Kununua Nyumba kwa Njia ya Ugharami...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kununua Nyumba kwa Njia ya Ugharamiaji wa Benki

Question

Tafadhalini niambie ni hukumu ya kisheria juu ya kununua nyumba hapa Australia kwa njia ya benki, ambapo benki ina shiriki kama ni mtoaji fedha, hapo bei ya nyumba inakadiriwa kwa mfano Dola laki moja, na utaratibu wa benki ni kama ufuatavyo:
1- Benki inafanya mkataba wa deni kwa mnunuzi kwa kiasi cha Dola laki moja na elfu ishirini, kwa ziada yakiasi cha Dola elfu ishiri ni mbali ya thamani ya asili, hapo kiasi cha asili kitalipwa kwa makato yanayogawanywa katika miaka kadhaa, kwa mujibu wa makubaliano.
2- Benki italipa kiasi cha Dola laki moja kwa mwenya nyumba.
3- Benki kwa upande wake ima itauhifadhi mkataba wa kumiliki nyumba na hapo haiukabidhi kwa mnunuzi ila baada ya kulipa kiasi chote, au inamkabidhi mkataba lakini mnunuzi hawezi kuiuza nyumba bila ya kupata ruhusa ya Benki.
4- Katika hali ya kuwepo mnunuzi mpya, na mnunuzi wa kwanza anataka kuuza, hapo pande mbili wanakubaliana na kiasi kipya kiwekwa mfano Dola laki moja nanusu, makato yaliyokwishalipwa ya mnunuzi wa kwanza yatakatwa yawe kwa mfano Dola elfu sitini, na mabaki ya kiasi yawe Dola elfu tisini yatalipwa kwa mnunuzi wa kwanza, na kiasi cha Dola laki moja na hamsini kitalipwa kwa makato, pamoja na ziada inayohusu mnunuzi wa kwanza aliyokubaliana na Benki.
 

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Matendeano haya kwa uhakika wake ni kuuza kwa makato; na inaamuliwa kisheria kuwa: Inasihi kuuza kitu kwa bei fedha taslim au kwa bei ya kuahirishwa kwa muda maalum, na ziada ya bei kwa kuahirishwa muda maalum inajuzu kisheria kwa mtazamo wa wanachuoni wengi; kwa sababu sura hii ni mfano wa Mrabahah (uwekezaji), nayo ni aina ya mauziano ya kujuzu kisheriaambapo ndani yake ziada katika bei ni kutokana na kuahirishwa kwa muda, kwa sababu ingawa muda katika hakika yake si mali lakini katika matendeano ya Mrabahah thamani huongezwa kwa ajili yake, na unapotajwa muda maalum kwa mkabala wa nyongeza ya thamani, na kwa ajili ya makubaliano ya pande mbili juu ya hilo, na kutokuwepo ulazima wa katazo, na kwa ajili ya mahitaji ya watu wakiwa wauzaji au wanunuzi, na haya hayahesabiwi kuwa aina ya riba, kwa sababu msingi wa sheria kuwa: Kuwepo bidhaa huondosha riba.
Kwa mujibu wa swali: Matendeano haya ni aina ya kuuza kwa makato, na pia ni aina ya Mrabahah ambao unajuzu, pia inajuzu kwa mnunuzi wa kwanza kuuza kwa mtu yeyote kwa kupitia Benki, na kwa bei inayokubaliwa na yeyote amtakaye, na hakuna ubaya wowote kisheria katika matendeano haya.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi ya wote.

 

Share this:

Related Fatwas