Mirathi ya Bahaii Kutoka kwa Mwisl...

Egypt's Dar Al-Ifta

Mirathi ya Bahaii Kutoka kwa Mwislamu

Question

Je inajuzu Bahaii kumrithi mwislamu akiwa ni katika warithi wake au haijuzu? 

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Ofisi ya Fatwa ya Misri imekwisha bainisha msimamo wa Uislamu juu ya Ubahaii na Ubabii katika Fatwa yake nambari 329 ya mwaka wa 1980 kuwa: Ubahaii au Ubabii ni kundi linalonasibishwa na mtu anayeitwa Mirza Ali muhammad, na lakabu yake ni Bab, na Yeye alianza kulingania mwito wa madhehebu yake katika mwaka 1260 H.\1844M., kwa kutangaza kuwa analenga usahihishaji wa yaliyovurugwa katika hali za waislamu, na kurekebisha yaliyoenda kombo.
Yeye alianza mwito wake huko Shiraz kusinimwa Iran, na baadhi ya watu wakamfuata, akatuma kikundi kati yao kwa pande mbalimbali za Iran kutangaza kuwepo kwake, na kueneza madai yake kuwa yeye ni Mtume wa Mungu, akatunga kitabu kiitwacho [Al-Byan], ambapo alidai kuwa kilicho ndani yake ni sheria iliyoteremshwa mbinguni, akadai kuwa risala yake imeitengua sheria ya kiislamu, akazua kwa wafuasi wake huku muzinazopinga hukumu za kiislamu na misingi yake; akafanya saumu kuwa siku kumi na tisa, akaainisha siku hizi ziwe katika majira ya hewa nzuri ya Vuli, ili siku kuu ndogo kuwa siku ya Nairuzi kila mara, akahesabu siku ya kufunga kutoka kuchomoza Alfajiri mpaka kuzama jua, akataja katika kitabu chake [Al-Bayan] Ibara ya: “Siku maalum, tukaifanya siku ya Nairuzi kama siku kuu kwenu baada ya kuzimaliza”.
Hivyo mwanzilishi wa madhehebu hii aliitisha mkutano uliofanyika katika Jangwa la Badasht huko Iran katika mwaka 1264H.\1848M., akatangaza misingi ya madhehebu hii na matawi yake kuwa imeondolewa na kuepushwa na Dini ya Uislamu na sheria yake. Wanachuoni wa zama zake walipinga wito wake na kudhihirisha ubaya wake, na wakatoa Fatwa na kubainisha ukafiri wake, akafungwa Shiraz na baadaye Asfahan, na baada ya fitina na vita kati ya wafuasi wake na waislamu, aliadhibiwa kwa kifo kwa kusulubiwa juu ya msalaba mwaka 1265H.
Kisha Khalifa wake Mirza Hussein Ali, aliyejiweka lakabu ya Bahaullahi, na akatunga kitabu kiitwacho [Al-Aqdas], kikifuata njia ya kitabu cha [Al-Bayan], kilichotungwa na kiongozi wa madhehebu hii Mirza Ali Muhammad, na yeye alipinga misingi ya Uislamu, bali ailizipinga Dini zote, akavunja kila lililopo katika Uislamu Imani na Sheria. Aliifanya sala kuwa Rakaa tisa katika mchana na usiku, na kibla ya wabahaii katika sala yao wanaelekea upande ambao Mirza Hussein aitwaye Bahaullahi yupo, kwa kuwa alisema katika kitabu chake hicho: “Mkitaka kusali mwelekee nyuso zenu upande wangu uliotakasika”, vile vile aliondosha Hija, akatoa usia wa kuporomosha Nyumba tukufu ya Mwenyezi Mungu wakati wa kuwepo mtu mwenye uwezo na shujaa kati ya wafuasi wake. Pia wabahaii walifuata kauli za wanafalsafa waliotangulia ambapo walisema kuwa ulimwengu ni wa kale: “Bahaai alijua kuwa ulimwengu hauna mwanzo wa zamani, nao umetolewa kwa milele kutokana na uumbaji wa kwanza, na siku zote viumbe walikuwa na muumbaji wao na Yeye alikuwa nao”.
Kauli ya muhtasari katika madhehebu hii, nayo ni Ubahaii na Ubabii kuwa: Ni madhehebu ya kubuni na ya mchanganyo watofauti katika dini zote, kama vile: Ubudha, Ubrahama, Upagani, Uzradishti, Uyahudi, Ukristo, Uislamu, na Imani za undani. Wabahaii hawaamini ufufuo baada ya mauti, Pepo wala Moto, wamefuata kauli ya watu wa Dahari, na kiongozi wao wa kwanza alidai katika tafsiri ya Suratu Yusuf kuwa yeye ni bora kuliko Mtume Muhammad S.A.W, na akapendelea kitabu chake [Al-Bayan\ kuliko Qur`ani Tukufu. Wao hawaamini Unabii wa Bwana wetu Muhammad S.A.W, na kuwa yeye ni Mwisho wa Manabii. Kwa hiyo wao si Waislamu ; kwa sababu waislamu kwa jumla wanaamini Qur`ani kuwa kitabu cha Mwenyezi Mungu, na ilivyokuja ndani yake kauli tukufu: {Muhammad si baba wa yeyote katika wanaume wenu, bali yeye ni Mtume wa Mungu na Mwisho wa Mitume}.
Mtaalamu Al-Alusiy katika tafsiri yake ya Aya hii alitaja kuwa: “Kikundi cha Mashia wenye msimamo mkali wa medhihiri katika enzi hii, wakajipa jina la (Wababii), na wao wana maoni ambayo hukumu yake ni ukafiri kutokana na maoni ya wenye akili”, Al-Alusiy akaongeza: “Kuhusu Mtume S.A.W ni Mwisho wa Manabii kama kilivyotamka kitabu na ilivyobainisha Sunna na ulivyokubaliana Umma wote, basi anayedai kinyume cha hayo ni kafiri na akiyashikilia madai yake anauwawa”.
Kwa hiyo waislamu walikubaliana kwa pamoja kuwa imani ya Ubahaii au Ubabii si imani ya kiislamu, na anayeamini madhehebu hii si miongoni mwa waislamu, na ni mwenye kuritadi katika Dini ya Uislamu; Mwenye kuritadi ni mtu aliyeacha Dini ya Uislamu na kwenda dini nyingine, na Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: {Na watakaotoka katika dini yao katika nyinyi, kisha wakafa hali ya kuwa makafiri, basi hao ndio ambao amali zao zimeharibika katika dunia na Akhera. Nao ndio watu wa motoni, humo watakaa milele}.
Wanachuoni wa Fiqhi ya Uislamu walikubaliana kwa pamoja kuwa: Inawajibika kumuua Menye kuritadi akishikilia msimamo wake kwa Hadithi tukufu iliyopokelewa na Bukhariy na Abu-Dawud: “Aliyebadilisha dini yake muueni”, pia wanachuoni walikubaliana kwa pamoja kuwa: Mwenye kuritadi katika Uislamu akioa haisihi ndoa yake na mkataba wa ndoa yake ni batili, akiwa na mwanamke mwislamu au asiyemwislamu; kwa sababu hana uamuzi wa kisheria kufunga ndoa; pia damu yake haiheshimiwi kisheria asipotubu na kurejea Uislamu tena na asikane dini aliyokea.
Katika hali hii mtu mwenye jukumu akiamini Ubahaii iwe dini yake basi huwa ni mwenye kuritadi katika Dini yaUislamu, na haijuzu kwa mwanamke mwenye swali, naye ni mwislamu aolewe naye, na wakifunga ndoa basi mkataba ni batili kisheria, na kuingiliana kwao ni zinaa haramu katika Uislamu: {Na anayetaka dini isiyokuwa ya Kiislamu basi haitakubaliwa kwake. Naye Akhera atakuwa katika kwenye khasara (kubwa kabisa)}. [AALI IMRAN: 85].
Kwa mujibu wa hayo, na katika hali ya swali: Mtu akiamini Ubahaii kama dini yake na kushikilia maamrisho yake, yeye anakuwa hana haki ya mirathi ya mrithiwa wake mwislamu.
Na Mwenyezi Munguni Mtukufu ni Mjuzi zaidi ya wote.

 

Share this:

Related Fatwas