1- Ujira wa Mwenye Jukumu la Wasia kwa Ajili ya Kuusia Juu ya Mali ya Watoto Wachanga
Question
Je, Inajuzu kwa mwenye jukumu la wasia kuchukua malipo kwa kazi ya kusimamia wasia juu ya watoto wachanga?
Answer
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Baadhi ya watu wanafanya kazi ya kusimamia wasia juu ya watoto wachanga, watu hao daima huwa ni jamaa za watoto hao, na hasa watu hao wanapata usaidizi wa vyombo vya sheria, ni sawa sawa iwe maiti alitoa wasia mwenyewe au hapana, na wala haiwi katika kila hali uwepo wa fedha za kutosha kwa namna ambayo panakatika utekelezaji wa masilahi ya kifedha ya watoto wadogo, basi huelekea kuchukua ujira kwa ajili ya kutenga muda kwa ajili ya kazi ya kusimamia mali.
Na jambo hili wanachuoni wa Fiqhi na wazungumzaji wa wasia juu ya mali ya mayatima, wanalisema kama vile wanavyuoni wa Tafsiri wanavyoelezea aya ya Surat An-Nisaa inayoambatana na jambo hili.
Lakini hukumu iliyopo katika suala hili nayo ni kujuzu kuchukua mali kwa ajili ya kuisimamia mali ya mtoto yatima na kuilinda pamoja na kuiwekeza.
Na dalili juu ya hayo ni kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na wajaribuni mayatima mpaka wafike umri wa kuoa.Mkiwaona ni wekevu, basi wapeni mali yao. Wala msiyale kwa fujo na pupa kwa kuwa watakuja kuwa watu wazima. Na aliye kuwa tajiri na ajizuilie, na aliyefakiri basi na ale kwa kadri ya ada. Na mtakapo wapa mali yao washuhudizieni. Na Mwenyezi Mungu anatoshakuwa Mhasibu.} [AN NISAA 6]
Na dalili hapa ni wazi, ambapo aya tukufu imetaja kwamba inajuzu kwa mwenye jukumu la uwasia akiwa ni fakiri huchukua kutoka mali ya yatima kwa kadri ya ada, baadhi ya wanafasiri walisema: "Kinachoeleweka ni kuwa achukue mali yote kwa kiasi cha kuisimamia kwake pamoja na ujira wa kazi yake, na wala hakuna kuilipa, na hiyo ni kauli ya Aisha R.A. na kundi moja miongoni mwa wenye elimu". [Tafsiri ya Al Baghawiy 169/2 Ch. Twibah].
Shekh Al Maraghiy amesema: "Ama kwa upande wa kuila mali ya yatima bila ubadhirifu wala pupa kwa kuchelea kuichukua atakapo baleghe, basi Mwenyezi Mungu Mtukufu Ametaja hukumu yake katika kauli yake: {Na aliye kuwa tajiri na ajizuilie, na aliyefakiri basi na ale kwa kadri ya ada}. Yaani mtu yeyote miongoni mwenu atakayekuwa tajiri na wala si muhitaji wa chochote katika mali ya yatima iliyo chini ya himaya yake basi na ajizuie kuila mali hiyo ya yatima. Na yoyote atakae kuwa fakiri na hawezi kuacha kunufaika na kitu kwa mali ya yatima ambaye anautumia baadhi ya muda wake katika kuwekeza mali hiyo na kuilinda basi na aile kwa wema. Na hicho ni katika kile kinachohalalishwa na sheria na wala watu wema hawakukanusha au kukizingatia kuwa ni hiyana na tamaa.
Na Ibn Jarer alisema: "Kwamba Umma unakusanyika kwa kuwa mali ya yatima siyo mali kwa walii, na hana haki ya kula kutoka mali hiyo. Lakini yeye analazimika kukopa kwa kiasi cha mahitaji yake kama anavyomkopea, na analazimika kujiajiri yeye mwenyewe kwa ajili ya mtoto yatima kwa ujira unaotambulika kama mtoto huyo atahitaji hivyo kama anaweza kutafutiwa mfanyakazi mwingine tofauti na yule miongoni mwa wafanyakazi asiye maalum kwa kazi hiyo sio katika hali ya utajiri au umaskini na kadhalika hukumu hiyohiyo kwa mali ya mwendawazimu na mjinga. Na Ahmad amepokelea kutoka kwa Ibn Omar R.A. kwamba mtu fulani alimwuliza Mtume S. A.W., mimi sina mali yoyote na mimi ni mwenye jukumu la wasia juu ya yatima. Basi Mtume S.A.W. akasema: "Kula kutoka mali ya yatima uliye naye bila ubadhirifu na bila ya kuchukuliwa sehemu ya mali ya asili ya yatima, bila ya kuichunga mali yako kwa mali ya mtu mwingine" na hekima katika jambo hili ni kwamba yatima katika nyumba ya walii kama mwanawe, na ni bora zaidi kwa ulezi wake kuwa amchanganye mtoto yatima na watu wake katika chakula na kwa kumlea kwake yatima basi walii akiwa tajiri na hana tama katika mali ya yatima basi mchanganiko utakuwa ni maslahi kwa yatima, na kama akiwa anatumia kitu chochote kutoka mali ya yatima basi lazima iwe kwa kiasi cha haja yake. Na anapokuwa fakiri hawezi kuacha kutumia sehemu ya mali ya yatima tajiri ambae yuko chini ya ulezi wake, kwa kiasi cha mahitaji yake ya fedha.
Basi kama akila kutoka chakula chake kama ilivyozoeleka baina ya waliochanganyika hakuigusa mali ya mtoto yatima wala hajipendelei yeye mwenyewe kwa nyumba au mali nyingine wala kutoa mali yake kwa masilahi yake binafsi na kuwa pamoja nae atakuwa kwa kazi yake hiyo akila kwa wema. [Tafsiri ya Al Maraghiy 189/4, Ch. Mustafa Al Babiy Al Halabiy].
Na miongoni mwa dalili pia yaliyotaja wazi katika Sunna katika Hadithi ya Amru Bin Shua'ib kutoka kwa babake, kutoka kwa babu yake R.A. kwamba mtu mmoja alikuja kwa Mtume S.A.W. na akasema: "Mimi ni fakiri na wala sina chochote isipokuwa nina mtoto yatima? Akasema: kula katika mali ya yatima wako bila ya ubadhirifu wala pupa au ulafi". [Ilitolewa na Abu Dawud na wengineo].
Al Khatwabiy alisema: Na kauli yake "Ghair Mutamthel" maana yake ni: Bila ya kuchukuliwa sehemu ya mali ya asili ya yatima na neno la Kiarabu" athlah" lina maana ya asili ya kitu. Na mwelekeo wa uhalali wa kula mali ya yatima ni kuwa hivyo kwa maana ya kula anachokistahiki kutokana na kazi aifanyayo halali, na anachukua kwa kiasi ya kufanya kazi nayo [Maalim Asunan 86/2, Ch. Al Matwuba'ah Al Elmiyah, Halab].
Na hayo pia yalikuja katika matamko ya baadhi ya Maswahaba; Al Qasem Bin Muhamad akasema: Mtu mmoja alikuja kwa Abdullah Bin Abaas, basi akasema: mimi nina yatima ana ngamia, je mimi naweza kunywa kutokana na maziwa ya ngamia wake? Basi Ibn Abaas akasema: Ukiwa unamkusudia ngamia wake aliyepotea na unampongeza... Na unamwandalia manywesho yake na unamnywesha siku ya zamu yake basi kunywa bila kuleta madhara yoyote ya kizazi chake na wala huzuiwi maziwa yake. [Malik aliipokelea katika kitabu chake Al Muwata'].
Na mwenye jukumu la kusimamia wasia ni kama wakili, basi ikiwa wakili inajuzu kuchukua ujira kwa ajili ya kazi yake, basi kadhalika mwenye jukumu la kusimamia wasia.
Na Hapana shaka kuwa tamko la kutosema kujuzu hupelekea upotevu wa mali ya mayatima kwa kutokubali mtu yoyote kuisimamia mali ya mtoto yatima isipokuwa wachache.
Na kama tulivyosema hapo juu, makundi ya wanavyuoni walisema:
Ibn Qudamah akasema; Na inajuzu kumfanya ampe uwakilishi aliyeusiwa kwani hiyo ni kama nafasi ya uwakilishi na uwakilishi unajuzu kufanywa kwa kupewa, na wasia pia ni hivyo hivyo. Basi Ishaq Bin Ibrahim alinukulu katika hali ya mtu humuusia mwingine na kumtengea kiwango cha pesa kiasi kilichotajwa na wala hakuna ubaya wowote. Na ugawaji wa muusiaji kwa anaeusiwa inajuzu kwa warithi kwani yeye ni mwakilishi wao, na kuwagawia warithi dhidi ya aliyeusiwa haijuzu kwani yeye sio mwakilishi wao. [Al Mughniy kwa Ibn Qudamah 248/6, Ch. Matwaba't Al Qahirah]
Na Al Khatwib As Sherbiniy alisema: Na ikiwa msimamizi wa jambo la mtoto ni mtu mgeni, basi anaweza kuchukua katika mali ya mtoto kiasi cha malipo ya kazi yake na iwapo haitoshi basi atachukua kiasi kinachomtosha kwa sharti la dhamana. Na akiwa ni baba au babu au hata mama ndiye aliye katika hukumu ya kuusiwa na ni fakiri basi matumizi yake yanatoka kwa mtoto huyo na atajihudumia mwenyewe kwa wema. Na yeye hahitaji idhini kutoka kwa mwenye sheria (Mtawala). [Mughniy Al Muhtaaj Sharhu Minhaaju Atwalibeen 124/4, Ch. Dar Al Kutub Al Elmiyah]
Kutokana na yaliyotanguliza inadhahiri kuwa inajuzu kuchukuwa ujira kwa ajili ya kuangalia kwa mali ya yatima na kuhifadhi kwake na kuishughulisha.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.