Hukumu ya Kuupaka Rangi Msahafu

Egypt's Dar Al-Ifta

Hukumu ya Kuupaka Rangi Msahafu

Question

Tumeliona ombi lililoletwa kwetu, ambalo linajumuisha swali kuhusu: kuupaka rangi Msahafu; Je, kazi hii ni kuboresha au ni bidaa? Hakika baadhi ya wachapishaji Msahafu wanafanya hivi kwa makusudio na malengo yanayowahusu, kama vile: hukumu za Tajwidi kutokana na kanuni maalum zenye maelezo katika chapa yenyewe, pengine, rangi huonesha kukusanya Aya zenye maudhui moja chini ya rangi hii, pengine, kwa lengo la kuainisha na kutambulisha Lafudhi ya utukufu (Allah), pamoja na maambatanisho yake, yakiwa maneno au nafsi, kama vile, (Rab), (Ilaah), (Ar-Rahman), (Huwa), (Ana) n.k. 

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, na Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, Rehema na Amani zimshukie Bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, Aali zake na Masahaba zake, na waliomfuata, na baada ya hayo:
Mwenyezi Mungu anasema: {Na bila ya shaka Sisi tumeifanya Qur`ani iwe nyepesi kufahamika. Lakini yupo anaye kumbuka?} [AL-QAMAR: 17], kuna dalili katika Aya hii kuwa kupata na kuleta kila linalorahisisha kusoma Qur`ani, kuizingatia, kuifahamu, kuitambua, na kuitekeleza, hayo yote yanatakiwa kisheria.
Kwa mujibu wa hayo, kila linalosaidia kurahisisha hivi miongoni mwa mbinu za kisasa, linaingia hukumu hii, sharti la kuihifadhi utukufu wa Aya za Qur`ani, mbali na mabadiliko, kugeuza, ziada, au upungufu.
Kwa mtazamo wa asili hii, tunaweza kujadili maudhui ya swali, tukisema: Alama zenye rangi zinazofanywa na mashirika ya uchapishaji zina hukumu tofauti, kutokana na wadhifa wake; kama zikiambatana na kuashiria hukumu za Tajwidi na kuzitambua, basi inajuzu, na hakika ni ombi la kisheria, na mfano wake ni zinazotumiwa katika kuvitambua visomo vilivyopokelewa na wengi (Mutawatiri) na mashuhuri zenyewe kwa zenyewe, na wanachuoni wa njia za kuandika Msahafu miongoni mwa Salaf walikuwa wakiunganisha baadhi ya herufi zilizoachwa katika hati za Misahafu ya Uthmani, ambazo ni lazima kuzitamka, kwa rangi nyekundu, kulingana na herufi za asili.
Imamu Abu-Amr Ad-Daniy katika kitabu cha [Al-Muhkam Fi Naqt Al-Masahif: Uk. 24, Ch. ya Dar Al-Fikr] anasema: “Abu-bakr Ibn Mujadid katika kitabu cha An-Naqt anasema: kuweka Irabu ni alama ya kuandika, kama kwamba Sarufi ni alama ya maneno ya ulimi, na bila ya Irabu haijuliwi maana ya kuandika, na bila ya Sarufi haijuliwi maana ya maneno. Na kuweka Irabu ni kwa kile kilichotata, kwa hiyo si kila herufi inahitaji kuweka Irabu, bali ni lazima katika hali ya utata tu, na lau kuwekwa Irabu katika herufi zote za neno, basi hupelekea utata na faida yake itapotea; na baadhi yake kutosha na nyingine, na kuweka Irabu na Nukta ni kitu kimoja, lakini msomaji anaangalia Irabu upesi kuliko Nukta, kwa sababu Irabu ina sura tofauti na Nukta ina sura moja tu. Anasema: baadhi ya watu wa zamani walitaka kuzidisha na kubainisha matumizi ya Nukta, katika nakala ya pekee ya msahafu, wakaweka hivi kwa alama yenye rangi, kama vile nyekundu, kijani, na manjano, na hii inarahisisha kuangalia Irabu kuliko rangi moja. Akasema pia: kuweka Nukta ni elimu kubwa, na ipo tofauti kati ya wataalamu, na mtu hawezi kusoma katika msahafu wenye Nukta, isipokuwa ana elimu ya njia ya kuweka Nukta hizi, kwa hiyo pasipo na elimu ya njia haipo faida. Na Abu-Amr anasema: Yote yaliyotajwa katika mlango huu na Ibn Mujahid, ni sahihi na kukubalika, na Mwenyezi Mungu ni mwenye kusaidia”. [Mwisho].
Imamu Al-kasaniy mfuasi wa Madhehebu ya Hanafi katika [Badaiu’ As-Sanaii’: 5/127, Ch. ya dar Al-Kutub Al-Elmiyah] aliposema katika hukumu ya kuweka alama kwenye kila Aya kumi, na kuweka Nukta katika Msahafu, na kuwa kazi hii ni Makuruhu katika rai za baadhi ya Salaf, akisema baada ya hayo: “lakini katika nchi za waajemi si makuruhu, kwa sababu, waajemi hawawezi kujifunza Qur`ani pasipo hivi, kwa hiyo, kazi hii ilijiri kama desturi katika nchi zote, bila ya kukanushwa, basi ikiwa Sunna na si Makuruhi’. [Mwisho].
Imamu Al-Ghazaliy katika [Al-Ihiyaa: 1/276, Ch. ya Dar Al-Maarifah] anasema: “Inapendelewa kuandika Qur`ani kwa uzuri na uwazi, na haidhuru kuweka Nukta na alama ya rangi n.k., kwa sababu ni pambo na bainisho, na kuhifadhi dhidi ya kosa na badiliko la msomaji, na Al-Hassan na Ibn Siriin walikanusha alama za Aya tano, na Aya kumi, na juzuu, kama ilivyopokelewa na Ash-Shaabiy na Ibrahimu kuwa wanakanusha kuweka Nukta yenye rangi, pamoja na kupata ajira ya kazi hii, na wao wakasema: Safisha Qur`ani. Na maana ya hayo ni kuwa walichukia kufungua mlango huu kuhofia upelekeaji wa kuwepo ongezeko, na kuziba mlango na kuangalia ulindaji wa Qur`ani na mabadiliko.
Na kama kazi hii isipopelekea kosa, na maoni ya umma yalielekea kuwa inazidisha maarifa, basi hakuna ubaya; na haidhuru kuwa ni kitu kipya, huenda kipya ni kizuri, kama ilivyosemwa katika kutekeleza sala ya Tarawehe jamaa, kuwa ni miongoni mwa vitu vipya vya Umar R.A, ambavyo ni bidaa nzuri, kwani bida mbaya ndiyo inayopingana na Sunna ya asili, na hupelekea mabadiliko. Na baadhi ya wanachuoni walisema: Soma katika Msahafu wenye Nukta, lakini usiweke nukta wewe mwenyewe. Na Al-Awzai’y, kutoka kwa Yahya Ibn Abi-Kathiir anasema: Qur`ani imeandikwa peke yake katika Misahafu, na mwanzo wa vitu vipya vya hivi ni kuweka Nukta ya herufu (ba) na herufi (ta), na wakasema: hakuna ubaya, kwani ni nuru ndani yake, kisha waliweka Nukta kubwa mwishoni mwa Aya, na wakasema; hakuna ubaya kwani ni alama ya Aya, kisha waliongeza mianzo na miisho.
Abu-Bakr Al-Hudhliy anasema: Nilimuuliza Al-Hassan kuhusu kuweka Nukta yenye rangi katika msahafu, akasema: Nukta ni nini? Nikasema: alama ya Irabu ya maneno ya kiarabu, akasema: hakuna ubaya. Na Khalid Al-Hadhaa anasema: Niliingia kwa Ibn Siriin, nikamwona akisoma katika Msahafu wenye Nukta, wakati yeye alikuwa akichukia kuweka Nukta”. [Mwisho].
Imamu An-Nawawiy katika kitabu chake [At-Tibyan Fi Adaab Hamalat Al-Quran: Uk. 189, Ch. ya Dar Ibn Hazm] anasema: “Wanachuoni wamekubali kuwa inapendeza kuandika Misahafu kwa uzuri, kuibainisha, kuidhihirisha, na kuipangilia hati kwa uzuri. Na wao wanasema: inapendeza kuweka Nukta na Irabu katika Msahafu, kwani ni kuulinda kutokana na kosa na mabadiliko. Na msimamo wa Ash-Shaabiy na An-Nakhiy juu ya kuweka Nukta katika wakati wao, hivyo kwa kuogopa mabadiliko, lakini leo hakuna hofu, basi haikatazwi, na haisemwi kuwa ni kitu kipya, kwani ni kipya kizuri, basi haikatazwi, kama vile; kubuni elimu, kujenga shule, madrasa, n.k.”. [Mwisho].
Al-Hafidh As-Sayuti katika [Al-Itqan: 4/186, Ch. ya Al-Haiah Al-Masriyah Al-Amah Lil-kitab] anasema: “Irabu katika wakati wa kwanza ilikuwa sura ya Nukta; kama vile: (Fataha) ni Nukta iliyowekwa mwanzoni mwa herufi, na (Damah) ni mwishoni mwake, na (Kasrah) ni chini yake, na huu ni mfumo alioukubali Ad-Daniy, lakini kwa sasa ni Irabu zinazochukuliwa kwa herufi, na huu ni mfumo wa Al-Khalil, ambao ni wazi na kutumiwa kwa wingi, na kutekelezwa, kwa mfano; (Fatah) ni kistari juu ya herufi, (Kasr) chini yake, na (Dam) ni waw ndogo juu ya herufi; pamja na kutumia herufi za rangi”. [Mwisho].
Ilivyonukuliwa na baadhi ya Salaf kuwa kuweka Nukta na alama ya Aya kumi katika Msahafu ni makuruhu, hakika sababu yake ni hofu ya kuingia katika Qur`ani ilivyo mbali nayo, au kuwa sababu ya kutozingatia na unyenyekevu.
Mtaalamu Ibn Rushd katika [Al-Bayan wat-Tahsiil: 1/241, Ch. ya dar Al-Gharb Al-Islamiy] anasema: “Imamu Malik aliulizwa juu ya alama ya Aya kumi katika Msahafu, akasema: alama hii inawekwa kwa nyeusi, na mimi ninachukia nyekundu, kisha akasema; nachukia nyekundu katika Misahafu mikuu, lakini inajuzu katika Misahafu ya kufundisha watoto, na mwelekeo wake kuhusu kuweka alama nyekunudu ni wazi; kwa sababu msomaji akiona rangi basi anavutiwa kwake kuliko kuchunguza na kuzingatia katika Aya za Qur`ani. Na Mtume S.A.W, alitia vikanda vipya katika kiatu chake, kisha akaviondoa, akarejesha makongwe, na akasema: “Nilivitazama katika sala”, na akasali katika joho la Sham lenye zari, na alipomaliza sala, akalirejesha kwa aliyetoa kama zawadi, naye Abi-Jahm, na akasema: “Mimi niliitazama zari katika sala, hata ilitaka kunifitinisha”. Na kama yeye akihofia fitina, basi kwa mwingine ni kubwa mno, na kwa maana hii ilichukiwa kupambwa msikiti.
Kuhusu kuchukia kuweka rangi katika Misahafu mikuu, maana yake kuwa: sura ya kuweka rangi ina tofauti katika maoni ya wasomaji Qur`ani, na njia yake haina kauli ya pamoja, basi haina elimu ya yakini ipi sura itegemewe, na huenda maana inaathiriwa kwa tofauti ya sura, kwa hiyo, ilichukiwa kuwekwa tofauti katika Misahafu mikuu, na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusaidia”. [Mwisho kwa mabadiliko].
Na hofu kama hizi hazipo kuhusu Misahafu inayoulizwa kwa kupakwa rangi, kwa sababu hii si miongoni mwa Misahafu mikuu, na anayejifunza Qur`ani ameombwa kuisoma Qur`ani vizuri, pamoja na unyenyekevu, na kama akisoma kwa makini, basi hajakuwa na uvutio wa kupaka rangi, na kila hali ina makala. Pia kila mtu anaweza awe na zaidi ya Msahafu mmoja, kama wanavyofanya watu wengi, mmoja kwa kusoma, na mwingine kwa kujifunza, n.k. Na hii ilifanywa na waislamu wa zamani, na wa kisasa, na ilikuwa na heri nyingi, kama kwamba mbinu kwa jumla ina hukumu ya malengo.
Bukhariy amepokea kutoka kwa Zaid Ibn Thabit R.A, akisema: “Abu-Bakr alinituma habari ya mauaji ya wapiganaji wa Vita vya Al-Yamamah, na Umar Ibn Al-Khattab R.A, alikuwa yuko hapa, na Abu-Bakr R.A, alisema kuwa Umar alikuja na kusema: “Mauaji ya waliohifadhi Qur`ani yalikuwa makubwa katika Siku ya Al-Yamamh, na mimi nahofia kuwa mauaji ya wasomaji Qurani yatazidi vitani, hivyo sehemu kubwa ya Qur`ani itapotea, basi lazima uamuru kuikusanya Qur`ani”, nilimwambia Umar: “Vipi unafanya kitu kisichofanywa na Mtume S.A.W”, na Umar alisema: “Wallahi ni heri”. Kisha Umar aliendelea kunikinaisha, mpaka Mwenyezi Mungu alipoutuliza moyo wangu kuwa nifanye jambo hilo, nikaona yale yale aliyoyaona Umar”, na Zaid alisema: Abu-Bakr alisema: “wewe ni kijana mwenye akili na mwaminifu, ulikuwa ukiandika Wahyi kwa Mtume S.A.W, basi ifuate Qur`ani na kuikusanya, naapa kwa Allah, wangaliniamuru niondoshe mlima miongoni mwa milima, pasingekuwa na uzito kuliko ile amri ya kukusanya Qur`ani, nilisema: Vipi mnafanya kitu kisichofanywa na Mtume S.A.W, akasema; wallahi ni heri. Basi Abu-Bakr aliendele kunijadili, hata Mwenyezi Mungu aliutuliza moyo wangu, kama vile alivyotuliza moyo wa Abi-Bakr na Umar R.A”.
Mwelekeo wa dalili ni dhahiri, kuwa wao walifanya kitu kipya hakikuwepo katika wakati wa Mtume S.A.W, kama alivyoeleza Hudhaifah RA.
Na jambo hili ni miongoni mwa Masilahi ya kawaida, ambapo wingi wa wanachuoni walieleza kuwa ni dalili. Imamu Al-Qarafiy katika [Sharh Tanqiih Al-Fusuul: Uk. 446, Ch. ya Sharikat At-Tibaah Al-Faniyah Al-Mutahidah] anasema: “Ilitangulia kuwa Masilahi ya kawaida yanatekelezwa katika Madhehebu yote kwa uhakiki; kwa sababu wanapima na kufasiri kwa mujibu wa minasaba, na wala hawaombi ushahidi wa kutambulisha, na hii ni maana ya Masilahi ya kawaida, na ilivyotilia mkazo kwa kuitekeleza Masilahi ya kawaida kuwa: Masahaba R.A, walifanya mambo kwa ajili ya masilahi tu, na si kwa kuwepo ushahidi wa kutambulisha, kama vile; kuandika msahafu, ambapo hakutangulia dalili wala mfano”. [Mwisho].
Hukumu za kusoma Qur`ani na Tajwidi zina elimu thabiti na kanuni zinazotawala, ambapo haziwezi kuzigeuza wala kuzibadilisha, kwa hiyo, Kamati ya mapitio ya Msahafu mtakatifu ya Al-Azhar iliamua usahihi wa alama hizi, na kuipaka rangi, katika ripoti yake inayoambatana na barua yetu hii, na ilivyotegemezwa kwa Ofisi ya kutoa Fatwa ya Misri.
Mifano yake kuipaka rangi Lafudhi ya Utukufu na nyingine miongoni mwa Majina Mazuri ya Mwenyezi Mungu, hakuna ubaya kufanywa hivi, kwa kuwa ni yenye faida, kwa sababu inavutia mawazo kwenye kutaja Lafudhi ya Utukufu, na hii inasaidia msomaji azingatie na kuleta unyenyekevu kwenye kumtaja Mwenyezi Mungu, kwa kusadikika kauli yake Mwenyezi Mungu: {Ambao, anapotajwa Mwenyezi Mungu, nyoyo zao hutetemeka}. [AL HAJJ: 35].
Kuhusu kuipaka rangi kwa kuzingatia maudhui si lazima kufanywa, kwa sababu ruhusa zinazopokelewa na Salaf hakika zimewekwa kwa ajili ya kudhibiti usomaji na hukumu za Tajwidi pasipo zingine, na maudhui hayana mwisho, na huenda kila kundi lina maudhui yake pekee, na hii itachochea tofauti. Kwa hiyo, kuna katazo la tofauti katika Qur`ani; Bukhariy na Muslim walipokea, kutoka kwa Jundub Ibn Junadah R.A, kuwa Mtume S.A.W, alisema: “Someni Qur`ani namna ya nyoyo zenu zinaungana, na mkitofautiana basi simameni nayo”.
Imamu An-Nawawiy katika [Shrh Muslim; 16/218, Ch. ya Dar Ihiyaa At-Turath Al-Arabiy] anasema: “Amri yake kwa kusimama kwenye tofauti katika Qur`ani, kwa rai ya wanachuoni, ni tofauti isiyojuzu, au tofauti hupelekea yasiyojuzu; kama vile tofauti katika Qur`ani yenyewe, au katika maana isiyo na jitihada, au tofauti hupelekea shaka, wasiwasi, fitina, uhasama, mgongano, n.k.”. [Mwisho].
Pia hii ni aina ya tafsiri na kubainisha maana ya maneno ya Mwenyezi Mungu, na Msahafu si mahali pake, ambayo ni nidhamu wazi na kitabu kipana cha mawazo yote yanayotabahari katika lugha na kanuni za kutafsiri matini yanayokubalika na kauli ya pamoja ya waislamu; kwa hiyo, kila alama huainisha maana maalum ya maneno ya Qur`ani pasipo nyingine, miongoni mwa maana yote, alama hii ni kinyume cha makusudio ya Qur`ani, ambayo yana upana na utajiri, kadhalika, ni namna ya kuingiza tafsiri katika Msahafu, na imepokelewa na baadhi ya Salaf, kama vile: Ibn Masu’ud R.A, kuwa ni Makuruhu, na yeye alichukia kuweka tafsiri katika Msahafu. Na Al-Haithamiy katika [Majma Az-Zawaid; 7/158, Ch. ya Maktabat Al-Maqdisiy] anasema: “At-Tabaraniy ameipokea, na wapokeji wake ni waaminifu”. [Mwisho], kwa hiyo, dhana ya bidaa nzuri haiambatani na sura hii, hasa inaweza kuwepo geuzi la maana inayotakiwa katika Aya na kuibadilisha.
Kwa hiyo, ni afadhali kutopaka rangi maneno ya Qur`ani, kutokana na maana yake au maudhui yake, na lazima kuachwa kwenye kuigeuza maana ya Qu`rani au kuibadilisha, hasa jambo hili lenye ugumu wa kulidhibiti na kulielekeza kimatendo; kutokana na wingi wa mashirika na wahusika wa uchapishaji, na kwa mtazamo wa kutoangalia matokeo na makosa yatakatokea na kazi hii, na hakika mfano wa hayo umetokea, lakini wanachuoni walitanabahisha na kulisahihisha, na kuondoa mabaya kunatangulizwa juu ya kuleta masilahi.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.
 

Share this:

Related Fatwas