Hukumu ya Kucheza Chess.

Egypt's Dar Al-Ifta

Hukumu ya Kucheza Chess.

Question

Nini hukumu ya kucheza chess katika Uislamu? Na Wanavyuoni wamesemaje kuhusu mchezo huu? 

Answer

 Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Wanavyuoni wamezungumza tangu zamani na katika zama hizi kuhusu hukumu ya chess. Na Wanavyuoni wa Fiqhi miongoni mwao wameuzungumzia mchezo huu katika sehemu inayohusiana na shuhuda, ambapo wanavizungumzia vitendo vinavyofuta ushahidi.
Tukitaka kutoa hukumu ya Chess, inatupasa kujua kuwa miongoni mwa michezo kuna ya (Mubah) halali, kupendekeza, Makruhu (kuchukiza), na Haramu. Tukitaka kuingiza Chess katika hukumu mojawapo kati ya hukumu zilizopita, rai inayochaguliwa kwetu ni Mubaha (Halali). Ama tukiangalia vitu vinavyoweza kuandamana nayo pengine hukumu yake inaweza kugeuka, katika wakati huu, hukumu ya Chess pengine ni Makruhu au Haramu kwa ajili ya vitu vinavyoweza kuandamana nayo na kuigeuza hukumu yake.
Dalili ya Chess ni Mubaha na hakuna matini ya kuiharimisha kama mchezo wa bao la kete, wala hakuna matini ya kuihalilisha ili iwe Mubaha. Chess inatofautiana na kete katika pande mbili; ya kwanza ni kwamba katika Chess usimamizi wa vita, hali hii inafanana na kupiga vita, ushindani wa Farasi. Kutoka upande wa pili, katika mchezo wa bao la kete kuna namba zinazojitokeza kama vile kupiga ramli, lakini katika Chess kuna ujanja na kufikiri kama ushindani wa mishale.
Chess imechezwa kwa ajili ya kujifunza mambo ya Vita na mapigano, na kila kitu kinafundisha mambo ya Vita na mapigano hukumu yake ni Mubaha; kwa mujibu wa dalili iliyotajwa katika Sahihi mbili (Sahihi yake Al-Bukhari na Sahili yake Muslim) iliyopokelewa kutoka kwa Aisha R.A kuhusu Wahabeshi waliokuwa wakicheza kwa mishale katika Mskiti wa Mtume S.A.W. naye alikuwa akiwatazama.
Al-Bayihaqi alifupisha madhehebu ya Wanavyuoni waliotangulia kuhusu Chess, akisema: Imepokelewa kutoka kwa Ibn Omar, Ibn Abbas, Ibn Said Al-Khudari, Ibn Al-Musaib, Al-Qasim Ibn Mohamad, Abi Jaafar, Mohamad Ibn Siriin, Al-Zahri, An-Nakhi, Yazid Ibn Abi Habib, na Malik Ibn Anas kwamba walisema kuwa hukumu ya Chess ni Makruhu. Ama Said Ibn Jubair, Ash-Shaabi, Al-Hasan, na Hisham Ibn Orwah walisema kuwa Chess inaruhusiwa kuchezwa. Lakini kutocheza Chess ni bora zaidi. [Al-Adaab, uk.253, Muasasatul Kutub Al-Thaqafiyah, Beirut - Lebanon].
Al-Mawardi alifupisha madhehebu ya Wanavyuoni wa Fiqhi, akisema: “Wanavyuoni wa Fiqhi wametofautiana kuhusu uhalali wa Chess na uharamu wake katika mitazamo mitatu: Mtazamo wa kwanza ni mtazamo wa Imam Malik anayeona kuwa Chess ni Haramu. Mtazamo wa pili ni mtazamo wa Abu Hanifa anayeona kuwa Chess ni Makruh kabisa kwa njia inayolazimisha kukataza, ingawa haifikii kiwango cha uharamu. Mtazamo wa tatu ni wa Shafi R.A. aliyesema kuwa Chess siyo Haramu kama alivyosema Malik R.A. wala ni Makruh kabisa kama alivyosema Abu Hanifa, kisha akasema: “Kwa sababu gani tuuchukie hivyo! Anakusudia Karaha siyo sana. Wenzake na Abu Hanifa walitofautiana kuhusu Karaha hii katika mitazamo miwili: Mtazamo wa kwanza unasema kuwa hukumu yake Karaha, kwani Chess ni aina ya michezo. Mtazamo wa pili unasema kuwa Karaha hiyo inatokana na uovu unaojitokeza katika Chess, na jambo hili likijulikana kwa masahaba, wafuasi na Wanavyuoni wengi sana ambao hawana idadi waliufuata mtazamo huu. Katazo la Ali R.A, halikuwa kwa ajili ya kuiharamisha Chess. Inasemekana kwamba waliokuwa wakicheza Chess walisikia Adhana na wakaendelea na kazi. [Al-Hawi, 17/177, Ch. Darul Kutub Al-Elmiyah, Beirut -Lebanon].
Imam wa Misikiti Miwili Mitakatifu: “Wenzangu wengi walisema kuwa kucheza Chess ni Halali, wengine walisema kuwa ni Makruh, na mtazamo wao huu ni sahihi Zaidi. Na waliosema kuwa ni halali pengine walitaka kukataza uharamu wake, lakini hukumu yake ya Makruh na Mubah ni mitazamo ya Wanavyuoni wa sasa. Kisha wenzetu walisema kuwa Chess haiharamishwi kama hakuna matusi au kuacha Sala, kwani kilichoharamishwa ni kuacha swala na matusi. Vile vile wanasema kuwa Chess inaharamishwa kama ikikusudiwa kuchezwa kama kamari. Iliyoharimishwa ni nia yake tu, siyo Chess yenyewe. Inasemekana kuwa Said Ibn Jubair alikuwa akicheza Chess akageuka nyuma. Na Hadithi iliyopokelewa kutoka kwa Ali R.A, aliwapitia watu waliokuwa wakicheza Chess, akasema: “Ni nini haya Masanamu ambayo nyinyi Mnaketi mbele yake” Bwana wetu Ali alisema hivyo kwani aliona kuwa masanamu ya Chess yana picha ya Farasi na ndovu” [Nihayatul Matalb Fi Dirayatul Madhahab, 19/19 Darul Manhaj]
Muhtasari ni: Rai iliyochaguliwa kuhusu kucheza Chess ni Uhalali kama hakuna kucheza Kamari ndani yake, na hakusababishi kuacha wajibu au kufanya jambo lolote la haramu.

Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi ya wote

Share this:

Related Fatwas