Mwanamke Kufanya Kazi Nje ya Nyumba
Question
Je, ipo tofauti kati ya mitazamo ya kifiqhi kuhusu suala la mwanamke kufanya kazi nje ya nyumba; ambapo watu wengi wa Pakistani wapinga jambo hili, na wanaona kuwa mwanamke si lazima kutoka nje ya nyumba?
Answer
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Suala hili linategemea uuwiano wa maslahi na ufisadi, na linategemea mila na desturi za kila nchi, pamoja na kutahadharisha kwamba mwanamke hakuwa na tatizo lolote katika historia ya Kiislamu, mwanamke alikula kiapo cha utii kwa Mtume S.A.W, akashiriki katika jihadi, maisha ya kitamaduni, kisiasa, kijamii, na kielimu katika historia ya Uislamu. Mpaka Bibi Aisha alitoka kwa ajili ya kukataza maovu kwa mujibu wa maoni yake.
Vile vile katika enzi ya Omar Ibn Al-Khattab R.A Al-Shifaa binti Abdullah alikuwa akiamrisha mema na akikataza maovu sokoni. Al-Hafidh Ibn Hajar Al-Asqalani amesema kuwa alichukua elimu kutoka kwa wanawake hamsini na mbili, na Mwenyezi Mungu amekieleza kisa cha Malikia Saba’a ambaye aliwaongoza watu wake kwa mafanikio kutokana na imani yake kwa Bwana wetu Sulaiman amani iwe juu yake na juu ya Mtume wetu S.AW.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi ya wote.