Kutoa Zaka ya Mali kwa Wanao Simami...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kutoa Zaka ya Mali kwa Wanao Simamia Kufundisha Lugha ya Kiarabu

Question

Naishi katika moja ya nchi za Ulaya na huko niliko palianzishwa Jumuiya ya Wamisri. Je? inajuzu kuitolea Zaka Jumuiya hii? Na hasa kwa kuzingatia kuwa inalishughulikia suala la ufundishaji wa lugha ya Kiarabu kwa watoto wa wamisri wanaoishi nchini humo?

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Zaka ni mojawapo ya Nguzo za Uislamu. Quraani Tukufu imeainisha njia za kutoa Zaka kwa mujibu wa kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Sadaka hupewa (watu hawa): Mafakiri na Masikini na Wanaoitumikia na Wanaotiwa nguvu nyoyo zao (kwa ajili ya Uislamu) na katika Kuwakomboa watumwa na katika Kuwasaidia Wenye kudaiwa na katika (Kutengeneza) Mambo aliyoamrisha Mwenyezi Mungu na katika (Kupewa) Wasafiri (walioharibikiwa). Ni faradhi inayotoka kwa Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi (na) Mwenye hikima} [AT TAWBA,60]
Kwa hiyo, Jumuiya iliyoanzishwa na Wamisri katika hiyo nchi inashughulikia mafundisho ya Lugha ya Kiarabu, na elimu za Dini na wala haina chanzo chochote cha mapato. Wale wanaofundisha wanalipwa kwa ajili ya mafundisho hayo na kwa mujibu wa haja zao, na kwa hiyo basi, hakuna kizuizi chochote cha kisheria kinachotaka isitolewe Zaka kwa ajili ya Jumuiya kama hii ili ipatiwe kiasi cha kutosheleza Jumuiya na wanaoishughulikia.
Kutokana na yaliyotangulia jibu limepatikana
Naye Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi ya wote

Share this:

Related Fatwas