Mfumo wa Kimaarifa wa Kiislamu na U...

Egypt's Dar Al-Ifta

Mfumo wa Kimaarifa wa Kiislamu na Uboreshaji wa Fikra ya Dini

Question

Ni upi mfumo wa kimaarifa wa Kiislamu? Na una athari gani katika uboreshaji wa fikra ya kidini? 

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, na sifa njema ni zake, na rehema na amani zimshukie Bwana wetu Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na Aali zake na Masahaba wake na wafuasi wake, na baada ya hayo:

Ni wazi kwamba sisi tuna haja ya kuunda mfumo wa kimaarifa unaojenga akili ya Mwislamu kwa mujibu wa imani yake na mtazamo wake wa kiujumla juu ya binadamu, ulimwengu na maisha na yaliyo kabla ya hayo pamoja na yaliyo baada yake. Mfumo ambao unawakilisha wigo na kipimo kinachotegemewa ndani ya akili ya mtu na nafsi yake nao ni msingi mkuu wa haiba ya Mwislamu na udhibiti wa fikra yake.

Tunahitaji kutengeneza tena upya mfumo huo ili tuweza kujibu maswali ya jumla kuhusu maisha ya mwanadamu, na mtazamo wake yeye mwenye na wanaomzunguka, mpaka tuweze kupambana na mahitaji ya zama hizi, na wengine watufahamu angalau kwa uchache, ikiwa hawatavutiwa na mfumo huu na kufanya haraka kuufuata kuuamini na kuujenga.

Mfumo huu wa kimaarifa tutauona upo katika dhamira yetu, na vyanzo vya ujenzi wake vipo kwenye imani yetu na hukumu zetu, lakini kuujenga tena upya kutatuwezesha kuuboresha na kuufanya ndio msingi wa maisha.

Lile ambalo tutalifanya pamoja na msomaji ni kufanya safari kwenye akili ya Mwislamu na kugundua ndani yake misingi ya kufikiri kwake sifa pekee ya akili yake na dhamira yake, na kubainisha ni namna gani hivyo vimeathiri katika fasihi sanaa na maisha, na namna gani yawezekana kuathiri kwa mara nyingine tena na kutoka Mwislamu kwenye huzuni yake na kuanza kujiimarisha na kazi za ujenzi wa Dunia pamoja na Akhera na kumpatia yale aliyokuwa anayahitajia sana.

1-Mwislamu amejibu swali la kwanza kwa mujibu wa imani yake: Sisi tunatokea wapi? Nalo ni suala linafungamana na wakati uliopita, lakini limezaliwa kutokana na mchanganyiko wa mwanadamu na ujinga wake wa kihisia wa kuanza kwake na makuzi yake, ni kama mtoto mdogo anapoulizwa umekuja kutoka wapi? Hakika hakumbuki siku ya kuzaliwa kwake, na wala hakuwa na uwezo wa kujua hilo, Mwenyezi Mungu Mtukufu Anasema: {Sikuwashuhudisha kuumbwa kwa mbingu na ardhi, wala kuumbwa kwa nafsi zao.Wala sikuwafanya wapotezao kuwa ni wasaidizi}[AL KAHF: 51].

Mwislamu anajibu sawa na imani yake kuwa Mwenyezi Mungu Ameumba mbingu na Akamuumba mwanadamu lakini Yeye ndiye Muumba wa kila kitu. {Arrah'man, Mwingi wa Rehema * Amefundisha Qur'ani Amemuumba mwanaadamu} [AR RAHMAAN, 1: 3].

2-Mwislamu anaamini upwekeshaji si upwekeshaji tu wa Mwenyezi Mungu, bali upwekeshaji unaokusanya kila kitu katika ujenzi wake wa kiimani, Mtume wake ni mmoja naye ndiye Mtume wa mwisho, Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema: {Muhammad si baba wa yeyote katika wanaume wenu, bali ni Mtume wa Mwenyezi Mungu na Mwisho wa Manabii,na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa kila kitu}[Al-Ahzaab, 40].

Na kitabu chake ni kimoja, hivyo basi kimehifadhiwa na uzushi na kufanywa ni kimoja na si vingi, Mola Mtukufu Amesema: {Hakika Sisi ndio tulioteremsha Ukumbusho huu, nahakika Sisi ndio tutao ulinda}[AL HIJR, 9].

Na umma wa Kiislamu ni mmoja, Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema: {Kwa hakika huu umma wenu ni umma mmoja, na Mimi ni Mola wenu Mlezi. Kwa hivyo niabuduni Mimi}{Al-Anbiyaa, 92}.

Na Qibla yao pia ni moja. MMwenyezi Mungu Mtukufu Amesema: {Kwa yakini tukiona unavyo geuza geuza uso wako mbinguni. Basi tutakuelekeza kwenye Kibla ukipendacho.Basi elekeza uso wako upande wa Msikiti Mtakatifu; na popote mnapokuwa zielekezeni nyuso zenu upande huo; na hakika wale walio pewa Kitabu wanajua kwamba hiyo ni haki itokayo kwa Mola wao Mlezi. Na Mwenyezi Mungu si mwenye kughafilika na yale wanayo yatenda}[AL BAQARAH, 144].

Ujumbe wao ni mmoja ndani ya nyakati zote, Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema: {Na fanyeni juhudi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu kama inavyo stahiki jihadi yake. Yeye amekuteueni. Wala hakuweka juu yenu mambo mazito katika Dini. Nayo ni mila ya baba yenu Ibrahim. Yeye (Mwenyezi Mungu) alikuiteni Waislamu tangu zamani, na katika hii (Qur'ani) pia, ili awe Mtume shahidi juu yenu, na nyinyi muwe mashahidi kwa watu. Basi shikeni Sala na toeni Zaka na shikamaneni na Mwenyezi Mungu. Yeye ndiye Mlinzi wenu, Mlinzi bora kabisa, na Msaidizi bora kabisa}[AL HAJJ, 78].

Na upwekeshaji kwa maana hii ambayo imekusanya vitu watu na kufanya kazi wakati wowote na popote, lazima iathiri kwenye akili ya Mwislamu wa zama hizi, na kuwa ndio msingi wa kufahamu kwake maisha pamoja na kushirikiana na walimwengu hasa mwanadamu.

3-Naye Mwislamu anaamini kuwa Mwenyezi Mungu hakumwacha kiumbe bila kumpa amri za kutekeleza, kuna sheria vitabu na ufunuo “Wahyi” Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema: {Na tumekuteremshia wewe, kwa haki, Kitabu hiki kinachosadikisha yaliyo kuwa kabla yako katika Vitabu na kuyalinda. Basi hukumu baina yao kwa aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu, wala usifuate matamanio yao ukaacha Haki iliyo kujia. Kila mmoja katika nyinyi tumemwekea sharia yake na njia yake. Na lau kuwa Mwenyezi Mungu Angelitaka angekufanyeni nyote umma mmoja, lakini ni kukujaribuni kwa aliyo kupeni}[Al-Maaida, 48].

Lakini Mola ameufanya Uislamu kwa jina hili ambalo lenye kuridhiwa kwa muda mrefu tokea kwa Adam mpaka kwa Muhammad S.A.W. Mwenyezi Mungu Amesema: {Bila ya shaka Dini mbele ya Mwenyezi Mungu ni Uislamu. Na walio pewa Kitabu hawakukhitalifiana ila baada ya kuwajia ujuzi, kwa sababu ya uhasidi uliokuwa baina yao}[AAL IMRAAN, 19].

Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Leo nimekukamiliishieni Dini yenu, na nimekutimizieni neema yangu, na nimekupendeleeni Uislamu uwe ndiyo Dini. Na mwenye kushurutishwa na njaa, bila ya kupendelea dhambi, basi hakika Mwenyezi Mungu ni Msamehevu na Mwenye kurehemu}[AL MAAIDAH, 3].

Kadhia ya kukalifishwa inajibu – au inapaswa kujibu – swali la pili, ambalo ni, nini tunafanya hapa? Na misingi ya kukalifishwa huku ni mitatu, wa kwanza wake: kumwabudu Mwenyezi Mungu, ibada hiyo ambayo ni lazima imwanzilishie mwanadamu ujenzi na ustaarabu, Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema: {Nami sikuwaumba majini na watu ila waniabudu Mimi * Na sitaki kwao riziki, wala sitaki wanilishe * Hakika Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kuruzuku, Mwenye nguvu, Madhubuti}[ADH DHARIYAAT, 56: 58].

Msingi wa Pili: Ni kuujenga ulimwengu, na hilo ni kwa kuendesha harakati za ujenzi na kujizuia na vitendo vya kubomoa, Mola Mtukufu Amesema: {Yeye ndiye aliye kuumbeni katika ardhi, na akakuwekeni humo. Basi mwombeni msamaha, kisha mtubu kwake. Hakika Mola wangu Mlezi yupo karibu, anaitikia maombi}[HUD, 61].

kwa maana amekutakeni kuujenga huu ulimwengu, Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema: {Na Musa alipoomba maji kwa ajili ya watu wake, tulimwambia: Lipige jiwe kwa fimbo yako. Mara zikatimbuka chemchem kumi na mbili; kila kabila likajua mahali pake pa kunywea. Tukawaambia: Kuleni na mnywe riziki ya Mwenyezi Mungu, wala msiasi katika nchi mkafanya uharibifu}[AL BAQARAH, 60].

Msingi wa Tatu: Ni kuitakasa nafsi, Mola Mwenye nguvu ya kusema Amesema: {Hakika amefanikiwa aliyeitakasa * Na hakika amekhasiri aliyeiviza}[ASH SHAMS, 9: 10].

4-Na Mwislamu anaamini kwamba kuna siku ya hesabu – thawabu au adhabu – Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema: {Basi anaye tenda chembe ya wema, atauona! * Na anaye tenda chembe ya uovu atauona!}{AZ ZALZALAH, 7: 8}.

Na imani hii inaathiri katika mwenendo wa Muumini kwa kurudi nyuma na kusonga mbele, utamwona anakimbilia kitu ambacho ndani yake kina uzito au kupitwa na matamanio pindi anapoona kuwa kitu hiko kinamuweka karibu na Pepo na kupelekea pia kupata thawabu, na utamwona akijizuia kufanya kitu chenye matamanio na kurudi nyuma, kwa sababu anakiona kitamuweka karibu na adhabu ya moto, na hili linafungamana na kadhia ya imani kwa Mwenyezi Mungu na imani ya kuamrishwa kutekeleza amri za Mola, na inaathiri maisha, na lazima iathiri kwa athari nzuri kinyume na hivyo hubadilika hali ya wasi wasi na mategemeo kuwa ni sababu ya kukwamisha maisha, ukweli ni kuwa Mwenyezi Mungu Ameweka sheria ili kulinda maisha, ikiwa matendo yetu yamebadilisha na kuwa ni kikwazo cha maisha hilo linakuwa kinyume na makusudio ya sheria takatifu.

Ibada ya Hijja imewekwa ili kuhifadhi nafsi katika sura zake zote, basi wala haipaswi kuigeuza na kupelekea yenye kuua nafsi ambayo Mwenyezi Mungu Ameharamisha kuiua isipokuwa kwa njia ya haki, ambapo tunapaswa kufahamu wakati na yale yaliyotokea ndani yake, na kufahamu sehemu na mapana yake, watu na viwango vyao vya elimu ya Dini yao, na hali pamoja na yale yaliyotokea miongoni mwa mabadiliko, basi tunafikia makusudio ya sheria kutokana na hayo.

Maswali haya matatu makubwa yameanzisha mjumuiko wa uwezo wa kiakili ambao umeanzisha haiba ya Mwislamu na ambao tunatarajia Waislamu warejee kwenye njia yake ambayo Mwenyezi Mungu Ameiteremsha kwa ajili yake na kufahamu makusudio ya Mwenyezi Mungu ya Wahyi wake.

5-Mwislamu anaamini moja kwa moja kuwa ameamini Mwenyezi Mungu hana mwisho wala mipaka, kukosekana mwisho na mipaka kumekuja kutokana na imani yake ya majina yake na sifa zake, majina ya Mwenyezi Mungu yaliyo mazuri ambayo yamepokelewa ndani ya Qur`ani na Sunna yamekuwa ni umbile la kimalezi kwa Mwislamu, Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na Mwenyezi Mungu Ana majina mazuri kabisa, basi muombeni kwa hayo. Na waacheni wale wanao haribu utakatifu wa majina yake. Hao watakuja lipwa waliyo kuwa wakiyatenda}[AL A'RAAF, 180].

Na majina ambayo Mwenyezi Mungu Amejisifia nayo ndani ya Kitabu chake ni zaidi ya majina 150, imepokelewa kwa Sunna zaidi ya majina 160, na jumla yake yote ni majina 220 baada ya kuondoa yale yaliyojirejea, majina haya pamoja na sifa hizi yawezekana kuzigawa kwenye sifa nzuri: Kama sifa ya kuwa mwingi wa rehema, mwenye kurehemu, mwenye msamaha na kusamehe, na sifa mbaya: Kama ulipizaji kisasi, mtenza nguvu, mwingi wa kunyongesha, na sifa za ukamilifu: Kama kuwa ni wakwanza na wa mwisho wadhahiri na wa siri, na kila anachosifika nacho Mwenyezi Mungu.

6-Muumini anajipamba kwa sifa nzuri, na wala hajipambi sifa zisizo nzuri isipokuwa anazifanyia kazi, husamehe na kupuuza, huizuia nafsi yake wakati wa hasira, Mwenyezi Mungu Amesema: {Enyi mlio amini! Kuweni wasimamizi madhubuti kwa ajili ya Mwenyezi Mungu mkitoa ushahidi kwa haki. Wala kuchukiana na watu kusikupelekeeni kutofanya uadilifu.Fanyeni uadilifu. Hivyo ndio kuwa karibu mno na uchamngu}[AL MAAIDAH, 8].

Na Mwenyezi Mungu Mtukufu Akasema: {Wengi miongoni mwa watu wa Kitabu wanatamani lau wange kurudisheni nyinyi muwe makafiri baada ya kuamini kwenu, kwa ajili ya uhasidi uliomo ndani ya nafsi zao, baada ya kwisha wapambanukia Haki.Basi sameheni na wachilieni mbali mpaka Mwenyezi Mungu Atapo leta amri yake. Hakika Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu * Na shikeni Sala na toeni Zaka; na kheri mtakazo jitangulizia nafsi zenu mtazikuta kwa Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu Anayaona mnayoyafanya}[AL BAQARAH, 109: 110].

Na hapa Mwenyezi Mungu Mtukufu Ameisifu sifa ya subra katika amri zake za kilimwengu au amri zake za kisheria kuwa Subira ni njema. {Lakini subira ni njema; na Mwenyezi Mungu ndiye wa kuombwa msaada kwa haya mnayo yaeleza}{YUSUF, 18} .. {Basi subiri kwa subira njema}[AL MA'AAREJ, 5] .. {Na vumilia hayo wayasemayo, na jitenge nao kwa vizuri}[AL-MUZZMMIL, 10].

Kujipamba na sifa nzuri na kuzifanyia kazi sifa mbaya kuamini sifa kamilifu ni katika uwezo wa akili ya Mwislamu.

7-Muumini anaona kuwa mwanadamu ni mwenye kutukuzwa, na wala si kwa vile tu ni sehemu ya ulimwengu, Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema: {Na hakika tumewatukuza wanaadamu, na tumewapa vya kupanda nchi kavu na baharini, na tumewaruzuku vitu vizuri vizuri, na tumewafadhilisha kwa fadhila kubwa kuliko wengi miongoni mwa tulio waumba}[AL ISRAA, 70].

Mwanadamu ni kiumbe wa pekee katika ulimwengu huu, kwa sababu yeye amekubali kubeba amana, Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema: {Kwa hakika Sisi tulikadimisha amana kwa mbingu naardhi na milima; na vyote hivyo vikakataa kuichukua navikaogopa. Lakini mwanaadamu akaichukua. Hakika yeye amekuwa dhaalimu mjinga} [AL AHZAAB, 72].

Muumini anaona kuwa mwanadamu ndiye bwana katika ulimwengu huu, na wala siyo bwana wa ulimwengu, kwani bwana wa ulimwengu huu ni Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema: “Ubwana ni wa Mwenyezi Mungu Aliyetukuka na utukufu”, basi ulimwengu ni wenye kutakasa. 

{Zinamtakasa zote mbingu saba na ardhi na vyote vilivyomo ndani yake. Na hapana kitu ila kinamtakasa kwa sifa zake. Lakini nyinyi hamfahamu kutakasa kwake. Hakika Yeye ni Mpole na Mwenye maghfira}[AL ISRAA, 44].

Na inasujudu pia kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu {Je! Huoni kwamba vinamsujudia Mwenyezi Mungu vilivyomo mbinguni na vilivyomo katika ardhi, na jua, mwezi, nyota, milima, miti, wanyama, na wengi miongoni mwa watu. Na wengi imewastahiki adhabu. Na anayefedheheshwa na Mwenyezi Mungu hana wakumhishimu. Hakika Mwenyezi Mungu hutenda Apendayo} [AL HAJJ, 18].

Lakini Muumini anapokuwa katika kutekeleza ibada za Mwenyezi Mungu Anakwenda mwendo wa bwana, na wala sio mwendo wa vitu vigumu.

{Na amefanya vikutumikieni vilivyomo mbinguni na vilivyomo katika ardhi, vyote vimetoka kwake. Hakika katika hayo zimo Ishara kwa watu wanao fikiri} [Al-Jaathiya, 13].

Na Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Je! Huoni kwamba Mwenyezi Mungu Amevidhalilisha kwenu vilivyomo katika ardhi, na marikebu zipitazo baharini kwa amri yake, na amezishika mbingu zisianguke juu ya ardhi ila kwa idhini yake. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye huruma kwa watu, Mwenye kurehemu}[AL HAJJ, 65].

8-Muumini anaamini kuwa zama sehemu watu na hali ni vitu vitukufu na anavipa uzito katika kuishi navyo, kwa mfano utamwona unautakasa usiku wa (Lailatul-Qadri) wenye cheo. Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema: {Hakika Sisi tumeiteremsha Qur'ani katika Laylatul Qadri, Usiku wa Cheo Kitukufu} [AL QADR, 1] ..  {Hakika tumekiteremsha katika usiku ulio barikiwa.Hakika Sisi ni Waonyaji} [Ad-Dukhaan, 3].

Anaitaka Ka’aba {Hakika Nyumba ya kwanza walio wekewa watu kwaibada ni ile iliyoko Bakka, iliyo barikiwa na yenyeuwongofu kwa walimwengu wote} [AAL IMRAAN, 96].

Na akasema Mtume S.A.W.: “Uzuri wako ulioje na uzuri wa harufu yako, ukubwa wako ulioje na ukubwa wa utukufu wako, ninaapa kwa yule ambaye jina la Muhammad lipo mikononi mwake, utukufu wa Muumini ni mkubwa zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu kuliko utukufu wako wewe na wa mali yake damu yake na utukufu wa kumdhania kheir” ([1])

Na anatakasa Msahafu. {Hapana akigusaye ila waliotakaswa} [Al-Waaqia, 79].

Anamtukuza Mtume S.A.W. kwa cheo cha juu {Msifanye wito wa Mtume baina yenu kama wito wa nyinyi kwa nyinyi. Hakika Mwenyezi Mungu Anawajua miongoni mwenu wanao ondoka kwa uficho. Basi nawatahadhari wanao khalifu amri yake, usije ukawapata msiba au ikawapata adhabu chungu}[AN NOOR, 63].

Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema: {Enyi mlio amini! Msinyanyue sauti zenu kuliko sauti ya Nabii, wala msiseme naye kwa kelele kama mnavyosemezana nyinyi kwa nyinyi, visije vitendo vyenu vikaharibika, na hali hamtambui}[Al-Hujuraat, 2].

Na katika jumla ya hayo yote yanatengeneza akili ya Mwislamu na nafsi yake, ili awe ni mtu wa pekee anaona ulinganio wote, na kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu kama Alivyoleta Mitume ndani ya mafundisho ya Kitabu cha Agano la Kale na Agano Jipya, basi amekamilisha Mitume hao kwa kumleta Mtume Muhammad na Agano la Mwisho na kuwa ndiye Mtume wa mwisho, na Mwenyezi Mungu pia Akaufanya kuwa ni umma mmoja kuanzia kwa Nabii Adam mpaka leo hii.

{Na pale Mwenyezi Mungu Alipochukua ahadi kwa Manabii: Nikisha kupeni Kitabu na hikima, kisha akakujieni Mtume mwenye kusadikisha mliyo nayo, ni juu yenu mumuamini na mumsaidie. Akasema: Je, mmekiri na mmekubali kushika agizo langu juu ya hayo? Wakasema: Tumekubali. Akasema: Basi shuhudieni, na Mimi ni pamoja nanyi katika kushuhudia} [AAL IMRAAN, 81].

Na huu mfumo wa kimaarifa unapaswa kuwa ni wenye kufanyiwa tathmini, na kipimo cha kukubalika kwa fikra za watu na miongozo yao, na kuwa ni msingi wa uboreshaji wa ulinganio Dini ambao unakubaliana na uelewa wa uhalisia wa mazingira tofauti.

Mfumo wa Kimaarifa wa Uislamu na Mfumo wa Mwenyezi Mungu:

1-Unatengeneza akili ya Mwislamu mjumuiko wa uelewa wa mfumo wa Mwenyezi Mungu, anaona yanayomzunguka miongoni mwa ulimwengu mpana, mpaka amesema Abu Al- Atahiya:

Na katika kila kitu kuna alama inayojulisha kuwa Yeye ni mmoja.

Qur`ani imezungumzia kuhusu mfumo na mwenendo huu wa Mwenyezi Mungu pamoja na kuubainisha, ambao unazingatiwa kuwa ni mazingira ya nje ya harakati za watu, na kumwongoza Mwislamu kwenye harakati zake na kuteua kwake na kuweka programu yake pamoja na malengo yake, mpaka ufahamu huu unapoondoka kwenye akili ya Mwislamu, basi anakuwa ni mwenye kujigonga na kupoteza vipimo sahihi kwenye maamuzi sahihi, na kuweka mikakati mingine isiyokuwa ile ambayo ameamrisha Mwenyezi Mungu.

Tunataja katika mfumo huo mifano mitatu tu, kwa sababu zenyewe ni zaidi ya mifumo hamsini ambapo nafasi haitoshi kutaja yote, isipoku kila mfumo au mwenendo unahitaji mazungumzo maalumu:

(1)                     Mfumo Shirikishi:

Mwenyezi Mungu Mtukufu Ameumba ulimwengu wenye sura mbalimbali, lakini wenyewe ni wenye kuungana kwenye malengo na makusudio, tofauti hizi ni katika aina na wala si katika vinyume, usiku na mchana vinatengeneza siku moja, na kila mmoja kati yao unasifa maalumu, mwanamume na mwanamke kila mmoja anasifa maalumu na kazi maalumu, mtawala na mtawaliwa kila mmoja anakazi yake, tajiri na masikini, pande mbili nyingi ni za maumbile au (kadari) makadirio, maumbile kama vile usiku na mchana mwanamme na mwanamke, kadari ni kama vile mtawala na mtawaliwa tajiri na masikini, tumeita kadari ili kutofautisha na maumbile, hata kama kutakuwa ndani yake kuna juhudi za mwanadamu kuteua na kufanikiwa, isipokuwa hayo ni kwa fadhila za Mwenyezi Mungu na (kadari) makadario yake pia.

 Kufahamu mfumo shirikishi kunafanya kwa Mwislamu asili ya kuumba ni kushirikiana na si kugombana, kwa sababu hiyo mahusiano ya mwanamme na mwanamke yanafahamika kuwa yemeumbwa ili kushirikiana, tofauti na mielekeo ambayo inalingania kwamba asili ni kugombana, na mwanamke analazimika kuvutana na mwanamume ili aweze kupata haki zake, na mwenye kutawaliwa au kuongozwa ni lazima agombane na kiongozi au mtawala ili naye aweze kupata haki zake, mwanadamu analazimika kuvutana na ulimwengu ili aweze kupata manufaa yake, hayo ndiyo yaliyokubalika kwenye fikra za Kigiriki katika nadharia ya mvutano wa Miungu mwishowe ni ushindi kwa mwanadamu.

Na kufahamu mfumo shirikishi hakukanushi kutokea kwa mvutano na ugomvi au uwezekano wa kutokea kwake na kutokea kwenyewe, lakini kunatofauti ya kufanya kuwa ni asili ya maumbile isiyowezekana kuachika, na kuifanya ni yenye kuzuka lazima tuimalize ili mambo yaweze kutulia katika hali yake ya kwanza ambayo Mwenyezi Mungu Ameiumbia.

Ushirikiano huu ndio ambao unatenganisha ufahamu wake kati ya maana ya kiroho ya jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu na vita ambavyo vinaanzishwa huku na kule kwa ajili ya masilahi utawala ukubwa Duniani pia na kufanya ufisadi.

Basi angalia kauli ya Mola Mtukufu mwanzoni mwa Surat an-Nisaai:{Enyi watu! Mcheni Mola wenu Mlezi aliye kuumbeni kutokana na nafsi moja, na akamuumba mkewe kutoka nafsi ile ile. Na akaeneza kutokana na wawili hao wanaume na wanawake wengi. Na tahadharini na MwenyeziMungu ambaye kwaye mnaombana, na jamaa zenu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuwaangalieni}[AN NISAA, 1].

Na Akasema tena: {Na tumefanya usiku na mchana kuwa ishara mbili. Tena tukaifuta ishara ya usiku, na tukaifanya ishara ya mchana ni yenye mwangaza ili mtafute fadhila itokayo kwa Mola wenu Mlezi, na mpate kujua idadi ya miaka na hisabu. Na kila kitu tumekifafanua waziwazi} [AL ISRAA, 12].

Akasema tena Mwenyezi Mungu Mtukufu:{Sema: Ewe Mwenyezi Mungu uliye miliki ufalme wote! Wewe humpa ufalme umtakaye, Na humwondolea ufalme umtakaye, Na humtukuza umtakaye, na humuangusha umtakaye. Kheri yote iko mikononi mwako. Hakika Wewe ni Muweza wa kila kitu} [AAL IMRAAN, 26].

Mola Mtukufu Akasema tena: {Kwani wao ndio wanao gawa rehema za Mola wako Mlezi? Sisi tumewagawanyia baina yao maisha yao katika uhai wa duniani, na tukawanyanyua baadhi yao juu ya wengine kwa daraja nyingi; kwa hivyo baadhi yao wanawafanya wenginewe wawatumikie. Na rehema za Mwenyezi Mungu ni bora kuliko hayo wanayo yakusanya} [AZ ZUKHRUF, 32].

Kupigana Jihadi ndogo au kubwa katika njia na misingi ya Mwenyezi Mungu, jihadi ndogo na kubwa zinatokana na wakati ambao unachukuwa kila moja. Mtume S.A.W. amesema “Tumerejea toka kwenye Jihadi ndogo na sasa tunaelekea kwenye Jihadi kubwa, nayo si nyingine isipokuwa ni Jihadi ya nafsri”, na Mwenyezi Mungu Mtukufu Akasema: {Na fanyeni juhudi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu kama inavyo stahiki jihadi yake. Yeye amekuteueni. Wala hakuweka juu yenu mambo mazito katika Dini}[AL HAJJ, 78].

Mwenyezi Mungu Mtukufu Akasema:{Na wanaofanya juhudi kwa ajili yetu, Sisi tutawaongoa kwenye njia zetu. Na hakika Mwenyezi Mungu yu pamoja na watu wema} [Al-Ankaboot, 69].

Kupigana Jihadi kunakopelekea mauaji hakuchukui zaidi ya muda wa mapigano tu nao ni muda mdogo kwa hali yeyote ile, ama mapigano yanayochukuwa muda mrefu sana na kushirikisha watu wote na kutumika ardhi yote hiyo ndiyo jihadi ya nafsi.

Jihadi ya kupigana mtu hufanya vizuri kwa lengo la kuleta furaha kwa mwingine inachukuwa maana ya ukombozi, kutajwa kwake kuwa ni jihadi ndogo hakupunguzi umuhimu wake ila kunaashiria muda wake, na ni mapigano yanayoibuka kwa lengo la kurejesha hali ya utulivu na uwiano ambao Mwenyezi Mungu Amewaumbia watu tokea mara ya kwanza.

Kwa ajili hiyo ndiyo maana tumeona kuwa muuaji ni tofauti na mpambanaji, na yule aliyeanza kufanya kitendo cha uuaji kwa mara ya kwanza anabeba dhambi za kila anayejihusisha na kitendo hiki kwa kipindi kirefe. Mwenyezi Mungu Anatuhadithia kisa cha watoto wa Nabii Adam kwa lengo la kupata fundisho, Anasema: {Na wasomee khabari za wana wawili wa Adam kwa kweli. Walipo toa mhanga, ukakubaliwa wa mmoja wao, nawa mwengine haukukubaliwa. Akasema: Nitakuuwa. Akasema mwengine: Mwenyezi Mungu huwapokelea wachamngu * Ukininyooshea mkono wako kuniuwa, mimi sitakunyooshea mkono wangu kukuuwa. Hakika mimi namwogopa Mwenyezi Mungu, Mola wa walimwengu wote * Mimi nataka ubebe dhambi zangu na dhambi zako,kwani wewe utakuwa miongoni mwa watu wa Motoni. Na hayo ndiyo malipo ya wenye kudhulumu * Basi nafsi yake ikampelekea kumuuwa nduguye, akamuuwa na akawa miongoni mwa wenye kukhasirika * Hapo Mwenyezi Mungu Akamleta kunguru anaye fukua katika ardhi ili amwonyeshe vipi kumsitiri nduguye. Akasema: Ole wangu! Nimeshindwa kuwa kama kunguru huyu nikamsitiri ndugu yangu? Basi akawa miongoni mwa wenye kujuta * Kwa sababu ya hayo tuliwaandikia Wana wa Israili ya kwamba aliye muuwa mtu bila ya yeye kuuwa, au kufanya uchafuzi katika nchi, basi ni kama amewauwa watu wote. Na mwenye kumuokoa mtu na mauti ni kama amewaokoa watu wote. Na hakika waliwajia Mitume wetu na hoja zilizo wazi. Kisha wengi katika wao baada ya haya wakawa waharibifu katika nchi * Basi malipo ya wale wanao mpiga vita Mwenyezi Mungu na Mtume wake na wakawania kufanya uchafuzi katika nchi, ni kuuwawa, au kusulubiwa, au kukatwa mikono yao na miguu yao kwa mabadilisho, au kutolewa nchini. Hii ndiyo hizaya yao katika dunia; na katika Akhera watapata adhabu kubwa * Isipokuwa wale walio tubu kabla hamjawatia nguvuni. Na jueni kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwenye maghfira na Mwenye kurehemu * Enyi mlio amini! Mcheni Mwenyezi Mungu, na tafuteni njia ya kumfikilia. Na wanieni kwa juhudi kwa ajili yake ili mpate kuokoka} [AL MAAIDAH, 27: 35].

Inakuwa wazi kwa maelezo haya kuwa Jihadi katika njia yake lengo lake ni mafanikio na kumaliza uharibifu Duniani, na kuachana na maana ya uuaji ambao Mwenyezi Mungu Ameufanya kuwa ni alama ya udhalilifu wa mwanadamu na adhabu yake, na kwenda kwenye uelewa wa kupambana kwa lengo la kuondoa uadui na upotovu, na kutonyamazia uovu, na ufisadi mbaya Duniani.

(2)                     Mfumo wa Kujitetea:

Nao ni mfumo uliochukuliwa ndani ya kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu pale Aliposema:{Kwa idhini ya Mwenyezi Mungu waliwatimua, na Daudi akamuuwa Jaluti, na Mwenyezi Mungu Akampa Daudi ufalme na hikima, na akamfundisha aliyo yapenda. Na lau kuwa Mwenyezi Mungu hawapambanishi watu kwa watu basi dunia ingeliharibika. Lakini Mwenyezi Mungu ni Mwenye fadhila juu ya walimwengu wote} [AL BAQARAH, 251].

Maelezo haya ya Qur`ani yanaelezea ukweli wa ukubwa wa Qur`ani katika kutafsiri ambayo yamewekewa mkakati na mwanadamu, yenyewe haikuelezea kwenye maelezo haya mauaji au mvutano na ugomvi – kama ilivyopokelewa kwenye tafsiri mbalimbali – lakini maelezo yameelezea juu ya kujitetea kunako kusanya aina zote za ushirikiano na kutafautiana, bali mvutano na mgongano ili kufikia njia za utulivu na kufikia malengo ya Mwenyezi Mungu kwa viumbe vyake ambayo ni: Ibada, Ujenzi, Utakaso.

Kujitetea ni katika mfumo na mwenendo wa Mwenyezi Mungu unaobainisha kuwa mwanadamu ameumbwa na Mwenyezi Mungu Mtukufu kuwa ni mwanajamii mwenye kuhitaji wenzake, na wao wanamhitaji pia, hakumuumba kuwa mpweke mwenye uwezo wa kubakia peke yake, mpaka aweze afikie lengo la Mwenyezi Mungu la kumuumba kwake, bali ni lazima kwa mwanadamu kufanya kazi kwa pamoja ili kufikia lengo lake, kufanya kwake kazi katika kundi au timu na harakati zake kijamii pamoja na mihangaiko yake binafsi vyote hivyo vinahitaji kufahamu mfumo na mwanendo wa kujitetea, na kufahamu mfumo huu kunazaliwa ndani yake kanuni nyingi ili kudhibiti harakati hizi na mihangaiko hii, ni lazima mwenendo wa kifikra utangulie kitendo, nayo ni anaweza kuwa mwanadamu wa zama hizi hana ambapo fikra imetanguliwa na kitendo, na ilikuwa anapaswa fikra itangulie kitendo na kutangulia pia mazungumzo ya moyo na fikra, na kwa hili ni sehemu nyingine inasherehesha tofauti ya mambo haya mawili.

(3)                     Mfumo wa Uwiano:

Nao ni mfumo wa kidunia ameuashiria Mwenyezi Mungu, Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na ardhi tumeitandaza na humo tumeweka milima, na tumeotesha kila kitu kwa kiasi chake}[AL HIJR, 19].

Na wa kipimo: Mola Amesema: {Na wekeni mizani kwa haki, wala msipunje katika mizani} {AR RAHMAAN, 9}.

Na Akasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:{Mwenyezi Mungu ndiye Aliyeteremsha Kitabu kwa Haki, na Mizani. Na nini kitakacho kujulisha ya kwamba pengine Saa ya Kiyama ipo karibu?}[AS SHURA, 17].

Na Akasema tena: {Kwa hakika tuliwatuma Mitume wetu kwa dalili waziwazi, na tukateremsha Kitabu pamoja nao na Mizani,ili watu wasimamie uadilifu, na tumeteremsha chuma chenye nguvu nyingi na manufaa kwa watu, na ili Mwenyezi Mungu Amjue anaye mnusuru Yeye na Mitume wake kwa ghaibu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu Mwenye kushinda} [AL HADID, 25].

Tunaona kwa mara nyingine kuwa hali ya utulivu ndio msingi ambao harakati za mwanadamu lazima ziishie katika hilo baada ya msukosuko ambao anaanza nao, na tunapozungumzia mfano wa mfumo huu tutaona kuwa ni mfumo wa Dunia na mfumo wa kipimo, tunachukuwa sura yetu ya mazingira, sura yetu kwenye mtindo wa fikra na sura yetu katika ufahamu wa uadilifu hasa pindi tunapouona ukifika mpaka siku ya mwisho na hesabu na kuwa ni kijulisho cha uadilifu wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, Mola Amesema: {Nasi tutaweka mizani za uadilifu kwa Siku ya Kiyama. Basi nafsi haitadhulumiwa kitu chochote. Hataikiwa ni uzito wa chembe ya khardali tutaileta. Nasi tunatosha kuwa washika hisabu}[Al-Anbiyaa, 47].

Na Akasema tena: {Na Siku hiyo kipimo kitakuwa kwa Haki. Basi watakaokuwa na uzani mzito, hao ndio watakaofanikiwa} {AL A'RAAF, 9].

Na ambalo mwanadamu lazima atekeleza hilo, kisha inakuja utekeleza wa maamrisho kwa mujibu wa mfumo huu akiashiria kuwa utekelezaji wa amri kwa hukumu kunafungamana mfungamano kamili na mfumo wa Mungu unaotuzunguka, na kutekeleza hukumu hizi kupitia ufahamu wetu wa mfumo wa Mwenyezi Mungu na namna ya kuufanyia kwetu kazi ndiyo dhamana ya kufikia lengo na makusudio, Mwenyezi Mungu Mtukufu Anasema:{Na kwa watu wa Madyana tulimtuma ndugu yao Shua'ib. Akasema: Enyi watu wangu! Muabuduni Mwenyezi Mungu. Hamna Mungu mwengine isipo kuwa Yeye. Imekwisha kufikieni hoja wazi kutoka kwa Mola Mlezi wenu. Basi timizeni sawa sawa vipimo na mizani, wala msiwapunje watu vitu vyao, wala msifanye uharibifu katika nchi, baada ya kuwa imekwisha tengenea. Hivi ndivyo bora kwenu ikiwa nyinyi ni Waumini} [AL A'RAAF, 85].

Somo la mfumo wa Mungu bali na utulivu wake, ni elimu inayobainisha uhusiano wake na misingi mikuu ya Qur`ani ambayo inajenga pia akili ya Mwislamu, kwa kuonea kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Sema: Je nitafute Mola Mlezi asiye kuwa Mwenyezi Mungu, na hali Yeye ndiye Mola Mlezi wa kila kitu? Nakila nafsi haichumii ila nafsi yake. Na habebi mwenye kubeba mzigo wa mwenziwe. Kisha marejeo yenu ni kwa Mola wenu Mlezi, naye atakuambieni mliyo kuwa mkikhitalifiana}[AL AN'AAM, 164] .. Na kauli Yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Mtakuwa nao uhai mzuri katika kulipiza kisasi enyi wenye akili, ili msalimike} [AL BAQARA, 179] .. Na kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Enyi mlioamini! Msiue wanyama wa kuwinda nanyi mmeharimia katika Hija. Na miongoni mwenu atakaye muuwa makusudi, basi malipo yake yatakuwa kwa kuchinja kilicho sawa na alicho kiuwa, katika mifugo, kama wanavyo hukumu waadilifu wawili miongoni mwenu. Mnyama huyo apelekwe kwenye Al Kaaba, au kutoa kafara kwa kuwalisha masikini; au badala ya hayo ni kufunga, ili aonje ubaya wa jambo lake hili. Mwenyezi Mungu amekwisha yafuta yaliyo pita; lakini atakaye fanya tena Mwenyezi Mungu Atampa adhabu. Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye nguvu na Mwenye kuadhibu} [AL MAAIDAH, 95].

Na kauli yake Mola Mtukufu: {Na ya kwamba hatapata mtu ila aliyo yafanya mwenyewe?} {[AN NAJM, 39].. Na kauli yake pia: {Na fanyeni juhudi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu kama inavyostahiki jihadi yake. Yeye amekuteueni. Wala hakuweka juu yenu mambo mazito katika Dini. Nayo ni mila ya baba yenu Ibrahim. Yeye (Mwenyezi Mungu) alikuiteni Waislamu tangu zamani, na katika hii (Qur'ani) pia, ili awe Mtume shahidi juu yenu, na nyinyi muwe mashahidi kwa watu. Basi shikeni Sala na toeni Zaka na shikamaneni na Mwenyezi Mungu. Yeye ndiye Mlinzi wenu, Mlinzi bora kabisa, na Msaidizi bora kabisa} [AL HAJJ, 78].

Mpaka mwisho wa misingi na kanuni – inayobainisha kuwa madhara yanaondoshwa, uyakinifu hauondoshwi na shaka, mambo ni kwa makusudio yake …. Na mfano wa hayo.

Ninasema kuwa: Somo la mifumo ya Mungu limekuwa ni lazima ambapo linaweza kunufaisha mwanadamu na ubinadamu na kuwa na mtazamo mpya wa mkusanyiko wa sayansi ya kijamii na kiutu, na yawezekana kwa mtazamo huu kuandaa uboreshaji wa kisayansi wenye mwamko wa uhubiri wa Kidini.

1-Marehemu Sheikh Muhammad Al-Sadik Arjuon ametunga kitabu cha mifumo na mienendo ya Mwenyezi Mungu, na akatoa wito Sheikh Rashid Ridhaa katika kitabu “Al-Manar” wa kugeukia mifumo hiyo, na katika wazungumzaji amezungumzia hilo Dkt. Jamal Atiyya, na Bibi. Zainab Atiyya aliiandikia kamusi elezi, Dkt. Abdulkarim Zidan aliandika kitabu “Mustaqill”, kuna michango mingi ya uandishi akiwemo Dkt. Mustafa Al-Shakaa na mwanafunzi wake, ama kitabu cha Dkt. Seif Abdulfattah “Madkhal Al-Qiyam” kinazingatiwa ni jaribio la kweli la kuanza uandishi elimu hii ambayo imetufikia na kutengeneza elimu ya asili ya sheria “fiqh” ya ustaarabu baada ya Imam Shafi kutengeneza elimu ya asili ya sheria “fiqh” kwa maandiko matakatifu.

Kitendo cha kuasisi elimu, ambacho kilisimama katika karne ya nne Hijria, na utengenezaji wa ustaarabu ndani ya karne hiyo sawa na mahitaji ya zama za sasa tunazoishi – ni asili katika uboreshaji wa ujumbe wa Kidini na kuwa mbali kabisa na ujinga tamaa na kutarajia ambavyo vinapita kwenye akili zetu pamoja na uvivu mkubwa wa kuhangaikia elimu.

Mfumo wa kimaarifa na kufahamu ukweli:

1-Kufahamu ukweli na uhalisia wa mambo mbalimbali ya ulimwengu ni sehemu katika sehemu za uboreshaji wa ujumbe wa Kidini, na tunalazimika kuboresha maana ya ukweli wa maisha ambayo tunayaishi na kuyafanyia kazi, na ukweli na uhalisia unapande tano: Ulimwengu wa vitu, Ulimwengu wa watu, Ulimwengu wa matukio, Ulimwengu wa fikra na Ulimwengu wa mifumo, na inawezekana kuongeza katika vitu hivyo kila siku yale yanayokwenda sawa na kuusoma ukweli na uhalisia, pamoja na kuchambua nyenzo zake.

Kama vile ni lazima kufahamu kuwa mambo haya matano ni yenye mwingiliano mkubwa, na wala si yenye kuvitenga kwa sura yeyote ile, itakayofanya kufahamu uhusiano wa ana kwa ana kati ya kila jambo na mengine ni sehemu isiyogawanyika kwenye uelewa wa uhalisia ufahamu wa kina na wazi, na pia lazima juu yetu kufahamu kuwa mambo haya sio thabiti, hivyo hakuna budi kuyafahamu kwenye mabadiliko yake ya kila siku yanayoendelea kwa kuzingatia kuwa ni mfumo na mwenendo wa Mwenyezi Mungu ndani ya Ulimwengu wake.

 Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Vinamwomba Yeye vilivyomo katika mbingu na ardhi. Kila siku Yeye yumo katika mambo} [Ar-Rahmaan, 29].

2-Ulimwengu wa vitu unahitaji mfumo katika kuufanyia kazi, marejeo yake ni katika elimu ya vitendo ambayo imefikiwa na Waislamu na wasiokuwa Waislamu mafanikio makubwa katika kuunyenyekesha Ulimwengu na kunufaika nao pamoja na kupata nguvu katika mambo ya afya, maisha ya kila siku, elimu…..nk. kuelekea kwenye maisha yaliyobora, na elimu ya vitendo lazima tuichukue katika wigo wa uelewa wa wazi nao ni:

(a)                       Yenyewe haina mpaka kwenye utafiti wa kielimu kwa upande wowote ule utakao kuwa, amri ni jumla na kutokuwa na mipaka katika kupata elimu, na hayo ni katika aya mbili zenye kupambanua, aya ya kwanza inafidisha ujumla, na aya ya pili inafidisha kutokuwa na mipaka, Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema: {Je! Afanyae ibada nyakati za usiku kwa kusujudu na kusimama akitahadhari na Akhera, na akitaraji rehema za Mola wake Mlezi...Sema: Ati watakuwa sawa wale wanao jua na wale wasio jua? Hakika wanao kumbuka ni watu wenye akili}[AZ ZUMAR, 9].

Kukosa mipaka elimu na kutoainishwa nini anajifunza? Je anajifunza ya ulimwengu au ya kisheria yenye faida au kutokuwa na faida?

(b)                      – Kilicho sahihi ni kufahamu kuwa elimu katika lugha ya Qur`ani ni ile inayofikisha kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na katika watu, na wanyama, na mifugo, pia rangi zao zinakhitalifiana. Kwa hakika wanao mcha Mwenyezi Mungu miongoni mwa waja wake ni wanazuoni. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye kusamehe} [FAATIR, 28].

Wanachuoni ni uwingi wa neno mwanachuoni, na wala sio uwingi wa neno msomi, uwingi wa msomi wasomi na uwingi wa mwanachuoni ni wanachuoni, mfano wa mwingi wa hekima na wanahekima, mzoefu wazoefu mtambuzi watambuzi, Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Tunawatukuza kwenye vyeo tuwatakao; na juu ya kila ajuaye yupo ajuaye zaidi} [YUSUF, 76].

(c)                        Ni lazima kuifanyia kazi elimu na kutumika katika maisha kwa maadili amri na makatazo ya Mungu ambayo mwanadamu anahitaji maisha mazuri, yanayopelekea kwenye kujenga na wala si kubomoa, yenye kupelekea uhuru wa mwanadamu na wala si kuondoa matakwa yake, maisha yenye kupelekea usawa kati ya watu na wala si kupelekea ibada ya baadhi kuabudu wenzao, na kutawala eneo la kaskazini dhidi ya kusini, mwenye nguvu dhidi ya mnyonge, basi wala usitufikishe ujuzi wa uzazi wa kupandikiza mbengu za kiume, au teknolojia ya habari ya mwili mzima DNA/habari zote zilizo katika chembe za urithi… au kubadili chembe za urithi za vitu vilivyo hai RNA, au mwingiliano wa biolojia pamoja na elimu ya anga kwenye uharibifu wa kijamii, au mabavu ambayo yanapelekea masilahi kwa baadhi dhidi ya wengine, au kupelekea ramani ya maumbile kutawala utashi na uteuzi wa udanganyifu.

(d)                       Lazima kumalizana na nadharia potofu zisizo na ukweli, nazo ni akili zisizoweza tenganisha kati ya mambo mbalimbali wala kuleta dalili sahihi kuthibitisha kadhia inayojadiliwa, au kufuata mfumo maalumu uliowazi katika kuishi ukweli, au kutegemea vyanzo vya maarifa, nadharia hii au akili hii potofu ambayo tunahitaji kumalizana nayo lazima iwe kwenye masuala ya hisia, akili, na sheria, mifumo hii tofauti ambayo inalingania kwenye kujilipua, utekeji, kurudia yale yale pasi na kuleta mapya, mitazamo dhaifu na kujisahau – ni mifumo ya kukatiliwa, mfumo wa kujilipua au kujitoa mhanga unaopelekea kwenye kukufurisha mwishowe unapelekea kwenye kubomoa na kulipua pia wenye kukatiliwa, mtindo wa kuteka wengine na kushambulia vyanzo vya sheria kwa watu wasio weledi wa kupambanua kati ya ukati na kati katika Dini kisha na kutujia na mtazamo wa kupinga kauli za majopo ya wanachuoni, au kutojua mahitaji ya lugha, maana ya Uislamu, au kuugeuza Uislamu kuwa elimu ya utandawazi wa Uungu.

Mfumo wa mitazamo dhaifu na kujitenga unaopelekea kuacha ukweli unafanana na kukimbia siku kutambaa “kiyama” ni mfumo pia usiokubalika, kwa kuzingatia kuwa mchanganyiko wa watu na kuwa nao na subira ni bora mbele ya Mwenyezi Mungu kuliko kujitenga nao, Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema: {Lakini subira ni njema; na Mwenyezi Mungu ndiye wa kuombwa msaada kwa haya mnayo yaeleza} [Yusufu, 18].

Amesema Mtume S.A.W.: “Mwislamu anapokuwa anajichanganya na watu kisha akawa ni mwenye kuwavumulia kwa kero zao, ni mbora kuliko Mwislamu ambaye hachanganyiki na watu na wala si mwenye kuvumilia kero zao”.

Ama mfumo wa kurudia yale yale pasi na kuleta mapya ni kushikamana na masuala ya urithi ushikamanaji unaoelezea sura yake pasi na kuwa na mfumo ili iwezekane hata kuboresha ikiwa itahitajika uboreshaji, au kunufaika nao hata katika hali yake hiyo hiyo ikiwa inafaa.

Nao ni mfumo wa (kizamani) – ikiwa itafaa kuelezea hivyo – unahitaji kwa msisitizo mkubwa kufumbia macho ukweli wetu au uhalisia wetu, na kuendelea kwenye ukweli ambao unaweza kubadilisha maisha mpaka tumeona watu wengi wakitoka kwenye Dini ya Mwenyezi Mungu kwa dhana yao kuwa hii ni Dini ya Mwenyezi Mungu, na Dini ya Mungu kwa ukweli wake haiendani na wakati wetu huu, yeye na wao ni wenye makosa na kutumbukia kwenye makosa, ni mwenye makosa kwa sababu amekwenda kinyume na ukweli, na mwenye kutumbukia kwenye makosa kwa sababu amekwenda kinyume na uhalisia.

Ama mfumo wa kujisahau tunaona kwa wengi wakiwa nje ya masomo ya Kidini ya kiakademi, wale ambao wamejiingiza wenyewe kwenye masuala ya kuzungumzia sheria takatifu wakiwa na ari ya kutenganeza Dini kwa madai yao au kutoa rai zao ambazo wanaziona ni muhimu, na tunawaona pia kwa wasomeshaji wa masomo ya sheria katika hatua za mwanzo, pamoja na dhana isiyosawa na dhana ya wanachuoni waliobobea katika elimu, ambapo wanaamini kuwa wao wana haki katika kuleta maboresho kwenye Dini, wakisahau uchache wa uwezo wao wa sheria kwa upande mmoja, na masafa kuwa ni mapana sana kati yao na kufahamu ukweli kwa upande mwingine, na hapa inatupasa kuzinduka juu ya tofauti muhimu kati ya tafiti katika elimu fulani na kuzungumzia kutokana na elimu hiyo, na tofauti ya neno (katika/ndani ya) elimu, na (kutokana na/kuhusu) elimu, kwa sababu neno (katika/ndani ya) elimu linalazimisha kukamilisha mchakato wa elimu kwa pande zake tano: Upande wa mwanafunzi, mwalimu, kitabu, silabasi na mazingira ya kielimu, nao ni mchakato wenye kutoa umuhimu wa maarifa tathmini na ulezi wa umiliki, na unahitaji matokeo yake uwepo wa matawi weledi vifaa na muda wa kutosha, kuongezea pia maandalizi asilia kama utambuzi kwa kuzingatia ndiyo nguvu ya kuunganisha elimu, na shime ya kupata elimu ambayo inawezaitwa umuhimu, pamoja na kutoa juhudi endelevu.

Aliwahi kuashiria Imam Shafi hapo zamani katika yale yenye kubainisha kuwa mtaala au silabasi ya kielimu yenyewe haitofautiani lakini inakubali mwendelezo katika kuetengeneza kwake pale aliposema:

Ndugu yangu elimu haipatikani isipokuwa kwa kukamilika mambo sita, nitakueleza ufafanuzi wake kwa uwazi, ambapo ni utambuzi, shime, juhudi, gharama, na mwongozo wa mwalimu pamoja na muda mrefu.

Gharama inakusudiwa kuhusisha muda mwingi wa kutafuta elimu, na mwanafunzi awe na riziki ya kumtosha, nayo ni maana ambayo imefanywa na wakfu wa Kiislamu kwa muda mrefu, ilikuwa katika pande zake muhimu za kutumika mali za wakfu ni katika mambo ya elimu, afya na usalama wa ndani.

Mtindo huu wa kujisahau au kupuuza ni katika mitindo hatari, kwa sababu anaweza kupata elimu kidogo ya sheria isipokuwa anakuwa hajakamilisha hatua zake mpaka kufikia hatua ya kuwa ni katika waboreshaji wa Dini.

1- Hakika ulimwengu wa watu hutokea ndani yake mtu wa kuzingatia kama mtu, ambapo inapaswa kutoa umuhimu wa kumsoma kwake iwe pamoja na elimu nyingine isiyokuwa elimu ya mtu asili katika sheria ya fiqhi, yale yaliyopokelewa katika fiqhi hiyo kuhusu mtu asili ni sahihi, lakini mtu wa kuzingatiwa kama mtu anapaswa kuwa ni mwenye hukumu zingine zinazokubaliana na masilahi ya watu, na kufikiwa makusudio ya sheria, ikiwa itaondolea hukumu za mtu asili kwa mtu wa kuzingatiwa ni jambo si sahihi na ndani yake hakuna uwazi juu ya ukweli ambao tunataka kuufahamu.

Imethibiti katika fiqhi ya Kiislamu kuwa hukumu zinabadilika kwa kubadilika muda ikiwa hukumu zenyewe zimejengeka kwenye misingi ya desturi za ziada, na mila zilizo thibiti au zenye kubadilika, tofauti ya desturi hizo na mila kati ya wakati na wakati mwingine, au kutoka sehemu moja kwenda nyingine hubadilika hukumu, kama vile hukumu zinabadilika toka nchi za Kiislamu na zile zisizokuwa za Kiislamu katika masuala ya makubalino, kwa sababu Mwislamu ambaye anaishi katika nchi za Kiislamu anapaswa kuendesha maisha yake katika hali ya kawaida, na wala hapaswi kujitenga pasi na kujichanganya kwenye jamii yake, isipokuwa anapaswa kuwa ndani ya mchanganyiko huu, kwa sababu mwanzo mwisho ni mwenye kuamrishwa kulingania kwenye Uislamu kwa kauli zake au vitendo vyake au kwa hali yake.

Kama alivyosema Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W.: “Kila chepesi ni kile alichoumbiwa” wala halifikiwi hilo isipokuwa zinapotofautiana hukumu za makubaliano ambayo kati yake yeye Mwislamu na wasio kuwa Waislamu ndani ya nchi isiyokuwa ya Waislamu kwa hukumu kama hizo ndani ya nchi ya Kiislamu, na hayo ni madhehebu ya Abu Hanifa, amesema: madamu hayo ni kwa ridhaa zao, na akasema: kwa sababu nchi hii si sehemu ya kusimamisha Uislamu, nao ni mtazamo wa kweli wa maisha kwa upande mmoja, na tabia ya Dini ya Kiislamu katika ulinganiaji wake wa kigezo chema kwa upande mwingine, Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na vivyo hivyo tumekufanyeni muwe Umma wa wasitani, ili muwe mashahidi juu ya watu, na Mtume aweni shahidi juu yenu. Na hatukukifanya kibla ulichokuwa nacho ila tupate kumjua yule anaye mfuata Mtume na yule anaye geuka akarejea nyuma. Na kwa yakini hilo lilikuwa jambo gumu isipo kuwa kwa wale alio waongoa Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu hakuwa mwenye kuipoteza Imani yenu. Kwani Mwenyezi Mungu ni Mpole kwa watu na Mwenye kuwarehemu} [AL BAQARAH, 143].

Mtume katika ukweli wake ni kuwa ametumwa kama alivyoelezea yeye mwenyewe ni rehama yenye kuongoza. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:{Nasi hatukukutuma ila uwe ni Rehema kwa walimwengu wote}[AL ANBIYAA, 107].

basi ni lazima wafuasi wake wawe hivyo.

1-Ulimwengu wa matukio na ujumbe wa Kidini lazima awe ni mwenye kujifunza uchambuzi wa madhumuni na namna ya matumizi ya uchambuzi huu, imepokelewa kwenye Hadithi ya Mtume kuhusu hukumu ya watu wa Nabii Daud: “Mwenye akili anatakiwa kuwa ni mjuzi wa zama zake, mwenye kuushika ulimi wake, mwenye kupokea mambo yake” ([2])

Na ulimwengu wa matukio ukweli umepandana na vitu watu matukio na mahusiano ya ana kwa ana, nao ni ulimwengu wenye mwingiliano mkubwa na wa haraka, mpaka tunaona mawakala wakubwa wa habari wanarusha kila siku milioni 120 habari nyingi ya hizo ni matukio, ambapo yanaonesha juu ya umuhimu wa upande huu, na sisi hapa tunawazindua tu, tunazungumzia kuhusu na wala sio undani wake.

2-Ulimwengu wa fikra, huenda tukatenga sehemu yake ya kuzungumzia inayojitegemea, kutokana na umuhimu wake, na kwa kuzingatia ni msingi wa maadili mengi na utekelezaji wake.

Ufahamu wa ulimwengu huu hautoshi peke yake pasi na kuwa na elimu ya Kidini ya kufahamu mahusiano ya ana kwa ana na maandalizi ya kuingiliana kwake pamoja na kuweka njia sahihi ambazo zinafikisha kwenye makusudio ya sheria takatifu, ikiwa ni pamoja na kuhifadhi nafsi, akili, Dini, heshima ya mwanadamu na kulinda milki za watu, hayo ndiyo makusudio makuu ya sheria ambazo zimeashiriwa na watu wa asili katika Dini, na ambazo amezielezea kwa namna ya pekee Imam Al-Shatiby ndani ya kitabu chake “Al-Muwafiqat) nazo pia zinachukuwa nafasi ya nadhari ya kukaribiana na nadharia ya mfumo mkuu katika mifumo wa kanuni za sasa.

Na katika jumla ya yale tuliyoyataja yanatuweka wazi juu ya umuhimu wa mfumo wa kimaarifa, ni sawa sawa kwa upande wa mtazamo wa jumla au mfumo wa Mungu au misingi mikuu au misingi ya Qur`ani au kufahamu ukweli kupitia hayo yote pamoja na kuhifadhi urithi ambao umekuwa ndio ukweli kwa Waislamu.

Namwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi ya woye

Chanzo ni: kitabu Simat Al-Asr, cha Mufti wa Misri Dkt. Ali Juma

 

 

 


([1])Imetokana na Imam Tirmidhy ndani ya kitabu cha “Al-bir wa Al-Swilat” kwenye mlango wa “yale yaliyokuja katika utukufu wa Muumini” Hadithi ya (2032), na pia Ibn Maja ndani ya kitabu cha “Al-fitan” kwenye mlango wa “utukufu wa damu ya Muumini na mali yake” Hadithi ya (3932) katika Hadithi ya Ibn Umar R.A. na tamko la Ibn Maja.

([2])Imepokelewa na Imam Al-Baihaqi katika kitabu cha “Vipengele vya Imani” (268/4) namba (5047) na Hinad katika kitabu “Al-Zuhd” (580/2) namba (1226) na Maamar Ibn Rashid katika kitabu cha“Jamiya” (22/11)

 

Share this:

Related Fatwas