadilifu wale ambao hawakukupigeni vita, wala hawakukutoeni makwenu. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wafanyao uadilifu} [AL MUMTAHINAH: 8], Imamu Al-Tabari alisema: “Maana ya kauli yake: Mwenyezi Mungu hakukatazini kuwafanyia wema na uadilifu wale ambao hawakukupigeni vita” yaani watu amabo wanafuata dini yeyote Mweyezi Mungu hakukatazaini kuwafanyia wema na uadilifu, na kauli yake {Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wafanyao uadilifu} yaani Mwenyezi Mungu hupenda wanaofanya uadilifu na wengine, wanafanyia wema kwa wanaowafanyia wema” [Tafsiri Al-Tabari, 22/574, Darul Hijrah]. Kufanya wema ni aina juu ya kutendeana. Mwenyezi Mungu ameamuru kufanya wema kwa wazazi, na Mtume S.A.W, amefafanua jambo hili kwa kauli yake iliyopokelewa kutoka kwa Al-Nawwas ibn Samaan Al-Ansari R.A akisema: “Kufanya wema ni tabia njema”.
Al-Qarafi wakati alipohisabu aina za kufanya wema zilizoamriwa na Mwislamu kwa watu wa Dhima alisema: “Maneno laini kwa njia ya Upole na huruma kwao, siyo kwa njia ya kuogopa na udhalili, kuvumilia adha yao kama wakiwa majirani pamoja na uwezo wa kuiondoa, kwa njia ya upole kwao, siyo kwa kuwatisha wala kuwatukuza, kuombea dua ili waongoke, wawe miongoni mwa wenye furaha, kuwashauri katika hali zote za kidini, kama mmoja wao alisengenywa ni wajibu kumtetea, kuwatendea kila aina ya wema, hali hii inatokana na tabia njema, na vile vile kutendeana nao kama ilivyotangulia kuelezwa kwa amri ya Mwenyezi Mungu na amri ya Mtume S.A.W” [Al-Fruq, 3/ 15K Alam Al-Kutub].
Vile vile Sheria imetulazimisha tuwafanyie wema wazazi hata wakiwa miongoni mwa watu wa Dhima, Mwenyezi Mungu alisema: {Na pindi wakikushikilia kunishirikisha na ambayo huna ilimu nayo, basi usiwat'ii. Lakini kaa nao kwa wema duniani, nawe ishike njia ya anaye elekea kwangu. Kisha marejeo yenu ni kwangu Mimi, na Mimi nitakuambieni mliyo kuwa mkiyatenda} [LUQMAAN: 15].
Ibn Kathiir alisema: Kama wakikushikilia kabisa kwa ajili ya kuifuata dini yao, usikubali hali hii, lakini hakuna la kukuzuia kukaa nao (kwa wema) duniani [Tafsiri ya ibn Kathiir, 6/337, Dar Taibah], Mohammad ibn Al-Hassan alisema: Juu ya Mwislamu matumizi ya lazima kwa wazazi wake ambao ni miongoni mwa watu wa Dhima kwa ajili ya kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Lakini kaa nao kwa wema duniani}, na siyo kukaa nao kwa wema kumfanya ageuke katika neema za Mwenyezi Mungu na kuwaacha wazazi wanakufa kwa sababu ya njaa, babu na bibi wa baba na babu wa mama ni kama wazazi, sawasawa katika hali hii. [Al-Mabsut kwa Al-Sarkhasi, 5/206, Darul Maarif].
Na miongoni mwa kufanya wema ni kuwaombea dua ya uongofu. Mtume S.A.W aliliombea dua kabila la Daus. Imepokelewa kutoka kwa Imam Muslim katika sahihi yake kutoka kwa Abi Hurairah R.A alisema : Al-Tufail ibn Omar Al-Dausi na wenzake walikuja na wakasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu hakika kabila la Daus limekufuru na limekataa, basi liombee dua mbaya, imesemwa: Kabila la Daus litaangamizwa kwa dua yake, Mtume S.A.W akasema: “Ewe Mola wangu waongoze watu wa Daus na uwafanye waingie katika Uislamu”.
Sheria imetutahadharisha sana na kutuonya tusiwadhuru watu wa Dhima. Imepokelewa kutoka kwa Ibn Majah kutoka kwa Abi Hurairah kutoka kwa Mtume S.A.W, alisema : “Mwenye kumuua mtu aliyeahidiwa wenye Dhima ya Mwenyezi Mungu na Dhima ya Mtume wake hatanusa harufu ya Pepo na hakika harufu yake hunukia kwa masafa ya mwendo wa miaka sabini”.
Mwenye kufuatilia historia ya Kiislamu atapata usia wao na kuwafanyia wema; miongoni mwa hali hizi: Waraka uliyoandikwa na Omar ibn Al-Khattab akiwausia makhalifa waliomfuata wautekeleze waraka huo, na miongoni mwa mambo yaliyoandikwa katika waraka hii ni: Usalama kwa nafsi zao, fedha zao, watoto wao, heshima zao, mali zao na kuzilinda kutoka kuzishambuliwa ikiwa kutoka ndani na nje. Al-Akhtal Mkristo alikuwa mshairi wa Khalifa wa Banu Umayya, Vile vile Banu Umayya waliwashirikisha watu wa Dhima katika kazi za serikali. Sergoon Ibn Mansour Al-Rumi alikuwa mwandishi wa Muawia Ibn Abi Sufian, na mwenye kuificha siri yake, pia Ibn Athaal alikuwa daktari wake.
Mambo haya ya kweli yalitajwa na zaidi ya mwandishi mmoja kutoka Ulaya wenye uadilifu. Wiil Durant alisema : Watu wa Dhima, Wakristo, Wazaradsht, Mayahudi, na Wasabai walifurahia kwa kiasi kikubwa kwa usamehevu katika zama za Banu Umayya, hatukupata mfano wake katika nchi za Ukristo katika siku hizi. Walikuwa wenye uhuru kuhusu katika kudhihirisha alama za dini yao, wakahifadhi makanisa yao na mahekalu yao [Kisatul Hadhatah, 12/131, Darul Jiil], kisha akasema pia : Mayahudi walikuwa katika nchi za mashariki za chini waliwakaribisha Waarabu waliowaachia uhuru kutoka jeuri ya watawala wao waliotangulia, wakawa wakifurahia uhuru wao kamili katika maisha yao na katika kudhihirisha alama za dini yao.
Wakristo walikuwa na uhuru kusherehekea Iddi zao hadharani. Na mahujaji wa Wakristo wanakuja kwa makundi wana usalama kwa ajili ya kuzuru makaburi ya Wakristo nchini Palastina. Wakristo wapinzani wa Kanisa la dola la Byzantiumu, walioteswa sana na wale Mababu wa Konstantinopo, Yerusalemu, Alexandria na Antiokia, siku hizi Wakristo hawa walikuwa na uhuru na usalama chini ya utawala wa Waislamu [Kisatul Hadhatah, 12/131].
Thomas Arnold pia alisema : Hatukusikia kuhusu majaribio yeyote yaliyopangwa kwa ajili ya kuwalazimisha wasio Waislamu kujiunga Uislamu, au kuhusu mateso yaliyopangwa kwa ajili ya kutokomeza kwa dini ya Ukristo [Al-Dawah Ila Al-Islam, uk. 99, Maktabatul Nahdhatul Misriyah], halafu alisema (uk.51) :
Waislamu washindao walitendeana na Waarabu Wakristo kwa usamehevu mkubwa tangu karne ya kwanza ya Hijra, na usamehevu huu uliendelea katika karne zilizofuata, na tunaweza kuhukumu kwa ukweli kwamba makabila ya Wakristo waliojiunga Uislamu walisilimu kwa hiari yao na utashi huru, na kwamba katika siku hizi Waarabu Wakristo wanaoishi kati ya makundi ya Waislamu ni dalili ya usamehevu huu.
Blasco Ibáñez mwanafikira wa Kihispania alizungumza kuhusu Ufunguzi wa Kiislamu kwa Andalus akisema: Hispania iliwapokea vizuri watu waliokuja kwake kutoka bara la Afrika, iliwapa kijiji pasipo na uadui. Basi si hivyo tu, kundi la Waarabu walipokaribia kijiji kimoja, milango ilifunguliwa kwao moja kwa moja na kupokelewa kwa kukaribishwa, vita hivi vilikuwa vya utamaduni, sivyo vya ufunguzi na kutesa.
Watu wa ustaarabu huo hawakuacha kuwa na fadhila na uhuru dhamira, nao ni nguzo ambayo ukuu wa watu unajengwa kwayo. Katika miji walioimiliki walikubali Makanisa ya Wakristo na kuuza kwa mayahudi, na miskiti haikuogopa mahekalu ya dini yaliyoitangulia, walijua haki zao, wakakaa pasipo na kuhusudu kwao wala kutaka kutawala kwao [Fanul Hukm fi Al-Islam kwa Mustafa Abu Zaid Fahmi, uk. 387, Al-Maktabul Masri Al-Hadith].
Kutokana na yaliyotangulia, maneno haya yana makosa ya kihistoria. Katika historia yote ya Kiislamu watu wa Dhima walitekeleza na kudhihirisha alama za dini yao na ibada zao kwa uhuru na heshima kwa mujibu wa mpango wa Waislamu uliotawala na uliowalazimisha Waislamu kuwakubali wengine na kuwatendea wema na watu wa kitabu. Si kweli kwamba walikuwa hawaruhusiwi kutekeleza ibada zao au kushitaki katika mahakama, vitu hivi havikutokea katika historia yote isipokuwa katika hali za pekee ambazo ahaziwakilishi historia ya Kiislamu. Ni juu ya mtu kurejea yaliyoandikwa kuhusu Waislamu walipoingia Misri na nchi nyingine, namna gani walitendeana na watu katika nchi hizi, kama mtu akitaka kujua maelezo kuhusu dini maalum, ni juu yake kupambanua kati ya maandishi yenye uadilifu na kutopendelea, na maandishi yenye uadui. Na kwa upande mwingine kuna tofauti kubwa kati ya hukumu za dini na vitendo vya wanaohusika na dini hii katika baadhi ya wakati. Si vitendo vyote vya Waislamu vinabebwa na Uislamu au vinapitishwa na Uislamu.
Na Mweyenzi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi ya wote.

Share this:

Related Fatwas