Kusafiri Mwanamke kwa Idhini ya Mum...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kusafiri Mwanamke kwa Idhini ya Mumewe kwa Ajili ya Kutekeleza Ibada ya Umra na Hija kwa Kufuatana na Mtu Mwaminifu.

Question

Je, Inajuzu mke kusafiri kwa ajili ya kutekeleza ibada ya Umra na Hija bila ya kufuatana na maharimu wake, kwa kufuatana na mtu mwaminifu na kwa idhini ya mume wake? 

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Inajuzu kwa mwanamke kusafiri bila ya maharimu wake lakini kwa sharti la nafsi yake kupata utulivu na amani katika safari yake hiyo, kukaa kwake na kurudi kwake, na kutokupata migogoro au matatizo katika nafsi yake au dini yake.
Basi imepokewa kutoka kwa Mtume S.A.W. Miongoni mwa yaliyopokelewa na Al- Bukhariy na wengineo kutoka kwa Udaiy Bin Hatim R.A. kwamba Mtume S.A.W. Alimwambia: "Ukiishi maisha marefu utaona mwanamke msafiri anaondoka kutoka mji wa Al-Hirah hadi kutufu Kaaba haogopi mtu yeyote isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu". Na katika usimulizi wa Imamu Ahmad, Mtume S.A.W. amesema: "Wallahi ambaye nafsi yangu ipo mkononi mwake, Mwenyezi Mungu Mtukufu atatimiza amri hiyo (Uislamu) hadi mwanamke msafiri kutoka mji wa Al-Hirah na atufu Kaaba bila ya ukaribu wa mtu yetote".
Basi kutokana na Hadithi hiyo kwa simulizi zake mbili, baadhi ya wenye kujitihadi wamechukua hukumu ya kujuzu kwa safari ya mwanamke peke yake ikiwa kuna amani, na wameif anya maalumu Hadithi hiyo kutokana na Hadithi nyingine ambazo zinaharamisha kusafiri kwa mwanamke peke yake bila ya maharimu.
Na kadhalika tunaona wanachuoni wa Kimaliki na wa Kishafiy wanajuzisha kwa mwanamke kusafiri bila ya maharimu kama akiwa pamoja na wanawake waaminifu au kufuatana na mtu muaminifu, na hayo yalikuwa katika Hijja ya kifaradhi. Na wanachuoni hao wametoa dalili ya jambo hilo, kwa kutoka kwa akina mama waumini radhi za Mwenyezi Mungu ziwafikie wote, baada ya kifo cha Mtume S.A.W. kwa ajili ya kwenda kuhiji wakati wa zama za uongozi wa Omar Bin Al-Khatwab R.A. na Omar akamtuma Othman Bin Afaan R.A. aende nao kwa ajili ya kuwalinda.
Mwanachuoni mkubwa Al-Hatwab Al-Malikiy amesema katika kitabu chake: [Mawahib Ajalil Fii Sharhu Muhatswar Khalil]: "Al-Bajiy ameifungia Hadithi hiyo kwa idadi chache,(wasafiri wachache) na kauli yake ni: "Hayo kwangu mimi katika upekee ni idadi chache, ama katika safari kubwa (yenye watu wengi) basi kwangu mimi, inasihi kusafiri kwake bila ya wanawake au maharimu". Na akainukulu kutoka kwake katika kitabu cha: [Al-Ikmali] na ameikubalia na hakutaja uhitilafu wake.
Na Azanatiy akaitaja katika kitabu cha: [Sharhu Arisalah]; kwamba hayo ni madhehebu, basi ameifunga kauli ya Mtunzi na nyinginezo.
Na kauli ya Azanatiy ni: "Kama akiwa amefuatana na wenye uaminifu walio katika idadi kubwa na vifaa (zana), au jeshi lenye uaminifu lenye ushindi na nafasi kubwa, basi hakuna woga katika kujuzu kwa safari yake bila ya mtu maharimu katika safari za aina zote: Kuhusu safari katika hali zake hukumu yake ni wajibu, Sunna na halali. Kutokana na kauli ya Malik Na wengineo, yaani hapana tofauti baina ya yaliyotangulia kutajwa kwake na baina ya nchi (Mji)
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi ya wote.
 

Share this:

Related Fatwas