Siku ya Mwisho

Egypt's Dar Al-Ifta

Siku ya Mwisho

Question

Inazingatiwa kuwa “Siku ya Mwisho” ni katika imani za Kiislamu ambayo haina tofauti yeyote ndani yake, nayo ni siku ambayo watafufuliwa ndani yake wafu wote na kufanyiwa hesabu pamoja na hukumu zao kutolewa, na hii inamaanisha - kwa mujibu wa ufahamu wangu - kuwa watu wote waliofariki watabakia kwenye makaburi yao mpaka siku hiyo, lakini mimi ninadhani kuwa fikra zangu huwenda zikawa zinagubikwa na makosa na wala sio sahihi, na hili ni kwa sababu mbili zifuatazo:
Ya kwanza: Ni kuwa kila mwili wa mwanadamu unaharibika kikamilifu baada ya muda maalumu na kuwa udongo, na kitu kisicho kufa kwa mwanadamu ni ile nafsi, kwa maana ya maada ya roho ya Kiungu ambayo Mwenyezi Mungu aliipulizia kwa kila mwanadamu kwa kauli ya Qur`ani. Na Dini ya Kiislamu inafundisha - kwa kiwango cha utambuzi wangu - kuwa mwanadamu anapolala au pale anapofariki roho yake hukabidhiwa kwa Mwenyezi Mungu, kisha hurejeshewa tena katika hali ya kulala usingizi lakini hushikwa moja kwa moja na Mwenyezi Mungu katika hali ya kifo, na hili linamaanisha kuwa nafsi (roho) baada ya kufariki mwanadamu moja kwa moja inakuwa ipo mbele ya Mwenyezi Mungu na wala sio kaburini.
Ya pili: Imepokelewa kwa Mtume S.A.W. katika safari yake ya Israa kuwa, Mtume alisali na Mitume na kuwa Imamu kisha baada ya hapo alikutana kwa mfano na Nabii Mussa katika moja ya mbingu na kuzungumza naye, Mitume na manabii hawa walishafariki kwa muda mrefu na japo kuwa ni hivyo lakini Mtume alikutana nao hali ya kuwa wakiwa hai, na kwa hivyo basi,
Je Kiyama chao kilishasimama? Na je tunaweza kumalizana na hilo - na hili ndio asili ya swali langu - kuwa siku ya Kiyama kwa mujibu wa fikra za mwanadamu sio siku iliyopangwa, isipokuwa ni tukio lipo linatokea kwa mwendelezo, kiasi ambacho kila nafsi iliyokufa ambayo inarejea kwa Mweneyezi Mungu moja kwa moja inakamilika hesabu yake moja kwa moja? Je? mbele ya Mwenyezi Mungu kuna uelewa mwingine kama tunavyofahamu hilo kwenye Qur`ani?
 

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Kuhusu roho, na Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema: {Na wanakuuliza kuhusiana na roho, sema: Roho imetokana na amri ya Mola wangu, na wala hamjapewa elimu nalo isipokuwa ni kidogo}[AL ISRAA, 85].
Yenyewe haifungamani na kanuni duni ambazo zinahukumu maisha ya dunia, isipokuwa Ulimwengu wake ni mpana na haupakani na mipaka na wala mbele yake hakuna vizuizi.Na pindi Mwenyezi Mungu anapokuwa anatupa habari kuwa yeye anapozichukuwa roho za watu waliolala na zenyewe huwa zinakuwa kwake, kwa hakika hili halimaanishi kuwa aliyelala ni mwili tu pasi ya roho ndani yake, isipokuwa yeye yupo hai na roho ndio siri ya uhai huo, na imepokelewa toka kwa Mtume S.A.W. kuwa amesema: “Pindi anapolala mja hali ya kuwa amesujudu, Mwenyezi Mungu hujifaharisha kwa malaika na kusema: Muangalieni mja wangu, roho yake ipo kwangu na yeye akiwa amenisujududia”
Na vile vile hali ya mtu aliefariki, kupandishwa kwa roho yake kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu hakupingani na uhusiano wake na mwili wake, kiasi ambacho mwenye roho anamsikia yule mwenye kumtembelea pale kaburini na kumjibu yule anaemsalimia kama ilivyokuja katika Hadithi, na katika hilo anasema Ibn Al-qayyim katika kitabu “Roho” roho ni jambo lingine sio kama mwili, yenyewe inakuwa juu, mbele ya Mwenyezi Mungu hali ya kuwa imeungana na mwili wa maiti, kiasi kwamba anaposalimiwa mwenye roho hujibu na yenyewe ikiwa kwenye sehemu yake, na huyu ni Jibril A.S. Mtume S.A.W. alimuona akiwa na mbawa zake mia sita, miongoni mwa hizo mbawa mbili zimetanda na kufunika anga, na akawa anamsogelea Mtume S.A.W. mpaka akaweka magoti yake mbele ya magoti ya Mtume na mikono yake juu ya mapaja yake, na nyoyo za watakatifu hupanuka kwa imani, kwamba kuna uwezekano kuwa yeye alikuwa akisogea,na kusogea huku hali ya kuwa yeye yupo katika makazi yake ya mbinguni.
Maimamu wameuzungumzia Ulimwengu wa mfanano, na Imamu Suyuty akatunga ujumbe wake ambao aliuita: [Al-Munjiliy Fii Tatwawwuril Waliy], na kunukuu ndani yake toka kwa mwanachuoni Alaa Ddiin Al-Qaunawy kuwa amesema: “Na amethibitisha mwanachuoni wa kisufi kati ya Ulimwengu wa miili na ule wa roho wameuita “Ulimwengu wa mfanano” na wakasema wenyewe kuwa Ulimwengu huu ni wenye upole sana kuliko Ulimwengu wa miili na mpana kuliko Ulimwengu wa roho, na wakajengea juu ya hilo umbile la roho na kudhihirika kwa muonekano tofauti na Ulimwengu wa mfanano, na wakachukuwa dalili kwa kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: {aliyejifananisha kwake kama mtu kamili} [MARYAM, 17].
Kisha akasema Imamu Suyuty: Na katika ushahidi ni Hadithi iliyopokelewa na Ahmad na Annisai kutoka kwa mtoto wa Abbas R.A. anasema: Amesema Mtume S.A.W.: “baada ya kupelekwa safari ya usiku na kurudi Makkah nikafahamu kuwa kuna watu watanipinga… akaitaja Hadithi mpaka aliposema: Wakauliza je waweza tuelezea sifa ya msikiti? Kwani kuna watu wameshawahi kwenda kwenye huo msikiti, Mtume S.A.W. akasema: Nikawa ninatoa sifa zake nikaendelea mpaka zikanipotea baadhi ya sifa, basi msikiti ukaletwa hali ya kuwa ninaungalia mpaka ukawa karibu na nyumba ya Aqiil au Uqaal, nikawa ninatoa sifa zake hali ya kuwa ninaungalia”
Na hii ima ni katika hali ya ufananishaji kama vile kuona pepo au moto, ima ni katika hali ya kukunjwa kwa umbali, na katika yanayofahamika kuwa watu wa Baitul Maqdis hawakupoteza katika muda huo, mji wao, kutokana na hilo kama ilivyopokelewa na Ibn Jarir na Ibnu Abi Haatim na Ibn Mundhir katika tafsiri zao na kutoka kwa Ibn Abbas katika kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: {kama Yusuf asingeliona dalili ya Mwenyezi Mungu wake}.
Akasema: Alifananishiwa Yakobo, na imetokana na Ibn Jarir kama vile ilivyotokana na Said Ibn Jubeir na Hamid Ibn Abdrulrahman na Mujahid na Kassim Ibn Abibazza na Akrama na Muhammad Ibn Siirin na Qatada na Abisaleh na Shamar Ibn Atiyya na Dhihaak, na imetokana na Al-Hassan amesema lilikunjuka dari la nyumba na akamuona Yakobo, na katika tamko lake amesema aliona sanamu la Yakobo, kauli hii kutoka kwa hawa waja wema waliotangulia ni dalili ya kuthibitika hali ya mfananisho au kukunjwa ardhi na kupunguzwa masafa yake, nao ni ushahidi mkubwa katika maswala yetu ambapo Nabii Yussuf A.S. alimuona baba yake hali ya kuwa yeye yupo Misri wakati huo baba alikuwa katika ardhi za Shamu, basi ndani yake kuna uthibitisho wa kumuona mzee Yakobo A.S. sehemu mbili zilizo mbali ndani ya wakati mmoja na hii ni kutokana na misingi miwili ambayo tumeitaja. Na Mwenyezi Mungu ndiye Anayejua zaidi”
Kama vile ilivyo tofauti ya makadirio ya muda katika kitabu cha Mwenyezi Mungu yanarejea kwenye maana hii pia, kama kwa mfano wa kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na hakika siku moja kwa Mwenyezi Mungu wako ni sawa na miaka elfu ile munayo hisabu} [AL HAJJ, 47].
Lakini hili halipingani kwa hali yeyote ile na kuwepo kwa siku ya mwisho ambayo Mwenyezi Mungu Ameizungumzia ndani ya Kitabu chake na kupitia pia ndimi za Mitume yake yote, na kwa hakika siku hii watu watasimamishwa na kukusanywa wote kwa Mwenyezi Mungu Mola wa viumbe wote, na hii inahukumu kuwa siku hiyo wataiishi watu wote, kwa sababu Muumba wa nasaba muda na sehemu ni mwenye uwezo wa kuunganisha ufahamu wote na kuukusanya siku ya Kiyama ndani ya wakati wowote autakao.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi ya wote.
 

Share this:

Related Fatwas