Haki za Mwanamke Aliyepewa Talaka k...

Egypt's Dar Al-Ifta

Haki za Mwanamke Aliyepewa Talaka kwa Hukumu ya Kadhi Asiye Mwislamu

Question

Nimemwoa mwanamke wa Kibulgaria, aliyesilimu kabla ya ndoa yetu, tumeishi nchini Misri kwa zaidi ya miaka kumi, kwa hiyo hivi sasa anaishi nchini Uingereza kwa madai ya kupata matibabu, lakini ameamua kukaa huko na kutorejea nchini Misri, ameomba talaka katika mahakama ya Uingereza, na mahakama hiyo ikitoa hukumu ya talaka, basi ana haki ya kuchukua kiasi cha mali yangu ambayo itakadiriwa na kadhi, na hii hailingani na Sheria ya kiislamu.
Mahakama ikitoa hukumu ya talaka, je talaka hiyo ni sahihi kisheria? Na je ni halali kwake kuchukua kiasi cha mali ambacho amekipitisha Kadhi wa Uingereza? Na je ni zipi haki zangu, atakapo kataa kurejea Misri, kwa kujuwa sisi tumefunga ndoa huko uingereza?

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Maamuzi ya kisheria ni kuwa ombi la talaka la mwanamke mwislamu linakuwa kwa upande wa mume wake au upande wa kadhi mwislamu, kwa sababu ndoa na talaka ni mikataba ya kisheria inayotekelezwa na wanaohusika au wale wenye uwalii wa jambo hilo kisheria juu ya wahusika wao, na asiye mwislamu hana uwalii juu ya mwislamu. Kwa hivyo hukumu ya talaka ikitolewa na mahakama isiyo ya kiislamu basi haitambuliwi, isipokuwaikithibitishwa na mahakama za kiislamu au mabaraza rasmi ya kiislamu yanayoruhusiwa kwa kufunga mikataba ya ndoa na talaka.
Kwa mujibu wa hayo na katika uhalisia wa swali, mahakama ya Uingereza ikitoa hukumu ya talaka ya mke wako aliyetajwa hapo juu, basi talaka hii haitambuliwi kama talaka ya kisheria isipokuwa talaka hiyo itakapotolewa na wewe mwenyewe, au na kadhi mwislamu, au na hakimu mwislamu anayehusika na mambo kama hayo katika mabaraza ya kiislamu, au misikiti n.k. kwa kuwa kila kilichojengeka kwa batili, basi ni batili tu; hivyo kuchukua mali kutokana na hukumu ya mahakama ya Uingereza tu si sahihi, na wala haijuzu kuzipata mali hizi.
Wewe ulitaja katika swali lako kuwa ndoa imefungwa Uingereza: Basi mwanamke akikubali kukaa Misri kwa hiari yake kamili, hapo uhamiaji wake kwenda mahali pengine ni uasi, kwa hiyo haki yake ya kupata fedha za matumizi inaanguka, lakini asipokubali jambo hili na ikawa alikuja kwa ajili ya kujaribu maisha au kama kitu cha muda cha maisha ya kifamilia, hapo haki yake haianguki kutokana na kurejea kwake kwenda mahali pa ndoa amako ni Uingereza.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi ya wote.
 

Share this:

Related Fatwas