Mipaka ya Kuwa na Mwingiliano Katik...

Egypt's Dar Al-Ifta

Mipaka ya Kuwa na Mwingiliano Katika Jamii Isiyo ya Kiislamu

Question

Kwa kadiri gani inaruhusiwa kwa Waislamu kuwa na mwingiliano katika nchi za kimagharibi? Mambo gani miongoni mwa mila na desturi ambayo mtu anaruhusiwa kuyafumbia macho katika nchi hizi? Mambo gani yanaruhusiwa kuyaacha, kwa mfano: Hijab kwa wanawake, kutahiriwa kwa wanawake na wanaume?

Answer

`Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Asili ya uhusiano kati ya Waislamu na wasio Waislamu ni kuishi pamoja na kuwa na maingiliano. Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema katika Quraani: {Enyi watu! Hakika Sisi tumekuumbeni kutokana na mwanamume na mwanamke. Na tumekujaalieni kuwa ni mataifa na makabila ili mjuane. Hakika aliye mtukufu zaidi kati yenu kwa Mwenyezi Mungu ni huyo aliye mchamngu zaidi katika nyinyi. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua, Mwenye khabari.} [AL-HUJURAAT: 13], Hekima yake kutokana na kujaalia katika hali hii ni kwa ajili watu wajuane. Mgawanyiko huu ambao Mwenyezi Mungu amewafunulia ni mfumo wa kufafanua kwa ajili ya kuwaunganisha kwa tofauti zao bila ya ugumu au kutowezekana kwake.
Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema pia: {Mwenyezi Mungu hakukatazini kuwafanyia wema na uadilifu wale ambao hawakukupigeni vita, wala hawakukutoeni makwenu. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wafanyao uadilifu} [AL-MUMTAHINAH: 8] Quraani imebainisha kuwa Wema na uadilifu ni pamoja na wale ambao hawakukupigeni vita, wala hawakukutoeni makwenu. Wema ni: Aina zote za kheri, sheria imetuongoza tuwasiliane pamoja, Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: {Sema: Enyi Watu wa Kitabu! Njooni kwenye neno lilio sawa baina yetu na nyinyi: Ya kwamba tusimuabudu yeyote ila Mwenyezi Mungu, wala tusimshirikishe na chochote; wala tusifanyane sisi kwa sisi kuwa Waola Walezi badala ya Mwenyezi Mungu. Na wakigeuka basi semeni: Shuhudieni ya kwamba sisi ni Waislamu.} [AAL IMRAN: 64]. Na kwa kutekeleza uwasiliano huu Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: {Leo mmehalalishiwa kila vilivyo vizuri. Na chakula cha walio pewa Kitabu ni halali kwenu, na chakula chenu ni halali kwao. Na pia wanawake wema miongoni mwa Waumini, na wanawake wema miongoni mwa walio pewa Kitabu kabla yenu, mtakapo wapa mahari yao, mkafunga nao ndoa, bila ya kufanya uhasharati wala kuwaweka kinyumba.} [AL-MAIDAH: 5].
Mtume S.A.W, ametoa hotuba ya mwisho katika Hadithi iliyopokelewa kutoka kwa Jabir Ibn Abdullah R.A, akisema: “Enyi watu, hakika Mola wenu ni mmoja na wote mmetokana na Adam na Adam ameumbwa na udongo. Hakuna Mwarabu aliye bora kuliko Muajemi na Muajemi mbora kuliko Mwarabu isipokuwa kwa kumcha Mwenyezi Mungu” Imepokelewa kutoka kwa Al-Baihaqi na At-Termedhi katika tafsiri aya hii kutoka kwa Abi Hurairah R.A, alisema: Mtume S.A.W, alisema: “Hakika Mwenyezi Mungu amekuondoleeni kiburi cha zama za Ujahili na fahari yake hakuna kwa wazazi wa watu muumini anayemcha Mwenyezi Mungu au mwovu mpotofu, nyinyi ni wana wa Adam, na Adam ameumbwa kwa udongo.”
Mwislamu ameamuriwa kuonesha huruma, tabia nzuri, kuishi pamoja na watu wake au wanaoishi pamoja naye miongoni mwa wasio Waislamu, awe anawapa zawadi na awe anakubali zawadi zao, na awe anawasalimia kwa kuwakaribisha na kuwaheshimu, huku akicheka nao. Mwenyezi Mungu atawaongoza kwake, nayo ni dua nzuri ambayo Mwenyezi Mungu amemwamuru Mtume wake S.A.W, akisema: {Waite waelekee kwenye Njia ya Mola wako Mlezi kwa hekima na mawaidha mema, na ujadiliane nao kwa namna iliyo bora. Hakika Mola wako Mlezi ndiye anaye mjua zaidi aliye ipotea Njia yake, na Yeye ndiye anaye wajua zaidi walio ongoka.} [AL-NAHLl: 125].
Lakini hairuhusiwi kuingiliana kuwa kinyume cha utambulisho wa kiislamu, haachi yaliyofaradhishwa na Mwenyezi Mungu au kuhalalisha yaliyoharimishwa na Mwenyezi Mungu kwa madhumuni ya kuwa na maingiliano, basi hali hii hairuhusiwi, lakini hali hii ni kuyeyuka katika jamii siyo kuishi wala si kuingiliana. Mwislamu akilazimishwa kuacha faradhi au tendo la haramu, ni lazima kupambanua kati ya makundi mawili: La kwanza ni kundi la hukumu ambazo ni thabiti. La pili ni hukumu ambazo ni za kidhana; hukumu ambazo ni thabiti zinahusiana na masuala ambayo Waislamu wote wameyaafikiana; ambapo hakuna nafasi yeyote kwa ajili ya jitihada, kwa mfano: Wajibu wa kusali sala tano, kutoa katika Zaka, kufunga mwezi wa Ramadhani, kuharimisha uzinifu, riba, dhuluma, na vitendo vichafu. Hukumu hizi ni thabiti hazikubali kubadilika, na mwanadamu hathubutu kuyafanya makosa haya isipokuwa katika hali ya dharura kutegemea kadiri yake.
Kuhusu hukumu za kudhaniwa, ni zile ambazo dalili zake zinadhaniwa, ikiwa kwa upande wa mapokezi au kwa upande wa maana, na mifano yake ni mingi, nazo ni zile ambazo wanazuoni wamezitofautisha, na kuhusu anayelazimishwa kwa hukumu hizi huweza kufuata mtazamo ufaao kwake unaorahisisha maisha yake, na hakuna aibu katika hali hii.
Na mtu katika hali zote anatakiwa kufuata wenye elimu wakweli, anawauliza na anaongozwa nao, kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Basi waulizeni wenye ilimu ikiwa nyinyi hamjui.} [AL-ANBIYAA: 7].
Ama kuhusu Hijab: Ni wajibu kwa wanawake, na hairuhusiwi kwa mwanamke yeyote kuvua Hijab isipokuwa akiogopa dhara kwake au kwa jamaa zake.
Kuhusu tohara: Inaruhusiwa kwa mzazi kuwatahiri wanawe wakiume. Wanazuoni wana mitazamo miwili kuhusu tohara: Baadhi yao wamesema ni wajibu, nao ni wanazuoni wa madhehebu ya Shafi na ya Hanbali [Asna Al-Mataalib 4/165, toleo la Dar Al-Kitaab Al-Islami, Kashaaf Al-Qinaa1/81, toleo la Dar Al-Kitaab Al-Ilmiyah], na baadhi yao wanaona kuwa tohara ni Mustahab (Jambo lenye kupendekezwa) na hakuna dhambi yeyote kwa anayeiacha, nao ni wanazuoni wa madhehebu ya Hanafi na Maliki [Al-Inayah Sharhul Hidayah 7/422, toleo la Dar Al-Fikr, Al-Taj wal Ikliil4/394, toleo la Dar Al-Kitaab Al-Ilmiyah]. Lakini kuhusu kuwatahiri wa kike, fatua siku hizi ni kutoruhusiwa baada ya kujitokeza madhara yake, hali hii imethibitishwa kupitia tafiti, makongamano ya kitiba, uchunguzi na ufuatiliaji. Msingi unaozingatiwa kwa sheria ni kwamba hakuna madhara, na haikupokelewa kutoka kwa Mtume S.A.W, kuwa aliwatahiri wanawe wa kike A.S, lakini imepokelwa kutoka kwake kuwa amewatahari Al-Hassan na Al-Hussein A.S.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi ya wote.

Share this:

Related Fatwas