Tendo la Ndoa Kabla ya Ndoa
Question
Ni nini hukumu ya tendo la ndoa kwa mwanamume na mwanamke kabla ya kuoana?
Answer
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Uislamu umeharamisha zinaa na kulifanya tendo la ndoa kati ya mwanamke na mwanamme liwe katika mipaka ya ndoa tu. Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: {Wala msikaribie zinaa. Hakika hiyo ni kinyaa na ni njia mbaya} [AL ISRAA 32].
Na pia akasema kwa kuwasifia waja wake waumini: {Na ambao wanazilinda tupu zao, isipokuwa kwa wake zao au kwa iliyowamiliki mikono yao ya kulia. Kwani hao si wenye kulaumiwa.} [AL MUMINUUN 6-7].
Hivyo basi, hakika dini ya Kiislamu haihalalishi namna yeyote ile ya makutano ya kimwili baina ya mwanamke na mwanamume isipokuwa kwa kufunga ndoa sahihi, kinyume cha hivyo basi ni haramu.
Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi ya wote.