Hukumu ya Twahara Pamoja na Matumiz...

Egypt's Dar Al-Ifta

Hukumu ya Twahara Pamoja na Matumizi ya Kitanzi cha Kuzuia Ujauzito

Question

Ni hukumu gani kwa mwanamke anayetumia kitanzi cha kuzuia ujauzito, ambacho kinaendelea kuwepo mwilini muda wa wiki, na haifai kuking'oa kabla ya muda huo, kwani kitapoteza kazi yake kwa hali hiyo?
Vipi inasafishwa sehemu ya kitanzi baada ya tendo la ndoa?
 

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Inajuzu kwa mwanamke kutumia njia ya kuzuia mimba yake, na kuzuia mimba kuna malengo kadhaa; basi labda huwa kwa kuogopa mwanamke kuzaa na hatari ya kuachwa, na labda huwa kwa sababu ya kuogopa wingi wa watoto, na labda huwa kwa kujiepusha kutokana na haja na taabu ya kipato. Na wakati mwingine huwa ni kwa ajili ya kuendeleza uzuri wa mwanamke na sifa yake ya kuendelea kustarehe. Na huwa kwa ajili ya nia na malengo mengine ambayo yanapelekea kuzuia mimba.
Na hayo ni malengo ambayo sheria haikuyakataza kama anavyosema Hoja ya Uislamu Imam Al Ghazaliy katika kitabu chake: [Ihiyaa Uluum Adeen 52/2,Ch. Dar Al Maarifah]. Na malengo haya siyo mambo ya uboreshaji tu bali miongoni mwake yapo ya uboreshaji katika asili yake na ya kihaja kwa mwelekeo wake. Nalo ni jambo ambalo wanalizungumza wanachuoni wa Usuul kama ni Kikamilishaji cha mwenye kuhitaji, nalo ni lile lisilojitosheleza kwa haja isipokuwa kwa njia ya kuungana, basi huwa na hukumu ya kihaja. Kama vile mwanamke kuulinda uzuri wake kwa mlingano wa urefu wake na kutokuwa na mafuta yaliyounenepesha mwili kwa namna ambayo itamwepusha na matamanio na kumlinda kwa ndoa.
Na miongoni mwake yapo ambayo ni yenye kuhitajika tu Kama vile uzito wa wingi wa watoto pamoja na udhaifu au kuketi na kutofanya mambo yao. Na miongoni mwake yapo ambayo ni ya kidharura; kama vile kuogopea maisha ya mwanamke kutokana na hatari ya uzazi kwa kutolewa habari kutoka kwa daktari anayetegemewa.
Basi kutumia njia za kuzuia mimba -na miongoni mwake kitanzi cha kuzuia ujauzito- ni katika upande wa kujitibu ambapo huondosha uzito kwa wenye kubeba majukumu, na kitanzi hicho huwa wakati huo ni katika hukumu ya piopio (hogo) katika kujuzu kupaka maji juu yake ikiwezekana kufanya hivyo, na kuacha kupaka maji juu yake yakiwa maji hukidhuru au kuchelewesha kupoa kilichopo chini yake.
Na wanachuoni wa Fiqhi wameijulisha piopio kwamba ni bandeji yenye dawa huwekwa juu ya jeraha na mfano wake, au juu ya jicho lenye ugonjwa.
Na inayozingatiwa katika Fiqhi ni kwamba haishurutishwi katika piopio ambayo inajuzu kupaka maji juu yake kuwa ni katika jambo linalolazimishwa ambapo huogopwa ndani yake maangamizi au kukurubia maangamizi, bali huwa pia katika vitu ambavyo kwa kuviacha kwake mtu hujiepusha na matatizo.
Imam Al Qarafiy Al-Maliki amesema katika kitabu cha: [Azakhirah 319/1] "Amesema katika hiki kitabu: Patapakwa juu ya sehemu ya dawa ya kitanzi kwa kupitisha juu kucha, na karatasi juu ya shavu (upande mmoja wa uso) kwa ajili ya dharura. Mtungaji wa kitabu cha: [Atwaraz] amesema: Wala haishurutishwi katika hali hiyo kuwe ni kuosha, kwa kuwa ni dharura, au kuogopa kutumia maji kwa kuzidi ugonjwa au kuchelewa kupona.
Na wanachuoni wa Maliki wamesema juu ya kujuzu kupaka maji juu ya piopio katika hali ya ugonjwa mwepesi, Bali na juu ya kupaka kwenye kilemba kikiwa ni vazi kwa wale wenye vyeo na pakachelewa kukivua kwake. Na hapana shaka kuwa kuruhusiwa kwa mwanamke kupaka maji katika kitanzi kilichotumika kuzuia ujauzito ni bora kutokana na usheria wa kufanya hivyo, kwani haja yake kwa ruhusa wakati huo ni zaidi kabisa kuliko yaliyotajwa.
Sheikh Aswawiy amesema katika kitabu chake: [Hashiyat Aswawiy Ala Asharhu Aswaghiir] katika mlango wa kupaka maji juu ya piopio kwenye tamko la mwanachuoni mkubwa Adarderiy: "Na iwapo kaogopa kuosha sehemu hiyo, mfano wa jeraha kama vile kutayamamu basi atapaka maji juu yake". Kwa maana kuwa ikiwa kuna jeraha au uvimbe au lengelenge au mchubuko wa kuungua au mfanowe na kadhalika, na inaogopwa kwake katika kutawadha au kuosha, atapata ugonjwa au kuzidi ugojwa wake au kuchelewa kupona –kama ilivyotangulia katika Tayamamu- Hakika hiyo huruhusiwa kama wajibu iwapo yataogopwa maangamizo au madhara makubwa, kama vile kuzorotesha manufaa, na kujuzu pia ikiogopwa maumivu makali au kuogopwa kuchelewa kupona. (Na kama hakuweza basi juu ya piopio….. kisha juu ya karatasi kwenye upande mmoja wa uso kwa ajili ya dharura. Au kilemba kikiwa ni vazi kwa wale wenye vyeo na pakahofiwa kukivua kwake).
Na kauli yake: (Shida ya maumivu… na kadhalika), maana yake ugonjwa ambao hauzoroteshi manufaa, na hilo ni ambalo watu wengine wameelezea kwa ugonjwa mwepesi, ama kama aliogopa taabu kwa kuosha kwake basi haijuzu kupaka maji… na Tamko lake ikiogopwa kukivua: Ni kwa maana kukiondosha kwa kuwa kwake ni katika mabwana wakubwa wenye vyeo na ambao vazi lao ni kilemba.
Na pia Imamu Abu Hanifah amejuzisha katika yaliyopokelewa kutoka kwake na wanachuoni wa Kimaliki katika tamko lao kupaka maji juu ya pete pamoja kutofika maji chini yake; kwa kupimia juu ya Khofu ambayo imejuzu kupaka maji juu yake ingawa muda mrefu wa kuvaa kwake.
Imamu Burhanu Adiin Bin Mazahwa Hanafiy amesema katika kitabu cha: [Al Muhitw 7/1]: "Na iwapo katika mkono wake kutakuwa na pete na ikawa ni pana hakuna ulazima wa kuitikisa au kuivua, na iwapo itakuwa inabana basi katika dhahiri ya mapokezi (wamesema) maswahibu wetu, rehema ya Mwenyezi Mungu Mtukufu iwe juu yao, hapana budi kuivua au kuitikisa. Na Al Hassan alipokea kutoka kwa Abi Hanifah, na Abu Sulaiman kutoka kwa Abi Yusuf na Muhammad kwamba hakushurutisha kuivua au kuitikisa, na baina ya masheikhi ni tofauti katika sura hiyo".
Imamu Al Qarafiy amesema katika kitabu cha: [Azakhirah 258/1]: "Ya nane: Amasema: Katika pete kauli tatu; Malik amesema katika kitabu cha: [Al Wadheha]: Anaitikisa ikiwa inabana na kama sio hivyo basi hapana. Na Ibn Shabaan amesema: Anatikisa kwa vyovyote vile, na kwa Malik katika kitabu cha: [Al Mwaziyah]; Haitikisi kwa vyovyote vile; kwani yeye huvaa kwa muda mrefu kwa hiyo inajuzu kwake kupaka maji juu yake kwa kutumia Kipimo cha Khofu (kwato). Amesema: "Na kama tutajuzisha kupaka juu yake na ikawa finyu tukaivua baada ya udhu na sehemu yake haikuoshwa basi haitatosha kuwa na udhu isipokuwa kupata uhakika wa maji kufika sehemu hiyo chini ya khofu, na tofauti ilijulikana kwa wale waliotawadha huku mkononi mwake kuna mstari wa unga wa ngano ulioganda."
Na kitanzi cha kuzuia mimba kinaendelea kubaki mwilini mwa mwanamke kwa muda wa wiki moja au mfano wake, akiwa na haja nacho zaidi kuliko suala la pete.
Pia wanachuoni wa Kihanafi na Kimaliki wamesema kwa usahihi wa twahara kwa anayekuwa juu ya mkono wake kitu chepesi miongoni mwa unga wa ngano, matope (udongo), wino ambao maji hayafikii chini yake; ikiwa maumbile ya kazi zao hupelekea mchanganyiko huo kwa namna ambayo inakuwa vigumu kutenganisha; kwani jambo likiwa finyu hutanuka, na ugumu huleta wepesi.
Mtungaji wa kitabu cha: [Al-Fatawa Al-Hindiyah] na katika kitabu cha" Al-Jame' Aswaghiir] akaulizwa kwa mtu mwenye kucha nyingi ambapo hubakia katika kucha zake hizo maradhi, au kwa yule ambaye anafanya kazi ya ufinyanzi, au mwanamke aliyepaka hina vidole vyake, au muuza ngozi, au mtia rangi kwenye nguo, hao wote ni sawa; udhu wao huwa unakubalika; kwani haiwezekani kujizuia isipokuwa kwa dharura. Akasema: Yote hayo ni sawa; hutosheleza udhu wao; kwa kuwa haiwezekani kujizuia nayo isipokuwa kwa uzito.
Na hukumu ya fatwa ni kujuzu bila ya kupambanua baina ya watu wa kijijini au mjini, hukumu ni kama hiyo katika kitabu cha: [Zakhirah] na hukumu ni kama hiyo kwa mwokaji mikate akiwa na kucha ndefu, na kadhalika katika kitabu cha: [Azahidiy] akinukulu kutoka kitabu cha: [ Ajame' Al Asweghar].
Na Imamu Al Qarafiy amesema katika kitabu cha: [Azakhirah 272-273/1]: "Al Bajiy amesimulia kutoka kwa Muhammad Bin Dinar kwa kilichoganda kwenye mkono wake kiasi cha nyuzi kutokana na unga wa ngano au kitu kingine maji hayafiki chini yake, basi ataswala kwa hali hiyo na hapana kitu juu yake, kwani anazingatiwa katika mila ni mwenye kuosha, na kwa yaliyopokelewa na Adar Qutwniy: "Hakika yeye Rehma zimshukie aliswali swala ya asubuhi na alikuwa ameoga janaba, na ikawa katika viganja vyake kuna sehemu mfano wa dirhamu moja hivi ambayo haijapata maji, akaambiwa: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Sehemu hii haijafikiwa na maji. Akayagusa maji yaliyo katika nywele zake na kupangusa sehemu hiyo ambayo haijafikiwa na maji na wala hakuirejea swala yake aliyoiswali". Lakini Adar Qutwniy ameidhoofisha Hadithi hii. Na kupimia juu ya kiasi hicho kichwani na baina ya vidole na pete.
Na Ibn Al Qasim amesema atarejea swala, na ikiwa ni katika vile ambavyo haiwezekani kujiepusha navyo haikunukuliwa hukumu ya ufaradhi wake. Malik amesema katika kitabu cha: [Al Mwaziah] kuhusu aliyetawadha na juu ya mikono yake kuna wino basi akaona baada ya swala maji hayakubadilisha wino: Kwa hivyo atapipitisha maji sehemu hiyo na itamtosha kama atakuwa ni mwandishi kwa kutumia wino; kwani yeye ameona kuwa mwandishi ana udhuru kinyume na mwingine. Na hayafichikani mengi yaliyopo katika njia za kuzuia mimba miongoni mwa shida ambazo hazipo katika kitanzi hiki.
Ingawa kunapatikana njia nyingine za kuzuia mimba mbali na kitanzi hiki, isipokuwa hakika matumizi ya njia hii humuhifadhi mwanamke kutokana na kufichuka uchi wake ambapo huenda njia zote zilizobakia zikamlazimisha kufichua uchi wake, na wala hakuna shaka yeyote kuwa kusitiri uchi ni wajibu uliothibitishwa na unaotangulizwa mbele ya aina zingine za wajibu pale inapotokea mkanganyo. Kwa hiyo kufuta kwake wakati wa kuoga juu ya kitanzi cha kuzuia mimba ambacho kinazuia maji kufika chini yake hutangulizwa mbele ya ufichuaji wa uchi wake mwanamke mbele ya wasiokuwa ndugu zake. Na wala hatii shaka kwa mwenye kuyafahamu malengo ya sheria kwamba tatizo la kufichua uchi ni kubwa kuliko kutoiosha sehemu hii ndogo ya mwili wake.
Na baadhi ya wanawake wana miili haikubaliki njia hizo basi matumizi yake yatakuwa wakati huo ni wajibu, lakini kama inawezekana kwa mwanamke kutumia njia nyingine zisizokuwa njia hizo basi matumizi ya kitanzi cha kuzuia mimba inajuzu, kwa kuwa yeye anajiweka mbali na madhara yanayoweza kumpata kutokana na kutumia kwake njia nyingine, na kuondosha madhara ni kusudio la kisheria ambalo kwa ajili yake inaruhusiwa katika twahara.
Na hakika kwamba matumizi ya njia hiyo ni wepesi zaidi kwa mwanamke, na yenye usalama zaidi kwake, na yenye bei ndogo kwake, na sifa hizi zinagusa katika kujitibu huwa ni katika vikamilishi vinavyolifikia lengo linalokusudiwa, na panatakiwa katika misingi ya Fiqhi kwamba ruhusa katika kitu ni katika vikamilishaji vinavyokusudiwa, kama anavyosema Imamu Abu Al Fath Bin Daqiq Al-Idi katika kitabu cha: [Ihkaam Al Ahkaam Fi Sharhu Omdatu Al Ahkaam, uk. 479, Ch. Muasasat Arisaalah.]
Na kutokana na hayo: Hakika yake hutosheleza wakati huo kupaka kitanzi cha kuzuia ujauzito kwa maji ikiwezekana; kwa kuilinganisha na bandeji. Na ikiwa haitakuwa wepesi kufanya hivyo na mwanamke akaepusha kutofika maji katika kitanzi cha kuzuia mimba yeye mwenyewe basi anaweza kuweka juu yake kitu kitakachozuia baina yake na maji, na atapaka juu yake na itamtosha katika josho lake la twahara yake.
Yote haya iwapo plasta au bandeji itakuwa imezibika na haipitishi maji chini yake, au ina dawa lakini kwa kuiosha dawa hiyo huondoka. Ama iwapo itakuwa na dawa maji yanavuja bila ya hali hiyo kuzuia utendaji wa dawa: basi hapana tatizo lolote katika kujuzu kwake; kwani hivyo, iwapo pataoshwa na pakavuja maji basi josho hilo litazingatiwa kuwa josho kwa kilicho chini yake.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi ya wote.
 

Share this:

Related Fatwas