Mwanamke Kujipaka Vipodozi Hafifu

Egypt's Dar Al-Ifta

Mwanamke Kujipaka Vipodozi Hafifu

Question

Je, Inajuzu kwa mwanamke kujipamba macho na midomo kwa rangi za kawaida lakini huonesha sura na wasifu wa macho na midomo? 

Answer

 Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Naam, hayo yote yanajuzu kuyafanya iwapo tu ni kwa njia ya kawaida isiyopelekea fitna, kwani huingia katika mapambo ya wazi yanayoruhusiwa kwa mwanamke, jinsi yalivyo ni kama kupaka uwanja na kupaka hina ambavyo vyote vinaruhusiwa. Wamekubaliana wanazuoni wa Fiqhi kuwa inajuzu kwa mwanamke kujipaka wanja hata kama ni kwa kujipamba, na wakatoa tamko la kujuzu kuutia rangi nyekundu na kwa idhini ya mume wake, na hayo yote ni kwa kuwa sheria inachunga kuwa mwanamke huwa juu Zaidi ya mapambo kwa maumbile yake.
Na Qur`ani takatifu inaeleza hayo kwa kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Ati aliye lelewa katika mapambo, na katika mabishano hawezi kusema kwa bayana?} [AZUKHRUF: 18]. Yaani: Sheria haikumzuia mwanamke kupenda kujipamba kwake bali imemruhusu kujipamba kwa pambo linaloonekana. Basi Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema: {wala wasioneshe uzuri wao isipo kuwa unao dhihirika} [ANUUR 31] na hayo ni mavazi, uso na mikono miwili, na baadhi ya wanazuoni wamezidisha na miguu miwili.
Imamu Al Qurtubiy amesema katika Tafsiri yake [229/12], Pambo linalopatikana na lile ambalo mwanamke hujaribu kujipamba kwalo ni kama vile nguo, wanja au hina. Bali sheria imemuelekeza mwanamke aichunge tabia hii ya kupenda kujipamba na kuuhifadhi urembo au mapambo yake. Ikaja amri ya Mtume ikiwataka wanawake wajipake hina, kwa maana ya kujiremba viganja vyao kwa hina hiyo. Na katika maana yake ni kila kitu anachojipambia kwacho mwanamke viganjani mwake. Na Mtume S.A.W, akachukizwa kwa mwanamke huyo kuacha kujipamba mpaka mwili wake ukawa hautofautiani na mwanaume.
Kwa hivyo basi Imamu Ahmad amepokea katika Musnadi yake kutoka kwa Ibn Dhamrah Bin Sayed kutoka kwa bibi yake kutoka kwa mmja wa wakeze kwamba amesema: Na alikuwa akisali katika kibla mbili(ilipokuja amri ya kubadilisha kibla) pamoja na Mtume S.A.W, akasema: Mtume S.A.W. akaingia na akasema: "Paka hina; miongoni mwenu wapo wanaoacha kupaka hina mpaka mikono yao inakuwa kama ya kiume. Akasema: Hakuacha kujipaka hina mpaka alipoiaga dunia."
Na akitaka atajipaka hina hata akiwa na umri wa miaka thamanini. Lakini kwa wakati huo huo achunge isitokee hali hiyo kwa namna inayoibua hisia na fitna, kwani kumzuia kwake ni kumzuia kudhihirisha mapambo yake ambayo ni fitna, na kumzuia kuonesha mapambo hayo ya fitna isipokuwa hayo mapambo kwa yule aliyehalalalishiwa kuyaona kwa kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na waangushe shungi zao juu ya vifua vyao, wala wasionyeshe uzuri wao ila kwa wanaume wao, au baba zao, au baba wa waume zao, au watoto wao, au watoto wa waume zao, au kaka zao, au wana wa kaka zao, au wana wa dada zao, au wanawake wenzao, au iliyo wamiliki mikono yao ya kuume, au wafwasi wanaume wasio na matamanio, au watoto ambao hawajajua mambo yaliyo khusu uke. Wala wasipige chini miguu yao ili yajulikane mapambo waliyo yaficha. Na tubuni nyote kwa Mwenyezi Mungu, enyi Waumini, ili mpate kufanikiwa} [AN NUUR 31].
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni mjuzi zaidi ya wote.

 

Share this:

Related Fatwas