Mume Kuikubali Hukumu ya Talaka ya Kadhi Asiye Mwislamu.
Question
Mimi nilipeleka madai mahakamani ya kutaka mume wangu aniache. Na kutokana na hayo, Mahakama ya Wien ikatoa maamuzi yake tarahe 30 Oktoba 2002. Na kwa mujibu wa maamuzi hayo, mahakama ilimwita mume wangu na akakubali kuja na kuikubali talaka hiyo. Na hakukata rufaa ya hukumu ndani ya muda uliowekwa kisheria. Mwenye kesi anauliza: je talaka hiyo inatambulika kisheria au si ya kisheria? Mwenye swali anasema kuwa: Yeye na mume wake ni raia wa Austria, na ni Waislamu.
Answer
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Ikiwa maudhui kama ilivyotajwa katika swali, na kuwa mwenye swali amekwisha pata hukumu ya talaka kutoka kwa mume huyu, tarehe 30/10/2002, na mahakama ilimwita mume, akakiri kutokea kwa talaka hiyo na hakukata rufaa ndani ya muda uliowekwa kisheria, basi talaka hiyo imetuka kweli. Na kwa namna ilivyotajwa, jawabu limefahamika.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi ya wote.