Hukumu ya Kuvaa Viatu Vilivyotengen...

Egypt's Dar Al-Ifta

Hukumu ya Kuvaa Viatu Vilivyotengenezwa kwa Ngozi ya Nguruwe.

Question

Ni ipi hukumu ya kuvaa viatu vilivyotengenezwa kwa ngozi ya nguruwe? 

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Ni kweli katika sheria kwamba nguruwe ni haramu kula nyama yake na pia kwa matumizi yake, kwa kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Yeye amekuharimishieni mzoga tu na damu na nyama ya nguruwe na kilicho tajiwa, katika kuchinjwa kwake, jina la asiye kuwa Mwenyezi Mungu} [AL BAQARAH 173].
Na kama sheria ilimharamisha kuliwa nyama ya nguruwe na matumizi mengine ya mnyama huyu, basi imeharamisha pia kumuuza na kunufaika nae. Kwa hiyo basi kutoka kwa Jabir Bin Abdullah R.A.wote wawili, kwamba alimsikia Mtume wa Menyezi Mungu S.A.W. akisema: "Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu ameharamisha kuuza mvinyo, mizoga ya wanyama, nguruwe na masanamu". Basi pakasemwa ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Unaonaje mafuta ya mnyama aliyekufa, yakatumiwa katika kuzipakaa meli na kupakaa mwilini katika ngozi, na watu wakayatumia katika chakula cha asubuhi? Basi akasema: "Hapana; hayo yote ni haramu".
Kisha Mtume S.A.W. akasema: "Mwenyezi Mungu amewapiga vita mayahudi; Mwenyezi Mungu alipoharamisha mafuta yao, basi mayahudi wakayaboresha na wakayauza na wakala thamani yake". [Wanavyuoni wameafikiana juu ya hili jambo].
Na kutoka kwa Ibn Abaas R.A. wote wawili, alisema: Nilimwona Mtume S.A.W. akiketi katika pembe, basi akainua macho yake angani kisha akacheka na akasema: "Mwenyezi Mungu amewalaania mayahudi" mara tatu, "Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu aliwaharamishia mafuta, basi wao wakayauza na wakala thamani yake, na Mwenyezi Mungu Mtukufu anapowaharamishia watu fulani kula kitu chochote, basi huwaharamishia thamani yake". [Imepokelewa na Ahmad na Abu Dawud].
Na sababu ya uharamu wa kuuza nguruwe na kufaidika kwa pato linalotokana na nguruwe, Jamhuri ya wanavyuoni inaona kuwa nguruwe ni najisi akiwa hai na akiwa amekufa. Lakini wanavyuoni wa Madhehebu ya Maliki wanaona kuwa nguruwe ni twahara akiwa hai na ni najisi akiwa maiti.
Na kutokana na hayo na katika tukio la swali hilo: Basi haijuzu kuvaa viatu vilivyotengenezwa kutokana na ngozi ya nguruwe, kwani hayo yanakwenda kinyume na makatazo ya Mtume S.A.W. alipozuia kuuza nguruwe na kunufaika nao.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi ya wote.

 

Share this:

Related Fatwas