Kutokukubaliana Kifiqhi, na Udhibit...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kutokukubaliana Kifiqhi, na Udhibiti wa Ukanushaji wa Masuala Tata.

Question

Je, kila suala ambalo wanavyuoni wa Fiqhi hawakukubaliana baina yao, hali ya kutokukubaliana kwao inazingatiwa na wala haijuzu kukanushwa kwa aliyepinga maoni yaliyo sahihi zaidi kuliko mengine katika suala hilo? 

Answer

 Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehema na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Ikhtilaaf (kutokukubaliana) katika lugha: Maana yake ni kinyume cha Itifaq (kukubaliana), [Al-Muhkam Ibn Saidah 5/200, kidahizo cha: Khalafa, Darul kutub Al-Ilmiyah, Al-Misbah Al-Muniir uk. 179, kidahizo cha: Khalafa, Al-Maktabah Al-Ilmiyah].
Neno la Khilaaf (kinyume) na neno Ikhtilaaf (kutokukubaliana) maana yake ni moja, linapotumika katika lugha au katika istilahi, na huwa inajitokeza hali hiyo katika maneno ya baadhi ya wanavyuoni na wataalamu wa lugha na wataalamu wa Fiqhi. Wakati mwingine wao hutumia maneno mawili haya kwa maana moja. Kila mambo mawili moja wapo likipingana na lingine, basi huwa yametofautiana sana. Kutokana na hivyo, maneno ya wanavyuoni kutoka katika madhehebu ya Hanafi katika [Al-Fataawa Al-Hindiyah 3/312, Dar Al-Fikr]: “Kama wanavyuoni waliotangulia wakitofautiana kwa maoni mawili, kisha wanavyuoni waliokuja baada yao wamekubaliana kuhusu oni moja la kauli hizi. Je, makubaliano haya yanaondoa mzozo uliotangulia?”
Waliyoyaelezea mwanzoni kwa kutokukubaliana ni yale yale waliyoyaelezea katika mara ya pili kwa kupinga, kwa hivyo haya yote ni jambo moja.
Katika “Ad-Durr Al-Mukhtar kwa Al-Hasfakiy: “Asili ni kwamba mahakama yanaruhusiwa katika hali ya kutokukubaliana siyo katika hali ya upinzani, na tofauti kati yao ni kwamba hali ya kwanza ina dalili na ya pili haina dalili, Ibn Abdin alisema kuwa: “(Kauli yake: na tofauti ni) huu ni ubaguzi wa kimila kama Alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na wala hawakukhitalifiana ila wale walio pewa Kitabu hicho} [AL BAQARAH 213] Vile vile Mwenyezi Mungu Mtukufu Anasema: {Wala hawakufarikiana walio pewa Kitabu ila baada ya kuwajia hiyo bayana} [AL BAYINAH: 4] hakuna dalili kwao, na maana ya hivyo ni: Mzozo ambao hauna dalili kwa mujibu wa mkosaji, au mwenye kusema alipitisha dalili” [Hashiatu Ibn Abidin Ala Ad-Durr Al-Mukhtar 5/403, Dar Al-Fikr].
Na miongoni mwa wanavyuonini waliotofautisha kati ya maneno mawili haya ni, Abul Baqaa aliyesema katika kitabu cha Al-Kulliyaat: kutokukubaliana: Ni kama njia ambayo ni tofauti lakini makusudio ni moja. Mzozo ni kwamba njia na makusudi ni tofauti. Kutokukubaliana: Ni hali ya kutegemea dalili, lakini mzozo hali yake haina dalili ... kutokukubaliana kunatokana na athari ya rehema na mzozo unatokana na athari ya uzushi. Kama Kiongozi akihukumu kwa upinzani na hukumu hiyo ikapelekwa kwa mwingine inaruhusiwa kuifuta kinyume na kutokukubaliana, basi mzozo ni ule uliotokea katika nafasi ambayo hairuhusiwi kuwa na jitihada, ambayo ni kinyume na Qur`ani na Sunnah na makubaliano ya Wanachuoni” [Al-Kulliyaat, Abu Lbaqaa Al-Kufwi, uk.61, Muasasatu Rresalah].
Ar-Raghib Al-Aswfahaniy anasema: “Al-Ikhtilaaf (kutokukubaliana) na Al-Mukhalafah (Ukiukaji) ni: Kwamba kila moja inachukua njia nyingine katika hali yake au kauli yake. Ama mzozo ni: Ni neno la kiujumla zaidi kuliko kutokukubaliana, kwa sababu maneno ambayo ni kinyume ni tofauti na siyo maneno ambayo ni tofauti ni kinyume” [Al-Mufradaat fi Gharib Al-Qurani, Raghib Al-Aswfahani uk.294, Darul kalam].
Al-Tahanawi ni mmoja miongoni mwa waliotaja tofauti kati ya maneno haya mawili katika istilahi, alisema: “Baadhi ya Wanavyuoni walisema kuwa: kutokukubaliana kunatumika kwa maneno yanayotegemea dalili, na tofauti haina dalili kwayo ... na inasisitiza hivyo kuwa rai isiyochaguliwa inaitwa ni tofauti siyo kutokukubaliana” [Kashaaf Istilahat Al-Funuun kwa Al-Tahanawiy 1/116, Maktabat Lebanoni].
Mzozo ni miongoni mwa mambo ya ulimwengu, bado kuna kukhitalifiana kati ya wanadamu tangu enzi za Nuhu (A.S) hakuna hata Umma moja ambao haitokei tofauti kati yao, Mwenyezi Mungu alimema:
“Na Mola wako Mlezi angelipenda angewafanya watu wote wakawa umma mmoja. Lakini hawaachi kukhitalifiana, *Isipo kuwa wale ambao Mola wako Mlezi amewarehemu; na kwa hiyo ndio Mwenyezi Mungu amewaumba.”[HUUD: 118-119].
At-Tahar Ibn Ashour anasema katika kitabu cha: [At-Tahrir wat-Tanwiir 12/190, Ad-Dar At-Tunisiah, 1984]: “Alipowaumba kwa maumbile yanayowalazimishakuwa tofauti katika maoni yao na mielekeo yao, na alikuwa akiyataka yanayotakiwa na maumbile hayo na alikuwa mjuzi kwayo, basi tofauti ilikuwa ni sababu iliyolengwa kwa kuwaumba”. Miongoni mwa yaliyoandikwa na Mwenyezi Mungu juu ya Umma wa Kiislamu ni kwamba utakhitalifiana kama watu waliotangulia walivyokhitalifiana. Imepokelewa kutoka kwa Abu Dawud na At-Tirmidhi na Al-Hakim, Kutoka kwa Abu Hurairah, R.A. kuwa Mtume, S.A.W., amesema: "Mayahudi walitawanyika makundi sabini na moja au sabini na mbili, na Manasara walitawanyika kama hivyo hivyo, na Umma wangu uligawanywa katika kundi sabini na tatu".
Asili ya mzozo katika masuala ya kifiqhi ni hamu ya kufikia haki na wajibu, basi haki ni lengo la muumini analolitaka, Mwenyezi Mungu Mtukufu Anasema: {Na kipo kitu gani baada ya haki, isipokuwa upotovu tu?} [YUNUS: 32].
Al-Hajwi anasema katika [Al-Fikr As-samiy] akieleza hali ya Fiqhi ya Kiislamu katika karne ya pili: “Yanayotokana na kutofautiana na kuamini kuwa mpinzani wake ni mkosaji katika suala fulani kwa mujibu wa dalili inayosisitiza makosa yake kufuatana na dhana yake, si katika masuala yote, na inaaminika kuwa na udhuru kwa mujibu wa dalili yake, na wanafahamu kuwa kila mwanachuoni ana haki ya, kuheshimiwa mawazo yake, hivyo, tofauti haina madhara kwao, lakini tofauti ilikuwa kwa ajili ya kufikia haki, kwa hivyo, Fiqhi ilikuwa na nguvu mno” [Al-Fikr As-samifi Tariikh Al-Fiqhi Al-Islamiy 1/525, Darul Kutub Al-Ilmiyyah].
Haki ilitambuliwa kutokana na ujumla wa dalili, na kutokana na hivyo tofauti yenyewe haikuwa lengo pekee yake, lakini kila mmoja anatafuta haki kwa njia zake. Tofauti inatokea kwa sababu yeyote, ambapo hukumu za kifiqhi ni za kudumu kufuatana na dalili za kidhana, na dhana zote zinakubali upinzani, na wakati mwanazuoni wa fiqhi alipolazimika kufuata aliyoyadhani ni lazima kuwepo kutokukubaliana kwa mujibu wa dalili ya dhana hiyo.
Tunapaswa kuamua kuwa tofauti inafungika katika matawi ya kifiqhi na baadhi ya masuala yanayohusiana na vyanzo vya dini, pamoja na makubaliano kamili juu ya vyanzo vya dini ambavyo vinawakilisha utambulisho wa Uislamu, ambayo ni miongoni mwa utunzaji wa Mwenyezi Mungu Mtukufu na udhamini wake kwa dini hii mpaka Mwenyezi Mungu atakapo irithi dunia na wote waliopo ndani yake. Kwa hiyo haikutokea kutokukubaliana katika mambo ya yakini, ambapo kukubaliana katika mambo ya yakini ni muhimu, na kwamba tofauti katika matawi ni nafasi pana, hakuna umma uliobanwa na madhehebu fulani, kama ni madhehebu moja ni ngumu kwa umma unaelekea madhehebu nyingine. Sheikh Mahmoud Shaltout anasema katika kitabu chake: [Al-Islamu Akida wa Sharia uk. 550, Daru Ash-Shuruq]: “Kusisitizia haki ya jitihada ya kibinafsi na ya kipamoja kunafungua milango mipana ya utafiti kwa wanavyuoni wa Sheria ya Kiislamu, ili kuchagua Sheria ambayo inasimamia mambo ya jamii ya Kiislamu kufutana na tofauti ya hali yake, wana uhuru wakati wanapochagua ila jambo moja tu ambalo ni kutopinga kwa vyanzo vya Sheria vinavyothibitika pamoja na kuchungua njia za maslahi na haki, na huo ulikuwa msingi wa kudumu wa Sheria ya Kiislamu na kufaa kwake katika kila wakati na kila mahali” .
Na Zaidi ya haya wanavyuoni walichunga kwamba isiwe kutokukubaliana kwao ni alama ya matamanio na ukaidi, na kwamba kupitishwa kwa wazo la upanuzi wa kuwepo maoni mengi na jitihada kwa Maimamu waliotangulia na wa hivi sasa, ni kitu kisicho hitaji dalili na ushahidi, kwa kuwa hali zao zinajieleza zaidi kuliko kauli zao. Miongoni mwa hayo ni jambo lililofanyika kwa Imam Omar Ibn Abdul Aziz kuhusu kuunganisha madhehebu na kuwalazimisha watu kufuata jitihada moja tu. Imepokewa kutoka kwa Hamid At-Tawiil alimwambia Omar Ibn Abdul Aziz kuwa: Lau ungewaunganisha watu pamoja kwenye kitu Fulani. Akasema: Kinacho nifurahisha ni kwamba hawakuwa na tofauti. Kisha akawaandikia Maimamu katika nchi zote:“Mhukumu kwa watu wote kwa mujibu wa yale yaliyokubaliwa na wanavyuoni wao wa Fiqhi.”Imepokelewa kutoka kwa Ad-Darami katika Sunan yake. Pia imepokelewa kutoka kwa Wanavyuoni waliotangulia na wa hivi sasa kuwa mwenye kumhimiza Mwislamu kuacha madhehebu yake au maoni yake juu ya suala fulani, kama kuna maslahi, basi jambo hili lina faida kubwa kwake na kwa Waislamu wengine. Miongoni mwa hayo ni yale yaliyokuja katika Majmuu Al-Fatawa kwa Ibn Taimiah katika maneno yake kuhusu Bismillah, je, Bismillah ni aya mwanzoni mwa kila sura au sio? Je, Imamu anaruhusiwa kupaza sauti kwake au la? Baada ya kutaja maoni yote katika suala hilo, alisema: “Inapendekezwa (Mustahabu) kwa mtu kuwa na nia ya kuiunganisha mioyo kwa kuacha mambo yaliyopendekezwa, kwa sababu maslahi ya kuunganisha mioyo katika dini ni bora zaidi ya maslahi ya kufanya vile” (Majmuu Al-Fatawa 22/407, Mujama Al-Malikiy Fahd ya Uchapishaji wa Qur`ani Tukufu).
Wanavyuoni waliweka udhibiti kwa ajili ya tofauti iliyozingatiwa, na wanavyuoni wengi walitilia maanani kutaja dhibiti hizi, na wengine walitilia maanani kusimamia sababu za tofauti zao, baadhi yao wamezifanya kuwa sababu sita kama vile Ibn Rushd Al-Malikiy katika utangulizi wa kitabu chake: [Bidayatul Mujtahid], na baadhi yao wamezifanya kuwa sababu nane kama vile Abu Mohammed Al-Batliossi Al-Andalusi Al-Maliki katika kitabu chake: [Al-Tanbiih ala Al-Asbab allati Awjabt Al-Ikhtilaf baina Al-Muslimin], na miongoni mwao wamefikia sababu kumi na sita kama vile Ibn Juziy katika kitabu chake: [Taqriib Al-Wusuul Ila Ilm Al-Ussul], na sababu hizi hazikusababisha mgogoro kati ya pande zake, au kurithi ushabiki wa kiitikadi ambao unasababisha tofauti. Hali hii ni moja ya maumbo ya ujinga katika Sharia na misingi yake.Vile vile ni ujinga kwa kulingana na historia ya Maimamu na maneno yao, na tofauti yao pia haikuwaelekeza mbali na adabu katika kugusia masuala haya ya utata. Kwa upande wa vitendo, tumesikia kuhusu mijadala mingi iliyojaa adabu ya kupinga kupitia vitabu vya historia na wasifu, pamoja na misingi iliyowekwa na wanavyuoni katika kushughulikia hali ya upinzani na adabu ya mkiukaji, na kwa kuzingatia upinzani huu, kuruhusiwa kwa kufuata madhehebu nyingine, na mabadiliko kutoka madhehebu mpaka madhehebu nyingine.
Miongoni mwa misingi hii: Kutokanusha katika masuala yanayojadiliwa, na maana yake ni kwamba analaumiwa mtu mwingine, au kumkataza kufanya kazi kwa maoni yake, kwa sababu ni kinyume na kile anachoona, au kauli yake inahusiana na mwenye kukataa na kutumia njia tatu za kukataa zilizoelezwa katika Hadithi -mkono, au ulimi au moyo- njia ya kubadili, au kukataa kazi ambayo inakubalika na maoni yenye jitihada juu ya masuala hayo ya utata.
Mwenye kukataa ni kinyume na mwenye kujua, na kila kibaya kinachokatazwa na Sheria ndicho kinachokataliwa. [Lisan Al-Arab kwa Ibn Mandhur 5/233 kidahizo cha Nakara, Dar Sadir] kukataa kinyume na kukiri, na miongoni mwa maana zake ni kukanusha na kujinga [Tahdhiibu lugha kwa Al-Azahari 10/109, kidahizo cha: Nakara, Dar Ihyaa At-Turath,Tajul Aros 14/287, Darul Hidayah, na Al-Misbahul Muniir kwa Al-Faiyumiuk. 625, kidahizo cha: Nakara].
Mwenye kufuatilia maana za kukataa katika matumizi ya wanavyuoni anakuta kwamba kitenzi hicho kina maana mbili, nazo ni: mabadiliko na kukataza, basi kukataa kulitajwa katika maneno ya wanavyuoni kwa maana mbalimbali na inawezekana kurejesha maana zile mbili. Miongoni mwa maana zile ni pingamizi, kuzuia, na taarifa ya udhaifu wa kusema, ukosefu wa utambuzi kwa kusema au kwa kitendo, kasoro ya mkosaji, kulauma, unyanyasaji, kuhubiri, kuomba, kutakaza, na adhabu. Na maana hizi zina maana tofauti na sura tofauti pamoja na maana ya mabadiliko au kukataza.
Ni wazi kutokana na maana ambazo tumezitaja kwamba tunamaanisha kwa kutokataa kazi yeyote, si kusema kwa hukumu, migogoro ni katika kazi maalumu, kwa hivyo mijadala ya kisayansi kati ya wanavyuoni inajitokeza kama tunavyoona. Kwa hivyo basi mijadala ni kukataa hukumu, pamoja na kujua kwa wanaojadiliana kwamba kila mmoja wao hakatai kazi kwa yanayosemwa na upande mwingine.
Tulitaja kwamba madhehebu ya Wanavyuoni wote yanasema kuwa hakuna kukataa katika masuala tata. Rejea hivyo katika marejeo yafuatayo: [Aqd Al-Jaid fi Ahkaam Al-Ijtihaad wal Taqliid kwa Dahlawi, uk. 26, Al-Matbaah Al-Salafiyah- Kairo, Al-Frooqkwa Al-Qarafi 4/257, DarulMaarifa - Beirut, Al-Manthuur kwa Al-Zrkashi 3/364, Wizara ya Awqaf ya Kuwait, Al-Ashbah wan-Nadhair kwa Asuyuuti uk. 137, Darul Kutub Al-Ilmiyyah, Al-Fawaid Al-Janiyah kwa Al-fadani 2/333, Darul Bashair- Beirut, Al-Furuu kwa Ibn Mofleh 2/17, Alam Al-Kutub, na Kashaf Al-Qinaa kwa Al-Bahoti 1/479, Alam Al-Kutub].
Imepokelewa kutoka kwa Imam Ahmad kwamba anakanusha kitu kinachojadiliwa, Rejea: [Al-Adab Al-Shariyahkwa Ibn Mofleh 1/166, Muasasat Qurtubah].
Ibn Taimiah na Ibn Al-Qaiym walitofautisha kati ya masuala tata na masuala ya Jitihada [Al-Fatwa Al-Kubrah kwa Ibn Taimiah 6/96, Darul Kutub Al-Ilmiyah, na Iilaam Al-Muawiqiin 3/288, Darul Kutub Al-Ilmiyah].
Wakati wa kuzingatia na uchunguzi wa suala hili, tunakuta kuwa tofauti ni ya tamko, na taarifa ya hivyo ni kwamba makusudi ya masuala tata kwa Wanavyuoni wa Umma ni yale masuala yanayofichwa maana yake, kwa ajili ya kutokukubaliana juu yao, au kwa ajili ya kutokuwepo kwa dalili, kila suala ambalo halina matini inayohusiana nalo, au lina matini inayothibitika, basi suala hili ni la utata. Hii ina maana kwamba kuwepo kwa matini inayothibitika haina maana ya kuondoa utata, isipokuwa kama makubaliano yakifanyika juu ya kuainisha maana moja inayowezekana, hali ile kama kauli ya kiongozi kuhusu kuondoa kwa tofauti.
Udhibiti huu unatumika kwa baadhi ya masuala ya maneno na masuala mengi ya Kifiqhi. Hivyo, kwa sababu inajulikana kwamba wenye jitihada hawawezi kuathiriwa na tofauti katika masuala yenye matini inayothibitika, lakini tofauti yao ni bado katika masuala yasiyo na matini, na masuala yenye matini lakini isiyothibitika.
Wanavyuoni walieleza tofauti kuwa inayozingatiwa, nayo ambayo ina bahati ya kuiangalia, yaani: kutoka dalili, maana suala lisilo na dalili hailizingatiwi, au lina dalili lakini haina nguvu, kwa hiyo, wanavyuoni waliweka masharti yanayofanya tofauti yao inazingatiwa, na yanayotajwa chini ya masharti hayo yanazingatiwa, na masharti hayo ni:
La kwanza ni kuwa: Tofauti ni yenye nguvu, kama tofauti ni dhaifu basi haizingatiwi.
Al-Dardiir anasema katika [Al-Sharhul Kabiir] akizungumzia hukumu zinazoondolewa na zisizoondolewa: “Hairuhusiwi kwa Mufti kutoa fatwa kwa utata wa hukumu iliyotolewa na kiongozi, hali hii kuhusu tofauti inayozingatiwa kati ya wanavyuoni, lakini suala ambalo ni dhaifu kwa sababu limepingana na matini au imedhihirisha kipimo au makubaliano basi linaondolewa” [Al-Sharhul Kabiir 4/156, Daru Ihyaa Al-Kutub Al-Arabiyah].
As-Suyuti alielezea sharti hili akisema : “Tofauti iwe yenye nguvu ili isiwe dhaifu”kisha akatoa mfano kwa tofauti ambayo ni dhaifu akisema: "Kufunga katika safari ni bora kwa wenye nguvu. Na hakutilia maanani kauli ya Daud aliyesema kuwa: Hairuhusiwi kufunga katika safari. Imamu wa Misikiti Miwili Mitukufu (Al-Haramain) amesema katika suala hili: Wachunguzi hawazingatii tofauti katika maoni ya wenye madhehebu ya Adhahir” [Al-Ashabahu wan-Nadhairuk. 137, Rejea: Al-Muwafaqaat kwa Shatiby 4/172, Darul Marifah- Beirut].
La pili: kutosababisha kuzingatia tofauti katika maoni kuacha Sunna iliyothibitika, au kuvunjwa kwa makubaliano, basi inatokea tofauti nyingine, na mfano wake: Kutenganisha baina ya rakaa za Witri ni bora kuliko kutozitenganisha, na hakuzingatiwi maoni ya Abu Hanifa kuhusu suala hili, kwa sababu miongoni mwa wanavyuoni wapo ambao hawaruhu kusali rakaa za Witri mara moja.
La tatu: Mpingaji awe miongoni mwa wanavyuoni wanaozingatiwa, na kuhusu jambo hili Sheikh/ Mohamed Hassanein Makhlouf anasema katika kitabu chake: (Bulugh As-Suul fi Madkhal Elmul Usuul uk.15, Mustafa Al-Halabi): “Wanachuoni wa Usuul na miongoni mwa Wanavyuoni na wengine walizingatia maneno ya wenye jitihada juu ya wenye kufuata kama ni dalili za Kisheria zinazohusiana na wenye jitihada, sio kwa sababu maneno yao ni hoja kwa watu inayothibitisha hukumu za kisheria kama maneno ya Mitume (A.S) basi hakuna yeyote anayesema hivyo, lakini kwa sababu maneno yao yanategemea kasoro za Sheria, wamefanya bidii katika kuzisoma na kuzichunguza dalili zake pamoja na uadilifu wao na kuelewa kwao, kuzingatia kwa udhibiti wa Sheria na kuhifadhi matini zake, Kwa hiyo waliweka sharti kuhusu mwenye kuzalisha dalili anayefahamu hukumu za Sheria kutoka dalili zake kuwa na uwezo maalumu, nguvu maalumu, kipawa maalumu kinachomwezesha kuchunguza dalili kwa njia ya kufanya dhana zake ni kama elimu iliyothibitika kwa ajili ya kulinda hukumu za Dini mbali na makosa kama iwezekanavyo”.
Kulingana na hapo juu, tofauti katika maoni imegawanywa katika sehemu mbili:
Ya kwanza: Inaonekana wazi na inategemea dalili na misingi, pia inategemea vyanzo vya jitihada na kuelewa hukumu, hali hii ni kinyume na mambo yanayozingatiwa, hii ni maana ya maneno yao: Hapana kukanusha katika masuala tata, wanavyuoni wanaoiunga mkono sehemu hii ni wengi. Kuhusu hivyo, Al-Shatwibiy : “Tofauti inayozingatiwa ipo katika masuala mengi ya Sheria, lakini tofauti isiyozingatiwa ipo chache” [Al-Mwafaqaat 1/105], na kutokana na hivyo, kuna mengi ya masuala tata katika zama zilizopita na hivi sasa, miongoni mwao ni: Kuoa bila ya Walii, na kula kilichoachwa kutajwa jina la Mwenyezi Mungu baada ya kuchinjwa, kunyoa ndevu, na kuweka fedha katika mabenki ya kawaida, bima katika zama hizi ... nk.
Ya pili: Ni yenye ufahamu dhaifu, na mwenye kuelekea mbali na dalili, hii inarudishwa kwa mwenye kusema hivyo, sehemu hii ina majibu ya baadhi ya Maimamu juu ya baadhi yao, kukanusha kwa maneno yasiyo ya kawaida.
Wanavyuoni wa Umma waliondoa baadhi ya mambo katika kukanusha masuala tata, miongoni mwao ni: Udhaifu wa ufahamu, jambo hili limepita. Miongoni mwao pia ni: Hukumu ya kiongozi. Kama Wanavyuoni wametofautiana kuhusu uhalali na uharamu wa jambo fulani, huletwa suala hilo kwa kiongozi, lazima atoe fatwa kwa mujibu wa itikadi yake, na hukumu yake inaondoa tofauti hii. Miongoni mwao pia ni: Mwenye kukanusha awe na haki katika masuala tata. Mume ana haki ya kumzuia mkewe kunywa mvinyo mchache kama mkewe akidhani inaruhusiwa. Miongoni mwao pia ni: Kwamba anayefanya jambo la haramu anaitikadi kuwa jambo lile ni haramu tena analifanya, na hivyo kwa sababu amekiuka uharamu kwa mujibu wa itikadi yake, si kwa sababu anaitikadi kuwa ni halali.
Wanavyuoni wa Umma wametoa dalili kwamba katika masuala tata hayakanushwi kwa kuwa moja ya maoni mawili si bora zaidi kuliko ya mengine; kwa sababu masuala ya kifiqhi ni ya kidhana tu, na dhana inawezekana kupingwa, na hakuna ubora kati ya dhana na nyingine. Na kwamba kila mwenye jitihada ni mwenye kupatia, au mwenye kupatia ni mmoja ambaye hatumfahamu na wala hakuna dhambi juu ya asiyepatia, lakini kama akimshauri aache tofauti basi inapendekezwa hivyo.
Al-Jarhazi anasema katika kitabu cha: [Al-Mawahib Al-Sunniah 2/333, Darul Bashair]: “(Wakasema masuala amabayo ni utata hayakanushwi) huu ni msingi mkubwa unaotokana na tawi kubwa; kwa sababu uhusiano wake kwa yaliyoharimishwa si bora zaidi kuliko uhusiano wake kwa yaliyohalalishwa”.
Al-Fadani amesema: “(kwa sababu uhusiano wake) yaani: Ni jambo lililojadiliwa (kwa yaliyoharimishwa) yaani: Mwenye jitihada amesema juu uharamu wake kama Ash-Shafi aliyeharimisha mvinyo kwa mfano, (zaidi kuliko uhusiano wake) yaani: Ni jambo lililojadiliwa (kwa yaliyohalalishwa), yaani mwenye jitihada aliyesema kwa uhalali wake kama Abu Hanifa aliyehalalisha mvinyo, kwa mfano”.
Sheikh Zakaria Al-Answariy anasema: “(wala hakatai) Mwanachuoni (isipokuwa yaliyokubaliwa kwayo) yaani: Kuhusu kuyakataa, si yale yanayojadiliwa, au mkosaji anaona uharamu wake, kwa sababu kila mwenye jitihada ni mwenye kupatia, au mwenye kupatia ni mmoja ambaye hatumfahamu na wala hakuna dhambi juu ya mkosaji” [Asna Al-Matalib 4 / 180, Hashiat Ar-Ramli Al-Kabiir, Darul Kitab Al-Islami).
Imepokelewa kutoka kwa Imam Ahmad kwamba anakanusha jambo ambalo lina mjadala kwa mwenye kufuata na mwenye jitihada hakanushwi [Al-Adaab Al-Sharia kwa Ibn Mofleh 1/166], pengine riwaya hii inazuia yaliyotangulia, kwamba riwaya iliyotangulia– ambayo inaruhu kukanusha jambo lenye mjadala - Ibn Moflih ameiona ni kukataa kauli iliyopingana na dalili yenye nguvu au habari ya mmoja. Lakini Ibn Rajab kwa upande mwingine, alisema: “Iliyojulikana kuhusu Imam Ahmed ni kukanusha kwa anayecheza Chess, na Al-Qadhi alieleza kuwa anayecheza pasipo na jitihada au kuiga, ambapo hali hii inawezekana kujadiliwa, Iliyojulikana kuhusu Imam Ahmed ni kumwadhibu anayekunywa mvinyo aliyejadiliwa na kutekeleza adhabu ni kiwango cha juu zaidi cha kukanusha, ingawa hakuwa mpotovu kwake, hii inathibitisha kwamba Imam Ahmed anakanusha kila linalojadiliwa kwa udhaifu kwa kuonesha Sunna juu ya uharamu, wala mwenye kutenda uharamu huo hatoki mbali na uadilifu” [JamiiAl-Uluum wal Hikam uk. 325, Darul Kitabul Islami].
Ama kuhusu kutofautisha kati ya Ibn Taimiah, Ibn Al-Qaim, Al-Shawkaani na waliowaunga mkono katika masuala tata na masuala ya jitihada, Ibn Taimiah anasema katika kitabu cha: [Al-Fataawa Al-Kubra 6/96]: “Kauli yao kwamba masuala tata hayana kukanusha mtazamo huu si sahihi, ukanushaji unaelekeza kauli kwenye hukumu au kwenye kazi, ya kwanza -nayo ni kauli kwenye hukumu-, kama kauli ni kinyume na Sunna au makubaliano ya zamani ni lazima kuikanusha kwa muwafaka, kama si hivyo,basi inakanushwa hali ya kuonesha udhaifu wake kwa anayesema kuwa mwenye kupatia ni mmoja tu, nao ni wanavyuoni wa Fiqhi na wanavyuoni waliotangulia. Ama kuhusu kazi: Kama ikiwa kinyume na Sunna au makubaliano ni lazima kuikanusha kwa mujibu wa viwango vya ukanushaji. Vile vile hukumu ya kiongozi inabatilishwa kama ikiwa kinyume na Sunna, hata kama ikifuata baadhi ya wanavyuoni. Na kama hakuna katika suala fulani Sunna wala hakuna makubaliano, lakini kuna jitihada, basi atakayefuata rai ya jitihada hakanushiwi. Utata huu uliingia upande mmoja, nao ni mwenye kusema hivi anaaminika kuwa masuala tata ni masuala yanategemea jitihada kama walivyodhani jamii ya watu, na haki ambayo Maimamu wanaisisitizia ni kwamba masuala yanayotegemea jitihada hayana dalili ambayo ni lazima kuifuata, kama vile Hadithi Sahihi ambayo haina upinzani kutokana na jinsi yake, basi inaruhusiwa kuifuata, lakini kama kuna Hadithi nyingine kinyume na ile inaruhusiwa kufuata jitihada kwa sababu kuna dalili zinafanana au kwa sababu ya kuficha dalili. Kama ikitajwa kwamba suala hili limethibitika, basi hakuna tuhuma kwa wapinzani miongoni mwa wenye jitihada kama masuala mengine yote ambayo wanavyuoni waliotangulia walitofautiana, ingawa tumehakikisha kuhusu usahihi wa mtazamo mmoja miongoni mwa mitazamo miwili”. Ibn Al-Qayyim pia alisema kama yaliyotangulia hapo juu, pia alisema katika kitabu cha: [Ilaam Al-Mwaqiin 3/288]: Wakati alipotoa dalili ili kuthibitisha kauli yake: “Namna gani mwanachuoni wa Fiqhi anasema kuwa hairuhusiwi kuyakanusha masuala tata, pindi Wanavyuoni wa Fiqhi wamesema kuwa inaruhusiwa kuibatilisha hukumu ya kiongozi kama ikiwa kinyume na Qur`ani au Sunna”.
Sababu ya tofauti baina ya Ibn Taimiah na Ibn Al-Qaim katika masuala tata na masula yanyaotegemea jitihada ni kwamba masuala yanayotegemea jitihada hayana matini katika Qur`ani au katika Sunna au hata makubaliano, lakini masuala tata ni kinyume na hayo, na kwamba yeye anamkana mkiukaji katika hali ya pili, bila ya kumkana katika hali ya kwanza. Kwa maneno mengine: masuala yanayotegemea jitihada ni yale tata na yanahitaji kuyatilia maanani.
Hayo Makundi mawili yanakubaliana kwamba masuala ambayo yana matini au makubaliano – yakinifu – basi huwa anakanushwa mkiukaji ambapo makundi yote mawili yanayayaita masuala haya kuwa ni tata, lakini masuala yanayojadiliwa na hayana dalili inayoyathibitisha, basi makundi haya mawili yameafikiana kuwa hakuna kukana mkiukaji, ingawa Wanavyuoni wa Umma wanayaita masuala haya kuwa ni tata kama yale ya kwanza. Na Ibn Taimiah pamoja na Ibn Al-Qaim wanayaita hayo kama masuala yanayotegemea jitihada, na istilahi zote ni sahihi. Ni kweli kwamba masuala haya ni tata kwa sababu sio ya kutokukubaliana nayo, vile vile ni masuala yanayotegemea jitihada kwa sababu jitihada inaruhusiwa ndani yake.
Zaidi ya hayo, kila suala tata, kwa kweli, ni suala linalotegemea jitihada za wanazuoni kwa sharti kuwa utata huo uwe unazingatiwa kama iliyotangulia kuelezwa hapo juu. Lakini kama utata haukuzingatiwa, basi suala hilo halitegemei jitihada. Ukweli ni kwamba suala hilo ni tata, na utata huo hauzingatiwi, na kama ipo tofauti basi ni kati ya masuala ya Ijtihadi na masuala tata ambao hauzingatiwi.
Kwa hivyo maneno ya Ibn Taimiah yaliyotangulia hapo juu: “…kama si hivyo, basi inakanushwa hali ya kuonesha udhaifu wake kwa anayesema kuwa mwenye kupatia ni mmoja tu, nao ni wanavyuoni wa Fiqhi na wanavyuoni waliotangulia” kauli hii ni mbali na mgogoro, lakini mgogoro ni katika kazi tu kama ilivyoelezwa hapo juu.
Kwa mujibu wa maelezo yaliyotangulia hapo juu; Masuala utata ambayo kwayo hakanushwi mkiukaji pia hayakusanyi mambo yote ambayo yalipelekea mzozo, kwa sababu hayo ni masuala ambayo ufahamu wake ni dhaifu, au yasiyo ya kawaida, au miongoni mwa makosa ya wanavyuoni, na kama ni hivyo basi yatarejewa. Lakini kama masuala haya yanayokusudiwa ni yale ya utata, na utata wake unazingatiwa kwa masharti yake yenyewe, basi hakuna kukana katika masuala hayo.
Na Mweyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.

Share this:

Related Fatwas