Uhusiano Kati ya Uharamu na Dhambi....

Egypt's Dar Al-Ifta

Uhusiano Kati ya Uharamu na Dhambi.

Question

Hivi! kufanya mambo ambayo ni haramu kunawajibisha kupata dhambi kwa mtendaji wake? Vile vile, kila kinachotokana na kitendo chake cha haramu ni haramu? Ingawa ni hivyo, niliona baadhi yao wanasema kwamba hii si kama ilivyo katika tamko lake, lakini kuna mambo yanayotengwa na imepokelewa kutoka kwa mmoja wa Wanavyuoni wakubwa naye ni - Imam Al-Zarkashiy- katika maneno yake kuwa: (Uharamu hauwajibishi dhambi), ni nini maana ya maneno hayo? 

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema ni zake, na rehema na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu na jamaa zake na Masahaba wake na wafuasi wake. Na baada ya utangulizi huu :
Maneno yaliyotajwa na Badru Din Zarkashi Ash-Shafiy Mwenyezi Mungu Mtukufu Amrehemu ni sahihi, ambapo alisema katika kitabu chake : [Al-Bahrul Muhiit fi Usuul Al-Fiqh 1/337, i. Darul Ketbi]: “Uharamu hauwajibishi dhambi kamwe, mtu anaweza kupata dhambi kutokana na kitu kisicho haramu, kama vile anapomwendea mkewe akidhani kuwa ni mwanamke asiyemjua, na pengine huharamishwa kitu kisicho na dhambi, kama vile mtu anapomwendea mwanamke asiyemjua akidhani kuwa ni mkewe”.
Na muhtasari wa suala hili ni kwamba: Mtu pengine anapata dhambi kwa kitendo kisicho haramu, kama vile anapokunywa glasi ya maji akifikiri kwamba ni pombe. Kwa hivyo basi hakuna dhambi katika kunywa maji, lakini matokeo ya dhambi katika hali hii ya kunywa kitu alichodhani ni haramu ingawa kitu hicho chenyewe si haramu. Na kinyume chake pengine ni kuwa dhambi inatengana na mambo yaliyo haramu, kama vile mtu anapokunywa glasi ya pombe akidhani ni maji. Basi kinywaji hicho ni haramu lakini hakuna dhambi kwa aliyekunywa katika hali hii kwa sababu ya ujinga wake wa ukweli wa jambo hili. Aliyekosa, aliyesahau, na aliyelazimishwa wote hawa wamesamehewa kwa mujibu wa Hadithi iliyopokelewa na Ibn Majah katika kitabu chake cha Sunan kutoka kwa Abu Dhar Al-Ghafariy, amesema kwamba: Mtume wa Allah S.A.W: amesema : “Hakika Mwenyezi Mungu hawahisabii umma wangu kwa yale yanayowapitia, makosa yao (pasi na kukusudia) usahau, na wanayolazimishwa kuyafanya”.
Al-Zarkashiy alisema katika “Al-Bahrul Muhiit” (1/337): “Dhambi inategemea ufahamu, yaani mja akinuia kufanya kitu kimoja akidhani kitu hicho ni halali nacho ni haramu, basi hakuna dhambi kwake, bali huko ni kufanyiwa wepesi kwa mja. Na kama akinuia kufanya kitu kimoja akidhani kitu hicho ni haramu nacho ni halali ataadhibiwa kwa ajili ya ujeuri wake” kisha alielezea maana ya haramu na halali kwa kusema kuwa: “Tendo hili ni haramu, kauli hii ina maana kwamba jambo hili linatakiwa kuachwa, na maana ya kusema kuwa: tendo hili ni halali ina maana kwamba jambo hili linatakiwa kutoachwa.
Tendo ambalo ni haramu ni nile linalotakiwa kuachwa, kama watu wakijua au hawakujua, basi wakijua kwamba kitendo hicho ni haramu wamepata dhambi, lakini kama hawakujua na wakafanya hivyo, basi tendo hili ni haramu lakini dhambi yake imeondolewa kwa ukarimu wa Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu Mtukufu Anasema: {Wala Sisi hatuadhibu mpaka tumpeleke Mtume} [Isra: 15], Yaani Mitume hawa wamepelekewa kwa ajili ya kuwafahamisha watu mambo ambayo ni halali na ambayo ni haramu ya wajibu ya kiitikadi, kazi na tabia, Mwenyezi Mungu Mtukufu Anasema: {Ili watu wasiwe na hoja juu ya Mwenyezi Mungu baada ya kuletewa Mitume} [AN NISAA: 165].
Al-Zarkashiy anasema kuhusu jambo hili kuwa: “Yale tuliyoyataja hayana maana ya kukubali kauli ya wale waliosema kuwa: Uhalali na uharamu unaeleza hali yenyewe. Na maana ya hivyo ni kwamba : Uhalali na uharamu unaeleza hali yenyewe kama ikifanana na itikadi au la. Angalia yaliyosemwa na Al-Baydhawi: Wanavyuoni wa Fiqhi walisema: Kufunga ni lazima kwa wanawake katika hedhi, mgonjwa, na msafiri, pengine mtu akiacha jambo la wajibu atapata dhambi kama alivyofikiria, na katika hali ile ile ni haramu, na kinyume cha hivyo ni sawa. Sheikh Abu Hamed alisema kuhusu aliyesali akifikiri kwamba ana twahara: atakufa na ataulizwa kuhusu sala hii, lakini hatadhibiwa, basi huyu ameacha wajibu na hataadhibiwa kwa kuacha jambo la wajibu; kwani aliacha jambo la wajibu akifikiria Mwenyezi Mungu anataka jambo hili, na hakuliacha kwa maana ya faradhi”. (Al-Bahri Al-Muhiit 1/338).
Jamaalu Diin Al-Isnawi anaeleza kwamba kama dhambi ikiondolewa kwa aliyepata dhambi kutokana na usahau au kosa basi hali hii ina hukumu tatu: Ya Kwanza, ni halali. Ya pili ni haraamu, na Wanavyuoni wengi wa madhehebu ya Shafii walesema hivyo. Na ya Tatu: Haikuelezwa uhalali au uharamu, na kwa rai hii An-Nawawi alijibu kwa fatwa yake, na Al-Isnawi amechagua rai hii pia.
Alisema katika utangulizi wake (uk. 49, Muasastu Resalah.): “Kama Akifanya jimai pamoja na mwanamke asiyemjua akifikiria ni mke wake, je, jimai yake hii inaelezwa kwa uhalali au uharamu kama dhambi ikiondolewa? Au hali hii haielezewi kwa hukumu yeyote? Hali hii ina hukumu tatu, na hukumu iliyochaguliwa ni hukumu ya tatu iliyochaguliwa na An-Awawi katika kitabu cha ndoa ya fatwa yake; kwa sababu uhalali na uharamu ni miongoni wa hukumu za sheria, na hukumu ya sheria ni jambo linalohusiana na vitendo vya waliokalifishwa. Aliyekosa, na aliyesahau hakuwa miongoni mwa waliokalifishwa. Na alisisitiza katika kitabu cha Al-Muhadhaab kuwa ni haramu, Wanavyuoni wengi miongoni mwa wenzetu walisema hivyo. Na mgogoro huo unakuwa katika suala la kumwua mtu kwa makosa na kula mfu kwa anayelazimishwa.
Al-Zarkashi anaonesha kwamba mgogoro katika suala hili ni mgogoro kufuatana na istilahi, kwa sababu ya kutoa hukumu ya uhalali na uharamu mara moja kufuatana na dhambi, na hali hii ni istilahi Wanavyuoni wa vyanzo vya Fiqhi, na mara nyingine kufuatana na kutaka kwa Sheria kuacha kitendo hicho au kutokiacha kwa mujibu wa istilahi ya Wanavyuoni wengi wa Fiqhi. Al-Zarkashi anasema : “Hukumu ya uhalali na uharamu inatolewa mara nyingine kwa hali iliyo na dhambi na isiyo na dhambi pia, na rai hii ni ya Wanavyuoni wa Vyanzo vya Fiqhi waliposema : Uharamu ni jambo baya, na wakati mwingine uharamu ni jambo linalotakiwa kuachwa. Kwa hivyo, Wanavyuoni wengi walisema : Kufanya tendo la ndoa katika pahala penye shaka ni haramu. Pamoja na kuthibitisha kuwa hakuna dhambi katika hali hii. Vile vile Sheikh Abu Hamid alisema: Wanavyuoni walikubaliana kwamba suala la kumwua mtu kwa makosa na kula mfu kwa anayelazimishwa ni haramu. (Al-Bahrul Muhiit 1/338).
Alauddin Al-Bukhari Al-Hanafi alitaja matunda ya mgogoro katika maelezo ya kitendo cha haramu pamoja na kuondolewa kwa dhambi au kuelezea uhalali, akisema katika kitabu chake : [Kashful Asrar Sharh Ussul Al-Bazdoiy 2/322, Darul Kitab Al-Islami.]: “Jua kwamba wanavyuoni wametofautiana katika hukumu ya kula mfu, kunywa pombe, kula nguruwe n.k. katika hali ya dharura ni halali au ni haramu na dhambi inaondolewa. Baadhi yao walisema kuwa ni halali, lakini inaruhusiwa kufanya hivyo katika hali ya dharura, kula fedha za wengine, nayo ni mapokezi ya Abu Yusuf, na kauli ya Al-Shafii. Wengi wa wenzetu walisema kuwa uharamu unaondelewa katika hali hii. Manufaa ya tofauti yanaonekana kama akisubiri mtu mpaka akafa, basi hana dhambi kwa mujibu wa kundi la wanavyuoni wa kwanza, na atapata dhambi kwetu. Kama akiapa hakula haramu akala haramu katika hali ya dharura akavunja kiapo chake kwao, na havunji kiapo chake kwetu”.
Kutokana na maelezo yaliyotangulia hapo juu, inadhihirika kwamba kauli hii ya: “ Uharamu hauwajibishi dhambi” ni kauli iliosemwa na Imam Al-Zarkashi, pia ina maana ya kweli kwa kuzingatia kuwa kitendo kinachoelezewa kuwa ni haramu katika suala la kulitiwa mkazo, na kinatakiwa kuachwa hata kama aliyekalifishwa hakujua hali hii. Hali hii inaelezewa kuwa amefanya haramu pasipo na dhambi. Dhambi inategemea kujua uharamu wake na siyo haramu muda wa kuwa haramu.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.

 

Share this:

Related Fatwas