Kutambua Hali halisi kwa kutumia M...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kutambua Hali halisi kwa kutumia Misingi ya Fiqhi.

Question

 Wakati mwingi usemi unazunguka kuhusu hali halisi na umuhimu wa kuitambua kwa utambuzi sahihi mpaka tufikie hukumu yake ya kisheria, na kwa ajili ya kutoa sura ya (mtazamo wa) Kiislamu kuhusu hali hii hiyo. Kwa hiyo basi, vipi tunaweza kuitumia Misingi ya Fiqhi kama nyenzo ya kutambua hali hiyo halisi?

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, na sifa njema ni zake, na rehema na amani zimshukie Bwana wetu Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na Aali zake na Masahaba wake na wafuasi wake, na baada ya hayo:
Inawezekana kupitia kwa Nadharia ya Kiislamu, na ambayo inasema kwamba vyanzo vya maarifa ya Mwislamu ni: Wahyi pamoja na Uwepo wa Maisha, mpaka ukaenea mwelekeo wa kusoma kitabu cha Mwenyezi Mungu, hivyo basi inawezekana tukafikia tunayoweza kuiita Misingi ya Fiqhi ya kiutamaduni, na ambayo inaongeza katika Misingi ya Fiqhi ya kijadi inayohusika na ufahamu wa matini (Wahyi) jambo ambalo linaweza kuwa njia ya kufafanua hali halisi, ilhali tunafaidika na tunatumia mifumo yote iliyotumiwa mwanzoni, na kuchambua sayansi ya kijamii, kibinadamu na ya Ulimwengu, mifumo ya kusingizia au mbinu za kukurubisha pamoja, au makubaliano yasiyo na sharti, au kukataa yasiyo na sharti, au uteule wa kiholela. Faida itakuwa kwa kuunda nyenzo atakayoisomesha Mufti, na itakayomwezesha kuitambua hali hiyo halisi ambayo itakuwa inabadilika kwa nguvu na kwa kasi sana, hasa baada ya maendeleo haya ya njia za Usafiri, Mawasiliano, na zana za kisasa, na ambazo zinamfanya mwanadamu asifikiri isipokuwa mbele. Na kuyaeleza hayo yote inahitajika juhudi endelevu ili hayo yatimie polepole, yajenga yasiharibu, yanufaishe na wala yasidhuru.
Licha ya hayo Mufti anapaswa kufaidika na Misingi ya Fiqhi kama mfumo wa sayansi ya kijamii. Kwani fikra za kimsingi zilizochimbuka kupitia imani ya mtizamo wa mwanadamu na Ulimwengu na Maisha zimemzalishia Mwanadamu fikra mpya, kisha fikra hizo zikamzalishia mfumo wa kutendeana na Sayansi.mfumo huo ulidhibiti mifumo mingi mingine. Tukichambua amri hiyo tutaiweka akida ya Kiislamu kwenye waislamu na fikra za kimsingi zinazompambanua mwanadamu na viumbe vingine, na kupitia hivyo tutakuwa tumeweka mifumo inayokuwa na uwezo wa kuzalisha mifumo mingine kwa kila elimu miongoni mwa elimu zote, na tutafaidika kutokana na uhusiano wa mifumo ya kila sayansi na mifumo ya kimsingi, hivyo basi tunaweza kuitumia mifano hiyo katika kuanzisha mifumo mingine kwa kutumia elimu za kijamii na za kibinadamu kwa kupitia Misingi ya Fiqhi kwa njia ya kufanya hivyo.
Jambo hili ni nukta ya kwanza ambayo tunataka kuifikia kwa njia ya uhusiano kati ya mfumo wa Misingi ya Fiqhi na mifumo ya kimsingi, na vipi Misingi hiyo ilichimbuka kutoka kwake. Na vipi tunaweza kuizalisha pia mifumo kwa elimu ya kijamii kwa kufaidika nazo mbili.
Nukta ya pili ni ile inayochangia maana ya elimu. Inamaanisha kuwa mimi nina maudhui muhimu na masuala kuhusu elimu hii na maendeleo ya hii Elimu, pia yanayomaanisha kuwa bado tunaendelea kuuliza maana yake tutakwenda kupitia Elimu kwa Elimu…na maudhui ya Elimu ya Misingi ya Fiqhi ni: Dalili za kiujumla kwa maana ya utoaji wa hukumu za kisheria kutoka kwake. Na dalili hizo ni: Qur'ani, Sunna, Ijmaa, na Qiyasi. Dalili hizo zina njia nyingi; miongoni mwazo ni: Kuhifadhi Qur'ani na Sunna (anayehifadhi Qur'ani na Sunna tu hawezi kuwa Mwanazuoni wa Misingi ya Fiqhi (Mwenye Usuuli), maana ya kuhifadhi haimaanisha kueleza au kufafanua, lakini kutoa hukumu kutoka katika Qur'ani, Sunna, Ijimaa, na Qiyasi.
Hapa Swali la tatu ni kuwa: Ni nini Hukumu ya Kisheria? Hukumu ya kisheria ni maneno ya Mwenyezi Mungu yanayohusiana na vitendo vya waislamu waliobaleghe, kuhusu kutoa hukumu, Kutoa hiyari, na kuhusu uwekaji wa hali. Utoaji wa Hukumu una maana ya kutenda, Kutoa hiyari kunamaanisha kutenda au kutotenda, na Uwekaji wa hali kunamaanisha kuweka kitu kwa mkabala wa kitu kingine.
Hivyo basi maudhui yake inachangia na Kigezo, na namna ya kuchomoa hukumu kutoka kwake. Lakini kigezo hicho kinahusika na uchunguzi tu au nini? Hakika maana ya kiutamaduni kwa kigezo hiki ni yenye upana zaidi, kwani sisi hatuchunguzi Qur'ani na na Sunna kama wanaochunguza fani kwa ajili ya fani tu, au kama shule hizi za kiholela, bali tunazisoma ili ziwe zenye faida katika Maisha ya watu. Kwa hivyo ni lazima kuwepo kwa uwanja katika jitihada, na bila ya uwanja huo hakuna jitihada, kwa maana ya kwamba hakuna watu wanaoweza kutuambia kwamba mlango wa jitihada ulifungwa, ni kama tumeondoshwa katika hali halisi ya Maisha. Jitihada inahitaji uwanja kwani mwenye kujitahidi anahitaji awe na uwanja wa jitihada, lakini tukimnyima uwanja huo hataweza kukaa nyumbani kwake na kufikiri pamoja na kujitahidi. Kwani moja ya nguzo za jitihada ni kutekeleza kigezo chake katika hali halisi.
Kwa hivyo basi, kuna uhusiano kati ya Misingi ya Fiqhi na hali halisi, na hiyo ni sababu ambayo imewafanya wanazuoni wazungumzie hukumu za kisheria kuhusu kiwango cha Fiqhi, na kwa kiwango cha Fatwa, na kwa kiwango cha Ukadhi. Kuhusu kiwango cha Fiqhi ni kujua hukumu ya kisheria, na hali halisi inayotekelezewa hukumu hiyo bila ya kuibadilisha. Kwa sababu hii, Kadhi anapaswa ajue hukumu ya Mwenyezi Mungu, na hali halisi iliyo mbele yake, na vipi atakuwa na uwezo ya kuibadilisha. Lakini mwenye Fiqhi inatosha kwake ajue hukumu ya Mwenyezi Mungu tu, vile vile Mufti anapaswa ajue hukumu za Mwenyezi Mungu pamoja ya kujua hali halisi ambayo hukumu hiyo itatekelezwa kwake, bila ya kumlazimisha Mufti huyo kuibadilisha hukumu yeye mwenyewe.
kufafanua yaliyopita, kwa mfano mambo yaliyotokea zama za Laithu Bin Saad katika suala la Syprus, na je, watu wa Syprus (watu wa dhima) wamevunja Ahadi au hapana? Wanazuoni saba wakubwa wenye kujitahidi, wametoa Fatwa, na Fatwa zao zilihitilafiana kwa kuangalia hali halisi, kwani hali halisi ni jambo la kijamii. Na hivyo waliulizana, je watu wa Syprus wana sifa gani? Je, wao ni wavunjaji wa amri? Je, wao wamedhulumiwa? Je tukio hilo lilitokea kweli au halikutokea?. Kila Mwanazuoni wa Fiqhi ametoa maoni yake kutokana na ufahamu wake kuhusu hali halisi. Na ukiangalia Fatwa zao utazikuta hazitoki katika hukumu za Mwenyezi Mungu, lakini zinatofautina kutokana na tofauti ya hali halisi. Wanazuoni wote wa Fiqhi wanasema kwamba wavunjao ahadi miongoni mwa watu wa ahadi na dhima, basi hakuna dhima wala ahadi nao. Lakini je, wamevunja ahadi kweli? Je, wamefanya hivyo kwa hiari yao au sivyo? Au wamekua wakihitajia msaada wetu na sisi ndio tulioshindwa kuwalinda? Au mambo haya yote hayakutokea?
Hapa itatuelewekea kama kuchunguza hali halisi ya kisiasa –kwa mfano– Mwanazuoni wa Fiqhi anahitaji kuchunguza ili atoe Fatwa kama ipasavyo, na hiyo inahitaji masuala ya hali halisi wala haihitaji mfumo peke yake. Hivyo basi tunaweza kusema kuwa inawezekana kuwepo kwa uhusiano kati ya mfumo wa Msingi wa Fiqhi na mfumo wa Elimu ya kijamii, na pia kuna uhusiano kati ya masuala ya Misingi ya Fiqhi na Elimu za kijamii. Vile vile tutasema kuna uhusiano kati ya Elimu nyingine za kisheria na Elimu zote za kijamii. Na hii si maudhui yetu, lakini katika muktadha huu tumetambua uhusiano wa Fatwa inayohitaji kujua hali halisi inayohitajika kwa wenyewe; yaani wenye Elimu za kijamii na kibinadamu.
Kwa kweli tofauti ya hali halisi ni sababu ya tofauti ya Fatwa, sio sababu ya hitilafu ya wanazuoni wa Fiqhi… kwani wanazuoni hao wa Fiqhi wanatofautiana katika Fatwa zao kwa sababu nyingi miongoni mwake zina tofauti ya dalili…na tofauti ya kuzieleza dalili hizo, na katika daraja zao, bali ni katika dalili zenyewe, na tuzichukue au hapana? Na miongoni mwa dalili nyingi na ambazo waandishi wengi wa vitabu vya Kisheria wamezizungumzia; kama Ibn Taymiya katika kitabu chake [Rafuul Malam An Aimmat Al Aalaam), na pia Dahlawyi katika kitabu chake (Asbab Ihtilaful – Fuqahaa] Na shekhe Khafif – Mungu Amrehemu – katika kitabu chake: [Asbab Ihtilaful – Fuqahaa] na hawa wamezungumzia sababu za tofauti ya wanazuoni wa Fiqhi kwa upande wa kuangalia hali halisi. Na mimi natoa mifano mingine ili tufafanue jambo hilo kwa namna ya wazi Zaidi. Kwa mfano Mwanazuoni wa Fiqhi anasema "Mtu akimwambia mkewe kama wewe ni mtalaka, mke huyo atakuwa mtalaka na mke huyo baada ya kupita muda wa miezi mitatu baadaye anaweza kuolewa na mtu mwingine". Akija mtu wa kwanza akamwambia Mufti lililotokea na mkewe, Mufti hatampa Fatwa kama mwanamke huyo akiwa mtalaka, bali Mufti atamuuliza mume huyo hali ya kumuacha mke wake; je alikuwa analala au anaamka? Kwa nia au bila ya nia? Na je alimtamkia maneno hayo mke wake moja kwa moja au kwa njia ya kusimulia?
Hivyo basi, Mufti kwa kujua hali halisi ya jinsi mume alivyotamka maneno hayo, ataweza kutoa hukumu, na kwa namna hii Mufti anaweza kuchambua na kufikia hukumu, kisha atamuuliza mume huyo tena; je, mke wako alikuwa na hedhi? Basi akiwa na hedhi baadhi ya wanazuoni wanasema mke huyo ameachika, na wengine wanasema kajaachika, na Mufti akiwa na wanaosema kuwa mke huyo ameachika au na wale wanaosema kuwa mke huyo hajaachika, basi atapitisha Hukumu yake kuhusu jambo hilo.
Mambo mengi sana yanafanana na mfano uliopita. Kuchambua suala ni jukumu la Mufti si jukumu la mwanazuoni wa Fiqhi, mwanazuoni wa Fiqhi anazitoa hukumu na Kadhi anazitekeleza katika hali halisi (Kwa mfano anamtenganisha mwanamke aliyeachwa na mumewe) au anaweza kumtia mume gerezani kwa kumuudhi mtalaka wake.
Sasa tutazungumzia mfumo wa Misingi ya Fiqhi, na tunaulizana je, mwanajamii anaweza kufaidikaje na namna ya kufikiri kwa mwanazuoni wa Misingi? Na je, mwanajamii pia anaweza kufaidikaje na namna ya kuorodhesha fikra za mwanazuoni wa Misingi? Kwani mwanazuoni wa Misingi kwanza anakigezo akilini mwake kinachomwezesha kutofautisha kati ya yakini na dhana, na jambo hili linamsaidia sana katika kutendeana na matini za kisheria, na mwanajamii anaweza kufuata mifumo hiyo, basi ataweza kutofautisha kati ya dhana na yakini katika kuchunguza hali halisi. Na hapa mtaalamu wa Elimu zote zisizo za kisheria pamoja na Elimu za kijamii, anahitaji yale walioyakusudia wanazuoni wa Misingi na yale tulioyachukua kutokana na maneno yao na Maisha yao – na hayo hayakuja katika matini zao moja kwa moja – kwa ajili ya kuweza kutofautisha kati ya hali halisi na jambo hilo.
Rejea: Misingi ya Fiqhi na uhusiano wake na Falsafa ya Kiisalmu, Mtungaji ni Mufti wa Misri, Profesa: Ali Jumaa.

 

Share this:

Related Fatwas