Kuisoma Surat Yasin Baada ya Swala...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kuisoma Surat Yasin Baada ya Swala ya Al Fajiri

Question

Ninataka kujua ni ipi hukumu ya kisheria ya kuisoma Surat Yasin baada ya swala ya Al Fajiri ndani ya msikiti wa Imamu Al Hussein R.A. kila siku pamoja na kundi la watu wanaompenda? 

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu. Sifa zote njema ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Yamekuja katika Sunna tukufu ya Mtume S.A.W, maneno ya kusisitizia kumtaja kwa wingi Mwenyezi Mungu Mtukufu baada ya swala ya Al Fajiri, na miongoni mwa hayo ni yale yaliyopokelewa na Imamu At Tirmidhi katika kitabu chake cha: [Aj Jami.] kutoka katika Hadithi ya Anas Bin Malik R.A, amesema: Mtume S.A.W. anasema: "Atakayeswali swala ya Al Fajiri katika Jamaa, kisha akakaa na kumtaja Mwenyezi Mungu Mtukufu mpaka jua likachomoza, kisha akaswali rakaa mbili, basi ana ujira kama wa mtu aliyekwenda Hija na Umra, kiukamilifu, kiukamilifu, kiukamilifu."
Na katika dhikri iliyo tukufu zaidi ni kuisoma Qur`ani Tukufu. Na limepokelewa agizo la kisheria la kuisoma Qur`ani kila wakati, na amrisho lolote lisilo na mipaka huhukumiwa kuwa linabeba maana ya muda wowote, sehemu yeyote, watu wowote na makundi yeyote, na kwamba kulitii agizo hilo kunafanyika kwa mtu akiwa peke yake au watu wengi, kuisoma Qur`ani, iwe kwa siri au kwa uwazi. Na wala haijuzu kwenda kinyume na maumbile isipokuwa kwa dalili ya wazi.
Na pia imekuja katika sheria ufadhilishaji wa Surat Yasin na thawabu nyingi za kuisoma sura hii, katika maelezo yaliyotolewa na Ad Darmiy, At Tirmidhiy na Al Baihaiqiy katika kitabu cha: [Shua'b Al Iman] kutoka katika Hadithi ya Anas Bin Malik R.A. kutoka kwa Mtume S.A.W, anasema: "Hakika kila kitu kina moyo wake, na moyo wa Qur`ani ni Yasin. Na atakayeisoma Yasini basi Mwenyezi Mungu Mtukufu atamwandikia kwa kuisoma kwake thawabu ambazo ni sawa na kuisoma Qur`ani yote mara kumi".
Na Atwabaraniy na Ibn Marduweh wameipokea Hadithi ya Anas R.A: "Na anatakayedumisha usomaji wa Surat Yasin kila siku usiku kisha akafariki, atakuwa amekufa hali ya kuwa ni shahidi."
Na kutokana na maelezo hayo yaliyotangulia katika hali ya swali hilo: Basi hakuna kizuizi chochote cha kuisoma Surat Yasin baada ya Swala ya Alfajiri. Na wala si vibaya kuzoea kufanya hivyo. Lakini kuisoma kwa sauti katika swala ya Jamaa kunashurutishwa kuwe kwa wanaoswalia msikitini, kwa ajili ya utaratibu wa kulitembelea eneo hili tukufu; Na kwa kuwa na adabu kwa kuwepo kwake katika eneo la Imamu Hussein Amani iwe juu yake, yatimie hayo kwa njia isiyokuwa na ushawishi wowote ndani yake kwa wenye kufanya dhikri na kusoma kitabu cha Mwenyezi Mungu Mtukufu ndani ya Msikiti huo; kwa kufuata mwongozo wa maadili ya Mtume Mkarimu, katika kauli ya yake S.A.W, aliposema: "Wala msipigiane kelele nyinyi kwa nyinyi kwa Qur`ani". Imepokelewa na Imamu Malik katika kitabu cha: [Al Muwatwa'], na Imamu Ahmad katika kitabu cha: [Al Musnad].
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi ya wote

 

 

Share this:

Related Fatwas