Nadharia ya Kiislamu – Shina Lake n...

Egypt's Dar Al-Ifta

Nadharia ya Kiislamu – Shina Lake na Mtindo Wake – Sayansi Kigezo cha Misingi ya Fiqhi

Question

Taasisi za mazungumzo ni nyingi kuhusu upeo wa Uasili au Shina la nadharia ya Kiislamu, na uwezo wake wa kutumia mtindo salama (manhaj) wa kisayansi, basi nini upeo wa usahihi wa hayo?  

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, na sifa njema ni zake, na rehema na amani zimshukie Bwana wetu Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na Aali zake na Masahaba wake na wafuasi wake, na baada ya hayo:
Kwa hakika ubainifu wa Shina la nadharia ya Kiislamu na iliyoyatoa kwa ajili ya utu miongoni mwa juhudi za asili zilizosaidia kutukuka kwa ustaarabu wa watu kwa ujumla wao ni jambo lenye uwanja mpana.
Hayo ni kutokana na kutawanyika na kuenea kwa nyanja za kinadharia ambazo Waislamu wamesaidia kwa kiasi kikubwa. Na kwa ajili hiyo, hapa tutafupisha kuwasilisha mfano wa Shina hili na mtindo huu ambavyo Waislamu wananufaika navyo kupitia sayansi moja pekee. Nayo ni Sayansi ya Misingi ya Fiqhi.
1- Misingi ya Fiqhi na Mtindo Wake:
Misingi ya Fiqhi ni miongoni mwa sayansi ambazo zimeanzishwa na akili ya Mwislamu isiyokuwa na mfano, isiyokuwa ya kuuiga kutoka umma wowote ule uliotangulia katika dhumuni hili. Lengo lake katika hili ni lile lile lengo la elimu ya Msamiati wa Hadithi na Sayansi yake. Na kila moja kati ya elimu hizo inazingatiwa ni mtindo fulani kwa maana ya kina.
Hivyo, Misingi ya Fiqhi ni mtindo wa kuyafanyia kazi maandiko ya kisheria. Na katika maana yake kwa mujibu wa mafundisho ya Imamu Ar-Raaziy kwa mfano yanataja nguzo za mtindo wa kisayansi; ambapo Imamu Ar-Raaziy ametoa maana kwa ujumla wake kwamba: “Ni mkusanyiko wa njia za Fiqhi kwa njia ya kukusanya na namna ya kutolea dalili, na namna ya hali au mazingira ya kinachotolewa dalili.”
Na Imamu Al-Baidhwawiy ameitolea maana akisema: “Ni maarifa ya dalili au hoja za Fiqhi kwa ujumla wake na namna ya kunufaika nazo na mazingira ya anaenufaika. ”
Katika maana hizi inaweza kupatikanwa nguzo za mtindo huo, na kwamba zinatilia maanani kwenye maarifa ya:
A- Vyanzo vya Utafiti
B- Njia za Utafiti
C- Masharti ya Mtafiti
Hizi ni nguzo za kimantiki kwa mtindo wowote katika utafiti wa kisayansi ambao uko mbali na mambo ya kizushi, na uko mbali na ubinafsi, lakini unakaribiana na maudhui.
Elimu ya Hadithi kwa yale yaliyoandikwa katika Elimu ya Msamiati wa Hadithi, au Elimu ya Utiaji Kasoro na Usawazishaji, Elimu za Hadithi – Riwaya au Ustadi, bali inazingatiwa kuwa ni mtindo katika kutaamali na maandiko kwa uthabiti, na kuyayakinisha kwa maana ya jumla ambapo yatakusanya Elimu hizi juu ya ukosoaji wa utungo wa mapokezi na ukosoaji wa matini kwa pamoja, mpaka itimie hukumu yake kwa dalili za kimapokeo kwa kukubalika au kukatalika utungo wake wa mapokezi na matini yake. Mtindo huu ni wa kuvutia na wa kipekee kwa Waislamu pasi na watu wa umma nyinginezo.
Inaonekanwa kwamba Mayahudi wameyajaribu mambo hayo hapo kabla lakini wamefeli, ambapo mitungo ya wapokezi ambayo ipo mikononi mwetu sasa hivi ni zaidi ya laki moja , ilhali mitungo ya wapokezi Mayahudi kwa uchache wake hayafiki hata kwa Nabii Musa. Bali kati ya yalipomalizikia utungo huo wa mapokezi na kati ya Musa ni miaka elfu moja na mia tano au ni zaidi ya zama thelathini au vizazi thalathini.
Ibn Hazm anasema katika kitabu chake: [Al-Faswl fil Milal wal Ahwaa Wannihal] (Upambanuzi kati ya Itikadi, Matamanio, na Imani): Katika aina hii kuna nukuu nyingi za Mayahudi, bali ndiyo yaliyojuu zaidi walinayo, isipokuwa kwamba wao hawajikurubishi kwa Nabii Mussa kama tunavyojikurubisha sisi kwa Bwana Mtume S.A.W, Bali wanasimamia – na lazima iwe hivyo – kati yao na Mussa – A.S. kwenye zaidi ya zama thelathini katika zaidi ya miaka elfu moja na mia tano, bali wanafikia kwenye nukuu hadi kwa: Hilali, Shamaaniy, Sham’uun, Mur’uqaiba na wengineo.
Nadhani kwamba wana suala moja pekee ambalo wamelipokea kwa wino kutoka kwa nabii fulani miongoni mwa manabii wao wa mwisho-mwisho, wamelichukua kwa mdomo kuhusu mwanamme mmoja kumuoza binti yake ikiwa kaka yake amefariki. Ama Wakristu hawana kabisa sifa ya nukuu za namna hii isipokuwa tu kuharamisha talaka peke yake, ya kwamba mtoaji wa habari hii ni mtu mwongo ambae uongo wake umesihi.” N.k.
Kwa hakika kufikiria kimantiki kwa yeyote mwenye kutaka haki ni kuhakikisha kwanza yale yanayosimama kwa hoja ambayo yamethibiti kwa Mwislamu kwamba hayo ndio Qur`ani na Sunna. Hivyo ni lazima kuwepo njia ya kuthibitisha na kuviyakinisha vyanzo vyake, na kama vitathibiti, je kwa namna gani au vipi tutafahamu hivyo. Basi mtindo (manhaj) huo ukawa ndio mtindo wa kina kwa kutimiza lengo hilo.
Pia inawezekana kuifanyisha kazi elimu ya Misingi ya Fiqhi – kama ni mtindo – katika mahusiano na falsafa – kama ni uwanja fulani – ili kunufaika na sayansijamii kutokana na mtindo huo. Hayo yatatokea kwa kuyaondoa yale yote ambayo tunaweza kuyaita kuwa ni mitazamo ya Misingi na utekelezaji wake, au sehemu zake katika sayansi hizo.
Hivyo hoja ambayo inaainisha vyanzo vya asili, na kubainisha namna ya kusimamisha hoja kwa uhojaji wake au udalili wake, na kukiyakinisha chanzo chake, na kutaamali na mwanya au eneo la maamuzi ya mwisho na la kidhana, kisha namna ya kuyaambatanisha, kuchambua mgongano, kuhakikisha makusudio ya Elimu na kuitekeleza, na nyanja nyinginezo ambazo zinaweza kuwa na faida kutokana na Misingi ya Fiqhi katika sayansijamii na sayansiutu wakati wa kuivua na kuiondosha mitazamo yake, na kuoionesha kwa sura nyingine sio ile sura iliyorithiwa.
Ufafanuzi wa hayo ni kwamba:
Nadharia ya Shina kwa wanachuoni wa Misingi ya Fiqhi imeanzia kwa lengo fulani maalumu lililojaribu kuweka alama za njia ya kufikia lengo hilo. Hayo ni kwamba yeyote mwenye kujitahidi ambae anazitoa hukumu za matawi kutokana na hoja zake za uchambuzi na ufafanuzi anahitaji kuainisha chanzo cha hukumu, kisha ubainisho wa namna ya kutaamali na chanzo hicho, kisha ubainisho wa masharti ya mtafiti. Hayo yote ni mambo ambayo wameyajumuisha wanachuoni wa elimu ya Misingi katika kutoa maana ya Misingi ya Fiqhi, bali imekuwa ndio sababu katika kuita tamko “Misingi” kwa hali ya wingi. Wala halikuitwa tamko hilo katika hali ya umoja “Msingi wa Fiqhi” kwa ajili ya sayansi hiyo. Hivyo, mafundisho ya kimsingi ya Imamu Ar-Raaziy yanaatoa maana ya sayansi hiyo kuwa ni: Maarifa au ujuzi wa hoja za Fiqhi kwa ujumla na namna ya kunufaika nazo, na mazingira ya anaenufaika (ikimaanisha mwenye kujitahidi).
2- Hatua na Falsafa Zinaweka Wazi Kuhusu Mtindo Huo:
Ikiwa tunapita kwamba mtindo huo si mwingine isipokuwa ni falsafa inayoibuka kutokana na hatua fulani mbalimbali – nayo ni maana ya mtindo uliochaguliwa kwetu sisi-: inabainisha upeo wa mahusiano kati ya Misingi ya Fiqhi na falsafa ya Kiislamu.
Hivyo, misingi ya Fiqhi inakusanyika bila ya shaka yeyote kwenye ubainishaji wa hatua maalumu za lazima kwa ajili ya kutaamali na maandiko ili yafahamike, na kufikia kwenye wasifu wa matendo ya waja. Nao ni wasifu unaozungukia kwenye uzio wa kile kinachoitwa wanamisingi kwa hukumu.
Hivyo, maana ya ‘hukumu’ kwa uoni wao ni: “Ni ujumbe wa Mwenyezi Mungu unaohusiana na matendo ya waliobaleghe kwa mujibu wa ilivyoamuliwa au kuchaguliwa au kwa mujibu wa mazingira na hali ya mambo. ”
Nayo ina vigawanyo kadhaa. Navyo ni: Wajibu, haramu, kupendezewa kufanya, karaha, na kujuzu. Nao ni wasifu wa matendo ya waja ambayo yanakuwa ni kiima katika sentensi kamili, na neno ‘hukumu’ ni kiarifu chake; hivyo kutokana na hayo ndio masuala ya Fiqhi yanaundika.
Hivyo maudhui ya Elimu ya Fiqhi ni: Tendo la mtu. Na maudhui ya Elimu ya Misingi ya Fiqhi ni: Ushahidi jumla kutokana na utoaji hukumu wa ushahidi huo.
Na bila ya shaka yeyote, hatua hizi ambazo zinakusanyika kwenye Misingi ya Fiqhi zinaibuka na kuchimbuka kutokana na uoni jumla unaokuwa katika maudhui za falsafa ya Kiislamu na sayansi ya Maneno.
Imamu Az-Zarkashiy anasema katika kitabu chake kiitwacho “Al-Jaamiul Bahrul Muhiitw” akisisitiza kipengele cha uchukuaji hatua katika Misingi ya Fiqhi, na ambacho kimewapelekea baadhi yao kudai kwamba Elimu hiyo ni miongoni mwa Elimu za ukatinakati ambayo haijitegemei yenyewe. Wanajibiwa hivi:
“Ikisemwa: je Misingi ya Fiqhi ni kama mfano tu uliokusanywa kutoka sayansi au elimu mbalimbali? Ni kama mfano kutoka elimu ya sarufi (grama/nahau) kama maneno kwenye maana za herufi ambayo mwanafiqhi anaihitaji, kurejea kwa kiwakilishi kwa baadhi ya nomino, kuliunganisha neno fulani maalumu kwenye ujumla n.k.
Na mfano wa elimu ya Maneno, kama vile maneno katika utamu/uzuri wake na ubaya wake, na hukumu kuwa ni ya kale (iliyopitwa na wakati), maneno fulani maalumu katika kuthibitisha kufutwa kwa hukumu, na vitendo n.k. Na mfano katika lugha, kama maneno katika maudhui ya kuamrisha na kukataza, na mifumo ya ujumla, na ujumuishi na mbainishi, namna ya uwowote au namna ya umaalumu (uliodhibitiwa). Na mfano katika sayansi ya Hadithi, kama maneno kuhusu khabari. Hivyo mjuzi wa Elimu hizi hahitaji chochote katika elimu ya Misingi ya Fiqhi. Lakini asiyekuwa mjuzi wa hayo elimu ya Misingi ya Fiqhi haimnufaishi katika kuijua kinaganaga. Hivyo, elimu ya Misingi ya Fiqhi haikubakia chochote isipokuwa maneno fulani maalumu kwa mujibu wa makubaliano ya wanachuoni, na kutumika kipimo maalumu (qiyaas), mgongano na jitihada.
Na baadhi ya maneno katika makubaliano ya wanachuoni wa elimu ya Misingi ya Dini pia, na baadhi ya maneno katika elimu ya Qiyaasi, na mgongano kwa yale yenye kujitegemea kwa mwanafiqhi. Hivyo faida ya elimu ya Misingi ya Fiqhi yenyewe wakati huo ni chache.
Jawabu ni kuwa: Kuzuia hayo, wanaelimu wa Misingi wameingia ndani zaidi kutazama vitu mbalimbali katika maneno ya Waarabu ambavyo wanaelimu ya sarufi bado hawajavifikia wala wanalugha hawajavifikia. Kwa sababu maneno ya Waarabu yameenea, na kuyatazama ndani yake kuna matawi na pande mbalimbali. Hivyo vitabu vya lugha vinadhibiti matamshi na maana zake za wazi bila ya kuangalia maana za kina au za ndani ambazo zinahitajika kutazamwa kimsingi na kiShina kwa kusoma kwa upembuzi wa ziada dhidi ya upembezi wa kilugha.
Mfano wake: alama ya fomula ya kitenzi “افعل” (fanya) kwenye uwajibu, na kitenzi “لا تفعل” (usifanye) kwenye kuharamisha, na hali ya vitenzi saidizi vyenye kuonesha ‘ote’ na jamii ya vitenzi hivyo. Na mfano wa hivyo kwa yale yaliyotajwa na swali hili juu ya kuwa kwake ni lugha, kama utapekuwa hutokuta chochote katika hayo.
Na hivyo hivyo katika vitabu vya wanasarufi (wananahau) katika suala la ‘uteuaji katika orodha jumla’ ni kwamba kutoa kitu kabla ya hukumu au baada ya hukumu hiyo, na mengineyo katika uchambuzi wa kina ambao wanaelimu ya Misingi wanakumbana nayo na kuyachukua kutoka kwenye maneno ya Waarabu kwa upembuzi maalumu, na ushahidi maalumu ambao hauhitaji ufundi wa nahau/sarufi, na maajabu makubwa yatakupitia katika kitabu hiki” n.k .
Maana hiyo inasisitizwa hapo kabla na mwanachuoni As-Subkiy katika kitabu chake “Al-Ibhaaj Sharhul Minhaaj” ambapo anasema:
“Maana zote hizi kwa asili yake ni kwa mujibu wa maana za kilugha, hata kama wanalugha hawakuzitaja katika vitabu vyao. Nalo ni jambo wanalotutanabahisha kwamba wanaelimu ya Misingi wanakumbana na vitu mbalimbali ambayo wana lugha wao hawajakumbana navyo. ”
Katika maandiko haya tunabaini kuwepo kwa zana, hatua, mafungamano yake, na mchanganyiko wake kwa uoni jumla kwenye akili ya Mwislamu na juhudi kubwa ya kisayansi aliyoitanguliza inawakilisha baadhi yake katika yale waliyoyatanguliza wanaelimu ya Misingi katika sayansi ya Misingi ya Fiqhi.
3- Athari ya Misingi ya Fiqhi kwenye Nadharia ya Kisasa ya Kiislamu:
Kama tulivyotangulia kutaja, sayansi ya “Misingi ya Fiqhi” inaweza kuangaliwa kwa mazingatio tofauti. Hiyo ni elimu, na ni mchakato wa kinadharia wa kihatua kwa hatua. Nayo ni zana katika sayansi au elimu nyengine. Kama pia inavyoweza kunufaika nayo kwa kufikiria katika viunda vyake vyenyewe; vikiwemo: Maana yake, mitazamo yake, nyenzo zake za kutafakari katika maumbo yake kupitia historia ya kutokeza kwake na kunyooka (kustawi) kwake, kama vile tulivyotangulia kuwasilisha.
Hakika elimu ya “Misingi ya Fiqhi” inampa mtafiti wa elimujamii kwa mfano njia ya mtindo wa kinadharia ya kisayansi. Hivyo, mtafiti yeyote ni lazima kupitia utafiti wake – afanye michakato kadhaa au hatua mbalimbali: Aainishe vyanzo vya utafiti husika (ushahidi), aainishe mambo ya karibu ya utafiti husika (namna) au mtazamo uliojengeka nao, aainishe zana za utafiti; zana kwa kila michakato ya kitafiti: achanganue, atoe matokeo, atoe ushahidi na dalili, apekue n.k. Na aainishe masharti ya lazima kwa ajli ya kufanya utafiti. Na yote haya yanatofautiana na sayansi/elimu moja na nyingine katika sehemu zake hata kama zitawafikiana katika ujumla wake.
Vyanzo vya utafiti viko vya ngazi tofauti na maumbo tofauti: Miongoni mwake ni sayansi iliyotangulia au sayansi ya kuhudumia ambayo inasaidia kujenga suala la sayansi husika ambayo anaisoma. Hivyo sayansijamii na sayansiutu zinaingiliana na kusaidiana na wala baadhi ya elimu hizi haziwezi kujitegemea zenyewe bila ya kuwepo elimu mwenza. Miongoni mwa hizo ni kundi la kitafiti au kisayansi: Nalo ni lile linaloainishwa ndani yake yale yanayotokana na mtafiti miongoni mwa maelezo na viambata vya sayansi hii, mitazamo yake, mambo yake ya karibu ambayo yatatumika kuiboresha.
Inawezekana kutazama maendeleo ya kuundika kwa elimu ya “Misingi ya Fiqhi” kwamba ni mchakato wa kiutafiti ulioweka ndani yake miundo ya awali (maswali makuu) umeweka kwa mchango wake miundo ya kando – ya kimatawi, imeunda uchunguzi wa kisayansi na kiupekuzi na kimatokeo wenye kina kirefu. Umeanza kujiuliza kuhusu kadhia ya “Halali na haramu” na maamrisho ya sheria: Vipi tutafikia kwenye “Hukumu ya kisheria” katika masuala fulani au masuala makuu? Vipi tuziamue tofauti kati ya wazuoni wa Fiqhi katika “Hukumu za kisheria?" Wakasema kwa kutoa hoja, dalili na ushahidi:
“Sema: leteni ushahidi wenu kama nyinyi ni wasema kweli”.Na hii ndio asili ya elimu: Ushahidi.
Kwao ukajitokeza uelewa au kitu kigeni huru kilichobadilika jina lake ni “Ushahidi” unaoathiri katika kitu kigeni kilichobadilika kinachofwata jina lake (Hukumu ya kisheria). Hapa ikaja hatua ya kutoa maana ya kitu kigeni huru kilichobadilika (ushahidi) wakatoa maana yake kwa njia ya viashiria. Wakakuta kwamba vinakusanyika na viashiria vingine tofauti. Vilivyo muhimu zaidi ni: Iwe ni hoja, iwe thabiti na yakinifu, isiwe yenye kupinga kwa hoja au ushahidi mwingine au usiotiliwa mkazo. Hivyo, ikiwa zitatimia shuruti hizi au viashiria hivi basi hiyo ni hoja au ushahidi ambao utatumika kutolewa hukumu ya kisheria.
Lakini mchakato wa kutoa hukumu ya kisheria unasimama kwenye shuruti (maainisho ya uchanganuzi kama tunavyoona katika tafiti za kijamii, katika changanuzi za kisiasa, programu, matukio, na changanuzi za michakato mbalimbali. Nayo inawakilisha mazingira yanayopendeza au yasiyopendeza kwa matukio ya kitu kigeni huru kilichobadilika athari zake katika kitu kigeni tegemezi kilichobadilika. Shuruti hizi ni:
- Kusihi kwa uelewa wa hoja ya ushahidi, kwa sababu ushahidi – kwa wanaelimu ya Misingi ya Fiqhi – ni maandiko. Na maandiko yanahitaji zana maalumu ili kuyashughulikia; zana za lugha na sayansi yake kama vile Sarufi/Nahau, Swarfu, Balagha, Falsafa ya lugha, na zana nyinginezo zinazohusiana na mchakato wa utoaji ushahidi ulioongezwa na wanaelimu ya Misingi, kama vile kutenganisha kati ya hali za tamko na sentensi, kati ya ujumla na umaalumu, na uwowote na uliodhibitiwa, uwote-wote na usehemu au vipande vipande, uwazi na umalengo, na hali za viashiria kama ibara, ishara, hukumu, na mengineyo, na kunufaika katika hayo na Elimu nyengine kama mantiki ya Kiarabu iliyojificha katika lugha kama ilivyoashiriwa hapo kabla.
- Kupambanua kati ya hali ya dhana (ambayo inahukumiwa na mtazamo wa kukisiakisia na labda-labda) na hali ya kutoa maamuzi ya mwisho na athari za hayo kwa mchakato wa utoaji ushahidi. Sawa iwe katika kuithibitisha hoja (yaani kuiyakinisha) au katika kuelewa ushahidi wake. Mtafiti wa kijamii ambae anataka kufasiri uhalisia fulani au tukio fulani ni lazima apambanue kati ya nyenzo thabiti za uhalisia na nyenzo zenye shaka. Na kwa hivyo anajenga tafsiri yake ya kimsingi kwa lililothabiti sio la kudhania-dhania, na anajenga ukaguzi wake kwa ajili ya mustakbali wa tukio na malengo yake kwa msingi huo huo, kinyume na hivyo yatakuwa ni makisio-makisio na kumili kwa utashi binafsi.
- Katika hili inawezekana kunufaika na nyenzo ya “Makubaliano ya wanachuoni” ambayo yameimarishwa na sayansi/elimu ya Misingi ya Fiqhi, nayo yanahitajika katika kila Elimu. Hivyo bila ya makubaliano ya wataalamu mambo yote yatakuwa ni ya kudhania-dhania au yatakuwa yamebeba sura mbalimbali kama wanavyosema. Hivyo makubaliano ya wataalamu/wasomi ni fikra inayoweza kuwa ni muhimu mno khasa katika “tabia za Elimu ya kileo/kisasa”. Hivyo pamoja na kuenea hoja potofu (sophisticism) na uasi wa kiimani (Gnosticism) ambazo ni miongoni mwa nguzo za kile kinachoitwa “yale yaliyokuja baada ya usasa”, na kiwango fulani kisichofungamana na upande wowote ambacho kinatoa wito wa kutoka nje ya tabia za kielimu, na kutoa maelezo kuhusu sayansi/elimu kinyume na hali ilivyo kwa umbo la kifitina, katika hali hizi lazima kuwe na kidhibiti.
Kidhibiti hiki wanaelimu ya Misingi wamekiita “makubaliano ya wanachuoni/wasomi”. Pia inawezekana kuitwa vingine katika kila sayansi: “tabia za kisayansi”, “yaliyotulizana kwa wanautafiti”, “iliyomaarufu kwa wanasayansi”… na hili ndilo linalowakilisha uwowote na “uthabiti” katika sayansi yeyote, na inazingatiwa ndio uwanda mkuu na mwamvuli wa pamoja kwa wanasayansi: wanachuoni na wanafunzi.
- Upambanuzi kati ya aina za ushahidi na viwango vyake na daraja zake, na kutokutoa hoja kwa ushahidi mdogo mbele ya ushahidi wenye nguvu zaidi na wenye ushahidi uliothibiti. Jambo hilo katika utafiti wa kijamii na kimtazamo. Hivyo haitolewi hoja kwa masuala ya kimtazamo kwa rai zisizokuwa thabiti au kwa maandiko yenye ushahidi wenye kukanganya au ushahidi wenye tafsiri zenye pande kadhaa wa kadhaa. Pia katika masuala ya kisayansi (الإمبريقية) ushahidi uliothabiti zaidi ndio unaowasilishwa katika kuunda uhalisia na ufafanuzi wake, na mwenye kuyadiriki yaliyondani yake anachukua hatua, na akakaza ukaidi mkubwa katika masuala ya kubuni au kuwepo na lenye kuupinga ushahidi huo kikweli kweli.
- Hapa ndipo sayansi ya Misingi ya Fiqhi inapompa mtafiti nyenzo muhimu inayoitwa “uchawanyaji wa upingano” na “utiliaji mkazo/uzito” kati ya vyenye kupingana kwa upingano wa waziwazi. Nao katika mazingira ya mtafiti wa kijamii unamwelekeza kurejea kusoma maandiko yanayopingana, au kurejea kuchunguza uhalisia uliozuka upya, au kurejea kuangalia kwenye kanuni iliyotangulia na makisio-makisio yaliyowasilishwa, ima kutilia uzito kanuni hiyo (iliyokisiwa), ima kutilia uzito yaliyogunduliwa na uhalisia mpya kwa yale yenye shaka katika ukweli wa yaliyokisiwa… au ima umuwezeshe kukusanya kati ya mambo mawili wakati mgongano unapokuwa kwa kasoro isiyokuwa ya asili (ambayo ni pingaji)…n.k.
- Miongoni mwa mitindo ya Misingi ya Fiqhi ambayo utafiti wa kisayansi unaweza kunufaika nayo ni masuala ya “kuambatanisha” ambayo baadhi wanayaita kuwa “qiyaas” (kipimo), lakini la kwanza ndio la jumla zaidi kama ilivyotangulia kubainishwa. Na kuambatanisha kunahitaji uchunguzi na utafiti wa kina ili kuufanyisha kazi katika sayansijamii, ambapo inawezekana kufikiwa takwimu za kisayansi/kielimu, na kusaidia kuzalisha masuala ya kimatawi kwenye Misingi na ukuzaji wa kielimu pamoja na kuiendeleza.
Kuambatanisha kunahitaji kukiri kwa wanasayansi kwa misingi na masuala yaliyothibiti yaliyopitishwa na “makubaliano ya wanachuoni”, na kunahitaji kukiri kwa masuala mengine (yanayobadilikabadilika) ambayo yanazuka upya. Jambo jipya lililojitokeza linafanyiwa qiyaas pamoja na la kale na kuambatanishwa na tawi asili. Hili pia linahitaji utafiti wa “kivitendo” la kuambatanisha na hatua zake katika kuweka wazi kasoro na kuifanyia uchunguzi na kuisawazisha, pamoja na kudiriki maagizo ya michakato ya mzizi mkuu na kuugawa, na ambayo inaweza kutekelezwa kwenye uhalisia uliopo (الإمبريقية) wakati wa kutoa viashiria na kuvifanyia uhakiki, na kuvisawazisha viashiria hivi, hadi kwa vitendo kabisa viwe ni ushahidi wa kitu kigeni kilichobadilika (kilichojitokeza) katika mazingira tofauti.
Hakika njia hii ni bora zaidi kuichunga na kuizingatia; mpaka iiwezeshe sayansijamii kuwa na misingi na matawi, na michakato ya ujenzi na uimarishaji, kama ilivyotokea kwa Fiqhi ya Kiislamu mpaka ikawa jengo imara madhubuti.
Kwa mfano, “mfumo wa kidemokrasia” una viashiria thabiti vinavyowakilisha “misingi yake”. Hivyo, ikiwa kanuni katika sayansi ya siasa imekusanya tafiti (kwamba mfumo wa kidemokrasia ndio ulioegemea zaidi kwenye utulivu wa ndani na kusalimika nje ya nchi) kwa mfano, basi ukijitokeza mfumo wa kidemokrasia katika taifa fulani, litahukumiwa au kuhesabiwa kuwa litamili na kuegemea zaidi kwenye utulivu na kusalimika, lakini ni lazima kuhakikisha “udemokrasia” wa mfumo (serikali) hii. Hili ndilo lililowasilishwa na zana za uchunguzi na uhakiki, na kusawazisha maagizo katika mtazamo wa kuambatanisha.
Yote hayo yanaitwa – katika mtazamo wa wanamisingi – kuwa ni michakato ya kijitihada yenye kukubali kupatia na kukosea, na kumalizikia kwa ufupisho wa matokeo (matokeo ya utafiti – conclusions), na ambayo yanaitwa na wanaelimu ya misingi kuwa “hukumu” (nayo ni sentensi ya ujumla isiyoteremka kwenye uhalisia) au “fatwa” (inapohusiana na uhalisia fulani maalumu).
Toleo hili la Misingi ya Fiqhi na nyenzo zake katika kunufaika na sayansijamii haiwasilishi kitu kigeni kilichobadilika ambacho ni kigumu (kisichonyambuka), bali ni kisaidizi kinachoweza kunufaika nacho pamoja na uwezekano wa kuongezeka na kupungua na kubadilika kwa njia ya mitindo tofuati. Hili ni angalizo au mtazamo jumla, hwenda tukanufaika nao. Nao hauzuii kuwa kuna faida nyingine kinyume chake; ikimaanisha kutoka kwenye sayansijamii kwa ajili ya Misingi ya Fiqhi, hasahasa katika masuala ya udiriki wa uhalisia kama ni sehemu ya mtazamo wa kutoa maamuzi au kufutu jambo.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi wa yote
Vyanzo na Marejeo:
1) Kitabu kiitwacho “Al-Mahsuul” cha Ar-Raaziy (Fakhru Ddiin Mohammad bin Omar, amefariki mwaka 606 A.H.) kilichofanyiwa uhakiki na Dk. Twaha Jaabir Al-Alawaniy, chapa ya Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Imamu Muhammad bin Soud, chapa ya 1, 1399A.H./1979A.D.
2) Kitabu kiitwacho “Minhaajul Wuswuul ilaa Ilmil Usuul” – cha Kadhi Al-Baidhwawiy, Misri, Maktaba ya At-Tijaariya.
3) Kitabu kiitwacho “Fat-hul Mughiith” cha As-Sakhaawiy (Shamsu Ddiin Muhammad Abdurrahmaan bin Muhammad As-Shafiy Al-Masriy, amefariki mwaka 902 A.H.), kilichohakikiwa na Ali Husain Ali, chapa ya 1, Maktaba ya As-Sunna 1415 A.H. / 1995 A.D.
4) Kitabu kiitwacho “Al-Fiswal fil Milal wan Nihal” cha Ibn Hazm (Ali bin Ahmad bin Said bin Hazm Adh-Dhwahiriy Al-Andalusiy, amefariki mwaka 456 A.H.), na kwa tanabuhi (footnote) ya kitabu kiitwacho “Al-Milal wan Nihal” cha Shahrustaaniy, kilichotolewa nakala na Maktaba ya As-Salaam kwa chapa ya Muhammad Ali Swabiih, 1348 A.H.
5) Kitabu kiitwacho “Al-Ibhaaj” cha Aalu Ssubkiy (Taqiyyu Ddiin Ali bin Abdil Kaafiy As-Subkiy Ash-Shafiy, amefariki mwaka 756 A.H., na mwanawe Taaju Ddiin Abdulwahhaab bin Ali Ash-Shaafiy, amefariki 771 A.H.), chapa ya At-Tawfiiqil Adabiya.
6) Kitabu kiitwacho “Al-Hukmu in-dal Usuuliyyiina” cha Dk. Ali Juma, Maktaba ya Daarul Hidaaya, 1414 A.H. / 1993 A.D.
7) Kitabu kiitwacho “Al-Bahrul Muhiitw” cha Az-Zarkashiy (Badru Ddiin Muhammad bin Bahaadir bin Abdallah Ash-Shafiy, amefariki mwaka 794 A.H.), Maktaba ya Daarul Kutubiy, chapa ya 1, 1414 A.H. / 1994 A.D., na chapa ya Wizara ya Waqfu ya Kuweit, chapa ya 1, 1419 A.H. / 1988 A.D.
Chanzo: kitabu kiitwacho “Usuulul Fiqhi wa’alaaqatuhu bil Falsafatil Islaamiya” cha Mheshimiwa Mufti wa Jamhuri ya Misri, Pr. Dk. Ali Juma.

 

Share this:

Related Fatwas