Usahihi wa Hadithi ya: " Pepo iko C...

Egypt's Dar Al-Ifta

Usahihi wa Hadithi ya: " Pepo iko Chini ya Miguu ya Akina Mama"

Question

 Ni upi usahihi wa Hadithi ya: "Pepo iko chini ya miguu ya akina mama"?

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, na sifa njema ni zake, na rehema na amani zimshukie Bwana wetu Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na Aali zake na Masahaba wake na wafuasi wake, na baada ya hayo:
Basi kuwafanyia mema wazazi wawili ni miongoni mwa mambo ya lazima ambayo Mwenyezi Mungu Mtukufu ameyaagiza yatekelezwe, na akafuatanisha baina ya kuabudiwa kwake na kuwafanyia wema wazazi wawili ili kumaanisha uwepo wa umuhimu wa kuwatendea wema wazazi. Basi Mwenyezi Mungu Mtukufu Anasema: {Na Mola wako Mlezi ameamrisha kuwa msimu abudu yeyote ila Yeye tu, na wazazi wawili muwatendee wema. Mmoja wao akifikia uzee, naye yuko kwako, au wote wawili, basi usimwambie hata: Ah! Wala usiwakemee. Nasema nao kwa msemo wa hishima.* Na uwainamishie bawa la unyenyekevu kwa kuwaonea huruma. Na useme: Mola wangu Mlezi! Warehemu kama walivyo nilea utotoni} [AL ISRAA 23-24]. Na Mtume S.A.W. alisisitiza juu ya kuwafanyia wema wazazi wawili, na akajaalia kuwatendea uovu wazazi wawili kuwa ni katika Madhambi Makubwa.
Ama kuhusu hukumu ya usahihi wa Hadithi ya: "Pepo iko chini ya miguu ya akina mama", basi Ibn Audaiy alipokea katika kitabu chake: [Al Kaamel], kwa njia ya Musa BinMuhammad BinAtwaa, Abu Elmalih akatusimulia, Maimun akatusimulia, kutoka kwa Ibn Abaas amesema: Mtume S.A.W. anasema: "Pepo iko chini ya miguu ya akina mama, wakitaka huwaingiza peponi na wakikataa huwatoa peponi". Ibn Audaiy akasema: "Musa BinMuhammad Al Maqdisiy mkanushaji wa Hadithi".
Na imetajwa katika sehemu yake ya kwanza: "Pepo iko chini ya miguu ya akina mama", kutoka katika Hadithi ya Anas R.A, kwa usimulizi wa Abu Bakr Ashafiy katika kitabu cha: [Arubaiyaat], na Abu Ashaikh katika kitabu cha: [Al Fawaed], na Al Qadhaiy, na Adulabiy, kutoka kwa Mansuor BinAl Muhajer, kutoka kwa Abi Anadheer Al Abar, kutoka kwa Anas inachukua hukumu ya Marfugh kwake, na kwa mfumo huo huo ikapokelewa na Al Khatweeb katika kitabu cha: [Ajaamei' Lakhlaaq Araawiy], Assutwiy akaitaja katika kitabu cha: [Ajaamei' Aswagheer].
Na Al Mennawiy akasema katika kitabu cha: [Faidhul Qadeer]: "Ibn Twaher akasema: Maswuor na Abu Anadhar: wote wawili hawaijui, na Hadithi hii ina hukumu ya munkari". [Faidhul Qadeer kwa Sharhul Jaamei' Aswagheer 361/3, Ch. Al Maktabah Atujariah Al Kubra].
Na kama Hadithi hii ilikuwa ni dhaifu kwa lafudhi yake, lakini iko sahihi kwa kutajwa kwa maana yake, basi Ibn Magah na Anasaiy wameipokea, kwa lafudhi yake hiyo, na Ahmad, na Atwbaraniy katika kitabu cha: [Al Mua'jam Al Kabeer], kwa isnadi nzuri, na ikasahihishwa na Al Hakem, na Adhahabiy akaafikiana naye, na Al Mundheriy akaikubali, kutoka katika Hadithi ya Muawiyah BinJahemah kwamba alikuja kwa Mtume S.A.W., na akasema: "Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Ninataka kwenda kupigana vitani na nimekuja kukuomba ushauri? Akamuuliza: Je wewe una mama? Akasema ndio. Mtume akamwambia: "Basi, kuwa naye, Kwani Pepo iko chini ya miguu yake".
Ama simulizi ya Ibn Majah; kutoka kwa Muawiyah BinJahemah inasema: Nilimjia Mtume S.A.W, nikamwambia: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Mimi nilikuwa ninataka kwenda kupigana Jihadi pamoja nawe nikizitafuta kwa jihadi hiyo radhi za Mwenyezi Mungu pamoja na Pepo yake, akasema: ole wako! Je mama yako yu hai? Nikasema: Ndiyo Ewe Mtume ya Mwenyezi Mungu, Akasema: "Basi rudi na umfanyie mema".
Ama mapokezi ya Ibn Majah, kutoka kwa muawia Ibn Jahimah amesema nilimjia Mtume rehema na amani ziwe juu yake nikasema Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu Mimi nilikuwa ninataka kupigana Jihadi pamoja nawe nikiitafuta kwa jihadi hiyo radhi ya Mwenyezi Mungu pamoja na Pepo yake, akasema: ole wako! Je mama yako yu hai? Nikasema: Ndiyo Ewe Mtume ya Mwenyezi Mungu, Akasema:, "Basi rudi na umfanyia mema". Kisha nikamjia mbele yake, Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Mimi nilikuwa nataka Jihadi pamoja nawe nikiitafuta kwa jihadi hiyo radhi ya Mwenyezi Mungu pamoja na Pepo yake, akasema: "Ole wako, ufuate mguu wake kwani hiyo ndiyo Pepo.".
Al Mannawiy amesema: "Na maana inayokusudiwa ni: Kuwanyenyekea mama zetu na kuwatii katika kuwatumikia na kutoenda kinyume nao -isipokuwa katika mambo yanayokatazwa na Sheria ya Kiislamu- na hiyo ni sababu ya kuingia Peponi. [Faidhul Qadir kwa Sharhul Jaamei' Aswaghir 361/3, Ch. Al Maktabah Atujariah Al Kubra].
Kutokana na hayo: Basi hii Hadithi ambayo maana yake imeelezwa hapo mwanzoni ni sahihi, na Isnadi yake ni dhaifu, na inafaa kupendezesha katika kuwatendea wema mama zetu na kuwatii.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.

 

 

Share this:

Related Fatwas