Kujihusisha na Bahati Nasibu Katika...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kujihusisha na Bahati Nasibu Katika Nchi Zisizo za Waislamu

Question

 Mimi naishi katika nchi ambayo kujihusisha na Bahati Nasibu kunatokea kwa wingi sana. Watu wananunua tiketi za bahati nasibu kwa kutarajia kupata mali nyingi. Ninapojadiliana nao kuhusu jambo hili wanasema kuwa: Wanaposhinda watalipa kiasi cha moja ya tano ya mali hiyo kwa kuwa hiyo ni ngawira. Je inajuzu kufanya hivyo?

Answer

 Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Bahati Nasibu ni mashindano ambayo huwashirikisha watu wengi, na kila mmoja wao huwa analipa kiasi kidogo cha fedha, kwa kutarajia kupata heshima na tuzo ya fedha taslimu baada ya kufanyika kura na kutajwa kwa mshindi, na tuzo hii ni kiasi kikubwa cha mali, au mfano wake ni kama vile bidhaa, safari n.k., maana tuzo ni jumla ya vitu vyenye vipimo tofauti vilivyotolewa na wenye mashindano.
Kushiriki katika Bahati Nasibu kwa njia hii ndiyo kamari yenyewe, kwa sababu kamari ni mafungamano wa tuzo na thamani yake ambayo ni jumla ya malipo ya washiriki, ambapo kila mmoja anaweza kukabiliana na matokeo ya aina mbili: Kushinda zawadi au kupoteza mali aliyoitoa. [Taz: Matalibu Uli-Nuha na Ar-Ruhaibaniy: 3/706, Ch. ya Almaktab Al-Islamiy; Nihayatul-Muhtaj: 8/168, Ch. ya Dar Al-Fikr].
Sheria ya Kiislamu inaharamisha ushiriki wowote unaohusika na kamari, kutokana na madhara yake kwa watu, jamii, mzunguko wa uzalishaji, na maendeleo ya kiuchumi; na Mwenyezi Mungu anasema: {Enyi mlioamini! Bila shaka ulevi na kamari na kuabudiwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu, na kutazamia kwa mishare ya kupigia ramli; ni uchafu na ni katika kazi ya Sheteni. Basi jiepusheni navyo, ili mpate kufaulu. Hakika Shetani anataka kukutilieni uadui na bughudha baina yenu kwa ajili ya ulevi na kamari na anataka kukuzuilieni kumkumbuka Mwenyezi Mungu na kusali. Basi je, mtaacha (mabaya hayo)?}. [AL MAIDAH: 90-91].
Wafuasi wa Madhehebu ya Hanafi wanaona kuwa mikataba isiyo sahihi inajuzu kwa Mwislamu kuitekeleza na asiye mwislamu katika nchi zisizo za Waislamu; As-Sarkhasiy katika kitabu cha Al-mabsuut, baada ya kutaja Hadithi yenye Daraja la Mursal ya Makuhuul anasema: “Hakuna Riba kati ya Waislamu na Maadui (Watu wanaoupiga vita Uislamu) katika nchi ya Maadui hao”. [14/56, Ch. ya Dar Al-Maarifah], nayo, Hadithi Mursal ya Makuhuul ni dalili kwa Abu-Hanifa na Muhammad Ibn Al-Hassan, kuwa inajuzu kwa Mwislamu kumwuzia kafiri dirham moja kwa dirham mbili katika nchi ya Maadui.. vile vile akiwauzia nyamafu au akacheza kamari nao, na akachukua mali zao kwa njia hiyo, na mali hii ni halali, kwa mtazamo wa Abi-Hanifa na Muhammad, Mwenyezi Mungu awarehemu”. [Mwisho].
Nchi isiyo ya waislamu iliitwa Nyumba ya Vita katika maandiko yaliyotangulia kutokana na maana iliyokuwepo katika zama za Maimamu tunaowanukulu misamiati yao, ambapo Ulimwengu wote ulikuwa ukipambana na Waislamu, hivyo nchi zote zikagawanyika na kuwa za aina mbili: Nyumba ya Uislamu ambako unasimamishwa Uislamu na maamrisho yake yakawa yanatekelezwa, na aina ya pili ni Nyumba ya vita ambapo hukumu za waislamu hazikuwa zikitekelezwa.
Lakini mgawanyo wa kisasa wa wanachuoni wa Uislamu, baada ya hali ya vita vilivyokuwa vikiendelea kumalizike, ni nchi za Waislamu na nchi zisizo za waislamu, na hukumu zake ni zilezile za Nyumba ya vita, isipokuwa mambo yanayohusu vita vyenyewe ndio hayapo kutokana na kuwa vita hivyo kwa sasa ambapo havipo.
Udhahiri wa maneno ya wafuasi wa Madhehebu ya Hanafi katika kushirikiana kwa Mwislamu katika mikataba isiyo sahihi katika Nyumba ya vita ni kwamba hukumu yake ni pana mno kuhusu riba katika hali ya kuchukua au kulipa.
Lakini Al-Kamal ibn Al-Humam alitaja kuwa Maimamu wa Madhehebu ya Hanafi katika masomo yao waliweka sharti la uhalali wa riba kwa Mwislamu aliye katika Nyumba ya vita kuwa Mwislamu aipate kutoka kwa kafiri, pia akataja katika maneno yake suala la kamari; hivyo anasema katika kitabu cha: [Fathul-Qadiir: 7/39, Ch. ya Dar Al-Fikr]:
Kuwa: “Abu-Bakr RA, kabla ya Hijrah wakati Mwenyezi Mungu alipoteremsha kauli yake: {Alif Lam Mym. Warumi wameshindwa}. Makuraishi walimwambia: Waona kuwa Warumi watashinda? Akajibu: Ndio, wakasema: Unakubali kuweka rehani? Wakawekeana rehani, na kumwambia Mtume SAW, Mtume akamwambia: “Waendee, uzidishe kiasi cha rehani, na mtu yule akazidisha”, kisha Warumi wakawashinda Waajemi. Abu-Bakr akachukua rehani, na Mtume S.A.W alijuzisha jambo hili, na hii ndiyo kamari yenyewe iliyopo kati ya Abu-Bakr na washirikina wa Kikuraishi, na Makkah katika wakati huo ilikuwa Nyumba ya Ushirikina,
Uamuzi huu haufichiki kuwapo uhalali wa kufunga mkataba ikiwa mwislamu ataipata ziada, hata hivyo riba ni pana kuliko hivi kwa sababu inakusanya kuwa dirham moja kwa dirham mbili na pande mbili ambazo ni upande wa Kafiri au wa Mwislamu, na hukumu yake ni halali kwa kila njia. Vile vile kamari ndani yake huenda ikawa na ziada kwa kafiri pale anaposhinda, kwa hiyo uhalali wake ni katika hali ya Mwislamu kupata ziada.
Wanachuoni waliamua katika tafiti zao kuwa lengo lao la kuhalalisha riba na kamari ni pale ziada anapoipata Mwislamu kwa mujibu wa sababu yake, ingawa hukumu yake kwa ujumla ni kinyume chake, na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa yote kwa kweli”. [Mwisho].
Mtaalamu Ibn Abdeen anasema katika Hashiyah yake [5/186, Ch. ya Dar Al-Kutub Al-Elmiyah], baada ya kunukulu maandiko yaliyotangulia kutoka kwa Ibn Al-Humam: “Dalili ya hayo ilivyotajwa katika As-Siyar Al-kabiir na Sherehe yake, anaposema: Mwislamu akiingia Nyumba ya vita kwa ahadi ya amani, hakuna kosa kuchukua mali zao kwa maridhiano ya nafsi zao kwa njia yeyote iwayo, kwa sababu mtu akichukua kitu hicho cha kawaida kwa njia iliyo mbali na hadaa, basi kitu hicho huwa halali kwake, mfano wa mfungwa vitani na anayepewa amani, akiwauzia dirham moja kwa dirham mbili, au akachukua mali yao kwa njia ya kamari, hayo yote ni halali kwake [mwisho kwa muhtasari].
Tazama vipi suala hapa ni kuchukua mali zao kwa maridhiano yao, tujue kuwa muradi wa riba na kamari katika maneno yao ndivyo ilivyokuwa kwa njia hiyo, hata kama lafudhi ni pana hapa, kwa mtazamo wa kuwa hukumu mara nyingi hufuata sababu yake”. [Mwisho].
Kwa hiyo, inabainika kuwa; haijuzu kushiriki katika mashindano ya Bahati Nasibu yakifanyika katika nchi za waislamu au nchi zingine; kwa sababu katika hali zote hatari ya kupoteza mali inakuwepo, na inawezekana kuutekeleza udhahiri wa Madhehebu, kama kuna masilahi kwa Mwislamu.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi ya wote.

 

Share this:

Related Fatwas