Miongoni mwa Maadili ya Kiisilamu ...

Egypt's Dar Al-Ifta

Miongoni mwa Maadili ya Kiisilamu - Aliyenyamaza Hanasibishwi Neno

Question

 “Aliyenyamaza hanasibishwi neno” Ibara hii ina maana gani? Na inaathiri vipi katika mwenendo mzima wa maisha ya mtu?

Answer

 Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehema na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Hili ni jambo la msingi sana katika misingi ya sheria za hukumu za kiislamu, na ni misingi ya uwepo wa uadilifu na usawa. Hii ni ibara aliyoisema Imam Shafi baada ya kuzingatia upande wa sheria na upande wa maisha ya kawaida. Lakini katika yenye kusikitisha watu wengi sana hawazingatii ibara hii na wapo nje kabisa na ikawa aliyekaa kimya ndiye anayeshitakiwa kwa kuzuliwa makosa ya mwingine na kutakiwa aseme na asiposema basi kesi humuandama.
Haina budi sasa kurudi katika asili ya tamaduni zetu ambazo zinahimiza uadilifu, Mwenyezi Mungu Mtukufu Anasema: {Hakika Mwenyezi Mungu anaamrisha kufanya uadilifu, na hisani, na kuwapa
jamaa; na anakataza uchafu, na uovu, na dhulma. Anakuwaidhini ili mpatekuk umbuka.} [AN NAHL; 90] {Enyi mlio amini! Kuweni wasimamizi madhubuti kwa ajili ya Mwenyezi Mungumkitoa ushahidi kwa haki. Wala kuchukiana na watu kusikupelekeeni kutofanyauadilifu. Fanyeni uadilifu. Hivyo ndio kuwa karibu mno na uchamngu. Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu anazo khabari za mnayo yatenda.} [AL MAIDAH; 8]
1. Kikawaida mtu anaweza kusema matamshi au kutenda jambo na akanasibishiwa nalo au asiseme wala kutenda na akanasibishwa na mambo hayo vile vile, lakini inapotokezea watu kumzungumzia mtu huyo basi yaweza kuwa wakamzungumzia kwa wema au kwa ubaya, na iwapo atazungumziwa kwa wema hili halina tatizo (iwapo kweli ni mwema), hapa itakuwa wamemtolea ushahidi wa kweli kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Nasimamisheni ushahidi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. Hivyo ndivyo anavyo agizwa anaye muamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho. Na anaye mcha Mwenyezi Mung humtengezea njia ya kutokea.} [AT TWALAQ; 2]
Na utoaji wa shahada kunahitaji ukweli na kujaribu kutoingia katika hali ya udhaifu wa kibinaadamu, udhaifu huo ni kama:- kusahau, kwa maana akitokezea mtu wa kumkubusha basi hukumbuka. Kupoteza kumbukumbu, kwa maana akitokezea mtu wa kumkumbusha basi huwa hakumbuki. Kughafilika, kwa maana ni ile hali ya kuchanganya mtu matukio na ukweli ulivyo kiasi ambacho anashindwa kubagua jambo au neno gani sahihi na lipi si sahihi, na kosa hili hutokezea kwa sababu ya kujilazimisha auufahamu finyu au utekelezaji. Makosa yatokanayo na kujilazimisha ni kule kusikia sehemu tu ya maneno yasemwayo au kutoweza kufikia maana halisi ya maneno na ishara zake na mfano kama huo. Na makosa yatokanayo na ufahamu finyu yanatokana na kutoelewa uhakika na kiini cha jambo (kesi) lenyewe au mafumbo yaliyotumika, au kuchanganya maana ya meneno na kuyatumia sehemu isiyohusika si kama atakavyo msemaji au pia kutofahamu matumizi ya kilugha au kutafautisha maneno yatumikayo kwa maana moja na kukutanisha maneno yaliyotenganishwa kimaana na kimatumizi, au kutanguliza muundo wa maneno au kufanya kosa la kutokuchunga masharti ya maneno yaliyo na sifa maalumu na kuyatumia mahali pasipofaa.
Ama kosa la Utekelezaji, linahusisha matumizi ya ibara ambayo muhusika huwa anaisema na ambayo haiendani na ushahidi uliopo au kutoweza kulisema alitakalo kwa sababu ya kushindwa kwake kuelezea kilugha au kwa kuwa hajakusudia (anafanya mzaha).
Na katika udhaifu wa kibinadamu, uongo; nalo ni kosa la kimakusidi lililoambatana na nia mbaya, hivyo, ni kosa ambalo huenda likawa kwa sababu ya chuki au kusudio baya au woga na mfano wake.
Na pia miongoni mwa udhaifu wa kibinaadamu ni kubutwaa nayo ni hali ya kutozingatia jambo na kuwa na ufahamu mdogo wa jambo hilo na hutokezea kwa sababu ima ya mshangao utokezeao kwa ghafla.
Na katika udhaifu pia ni kulazimishwa na mwingine sawa iwe kwa adhabu ya kutozwa mali au ya kimwili.
Na udhaifu huu wote ambao humtokezea mtu humfanya kuwa “Aliyenyamaza hanasibishiwi neno”. Msemaji anaweza kufikwa na hali hizi za udhaifu wa kibinaadamu, na awapo kimya asiseme kitu basi huwa hanasibishwi na neno, na kwa ajili hiyo waislamu wamevumbua elimu –taaluma- ya uthibitisho kwa upande wa Qur`ani na kuweka misingi iliyo madhubuti si kwa kila aya pekee au kila neno au herufi lakini hata kwa upande wa matamshi (maneno yasemwayo). Kwa upande wa Hadithi za Mtume ( rehema na amani zimshukie) wameweka taaluma zaidi ya ishirini zenye kudhibiti mapokezi ya Hadithi, na Mtume ( rehema na amani zimshukie anasema kuhusu suala hili “Atakaenizushia uongo kwa makusudi basi na ajiandae makazi yake motoni” [Bukhari; 110, Muslim;3].
Na kwa upande wa taaluma nyingine wameweka kitabu chenye kukusanya mlolongo wa vitabu vyingine, kitabu chenye taaluma zote, na hili tunaliona kwa kuthibitishwa kwa kuwepo kwa hukumu ambayo inasisitiza uadilifu na uhakika (umakini) katika kutoa ushahidi, kwani si kila mtu hukubaliwa ushahidi lakini kwa wale ambao udhaifu wa kibinaadamu kwao ni mdogo sana, na hii ni kwenda sambamba na maneno ya Mtume (rehema na amani zimshukie), imepokewa kutoka kwa Ibn Abbas amesema; Mtume (rehema na amani zimshukie) aliulizwa kuhusu kutoa ushahidi. Akasema: “Je waliona jua?” Akajibu: “Ndio”, akasema: “Mfano wa hawa basi toa ushahidi.” [Al- Baihaqiy.Abu Naim].
2. Ama iwapo hakusema neno au kutenda jambo lolote hali ya huyu ni kubwa zaidi kuliko ya Yule (mfano wa mwanzo uliotangulia) na wala halazimishwi hata kidogo kujibu uzushi anaozushiwa, Imam Sakhawiy anasema katika kitabu cha [A dhaw`u l laami`i] beti za mwalimu wake akisema:
Wabaya wangapi wanaeneza uzushi *
* na wala hawamuogopi Mungu na kupata aibu
Wanatamani kuangamia wenzao *
* na hata kama hawatafaidika ila madhambi
Usikiapo maneno kuhusu wewe yaliyovuka mipaka *
* muachie mwenyewe aendelee nayo
Usijali hata siku moja pindi wakibweka *
* mbwa wote kwani haki ipo kwa Mungu pekee
Kwani umeingia nyumba iliyopangwa na mhunzi *
* na kupambwa na mjuzi mahiri
Na ikiwa utamrembe jiwe kila mbwa *
* basi mawe yangekuwa na thamani kama dinari
3. Na pamoja na kuwa ibara hii inatumika katika sheria na katika utoaji wa shahada na hukumu na hata katika Nyanja za kielimu, sheria pia imeiweka ibara hii kando –kama iwavyo katika ibara nyingine – kwa malengo mengine mazuri tu, imepokewa katika sahihi Bukhari kuwa Bibi Aisha (Mwenyezi Mungu amwie radhi) amesema: Mwanamke bikira huombwa ruhusa naye huona haya na hukaa kimya. Akasema: “Kimya chake ndio ruhusa yake”.
Hayo ndio masiku ambayo watu walikuwa wakiona haya na haya ilikuwa ni tabia njema na nzuri, mtoto wa kike alikuwa na haya alipokuwa mtu anakwenda kumchumbia na baba mtu anapomuuliza mwanawe -mtoto wa kike- mtoto huona haya. Kwa ajili hiyo sheria ikaikubali hii haya. Mtume (rehema na amani zimshukie) anasema. “Haya ni kheri zote” (Muslim) hivyo, kimya chake ndio ruhusa yake, naye pia pindi akimchukia au kumkataa hatakiwi kuwa na haya ya kusema mtazamo wake. Kwa ajili hiyo kuna tamaduni iliyoenea ya kusema kuwa “Kimya ni ishara ya kukubali”, ingawa makusudio ni kwa mwanamke bikira ila madhumuni yake yanaenea hadi katika hali nyingine.
Sasa je turekebishe asili yetu na kurejea tena tulikotoka na iwe ndio kama katiba au mfano wa mkataba madhubuti wa tamaduni au tubakie tukiendelea kama tulivyo katika mazungumzo pekee yasiyo na misingimadhubuti katika maisha yetu ya kiutamaduni na yasiyo na mwongozo.


Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.

 

Share this:

Related Fatwas