Kutendeana na Baraza la Kiislamu Ka...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kutendeana na Baraza la Kiislamu Katika Ndoa na Kutangaza Uislamu

Question

Mwanamke wa Kimisri ameolewa na Mmisri, wameishi Ujerumani wakapata uraia wa kijerumani, ndoa ilifungwa kwa mpangilio wa Sheria ya Ujerumani, kisha alikwenda pamoja na mume wake kwenye Baraza la Kiislamu Ujerumani na ndoa ilifungwa kwa kuwepo wakili wa mke na mashahidi wawili wa Kiislamu, na Mwenyekiti wa Baraza la Kiislamu alifunga ndoa kwa mujibu wa kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunna ya Mtume S.A.W, ikitimizwa na nguzo zote na masharti yake ya kisheria, na mfungishaji wa ndoa aliandika sehemu ya mahari iliyotolewa na iliyobaki, na kwa mujibu wa hayo mume na mke walipata muhuri wa Jumuiya ya kiislamu ya Ujerumani iliyopo Munich.
Nimeacha nyumba ya wazazi wangu ili kukaa pamoja na mume wangu katika nyumba ya familia, ugomvi ukatokea kati yetu, na hayo yalipelekea mume kuipinga hati ya ndoa iliyofungwa katika Baraza la Kiislamu kwa kudai kuwa Dini ya Uislamu haitambuliwi Ujerumani, pia akatushitaki mimi, mama yangu, na Mwenyekiti wa Baraza la Kiislamu.
Mwenye swali anaomba ufafanuzi wa hukumu ya kisheria kwa yafuatayo:
Kwanza: Upeo wa usahihi wa ndoa iliofungwa katika Baraza la Kiislamu, yenye muhuri wa Jumuiya ya Kiislamu ya Ujerumani?
Pili: Nini maana ya tendo la mume wangu dhidi ya mwenyekiti wa Baraza la Kiislamu na dhidi yangu (mke), je ni kutia shaka katika ndoa au jaribio la kukwepa majukumu aliyoyasaini mbele ya waislamu wengi wakati wa sherehe za ndoa hapo Ujerumani?
Tatu: Kuna tatizo lolote katika kutendeana kwa waislamu na Baraza la Kiislamu la Ujerumani?
Nne: Wajerumani wanaotaka kutangaza Uislamu wao wanakwenda kwenye Baraza la Kiislamu, na sisi tunawaongoza kwenda baraza hili, je kuna kosa lolote la kisheria au hapana?
 

Answer

 Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Kwanza: Miongini mwa Sunna za Mwenyezi Mungu katika viumbe vyake ni ndoa, Mwenyezi Mungu amesema: {Na katika Ishara Zake (za kuonesha ihsani zake juu yenu) ni kuwa Amekuumbieni wake zenu katika jinsi yenu ili mupate utulivu kwao, naye Amejaalia mapenzi na huruma baina yenu. Bila shaka katika haya zimo Ishara kwa watu wanaofikiri}. [AR RUUM: 21].
Na Bwana wetu Mjumbe wa Mwenyezi Mungu S.A.W amesema: “Enyi kongamano la vijana! Mwenye uwezo wa kuoa basi aoe, kwani hilo linamsaidia kuinamisha macho na kulinda uchi wake. Kwa yule asiyeweza basi afunge kwani kufanya hivyo kunampunguzia matamanio”, na ufungaji wa ndoa ukitimiza nguzo zake na masharti yake basi ni sahihi, na unaambatana na matokeo kama vile haki ya mke katika mahari, kupatikana starehe kwa mke wakati wa kuingiliana, na kuwepo talaka ikitokea kabla ya kuingiliana au baada yake.
Katika uhalisia wa swali:Kwa kuwa ndoa hiyo ilifungwa kwa njia iliyobainishwa na mwenye swali, yaani kuwepo walii, mashahidi wawili kwenye Baraza la Kiislamu, basi ndoa hiyo ni sahihi na hakuna ubaya wowote, na ndoa hiyo ipo, na inaambatana na majukumu yake yote.
Pili: Alivyofanya mume dhidi ya mkewe, mama yake na Mwenyekiti wa Baraza la Kiislamu kama vile madai na mashtaka na mengineo ni jambo lisilo la kiutu na halina kisingizio chochote wala msingi sahihi, isipokuwa kama kuna jambo jingine ambalo hatulijui, ikiwa swali ni kama lilivyo, inaonekana –na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi- kuwa anataka kukwepa majukumu aliyosaini wakati wa kufunga ndoa.
Tatu: Hakuna ubaya wowote juu ya Waislamu Ujerumani kutendeana na Baraza la kiislamu lililotajwa.
Nne: Wajerumani wanaotaka kutangaza Uislamu wao wanapokwenda Baraza la kiislamu Ujerumani ni jambo la kawaida, kwa sababu ni upande wa madaraka na usimamizi kukidhi masilahi ya dini ya Waislamu, na kuwaelekeza waislamu kwenye Baraza hili ni jambo lisilo ubaya kisheria.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi ya wote.

Share this:

Related Fatwas