Uoanishaji Kati ya Msingi wa Kutol...

Egypt's Dar Al-Ifta

Uoanishaji Kati ya Msingi wa Kutolazimisha Katika Dini na Jihadi

Question

 Mimi ni Mwislamu mpya, nimesoma katika rejea za Kiislamu kuwa Jihadi ni faradhi ya wajibu mpaka Siku ya Kiyama. Pia hapana kulazimisha katika Dini. Maana ya Jihadi ni nini? Je, inapaswa kwa Waislamu kupiga vita wasio Waislamu popote walipo na kuwachinja? Ni kwa njia gani hali ya kutolazimisha katika Dini inatekelezwa pamoja na uwepo wa Aya ifuatayo: {Na ikisha miezi mitukufu basi wauweni washirikina popote muwakutapo, na washikeni na wazungukeni, na wavizieni katika kila njia. Lakini wakitubu, wakashika Sala, na wakatoa Zaka, basi waachilieni. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe Mwenye kurehemu} [ATAWBAH: 5].
Na Hadithi ifuatayo pia inasema: “Nimeamrishwa niwapige vita watu mpaka washuhudie kwamba: Hapana mwenye kuabudiwa kwa haki ila Mwenyezi Mungu, na kwamba Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu, kusimamisha Swala na kutoa Zaka”. Naomba kwa ukarimu wenu mnibainishie namna jinsi inavyowezekana kuoanisha kati ya Jihadi na kukataza utenzaji nguvu katika Dini?

Answer

 Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Asili ya uhusiano kati ya Waislamu na wasio Waislamu ni kuishi pamoja kwa amani na wala siyo kwa vita; kwa mujibu wa kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Mwenyezi Mungu hakukatazeni kuwafanyia wema na uadilifu wale ambao hawakukupigeni vita, wala hawakukutoeni makwenu. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wafanyao uadilifu} [AL MUMTAHANAH: 8].
Na kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na wakielekea amani nawe pia elekea, na mtegemee Mwenyezi Mungu. Hakika Yeye ndiye Mwenye kusikia Mwenye kujua} [AL ANFAAL: 61]. Dalili za Kisheria zimo kwenye Qur`ani na Sunna na vitendo vya Waislamu katika zama zilizopita, dalili ambazo zinasisitiza kuishi pamoja kwa amani, ambapo Waislamu walifungua akili za watu kabla ya kufungua nchi zao, na hali hii haipingi kuwa Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu ni haki ya kujitetea dhidi ya uadui na kuondosha udhalimu, nayo ni kupigana siyo kuua, yaani Mwislamu hapigani na asiye Mwislamu kwa sababu yeye si Mwislamu tu, bali Mtume wa Mwenyezi Mungu ameharimisha kushambulia mahali pa Ibada pa wasio Waislamu, na kwamba adui kama akiacha udhalimu wake hairuhusiwi kabisa kwa Waislamu kumshambulia baada ya kuwa hivyo, kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu katika Aya ifuatayo {Na piganeni katika Njia ya Mwenyezi Mungu na wale wanao kupigeni, wala msianze uadui. Kwani Mwenyezi Mungu hawapendi waanzao uadui.} [AL BAQARAH: 190], yaani ni vita vya heshima kwa ajili ya kuondosha udhalimu na uadui na siyo kupigana kwa watu kama wanavyoeneza baadhi ya wajinga.
Kama nguzo na masharti ya Kisheria ya Jihadi hayakutekelezwa kama yalivyotajwa na Wanazuoni wa Sheria basi Jihadi hiyo hairuhusiwi, lakini mara itakuwa ufisadi katika ardhi, na mara nyingine itakuwa uhaini na kutotimiza ahadi. Siyo kila vita ni Jihadi, wala siyo kila mauaji katika vita huruhusiwa. Siyo kutoka katika Uislamu wala sio miongoni mwa mafunzo yake Waislamu kuwashambulia wasio Waislamu popote walipo. Jambo hili ni kuuzulia Uislamu au kutozifahamu hukumu zake.
Ama kuhusu Aya iliyotajwa katika swali hili inahusiana na waliovunja ahadi, wakapigana vita na Waislamu, wakawaua kwa uhaini, wakawafuatilia ili kuwaua, Mwenyezi Mungu amewaamuru Waislamu kujitetea dhidi ya Washirikina. Kwa hivyo maudhui ya Aya hizi inathibitisha hivi, ambapo Mwenyezi Mungu Mtukufu aliwasifu Washirikina akisema: {Hawatazami kwa Muumini udugu wala ahadi; basi hao ndio warukao mipaka} [ATAWBAH: 10] .
Ama kuhusu Hadithi iliyotajwa na Mtume wa Mwenyezi Mungu kuhusu wenye kuritadi ambao wametoka nje ya mfumo wa umma wa nchi za Kiislamu na waliojaribu kuwapiga vita Waislamu, mfano wa watu hawa wanahukumiwa katika kila mazingira na utamaduni kwa shutuma za hiyana kuu ambayo isiyosamehewa.
Pamoja na hivyo, Mtume S.A.W. alifungua mlango wa msamehe kwa waliotoka nje ya mfumo akisema mwishoni mwa Hadithi hii kama ifuatayo: “Basi mwenye kufanya hivyo, basi amejinusurisha nami nafsi yake na mali yake ila kwa haki yake.” Kisha akasema: “Na hisabu yake ni juu ya Mwenyezi Mungu”, yaani pigano hili kwao linategemea vitendo vyao kutoka nje ya mfumo wa Umma. Na kwamba uhuru wa itikadi una masharti ya kutotoka nje ya mfumo wa umma. Hali hii inalazimisha kutofautisha kati ya dhana mbili muhimu nazo ni: “Jihadi” na “Irjaf” (Kueneza habari za uongo ili kuchochea fitana): istilahi ya “Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu” ni istilahi ya Kiislamu muhimu ina dhana yake pana katika Uislamu; inaitwa kwa kupambana na nafsi, matamanio, na Shetani, inaitwa pia kwa kupigana na adui inayokusudiwa kuondosha kwa uadui na udhulumu. Aina hii ya Jihadi ina masharti haikuwa sahihi isipokuwa kwa masharti haya, miongoni mwao ni kuwepo kwa Khalifa wa Waislamu anayewahamasisha raia wake Waislamu kwa Jihadi, kuwepo kwa bendera wazi ya Kiislamu, kuongeza nguvu kwa Waislamu; nayo ni miongoni mwa faradhi za kutoshelezeana [Kifaya] zinazopangwa na Watawala waliojaliwa na Mwenyezi Mungu mamlaka ya nchi na ya waja[wa Mwenyezi Mungu Mtukufu] na wanao uwezo wa kujua matokeo ya maamuzi haya zaidi kuliko wengine, ambapo wanaangalia dharura ya Jihadi hii, kwa hivyo, amuzi wa Jihadi unachunguzwa kwa uhalisia kutoka pande zake zote kwa ajili ya kupambanua kati ya maslahi na ufisadi, pasipo na woga wala unyonge, wala kijujuu au vurugu au huruma isiyo na hakika isiyohukumiwa kwa hekima au akili, nao watalipwa thawabu kutegemea jitihada zao kwa kila hali, kama wakifikia malengo watalipwa thawabu mara mbili, na wakiyakosa malengo watalipwa thawabu mara moja tu, wakiwa na kasoro watapata dhambi, na yeyote hana la kusema ila kushauri tu kama akiwa miongoni mwa wenye kushauri. Kama hakuwa miongoni mwa wenye kushauri basi hairuhusiwi kusema kuhusu jambo hana ujuzi, wala haruhusiwi kuanza kwa nafsi yake katika Jihadi au atakuwa na masingizio juu ya Khalifa. Inawezekana madhara ya kutoka nje ya mfumo wa nchi ni zaidi kuliko manufaa, ilhali atapata dhambi ya ufisadi wake huu. Jihadi ni faradhi ya lazima katika nchi zinazoshambuliwa na madhalimu kwa utakatifu wa Waislamu na sehemu takatifu zao. Ni lazima Waislamu kuzitetea, na katika wakati huu hukumu ya Jihadi ni faradhi ya Kifaya kwa wanaoishi nje ya nchi, ila ikihitajiwa msaada wa majirani zao kutoka kwa Waislamu, hukumu ya Jihadi wakati huu itakuwa faradhi ya lazima. Lakini kutekeleza kwa hukumu hii ya Kisheria inapaswa kuwa na njia sahihi zinazohusiana na Watawala wanaojua mambo ya kivita, kisiasa, kiuhalisia, na wanaosimamia tathmini ya haja au kutokwepo kwa haja hii, na wanaozingatia matokeo, maslahi, na ufisadi unaohusiana na masuala ya kitaifa na mikataba ya kimataifa, na kujua ukubwa wa nguvu za kimataifa.
Vitu hivi vyote vinahitaji kuchunguzwa kwa kina na kusomwa kwa upande wa kivita, kisiasa, na inazingatiwa uchauzi wa amani uliotajwa katika kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu kama katika Aya ifuatayo: {Na wakielekea amani nawe pia elekea, na mtegemee Mwenyezi Mungu. Hakika Yeye ndiye Mwenye kusikia Mwenye kujua} [AL ANFAAL: 61]. na kulinda usalama wa nchi za Kiislamu, raia wao, maslahi yao kwa upande mwingine, uwezo wao wa kupambana na kuvumilia chaguo la vita kwa upande wa tatu, ili jambo hili lifanyike kwa njia rasmi na inayoainishwa umbo lake inaaminiwa watakao Jihadi ili wasiwe mateka kwa pande zinazotiliwa shaka, zinazowatumia hisia zao, na hamasa zao kwa kuhudumia malengo yao ya nje kwa jina la Jihadi kwa upande wa nne.
Hayo yote ni masuala yanayohusiana na fiqhi ya umma, ambayo yanaangaliwa na mifumo, majeshi, taasisi kubwa tu. Na hayahusiani na fiqhi ya watu, na hawawezi kuamua kuhusu hatima ya mataifa. Wanaotawala Waislamu tu ni wenye mamlaka juu ya masuala hayo, hata kama hawakujitihadi, basi hali hii haifanyi Jihadi ikalemazwa pamoja na kulinda mapengo na mipaka.
Na hakuna sababu yeyote kwa kukiuka mipaka ya mfumo wa ujumla wa kundi la Waislamu ili maumizi ya vita yawe kupitia watu ovyo, hali ambayo inasababisha kuangamia nchi maangamivu makubwa, licha ya vitendo hivi vya mabomu ambavyo havihusiani na Jihadi ya Kiislamu wala vita heshima. Istilahi ya Jihadi katika Sheria maana yake ni kutayarisha majeshi, kulinda mipaka, kuhifadhi mapengo, na mambo hayo ni miongoni mwa faradhi za Kifaya katika Jihadi.
Pia kutayarisha kwa “njia za kuzuia uhalifu” ni muhimu sana zaidi kuliko vita venyewe; kwa sababu njia hizi zinasitisha umwagikaji damu, Qur’ani imeashiria hali hii katika kauli yake: {Basi waandalieni nguvu kama muwezavyo, na kwa farasi walio fungwa tayari-tayari, ili kuwatishia maadui wa Mwenyezi Mungu na maadui zenu} [AL ANFAAL : 60].
Kisha Jihadi ambayo ina maana ya kupigana haikusudiwi yenyewe, kupigana na wasio Waislamu hakukusudiwi pia kinyume na wanaofikiri wenye mitazamo mikali inayofanya asili kwa wasio Waislamu kuwa damu yao ni halali, wakati ambapo wanazuoni wa Sheria wamebainisha kwamba Waislamu wanapofanya faradhi ya Kifaya kupitia kulinda mapengo na mipaka ya nchi za Kiislamu, basi ulinganiaji unatosha badala ya kupigana na wasio Waislamu, na ulinganiaji unapokuwa sahihi, basi hakuna haja ya Jihadi, na kwamba kumwua kafiri hakukusudiwi kamwe, na jihadi ni chombo tu haikusudiwi yenyewe.
Ama kuhusu wanayoyasema wale ni “Irjaf” siyo Jihadi, nayo ni istilahi inayotajwa katika Qur’ani katika kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Kama wanaafiki na wale wenye maradhi nyoyoni mwao, na waenezao fitna katika Madina hawatoacha, basi kwa yakini tutakusalitisha juu yao, kisha hawatakaa humo karibu yako ila muda mchache tu (60) Wamelaanika! Popote watakapo onekana watakamatwa na watauliwa kabisa (61) Hii ni ada ya Mwenyezi Mungu iliyo kuwa kwa wale walio pita zamani. Wala hutapata mabadiliko katika ada ya Mwenyezi Mungu.(62)} [AL AHZAAB : 60-62], nalo ni neno lenye maana yake mbaya, maana yake ni kueneza fitna kupitia kuhalilisha kumwaga damu na kushambulia mali kati ya wanajamii chini ya madai tofauti, miongoni mwao ni : Kudai kuwa mtawala katoka katika Uislamu, au serikali ya nchi, au makundi maalum ya watu, na miongoni mwa madai hayo ni kuhalilisha kumwaga damu za wasio Waislamu chini ya dai la kuamrisha mema na kukataza maovu, au kuhalilisha kumwaga damu za wasio Waislamu katika nchi zao, au wale walioingia nchi za Kiislamu kwa kudai kuwa nchi zao zinapigana na Uislamu…n.k kuhusu madai ya kueneza fitna zinazoshawishwa na Shetani kwa waenezao fitna, na ambazo baadhi yake zilikuwa sababu ya kujitokeza kwa Khawarij katika wakati wa Masahaba na wanaokuja baada yao wakatoa sababu za ufisadi wao katika ardhi na kumwaga damu ambazo ni haramu.
Katika wakati huu utawala unatofauti kufuatana na dhana yake; wanavyofanya wenye mitazamo mikali katika nchi za Kiislamu kuhusu kuwaua watalii, au katika nchi zisizo za Kiislamu miongoni mwa shughuli za kujitoa mhanga, au vitendo vengine vya ufisadi vinavyotokea mbinu za “Irjaf”, vitendo vyote hivi ni haramu, navyo ni aina ya dhuluma iliyoharimishwa katika Sheria, na kuwapiga wenye mitazamo hii kama hawajiepushi na kuwadhuru Waislamu na wasio Waislamu wakiwa wananchi waliopewa amani, na kuitoa jina la Jihadi ni uwongo ili wenye akili dhaifu wasadiki ufisadi wao na kueneza fitna zao, na hali hii ni jeuri katika nchi bila ya haki, wenye jeuri hii ni wadhalimu wapigwe kama wakiwa na nguvu mpaka waepushe udhalimu wao na kueneza fitna.
Siku hizi kuingia nchini kwa njia rasmi kupitia viza ya kuingia au ya kupita, na viza hii ni kibali cha kuingia nchi kwa amani kwa mujibu wa mikataba ya kimataifa na desturi za ubinadamu. Kuruhusiwa kwa kuingia nchi tu kuna maana ya kupata amani, na imetajwa kwamba amani anapewa kupitia chochote kinachomaanisha hivyo. Kwa hivyo, imethibitishwa kuwa viza ina maana ya kupewa amani, na ahadi zote zinazofanyika kupitia viza zitimizwe. Ahadi inafanyika kwa chochote kinachomaanisha hivyo, yaani asiye Mwislamu yeyote akiingia nchi za Kiislamu kwa haja yeyote - ikiwa kwa ajili ya utalii au haja nyingine- akapewa amani, basi hairuhusiwi kumwaga damu yake wala kuiba mali yake. Na hivyo ndivyo Wanazuoni walivyosema kuhusu dhana ya amani kunailazimisha kwa asiye Mwislamu\kupata amani hata akiwa ni adui wa kivita, hata akipewa amani kwa njia ya kosa.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi ya wote.

Share this:

Related Fatwas