Mgawanyo wa Malipo ya Serikali na M...

Egypt's Dar Al-Ifta

Mgawanyo wa Malipo ya Serikali na Mali ya Bima kwa Warithi Unapotokea Msiba.

Question

 Natarajia nitaijibiwa kuhusu hukumu za Sheria katika kile kilicholipwa na serikali na mashirika ya bima ya Uingereza kutokana na kifo cha mwanangu aliyekuwa akisoma huko; katika hali hii Sheria ya kiingereza inalipa haki na mirathi zote kwa mjane wa marehemu, na sio kwa warithi wote kwa mujibu wa sheria ya kiislamu, kwa hiyo tumefungua akaunti ya akiba kwa jina la mjane katika benki moja ili kupokea kila kilichotumwa, kama vile:
1- Bei ya nyumba iliyokuwa ikimilikiwa na aliyekufa, itauzwa baada ya kifo.
2- Bei ya gari lake binafsi, pia litauzwa baada ya kifo.
3- Kiasi cha malipo badala ya kifo yanayolipwa na wizara ya Afya ya Uingereza, ambapo hulinganisha na mshahara wa wa miaka miwili au mitatu kama ni haki ya aliyekufa.
4- Kiasi cha mshahara kamili kwa muda wa miezi mitatu na nusu, ambapo kifo chake marehemu kilitokea mwezi wa September 2004.
5- Kiasi cha fidia ya bima au ya upande mwingine, kwa mtazamo wa kwamba kifo hicho kilitokea wakati wa kazi.
6- Kiasi cha fedha kwa jina la aliyekufa kinachowekwa katika benki Uingereza.
7- Mshahara wa upande wa mwajiri wa Uingereza kwa mjane na kwa muda wa maisha yake yote.
8- Mshahara wa upande wa mwajiri wa Uingereza kwa mtoto wa kike, aliyezaliwa baada ya kifo mpaka atakapokamilisha masomo yake.
9- Vitu binafsi vya aliyekufa kama vile: vitabu, tafiti, tasnifu za kielimu, nguo… n.k.
Inatakiwa kubainisha kinachohusu mke mwenyewe; mke na mtoto wa kike mwenyewe; na mirathi inayogawanywa kisheria, kwa kujua kuwa wazazi wawili wa marehemu wangali hai, na waliamua wawili kuchangia malipo yao yote ya mirathi kwa mtoto mdogo wa kike.

Answer

  Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Kuhusu kiasi cha badala ya kifo na fidia ya bima au upande wowote pamoja na mshahara unaohusu mjane na mtoto mdogo; navyo ni vigawanyo vya mirathi vya: Tatu, Tano, Saba, na Nane, vyote ni haki halisi kwa anaehusika navyo kwa jina lake halisi, na mbali na warithi wengine; kwa sababu vitu hivi ni kama michango na tuzo, kwa hiyo haviingii katika mgawanyo wa mirathi ya kisheria.
Kuhusu vipengele vingine vyote ni mirathi ya aliyekufa, na ni haki za warirhi wake wote, kwa kuwa ni kwa jina lake na vilikuwa miliki yake alipofariki.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi ya wote.

Share this:

Related Fatwas