Mwanadamu na Ulimwengu Katika Uisi...

Egypt's Dar Al-Ifta

Mwanadamu na Ulimwengu Katika Uisilamu.

Question

Kuna uhusiano gani kati ya mwanadamu na ulimwegu katika uisilamu? 

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehema na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
1) Mwanzo kabisa tunakubaliana kabisa na marehemu profesa Abu Wafaa Al-Ghanimiy At-Taftazaniy ambaye ni mmoja wa wasomi wakubwa wa elimu ya falsafa ya kisasa ya kiislamu – ya kuwa, mwenye kuzingatia maendeleo ya kisayansi ya ulimwengu kwa upande wa gunduzi mpya ambazo hazikuwa zikijulikana itaonekana kuwa wale wenye kuchochea hisia wanawasisitiza watu umuhimu wa kuangalia kwa kina utamaduni wa dini kuwa hauna nafasi tena kwa wakati wetu huu, na jambo hili limepelekea kuwepo kwa hali ya kutokuwafikiana – migongano – ambayo haina ulazima kati ya maadili ya urithi wa utamaduni wa kidini na ustaarabu wa kisasa, pamoja na maadili mapya mageni ambayo yanasisitizwa na hao wasomi wenye kujishughulisha na mambo ya kimwili (kiroho). Mfano wa migongano hiyo ni ule unaojitokeza wa kutofahamu kwao namna ulivyo uislamu na kule kushikamana kwake pasina kuzingatia falsafa ya kisasa ya kimwili (kiroho). Kupiga hatua za kimaendeleo ya kisayansi sio sharti ya kunasibishwa na kutoamini Mwenyezi Mungu, na kutoamini Mungu pia si dalili ya kupatikana uwezo wa kuelewa dhana ya sayansi.
2) Na kwa kweli hali kama hii ya migogoro ya kimawazo ndio inayomfanya mtu ahisi – sawa katika ulimwengu wa Kimagharibi au ulimwengu wa Kiislamu – kuwa ana haja kubwa ya kufahamu utamaduni wa zama zake pamoja na tafauti iliyopo pamoja na kujua lipi linaloenda sambamba na urithi wa utamaduni wa dini na ustaarabu (mpya) ambao umekuja ili mtu asije akapoteza uhalisia wake. Na hasa kwa muislamu ambaye anahisi kuwa anashikamana na urithi wa utamaduni wa ustaarabu wa asili ambao ni sababu kubwa ya kuwepo kwa maendeleo ya mwanadamu, ingawa kwa baadhi ya wakati alikuwa yupo mbali na maendeleo hayo lakini ana uwezo bado wa kuendelea mbele na kuwafikia waliomtangulia katika ustaarabu na maendeleo.
3) Na kwa kuwa muislamu wa kweli hataki kuwafikia waliomtangulia kimaendeleo na ustaarabu kwa kufuata tu lakini ni wajibu wake kuhifadhi mawazo yake huru pamoja na ustaarabu wake, na kwa namna hii huwa hakuna tatizo. Na awe na utambuzi wa mawazo na fikira za wasomi wa madhehebu mengine ya kisasa. Na pia aweze kupambanua kati ya zuri na baya na kukuza uwezo wake wa kujiendeleza. na si lazima kwa kila jambo zuri linalokuja kutoka katika jamii nyingine za mashariki na magharibi huwa ni zuri pia katika jamii nyingine na kuweza kutimiza matakwa ya kifikira na kiroho (katika jamii hizo) na kuweza kufanikisha maendeleo ya kweli na sio ya kubuni (kufikirika).
4) Na miongoni mwa fikira ambazo zimeanzishwa na jamii nyingine ni uwepo wa falsafa tafauti, zipo zenye kuamini ufasiri wa uwepo wa roho, kwao wao ni kuwa kiwiliwili ndicho chenye kuendesha kila kitu ama akili ya mwanadamu si chochote isipokuwa ni matokeo ya uwepo wa kiwiliwili hicho, na ulimwengu haukuwepo isipokuwa kwa kuzuka tu, hakuna kiumbe wala muumbaji. Na miogoni mwa falsafa ngeni ni zile zenye kutaka kuamini majaribio ya kisayansi kwa kufanya kuwa kigezo pekee kinachotambulika kama ni ushahidi ni hisia tu, na kwa ajili hiyo mawazo ya kibinaadamu hayana nafasi ambayo yanajaribu kufikiri zaidi ya uwepo wa ulimwengu na vilivyo fichika.
5) Na matokeo ya falsafa nyengine za kisasa zinajieleza kuwa maisha ya mwanadamu hayana maana yeyote na wala hayana lengo, na wengine wanaamini kuwa uwepo wa mwanadamu ni balaa tupu, na wengine wanaamini kuwa mwanadamu anatakiwa awe huru kabisa (afanye atakavyo), na wengine hawaamini kabisa maadili ya aina yeyote au uhalisi wa uwepo wake wakisisitiza kuwa falsafa yao imeshikamana na vitu vya mpito. na aina zote hizo za falsafa ni za kipuuzi kabisa na zisizo na mwelekeo. Na katika yenye kusikitisha ni kuwa imeenea sana (falsafa hii) katika uandishi wa vitabu vya kisanaa na katika maonyesho ya kisasa katika nchi za Ulaya, na falsafa hii ina uwezo wa kufuta yale yote yaliyozalishwa na tamaduni zilizotangulia kwani hufisha kabisa matumaini ya mwanadamu na kumfanya asijue ni lengo gani analolitafuta (maishani).
6) Kupitia falsafa hii na mkondo huu wa fikira mpya watu katika jamii yetu wamegawanyika katika makundi matatu:- Wapo wanaofuata, kuigiza na kufurahishwa na kila jambo geni na jipya bila ya kuchunguza kwa kina au kufikiria kwa fikira huru. Na wapo wasiojali kupima kati ya mambo mageni na mambo mapya na wakawa wanaendelea pasina kutafautisha madhara yake. Na wapo wanaohuisha matatizo haya kisha baadae wakawa wanapata matatizo ya kweli wakawa wanatafuta majibu –tiba- (na kuikosa) na kusababisha fikira zao kutoondoka katika akili za wengine.
7) Na kutokana na kuwepo kwa msuguano endelevu kati ya uislamu na mielekeo ya kimawazo ya kisasa kama ya Ki Marxi, na wenye kuamini uwepo wa mantiki ya wanaofuata madhehebu ya (wadhi iyya), na wenye kuamini kila kitu kuwa kipo pasina mwekaji na wengineo, wakati ndio utakaobainisha kuwa fikira ya kiislamu ya kisasa ndio iliyo wazi zaidi ya fikira zote, bila ya kupoteza uasilia wake na kushikamana kwake na ustaarabu. Na kuwa (uislamu) unazingatia misingi ya kuwa sayansi haipingani na imani ya uislamu, na uislamu pekee ndio dini yenye kutumia maarifa (akili), na sayansi ndio inatuongoza kuujua ulimwengu na wakati huohuo kumjua Mwenyezi Mungu kitu ambacho hakipingani.
8) Suala liulizwalo kuhusu mwanadamu na ulimwengu katika uislamu, tunaweza kulielezea kupitia njia tatu:
A; Sayansi kama tuionavyo hivi sasa inaweka wazi (inafichua) siri za ulimwengu ambazo hazikuwa zimewapitia akilini mwa waliotangulia, na ubora unarejea katika mitaala waliyoianzisha na kujilazimisha nayo. Na je uislamu unakubali sayansi kimitaala na kiimani na kukubalika huko kunatizamwa kwa namna gani?
B - Iwapo sayansi mpya imetusaidia kufikia matokeo ya kuwa na picha maalumu ya ulimwengu huu na kama uwezo wa mwanadamu umesaidia kuwepesisha nguvu za maumbile (ya tabianchi), basi ni kwa kiasi gani picha hii inakubaliana pamoja na picha iliyochoreka kipindi cha kuanza kwa uislamu, kama ilivyoelezwa katika Kurani?
CNa iwapo sayansi inakwenda sambamba kama tuonavyo na imani kubwa ya kiroho, sasa kuna upeo gani wa kiroho kwa mtazamo wa kiisilamu ambao umewekea mipaka juu ya uhatari wa jambo hili?
9) Jambo linalotuhusu hapa ni katika maudhui yetu ni jibu la suala la tatu, ama kuhusu masuala mawili ya mwanzo: (uislamu na sayansi) na (Uislamu na ulimwengu) tutayazungumzia kila moja kwa kina zaidi katika maudhui yake pekee na kwa anuani yake.
10) Ufupisho wa hayo; sayansi katika uislamu ni nguzo miongoni mwa nguzo muhimu, na kuwafikiana kati yake ni kwa mtazamo wa juu, hakuna haja ya kusema kuwa vinapingana, uislamu upo pamoja na sayansi kwa kiroho na kimitaala (miongozo). Kwani Qur`ani tukufu imemhimiza mwanadamu kuhusu kujenga mbinu za kisayansi (kielimu) ambazo zinaweza kufupika kwa kuangalia ulimwengu kwa vipimo na kwa kisomi au kwa yote pamoja (vipimo na usomi) kwa ajili ya kufikia utambuzi wa sheria za kisayansi kwa ujumla, kisha kuendeleza njia hiyo kwa lengo la kumjua Mwenyezi Mungu, na kwa hilo tunaweza kuliweka wazi katika mchoro ufuatao:
Dalili za kisomi Dalili za vipimo
Kuangalia ulimwengu → Kuujua ulimwengu→ kumjua Mwenyezi Mungu
Mbingu na ardhi na vilivyomo, Sheria kwa ujumla, (Muumba ulimwengu)
11) kwa namna hiyo kuna njia mbili za kuuangalia ulimwengu:
Njia ya kwanza; mchunguzi atatumia njia za dalili za kisomi na kugundua sababu ya vitu na chenye kusababisha na kufikia hatua ya kutengeneza sheria kwa ujumla ambayo itafuatwa.
Njia ya pili; kutumia uwezo wa kufikiri kwa akili kwa lengo la kupata dalili ya vipimo ambavyo atafikia hatua ya kuthibitisha uwepo wa Mtengenezaji (Muumbaji) na mwendeshaji wa ulimwengu kwa njia ya vionekanavyo ambavyo havihitaji tafsiri ya uwepo wake kwa kuzuka tu. Qur`ani imeashiria kutokana na ufahamu huu wa njia mbili hizi Mwenyezi Mungu Mtukufu Anasema {Hakika katika kuumbwa mbingu na ardhi na kukhitalifiana usiku na mchana ziko Ishara kwa wenye akili. 191. Ambao humkumbuka Mwenyezi Mungu wakiwa wima na wakikaa kitako na wakilala, na hufikiri kuumbwa mbingu na ardhi, wakisema: Mola wetu Mlezi! Hukuviumba hivi bure. Subhanaka, Umetakasika! Basi tukinge na adhabu ya Moto.} [AALI IMRAAN; 190-191].
12) Na wachunguzi wanaweza kusimamia katika njia ya kwanza na wasifikie (njia) ya pili, na hawa ni {7. Wanajua hali ya dhaahiri ya maisha ya dunia, na wameghafilika na Akhera.} [AR RUUM; 7] Hawa wamefikia katikati ya njia na wakakosa lengo la utafiti wao juu ya dalili za Mwenyezi Mungu za uumbaji wa ulimwengu, na kwa hivyo wakashindwa kuuona uhakika na kufunikwa na mawazo ya kutokuwepo kwa Muumba na kushughulisha na vitu na kuacha kujua lengo, {Huo ndio mwisho wao wa ujuzi.} [AN NAJM 30]. Na uzuri ulioje wa maana ya aya hii kama alivyoelezea Imam Ibn Atwa llah Assakandariy katika hekima zake mashuhuri "kiumbe ndani ya ulimwengu, hajafunguliwa nyanja za vilivyofichikana, ni mfungwa wa vilivyomzunguka na amezungukwa na maumbo yake".
13) Ama kuhusu wayaonayo wengine kuhusu ulazima wa kujali maudhui na kujiegemesha na majaribio ya kimwili na kuangaza mtazamo wa juu kwa kupima vitu pekee wakati wa utafiti wa kisayansi, hawa hakuna shaka kuwa wapo katika njia ya kwanza nayo ni ya kutafuta ujuzi, ujuzi ambao utawafikisha katika njia ya pili ambayo ni ya imani, hii iwapo mtu anataka kuthibitisha utu wake na ubinaadamu wake na kuyafanya maisha yake yawe na maana.
14) Hakika mwisho wa sayansi ndio mwanzo wa imani sahihi na si imani ya kufuata tu, na zingatia undani wa maana ya maneno yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Sema: Ati watakuwa sawa wale wanao jua na wale wasio jua? Hakika wanao kumbuka ni watu wenye akili.} [AZ ZUMUR: 9] na maneno yake Mwenyezi Mungu Mtukufu {Kwa hakika wanao mcha Mwenyezi Mungu miongoni mwa waja wake ni wanazuoni} [FATIR: 28].
15) Na ilivyokuwa picha ya ulimwengu ishakuwa wazi kwa mtazamo wa kiislamu – kama ilivyoelezwa katika maudhui ya (uislamu na ulimwengu), sasa itabidi kuelezea hapa kuhusu uhusiano wa Mwanadamu na Ulimwengu, na maana ya kudhalilisha –kuwepesishwa- ulimwengu kwa ajili yake. Mwanadamu kama ilivyokuja katika Qur`ani kuwa yeye ni mhimili wa ulimwengu huu na katika viumbe vilivyo juu kabisa na kapewa umuhimu na ukarimu mkubwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu, ameumbwa kwa umbo bora kabisa na kufanywa kuwa na sura nzuri sana. Mwenyezi Mungu Mtukufu Anasema {Bila ya shaka tumemuumba mtu kwa umbo lilio bora kabisa} [AT TIN; 4].
16) Ama kuhusu masuala ya kuanza kuumba, jambo hili hatuwezi kujua uhakika wake kwa undani kabisa (maelezo ya kina) kwani ni katika mambo yaliyofichikana, {Sikuwashuhudisha kuumbwa kwa mbingu na ardhi, wala kuumbwa kwa nafsi zao. Wala sikuwafanya wapotezao kuwa ni wasaidizi.} (AL KAHAF: 51). Na Qur`ani tukufu imezungumzia juu ya uumbwaji wa Adamu kwa ujumla na namna alivyofunzwa majina yote na Mwenyezi Mungu, na kuamrishwa Malaika wamsujudie, hayo yametajwa katika Aya tafauti ndani ya Qur`ani tukufu na aya ya kwanza iliyopo katika suratul Baqara (aya ya 30 na zinazoendelea). Lakini hizi zote ni ishara ya mambo yaliyofichikana ambayo hatuyajui kina chake, na ishara hizi zinaweza kuwa na maana nyingine zaidi. Ama mambo ambayo yalikuwepo baada ya kuumbwa utafiti wa kisayansi unaweza kujishughulisha nayo.
17) Iwapo wasomi wanakisia umri wa kuwepo kwa mwanadamu katika ulimwengu kwa kusema ni miaka milioni kwa kuangalia mabaki ya machimbo, hii ina maana kuwa mwanadamu amekuja hali ya kuwa ni kiumbe cha mwisho katika mlolongo wa viumbe waliomtangulia katika uwepo juu ya ardhi hii. Si hivyo tu, mwanadamu mwenyewe amekulia kwa kupitia katika nyakati tafauti, na kwa hili Qur`ani inaashiria kwa kusema {Hakika kilimpitia binaadamu kipindi katika zama ambacho kwamba hakuwa kitu kinachotajwa.} [AL INSAAN;1] {Na hali Yeye kakuumbeni daraja baada ya daraja?} (NUH;14).
18) Na tusemapo: Mwanadamu ni kiumbe mwenye sifa mbili –kimwili na kiroho – sifa moja inashikamana na maeneo na wakati na nyingine inashikamana na ulimwengu mwingine wa hisia (sio ulimwengu wa kuhisi), matamshi yetu haya hayamaanishi kuwa tunazingatia fikira ya vilivyofichikana na kumuweka mbali mwanadamu kama anavyohisi yeye mwenyewe. Kwani manadamu ni kiumbe pekee anayehisi kupitia akili yake mambo yaliyo nje ya hisia, na tabia hii inakaribia kuwa jambo la kawaida kwake, na wala hatuwezi kupinga dalili juu ya jambo hili, kwani mwanadamu anakulia na kuendelea katika ardhi hii, lakini baada ya kuwepo katika ulimwengu ambao hatujui iwapo ni ulimwengu huu au mwingine, na kupitia ulimwengu mwingine Qur`ani inaashiria kwa kusema {Na pale Mola wako Mlezi alipo waleta katika wanaadamu kutoka migongoni mwao kizazi chao, na akawashuhudisha juu ya nafsi zao, akawaambia: Je, Mimi si Mola Mlezi wenu? Wakasema: Kwani! Tumeshuhudia. Msije mkasema Siku ya Kiyama sisi tulikuwa tumeghafilika na hayo} [AL AARAF: 172]. Na nyuma ya aya za Qur`ani zenye kuzungumzia uumbwaji wa mwanadamu na siri zake bado hatujazigundua, na kama ilivyokuwa elimu ya mwanadamu kuhusu yeye mwenyewe na uwezo wake mkubwa alionao pia hajaugundua (na kama kaugundua basi ni kwa kiwango kidogo sana) na pengine ameweza kujua kuhusu ulimwengu zaidi kuliko anavyojua siri za mwili wake.
19) Na mwanadamu katika ulimwengu huu ndiye aliyebeba ujumbe, kwani mwenyezi Mungu ndiye aliyemfanya kuwa ni kiongozi wa ardhi hii kwa kumtaka aijenge na atoe kheri zilizomo ndani yake si kwa kuziacha na kuziepuka, na hii ndio maana ya kuwa kiongozi kama alivyosema Mwenyezi Mungu {Na pale Mola wako Mlezi alipo waambia Malaika:Mimi nitamweka katika ardhi Khalifa (mfwatizi),} [AL BAQARAH; 30] na katika vitu vyenye kumpambanua kiongozi huyu ni akili ambayo ataweza kujua siri za ulimwengu na kumjua Muumba wake, na kujipangia mambo ya maisha yake, na kuijenga ardhi, na kwa ajili hiyo akili imekuwa ni nguzo muhimu sana miongoni mwa nguzo kuu za kiislamu, na kwa kutumia sayansi pia ni katika njia muhimu sana zenye kuweza kufikia lengo la uwepo wa mwanadamu katika ardhi, nalo ni kuijenga na kunufaika na kheri zake.
Na kwa kuangazia historia ya mwanadamu tangu kuwepo kwa ulimwengu mpaka sasa inatosha kujulikna hekima za Mwenyezi Mungu za kumweka mwanadamu, maendeleo ya hali ya juu ya uwezo wake ni dalili tosha ya kuwa Mwenyezi Mungu amemuwekea maandalizi ambayo hakuwawekea viumbe wengine bali mwanadamu pekee kama kudhalilishiwa tabia ya nchi kwa vitu ambavyo hatuvijui na vile ambavyo hata hatuwezi kuvifikiria.
20) Hakika mwanadamu ni kiumbe kilicho juu zaidi katika ulimwengu huu, ni mfano wa kioo, ni kiumbe pekee mwenye uwezo wa kuzingatia vilivyopembeni yake na kuvipa maana na kujua lengo lake. Na uzuri ulioje wa maana ya aya hii {Tutawaonyesha Ishara zetu katika upeo wa mbali nakatika nafsi zao wenyewe mpaka iwabainikie kwamba haya ni kweli.} [FUSWILAT; 53] na hakuna la kushangaza kwa kutukuzwa mwanadamu na Mweneyzi Mungu Mtukufu kwani Anasema {Na hakika tumewatukuza wanadamu} [AL ISRAA;70].
21) Na katika dalili kubwa za kuwa mwanadamu ameumbwa ili awe ni mhimili wa dunia hii ni wale Malaika ambao Mwenyezi Mungu amewaweka katika ulimwengu ambao mwanadamu anaishi, angalia kwa undani maneno yake Mwenyezi Mungu Mtukufu aliposema {Je! Ni vigumu zaidi kukuumbeni nyinyi au mbingu? Yeye ndiye aliye ijenga 28. Akainua kimo chake, na akaitengeneza vizuri. 29. Na akautia giza usiku wake, na akautokeza mchana wake.30. Na juu ya hivyo ameitandaza ardhi. 31. Akatoa ndani yake maji yake na malisho yake,32. Na milima akaisimamisha, 33. Kwa nafuu yenu na mifugo yenu.} [AN NAZIAAT, 22: 33.
22) Na aya zinazozungumzia kuhusu mwanadamu na ulimwengu ziko nyingi zimejaa ndani ya Qur`ani tukufu, na zote zinaonesha kuwa ulimwengu haukuja wenyewe kama wasemavyo wasioamini Mungu.
Na kwa hilo Imam Ibn Rushd, mwanafalsafa mkubwa wa kiislamu anasema katika kitabu chake cha: [Alkashf an Manahij Adillah, (uk. 81-82)] "kama ilivyo kwa mwanadamu akiangalia kitu anachoweza kukigusa na akakiona kipo katika umbile maalumu, na uzito maalumu na mkao maalumu na ikawa kinamnufaisha kitu hicho kwa kumpatia lengo alitakalo, kiasi ambacho lau kama kitu hicho kingelikuwepo lakini kwa umbile jingine na uzito mwingine basi ansingelipata manufaa hayo, na kuwa haiwezekani kukutana mambo hayo ili iwepo faida hiyo (sifa mbili kutafautiana ya kuwepo na kutokuwepo) na namna hiyo ndivyo ilivyo kwa ulimwegnu wote.
Mwanadamu akiangalia jua na mwezi na sayari nyingine ambazo ndio sababu ya kuwepo kwa miongo minne na sababu ya kupatikana usiku na mchana na sababu ya kupatikana mvua na maji na upepo na sababu ya kujengeka kwa baadhi ya maeneo katika ardhi na sababu ya kuwepo kwa watu, wanyama na mimea na kuwa ardhi inawezekana kuishi watu na wanyama wengine na kuwepo kwa maji ndio sababu ya kupatikana wanyama waishio kwenye maji, na kuwepo kwa hewa ndio ababu ya kupatikana wanyama warukao, kwa namna ambayo ingelikuwa kitu kimoja tu kati ya hivi hakiko kwenye mpangilio wake na umbile lake na uzito wake basi viumbe navyo visingelikuwepo.
Na hii ieleweke kuwa haiwezekani mambo haya yawe yamezuka tu kwa wanadamu, wanyama na mimea, lakini kuna malengo ndani yake na makusudio ambayo Mwenyezi Mungu ametaka yawepo, na hii inajulisha wazi kuwa hakuna shaka kwamba ulimwengu una muumbaji." Na haya ndio aliyoyasema Ibn Rushd kwa baada ya ufahamu wa Qur`ani tukufu juu ya aya zinazotaka kuangalia ulimwengu na kama hivyo wasomi wengi wa kisasa walio na fani tofauti wamesema.
Na kama tuonavyo katika kitabu muhimu cha: [Allahu Yatajalla fiy Asr Al Elm] nacho ni mkusanyiko wa makala za maulama kilichoandikwa na John Klofor na kufasiriwa kwa kiarabu na kuenezwa nchini Misri.
23) Na kwa kuwa maisha ya mwanadamu katika mgongo wa ardhi ni mafupi sana isipokuwa yana mafanikio mengi, je yaweza kumalizika haya yote kwa ghafla na kuweza kufanikisha mambo yote katika ardhi hii? Na je inaweza kuwa sawa kufanya juhudi za kutoa huduma kwa Mwanadamu –huduma halisi – yenye manufaa kwa mwanadamu aliyefanya uharibifu katika ardhi? Na je? mjuzi na msomi na mtu mwema na mbaya waweza kuwa sawa?
24) Na kama hali ni kama hivyo basi maisha ya mwanadamu yatakuwa hayana maana na upotevu usio na faida, na Mwenyezi Mungu amekwishajua wakati anamuumba mwanadamu kwamba anaweza kuzuiliwa na matamanio yake na mapendekezo yake kuuona ukweli na kumfanya aingie kwenye hadaa ya kilimwengu {Na walisema: Hapana ila huu uhai wetu wa duniani -twafa na twaishi, na hapana kinacho tuhiliki isipokuwa dahari. Lakini wao hawana ilimu ya hayo, ila wao wanadhani tu.} [AJ JATHIYAH: 24]. Hivyo basi, Mwenyezi Mungu anatuwekea wazi kuwa mwanadamu ana maisha mengine zaidi ya haya anayoishi ambayo atahesabiwa juu ya matendo yake, na ajuaye hawezi kufanana na asiyejua na wala aliyeamini hawezi kufanana na asiyeamini, na mwema hawezi kufanana na muovu {Sema: Ati watakuwa sawa wale wanao jua na wale wasio jua? Hakika wanao kumbuka ni watu wenye akili} [AZ ZUMAR; 9] {Ati aliye Muumini atakuwa sawa na aliye mpotovu? Hawawi sawa} [AS SAJIDAH; 18] {Sema: Haviwi sawa viovu na vyema ujapo kupendeza wingi wa viovu. Basi mcheni Mwenyezi Mungu, enyi wenye akili, ili mpate kufanikiwa} [AL MAIDAH: 100].
25) Mwanasaikolojia maarufu wa nchi za Magharibi ameandika William James makala yenye anuani (Je. maisha yana thamani) anataja ndani yake kuwa maisha yanastahiki kutukuzwa iwapo tunaitakidi kuwa ulimwengu huu si zaidi ya sehemu tu ya uwepo wetu, na pembeni mwetu kuna maisha ya kuhisika na yenye roho ya kudumu na nguvu hii ipo katika ulimwengu usioonekana.
26) Na ukweli ni kuwa itikadi yetu katika ulimwengu huu haionekani nayo ni asili ya itikadi yetu ya kuwa ulimwegnu usioonekana ni bora kwa mwanadamu. Na maana ya ubora ni ile hali ya kufaa katika ulimwengu kwa kuwepo maisha ya kidini yaliyo na manufaa, na kuamini ulimwengu usioonekana kunatupa imani ya kujiandaa na Nyanja nyingine mpya, na nguvu mpya itakayotuwezesha kuitegemea wakati wa kupambana na vita juu ya maisha haya tulionayo.
Na Williams James amesema kuhusu ukweli wa mwanadamu pale alipounganisha furaha ya mwanadamu kuwa inatokana na ukweli wa kufungamana kwake na imani ya kuwepo kwa ulimwengu usioonekana.
Nayo ni furaha ambayo haiwezekani kuijua itakiwavyo isipokuwa kwa yule aliyefanya jaribio la kuishi katika dini itakiwavyo na si kwa mtazamo wa juu juu tu na hiyo si kwa mtu asiyeamini Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi ya wote.
Chanzo: Profesa Abu Alwafaa Al ghnimiy Ata fastazaaniy (Profesa wa falsafa ya kiislamu – Chuo Kikuu cha Alazhar), Mwanadamu na Ulimwengu katika Uisiamu, Cairo. Kimesambazwa na Daru Nashri, 1995AD. Ukurasa wa 18-19, 39-41, 66-67)


 

Share this:

Related Fatwas