Kipimo na Utohoaji

Egypt's Dar Al-Ifta

Kipimo na Utohoaji

Question

 Baadhi ya nyakati huwa tunasoma katika tafiti za kifiqhi za kisasa kauli ya wanazuoni kuwa suala hili hukumu yake inapimwa na suala lengine, na kwamba suala hili lina hukumu maalumu kutokana na Utohoaji wa madhehebu ya Imam Al-Shafii kwa mfano. Je, nini tofauti kati ya Utohoaji na Kipimo?

Answer

Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, sala na amani ziwe juu ya bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, na familia yake, masahaba zake, wafuasi wake, na baada ya baada ya utangulizi huu:
Kipimo katika lugha: Neno hili limetokana na kupima, ambalo lina maana ya kukadiria. (Rejea: Muujam Maqaayis Al-lughah kwa Ibn Faris 5/40, Darul Fikr.).
Na katika istilahi imesememwa katika ufafanuzi wa Kipimo kwamba ni: Usawazishaji kati ya suala linalopimwa na suala la asili kuhusu sababu ya hukumu au kuongeza kwake katika maana inayozingatiwa katika hukumu hiyo. Imesememwa pia Kipimo ni: Kubebwa kwa jambo linalojulikana juu ya lingine linalojulikana pia kuhusu kuthibitisha hukumu zake au kuzikanusha kutokana na hukumu maalum au sifa au kuikanusha. Wanavyuoni wa Ussul wametofautiana juu ya ufafanuzi wa Kipimo, hata Imamu wa Misikiti Miwili Mitukufu amesema: Haiwezekani kupima kabisa; kwa sababu inahusisha ukweli tofauti, kama vile, hukumu, sababu, suala linalopimwa na mjumuisho. (Al-Bahrul Muhiit kwa Al-Zarkashi 5/7, Darul Ketbi, na Nihayatul Soul kwa Al-Isnawi 3/3, Aalam Al-Kutub).
Kipimo kimehitajika wakati majanga yalipoongezeka na hakuna matini zinazobainisha hukumu za majanga hayo, basi janga pia ni nadra kupata matini yake ya wazi, na kwa hivyo, ilikuwa ni muhimu kupata hukumu yake kupitia matini zisizo za moja kwa moja, na hali hii haitekelezwi isipokuwa kupitia Kipimo ambacho ni asili miongoni mwa dalili za hukumu nne zilizokubaliwa na wanavyuoni wa madhehebu manne na zilizofuatiwa na wengi wa wanavyuoni wa Kiislamu, nazo ni: “Qur'ani, Sunna, Makubaliano, na Kipimo”, hakuna mzozo kati ya wanavyuoni kwamba Kipimo ni hoja katika mambo ya kidunia kama vile chakula na madawa. Lakini Kipimo katika hukumu za kisheria wakati ambapo hakuna matini wala makubaliano ya wanavyuoni basi wengi wa masahaba, wafuasi na idadi kubwa ya wanavyuoni walisema kuwa Kipimo cha kisheria ni msingi miongoni mwa misingi ya sheria, kinakuwa ni dalili ya hukumu zisizotajwa katika Qur'ani, wala katika Sunna, wala katika makubaliano ya wanavyuoni. Imepokelewa kutoka kwa Imam Ahmad kuwa alisema: “Haiwezekani Kipimo kikaachwa”. (Rejea: Al-Bahrul Muhiit, 5/16, pia kitabu cha Al-Tahsiil Min Al-Mahsuul kwa Siraaju Diin Al-Armuwi 2/159, Muasastul Risalah, na kitabu cha Irashaadul Fuhuuluk. 185, Mustafa Al-Halabi).
Nguzo za Kipimo ni nne, nazo ni: Suala la asili, Suala linalopimwa, Hukumu, na Sababu. Kwa hivyo basi Suala la asili ni: Suala ambalo hukumu yake ilitajwa katika Sheria, na Suala linalopimwa ni: lile ambalo hukumu yake inatakiwa kubainishwa na hakuna matini ya wazi inayohusiana nalo katika Sheria. Hukumu ni: Uamuzi uliothibitishwa katika Sheria kama vile kukatazwa kwa pombe. Sababu ni: Maelezo yanayojumuisha kati ya Suala la asili na Suala linalopimiwa (kitabu cha Irashaadul Fuhuul cha Al-Shawkani uk. 204, na kitabu cha Al-Bahrul Muhiit 5/83).
Kwa mfano, kukatazwa kwa kila kinachopoteza akili -kama vile bia- ikipimwa pamoja na pombe, Suala la asili hapa ni pombe na hukumu yake imetajwa katika matini za Sheria; Qur'ani na Sunnah, na Suala linalopimwa ni bia ambayo hakuna matini ya wazi inayohusiana nayo, na Hukumu yake ni kuharimishwa kwake ikipimwa kwa kuharimishwa pombe ambako kumetajwa katika matini za Sheria. Na Sababu ni kusababisha ulevi na uharibifu ambao pombe imeharimishwa kwa ajili hiyo, na ni hali ambayo inajitokeza pia katika bia. Huu ni mfano unaoeleza haja ya Kipimo kwa ajili ya kujua Hukumu ya kisheria kuhusu majanga na matukio yote yaliyo mapya, kwa sababu haiwezekani kuwapo janga lolote pasipo na kuwepo Hukumu ya Mwenyezi Mungu kwake, Mwenyezi Mungu anasema: {Na tumekuteremshia Kitabu hiki kinacho bainisha kila kitu, na ni uongofu, na rehema, na bishara kwa Waislamu} [AN NAHL: 89].
Imamu wa Misikiti Miwili Mitukufu alisema katika kitabu chake “Ghaythul Umamu” (uk. 310, Darud Dawah): “Inaaminiwa kwamba haitegemewi kutuka tukio lolote na Sheria bado ipo duniani ila wapo wanaofuata hukumu ya Mwenyezi Mungu iliyotajwa katika Sheria hii”.
Rejeo la Kipimo ni kufahamu elimu ya Fiqhi na kujua kwa kina siri za Sheria, makusudio yake, na Sababu za Hukumu zake, na kwa hivyo, siyo kila mtu anaweza kutoa dalili kupitia Kipimo, bali ni kazi ya Wanavyuoni tu waliofikia kiwango cha Jitihada zisizo na mpaka, kama vile, Maimamu waliofuatwa kama Abi Hanifa, Malik, ASh-Shafii na Ahmad Mwenyezi Mungu Mtukufu awe radhi nao.
Na kwa sababu ya uhaba wa wenye kujitahidi kwa kupita nyakati haja imejitokeza kwa kile kinachoitwa Utohoaji kutoka madhehebu ya wenye jitihada, au kujitahidi katika madhehebu maalum. Utohoaji huu unafanana na Kipimo katika kupima Suala ambalo halikutajwa katika Qur'ani na Sunna kwa Suala lililotajwa katika Qur'ani na Sunna. Na Utohoaji unatofautiana na Kipimo kwa sababu kupima huku kunatekelezwa katika matini ya Imamu mwenye jitihada na misingi yake haimo katika matini za Qur'ani na Sunna kama ilivyokuwa katika Kipimo; Mtohoaji hakufikia kiwango cha mwenye jitihada kabisa ili kuweza kujitegemea na kupima masuala ambayo ni mapya na masuala yaliyotajwa katika Sheria, lakini hukumu za majanga na matukio hufikiwa kupitia misingi na vyanzo vilivyoanzishwa na maimamu wa jitihada kwa ajili ya kufahamu Sheria na Sababu na Makusudi yake.
Ibn Badran, miongoni mwa wafuasi wa Ahmad Ibn Hanbal ametaja katika kitabu chake: [Mlango wa madhehebu ya Imam Ahmad, uk. 35 140, Muasasatur Risalah.] kuwa: “Kueleza kwa neno la “Utohoaji” liko katika maneno ya wanavyuoni na wenye msimamo mkali, nalo ni aina ya Utohoaji maana kwa kutumia akili na maana yake ni: Utohoaji hukumu kutoka katika matini ya maoni ya Imamu mwenye jitihada katika sura iliyo sawa, au kutoka katika masuala ya asili ya madhehebu fulani kama vile Misingi iliyozingatiwa katika Sheria, au akili pasipo na kutajwa kwa Hukumu hii kutoka kwa Imam anaehusika. Mfano wake ni: Kupimwa kwa Msingi ambao ni “Kutokalifisha kwa yasiyowezekana”.
Kutokana na yaliyotangulia hapo juu inadhihirisha kwamba kuna tofauti kati ya Kipimo na Utohoaji ni kwamba Kipimo kwa maana yake ya istilahi ni chanzo miongoni mwa vyanzo vya Hukumu nne zilizoafikiwa na wengi wa wanavyuoni nacho hakitegemewi isipokuwa kwa mwenye jitihada tu katika kutoa fatwa, na jitihada za kifiqhi, wakati ambapo Utohoaji ni kama Kipimo katika sura yake tu, na unashughulikiwa na mwenye jitihada katika madhehebu ya imamu miongoni mwa maimamu wa jitihada zisizo na mipaka kwa ajili ya kufikia Hukumu ya Kisheria kuhusu majanga na matukio yasiyotajwa katika Qur'ani na Sunna, kwa njia ya moja kwa moja kupitia vyanzo vya imamu mwenye jitihada na Misingi ya Madhehebu yake katika kufahamu Sheria na makusudio yake.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi ya wote.

 


 

Share this:

Related Fatwas